Showing posts with label Umoja wa Ulaya. Show all posts
Showing posts with label Umoja wa Ulaya. Show all posts
Magari kumi maarufu duniani

Magari kumi maarufu duniani

The World Car of the Year awards will be handed out at the New York motor show on March 28. In order to determine a winner, a 66-strong panel of motoring journalists from around the world have agreed on what they regard as the 10 best new cars of the last 12 months. Click through this gallery to see their choices, as well as what we awarded each car when we tested it. Do you agree? 
Audi A3
Bei:£19,205 


Range Rover review
Land Rover Range Rover
Bei: £71,295

Mazda6 review
Mazda6
Bei: from £19,595

Mazda CX-5 review - May 5, 2012
Mazda CX-5
Bei: £21,395
Mercedes-Benz A-class review
Mercedes-Benz A-class
Bei: from £19,000
  
Peugeot 208 driving
Peugeot 208
Bei:  £9,995

Porsche Boxster review
Porsche Boxster/Cayman
Price: from £37,589

The world's best performance cars
Subaru BRZ/Toyota GT86
Bei:  £24,995
Volkswagen Golf review
Volkswagen Golf
Bei: from £16,285

Volvo V40 review
Volvo V40
Price: from £19,745
 Waziri mkuu wa Ukraine ajiuzulu

Waziri mkuu wa Ukraine ajiuzulu


Maandamano nchini Ukraine
Rais wa Ukraine, Viktor Yanu-kovich, amekubali ombi la kujiuzulu kwa waziri mkuu wa taifa hilo, Mykola Azrov, pamoja na baraza zima la mawaziri licha ya hatua muhimu kupigwa mnamo Jumanne.
Hata hivyo mawaziri hao waliojiuzulu wanasalia kuwa wasimamizi wa wizara zao hadi pale serikali mpya itakapo buniwa.
Awali bunge la Ukrain lilipiga kura ya kuifutilia mbali sheria kali dhidi ya maandamano ambayo ilizua ghasia tangu iidhinishwe mwezi uliopita.
Kura ya kuifutilia mbali sheria hio ilipigwa na asilimia kubwa ya wabunge wa taifa hilo. Sheria hio ilipiga marufuku waandamanaji kutumia majengo ya umma pamoja na kuvaa vinyago.
Mwandishi wa BBC nchini Ukraine, amesema kuwa upinzani utaiona hatua ya waziri mkuu kujiuzulu pamoja na kufutilia mbali sheria inayozuia maandamano kama ushindi kwao
Mgogoro wa kisiasa nchini Ukraine, ulianza kama maandamano ya amani mwezi Novemba wakati ambapo Rais Yanukovych alipokataa kutimiza ahadi yake ya kushirikiana na Muungano wa Ulaya.
Waandamanaji hata hivyo wameapa kuendelea kuandamana hadi Rais Yanukovych atakapojiuzulu.
Na BBCSwahili
Wakutana lakini hawasemezani

Wakutana lakini hawasemezani

Lakhdar Brahimi akiwaeleza waandishi wa habari kuwa wajumbe wa Syria watakutana chumba kimoja
Wajumbe wa pande mbili zinazopigana vita nchini Syria wanaohudhuria mkutano wa amani mjini Geneva walikutana kwa muda mfupi.

Walikaa chumba kimoja huku wamekabiliana, lakini hawakuzungumza moja-kwa-moja isipokuwa kwa kuptia mpatanishi wa Umoja Mataifa, Lakhdar Brahimi.
Kikao hicho cha kwanza kilidumu nusu saa tu, na mpatanishi pekee ndiye aliyezungumza. Mwandishi wa BBC mjini Geneva anasema utaratibu huo umewekwa ili kuepusha ugomvi kati ya wajumbe; na itifaki hiyo itafuatwa katika vikao vijavyo.
Wajumbe wakitarajiwa kukutana tena Jumamosi, na watalenga namna ya kufikisha misaada kwa wanyonge na kuwaachilia huru wafungwa wa kisiasa.
Upinzani unasema utaomba kuwa mapigano yasitishwe katika mji wa Homs.
Na BBCswahili
 Suala la mabadiliko ya tabia nchi lapewa kipaumbele Davos

Suala la mabadiliko ya tabia nchi lapewa kipaumbele Davos

Viongozi wanaokutana katika Kongamano la Kimataifa la Kiuchumi mjini Davos, Uswisi, wamelipa kipau mbele suala la kushinikiza kuimarishwa uchumi wa ulimwengu na kupunguza kiwango cha joto duniani kwa kuzingatia vyanzo safi vya nishati. 
Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, Christiana Figueres, amesema uchumi wa ulimwengu uko hatarini, kama hapatakuwepo na muafaka mjini Paris mnamo mwaka wa 2015 wa kupunguza kiwango cha gesi ya sumu kutoka kwenye makaa ya mawe na mafuta.
Mkutano huo ambao umeng'oa nanga hii leo, unahudhuriwa na zaidi ya viongozi 40 wa nchi na serikali pamoja na mawaziri wengi wa mambo ya kigeni kutoka kote ulimwenguni. 
Kwa mara ya kwanza katika mwongo mmoja, Rais wa Iran, Hassan Rouhani, atapewa fursa ya kulihutubia kongamano hilo hapo kesho. 
Rouhani anatarajiwa kuzungumza kuhusu mpango wa nchi yake wa nyuklia pamoja na nafasi za uwekezaji kwa makampuni ya kigeni.
EU yaionya serikali ya Ukraine dhidi ya ukandamizaji

EU yaionya serikali ya Ukraine dhidi ya ukandamizaji

Rais wa Halmashauri ya Ulaya Jose Manuel Barroso ametoa wito wa kusitishwa machafuko nchini Ukraine na akaionya serikali ya nchi hiyo kuwa Kamati Kuu ya Umoja wa Ulaya itatathmini "uwezekano wa kuchukuliwa hatua". 
Barroso amesema wameshtushwa na habari za karibuni kutoka Ukraine ambako waandamanaji wawili wameuawa mapema leo wakati polisi walipoivamia kambi moja ya maandamano na kuanza kupambana na waandamanaji wanaoipinga serikali. 
Rais Viktor Yanukovich leo anakutana na viongozi wakuu wa upinzani, ikiwa ni siku moja baada ya kufutilia mbali uwezekano wa kufanya mazungumzo ya aina hiyo. 
Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Ukraine Mykola Azarov amewashutumu waandamanaji wanaoipinga serikali akiwaita kuwa ni "magaidi". 
Maelfu ya Waukraine wamefanya maandamano mjini Kiev tangu rais Yanukovich alipokataa kusaini mkataba wa ushirikiano wa kibiashara na Umoja wa Ulaya, na badala yake akaimarisha mahusiano na Urusi.
Umoja wa Ulaya kutuma kikosi CAR

Umoja wa Ulaya kutuma kikosi CAR

Umoja wa Ulaya umekubali kutuma wanajeshi 500 katika Jamhuri ya Afrika ya Kati katika juhudi za kusaidia kurejesha amani.
Uamuzi huo ulipitishwa baada ya wabunge katika jamhuri hiyo kumchagua meya wa mji mkuu, Bangui, Catherine Samba Pinza kuwa rais wa mpito wa nchi hiyo, akichukua nafasi iliyoachwa na Michel Djotodia, kamanda wa wanamgambo wa Seleka aliyejiuzulu mwezi huu.
Mgogoro ulianza katika Jamhuri ya Afrika ya Kati baada ya wanamgambo wa kiislamu kuchukua hatamu za uongozi wa nchi.
Ujumbe wa Umoja wa Ulaya utaungana na wanajeshi 1,600 wa Ufaransa na wengine wapatao 4000 kutoka mataifa ya kiafrika ambao tayari wamewasili nchini humo. 
Mkuu wa Sera wa Umoja wa Ulaya Catherine Ashton amesema wanajeshi wao watafanya kazi katika mji mkuu Bangui kwa muda wa hadi miezi sita, wakisaidia  kulinda usalama wa watu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.

MAKARDINALI WOTE WATIMULIWA KWA KUJIHUSISHA NA FEDHA CHAFU...

Papa Francis II.
Makardinali wote isipokuwa mmoja waliokuwa wakisimamia benki ya Vatican wamefutwa kazi na Papa Francis.

Waliokumbwa na 'fagio hilo la chuma' ni makadinali wanne ambao ni pamoja na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya  Nje, Kadinali Tarcisio Bertone SDB, Kadinali Odilo Scherer kutoka Brazil, Telesphore Toppo kutoka India na Domenico Calcagno kutoka Vatican.
Kadinali Jean-Louis Tauran ambaye ni Mkuu wa Baraza la Upapa linalohusika na Mijadala ya Kidini, amenusurika kwa mujibu wa gazeti la kila wiki la Kikatoliki la The Tablet.
Gazeti hilo  lilieleza jana kuwa isipokuwa Calcagno, makadinali hao wote ndio kwanza walikuwa wametimiza miezi 11 tangu wateuliwe katika kipindi cha pili cha miaka mitano, wakiwa wameteuliwa na Papa Benedict XVI muda mfupi kabla ya kujiuzulu.
Benki hiyo ya Vatican ilikumbwa na kashfa ya utakatishaji fedha mwaka 2010 baada ya waendesha mashitaka wa Italia kugundua shughuli zenye shaka zihusuzo fedha chafu ndani ya benki.
Mwenyekiti wa Benki hiyo,  Ettore Gotti Tedeschi na naibu wake, Paolo Cipriani walichunguzwa baada ya polisi kukamata euro milioni 23 kutoka kwenye akaunti ya benki hiyo.
Ilidaiwa kuwa ingawa benki hiyo ilikuwa inadai kupambana na utakatishaji fedha, ilivunja sheria kwa kujaribu kuhamisha fedha hizo bila kutambulisha mtumaji wala mpokeaji, au zilikuwa zinatumika kwa shughuli gani. Tuhuma hizo zilikanushwa kwa nguvu zote na Vatican.
Papa Francis ameteua makadinali wengine kuziba nafasi za aliowatimua na kuunda alichokiita Tume ya Makadinali ya Kusimamia Taasisi kwa ajili ya Kazi ya Dini (IOR), ambao ni makadinali  Christoph Schรถnborn (Vienna), Thomas Collins (Toronto); Santos Abril y Castillo´ (St Mary Major) na Kadinali Pietro Parolin (Waziri wa Mambo ya Nje).
Wajumbe wa Tume hiyo watachagua rais katika siku chache zijazo itakapofanya mkutano wake wa   kwanza. Kadinali Bertone ndiye alikuwa Rais hadi alipoondolewa.
Kadinali Jorge Mario Bergoglio, ambaye alipewa jina la Papa Francis, ni Papa wa kwanza Muargentina na wa kwanza kutoka nje ya Ulaya kwa zaidi ya miaka 1,000 baada ya kuchaguliwa Machi 13 mwaka jana.
Papa Francis anaweza kuwa haoneshi mapenzi mengi kwa makadinali wake wa benki, lakini anajihusisha zaidi na wanandoa, kwani ametuma mialiko kwao kwa ajili ya kusherehekea Siku ya Wapendanao pamoja naye.
Kadi iliyoandikwa 'Furaha ya Ndiyo Daima' ilitolewa na Vatican ikiwaalika wanandoa wasio wa jinsia moja kukaa faragha na Papa mwezi ujao.
Kwa hafla hiyo iliyoandaliwa na Baraza la Upapa la Vatican kwa Familia, washiriki wametakiwa kujiandikisha ifikapo Januari 30 ili kupata nafasi ya kukaa.
UNSC: Kikosi cha kulinda amani kutumwa Mali

UNSC: Kikosi cha kulinda amani kutumwa Mali


UNSC: Kikosi cha kulinda amani kutumwa Mali
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limesisitiza juu ya kutumwa haraka kikosi  kingine  cha kulinda amani cha umoja huo nchini Mali. 
Taarifa iliyotolewa jana mjini New York imeeleza kuwa, Baraza la Usalama limelazimika kuchukua hatua hiyo ya dharura baada ya Ufaransa kutangaza azma ya kupunguza wanajeshi wake walioko nchini humo.
Umoja wa Mataifa unachukua maamuzi ya kutuma wanajeshi zaidi wa kulinda amani nchini Mali katika hali ambayo hivi sasa umoja huo una askari wake 5,500 tu,  jumla ya wanajeshi 11,200 wa kulinda amani walioko nchini humo. 
Ufaransa ambayo ina wanajeshi zaidi ya 2,500 nchini Mali inakusudia kupunguza wanajeshi wake hadi kufikia 1,000 ifikapo mwezi Julai mwaka huu.
Wakati huohuo Bert Koenders Kamanda wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa nchini Mali MINUSMA amesema kuwa, kuna udharura wa kutumwa askari zaidi wa kulinda amani  kutokana na kuendelea mapigano nchini humo.
Na Kiswahili.irib.ir
 AU yaisifia IGAD inavyoshughulikia mgogoro wa Sudan Kusini

AU yaisifia IGAD inavyoshughulikia mgogoro wa Sudan Kusini


Wajumbe kutoka upande wa waasi wakiwa Ethiopia kwenye mazungumzo ya kutafuta amani Sudan Kusini
Wajumbe kutoka upande wa waasi wakiwa Ethiopia kwenye mazungumzo ya kutafuta amani Sudan Kusini
Naibu mwenyekiti wa Umoja wa Afrika-AU anasema taasisi yake  inafanya kazi na washirika  wa kimataifa kuweka shinikizo kwa pande  hasimu za Sudan Kusini kubuni eneo la kibinadamu ambalo litaruhusu mashirika ya misaada kugawa  misaada zaidi inayohitajika kwa waathirika wa mgogoro.

Sikiliza sauti ya ripoti hii

Erastus Mwencha aliiambia Sauti ya Amerika-VOA kuwa AU pia inahamasishwa na juhudi za IGAD kwenye mazungumzo ya amani yanayoendelea nchini Ethiopia ya kusaidia kurejesha hali ya usalama huko Sudan Kusini. Mazungumzo yamekwama juu ya kuendelea kushikiliwa kwa wanasiana 11 walioshutumiwa na Rais Salva Kiir kwa kupanga kuiangusha serikali mjini Juba.

Makamu Rais wa zamani Riek Machar  hadi sasa anakataa kutia saini mkataba wa kusitisha mapigano akisisitiza kwamba maafisa waliokamatwa wanatakiwa kuachiwa kabla ya mkataba kutiwa saini. Mwencha anasema AU inaunga mkono juhudi za IGAD kusaidia kutatua masuala yanayodumaza mashauriano ya amani katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.

Mamia ya wa-Sudan Kusini wamekoseshwa makazi kutokana na ghasia. Mwencha anasema kuna haja kwa pande zinazopambana kutoa fursa kwa makundi ya misaada ambayo yanaweza kutoa msaada kwa waathirika wa mgogoro.
                                                                                                    
                                                                                                      
Rais wa Uganda Yoweri MuseveniRais wa Uganda Yoweri Museveni
Wakati huo huo Uganda inakiri kuwa majeshi yake yanalisaidia jeshi la Sudan Kusini kupambana na waasi ikibadilisha ukanushaji wa awali. Msemaji wa jeshi la Uganda  alisema Alhamis  kuwa majeshi ya nchi yake yanasaidia kuwafurusha waasi kutoka Bor, mji mkuu wa jimbo la Jonglei, Sudan Kusini.

Awali Rais Yoweri Museveni alisema majeshi ya Uganda yalishiriki kwenye mapigano  makubwa na waasi siku ya Jumatatu kiasi cha kilomita 90 kutoka mji mkuu, Juba.  Uganda awali ilisema majeshi yake yalikuwepo huko Sudan Kusini kuwalinda na kuwaondoa raia wa Uganda. 
Na VioaSwahili
 Vatican yahojiwa kuhusu ukiukaji wa kingono dhidi ya watoto

Vatican yahojiwa kuhusu ukiukaji wa kingono dhidi ya watoto

Maafisa kutoka makao makuu ya Vatican wamehojiwa hadharani kwa mara ya kwanza, kuhusiana na vitendo vya unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto, vilivyofanywa na mapadri wa kanisa Katoliki. 
Katika mahojiano hayo, Umoja wa Mataifa umewauliza maafisa hao maswali kadhaa, ikiwemo kwa nini taarifa muhimu hazikutolewa, na nini walikuwa wanafanya kuzuwia ukiukaji katika siku zajazo.
Vatican ni mwanachama wa mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watoto, ambao unatekelezwa kisheria, na unayalinda makundi ya kijamii yaliyo hatarini zaidi.
Mjumbe wa Vatican katika Umoja wa Mataifa Askofu Silvano Tomas amesema vitendo vya udhalilishaji watoto kingono haviwezi kukubalika, na hiyo ndiyo sera ya Vatican ya muda mrefu. 
Makao makuu ya Vatican yamesisitiza jana kuwa yamedhamiria kukomesha vitendo vya unyanyasaji wa kingono miongoni mwa viongozi wake wa kidini.

Serikali ya Ukraine yautetea muafaka wake na Urusi

Waziri Mkuu wa Ukraine Mykola Azarov ameutetea mkataba ambao nchi hiyo ilisaini na Urusi akisema umeiwezesha serikali kuepuka kufilisika pamoja na kusambaratika huduma za jamii.
 Azarov amesema muafaka huo uliotiwa saini na Rais wa Ukraine Viktor Yanukovych na mwenzake wa Urusi Vladmir Putin ulikuwa njia pekee ya kuuokoa uchumi wao uliokuwa umedorora kwa muda. Mapema leo, upinzani nchini Ukraine ulimkosoa rais Yanukovych ukisema anauza masilahi ya Ukraine kwa Urusi na kuinyima nchi hiyo nafasi ya kujiunga na Umoja wa Ulaya.
 Upinzani unahofia kuna mambo ya siri ambayo yalifungamanishwa na makubaliano hayo ya mkopo wa dola bilioni 15 pamoja na kuiuzia gesi Ukraine kwa bei ya chini. Kiongozi wa upinzani Vitali Klitschko ameahidi kuendelea kumshinikiza rais Yanukovych aitishe uchaguzi wa mapema.

Merkel asema EU inastahili kuirekebisha mikataba yake

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema leo kwamba wanachama wa Umoja wa Ulaya lazima wawe wepesi wa kuifanyia mabadiliko mikataba ili kuimarisha uongozi wa pamoja wa kiuchumi katika umoja huo wenye mataifa 28. 
Merkel aliyasema hayo siku moja baada ya kuanza muhula wake wa tatu kama kansela wa taifa kubwa kiuchumi barani Ulaya, kabla ya kuelekea Paris kwa mazungumzo na Rais Francois Hollande. Baadae atakwenda Brussels kuhudhuria mkutano wa kilele wa siku mbili wa Umoja wa Ulaya unaoanza kesho. 
Bibi Merkel ameliambia bunge la Ujerumani kuwa Umoja wa Ulaya unahitaji kufanya kazi kwa kuzingatia uongozi wa pamoja wa kifedha na kiuchumi, ambapo wanachama wanaweza kushurutishwa kutimiza malengo kadhaa ya bajeti, hata kama kutahitajika mabadiliko katika mikataba muhimu ya Umoja huo. 
Rais Hollande wa Ufaransa anapinga kufanyiwa mabadiliko mikataba ya Umoja wa Ulaya, na badala yake anashinikiza kuwepo sera za kuwezesha ukuaji zaidi wa uchumi na kupunguza kiwango cha kubana gharama za matumizi ndani ya mikataba iliyopo
Na DW.DE

UN yaomba msaada wa Dola bilioni 13

Umoja wa Mataifa umetoa ombi la kutolewa kiasi cha Dola bilioni 13 kwa ajili ya shughuli za misaada kwa mwaka ujao wa 2014. 
Katika mkutano uliofanyika Geneva, Uswisi, Mratibu wa masuala ya kibinaadamu na dharura wa Umoja wa Mataifa, Valerie Amos, amesema kuwa nusu ya kiasi hicho cha fedha kinahitajika kwa ajili ya Syria na mataifa jirani. 
Kwa ujumla msaada wa mwaka mzima utawasaidia watu milioni 52 katika mataifa 17.

Urusi huenda ikaipa Ukraine mkopo

Shirika la habari la Urusi, Interfax, limemnukuu msaidizi wa rais wa nchi hiyo, Andrei Belousov, akisema kuwa Urusi huenda ikaipatia Ukraine mkopo, ikiwa utawala mjini Kiev utauomba. 

Belousov alinukuliwa akisema hali imefikia mahala ambapo bila mikopo kutoka upande mmoja au mwingine, Ukraine itashindwa kuendeleza utulivu wa kiuchumi. 
Wakati huo huo, kiongozi wa upinzani Vitali Klitschko, anasema wataandamana hadi waiangushe serikali.
Ukraine inatafuta msaada ili iweze kujaza pengo na ufadhili wa nje unaofikia dola za Marekani bilioni 17 mwaka ujao. 
Rais Viktor Yanukovych wa Ukraine, ambaye amekabiliwa na maandamano tangu serikali yake ilipoamua kutosaini makubalinao ya biashara uhuru na Umoja wa Ulaya, anaizuru Urusi kesho Jumanne, na Belousov alisema huenda akaomba mkopo wakati wa ziara hiyo.

Yanukovich kukutana na upinzani

Rais Viktor Yanukovich  amesema  leo  kuwa  yuko  tayari kukutana  na  marais  watatu  wa  zamani  wa  Ukraine kujadili njia  za  kujitoa kutoka  katika  mzozo  wa  kisiasa ambao  umeidhoofisha  nchi  hiyo. Mkuu  wa  sera  za mambo  ya  kigeni  wa  Umoja  wa  Ulaya  Catherine Ashton anaelekea  Ukraine  kusaidia  kuutatua  mzozo  huo. 
Akizungumza  na  waandamanaji  kiongozi  wa upinzani kutoka  chama  cha  UDAR Vladimir Klitschko amewataka kuandamana kwa amani.
Mamia  ya  polisi  wameingia  katika  eneo  la  kati  la  mjini Kiev leo wakati  maandamano  ya  kupinga  serikali yakiikumba Ukraine  kwa  wiki  ya  pili sasa, na  kuzusha hofu  ya  hatua  kali  zitakazochukuliwa  na  serikali. 
Rais Viktor Yanukovich amekumbana  na  wiki  kadha  za maandamano  baada  ya  kukataa  kutia  saini makubaliano  na  Umoja  wa  Ulaya  mwezi  uliopita  na kuamua  kuhusiana  na  Urusi.
Polisi  wamewekwa  katika maeneo  nje  ya  jengo  la  halmashauri  ya  mji wa  Kiev, wakati  ambapo  waandamanaji  nao  wameweka  vizuwizi katika  baadhi  ya  mitaa .

Georgia, Moldova zakubaliana na Umoja wa Ulaya

Umoja wa Ulaya umefanikiwa hivi leo kuanzisha makubaliano ya ushirikiano na Georgia na Moldova, lakini ukashindwa kuishawishi Ukraine, katika jitihada zake za kuimarisha mafungamano na mataifa sita, yaliyokuwa sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Kisovieti. 
Ukraine, ambalo ni taifa kubwa kabisa miongoni mwa hayo sita, ilikuwa tayari imeanzisha makubaliano ya kisiasa na kibiashara na Umoja wa Ulaya, lakini ilisita kuyasaini baada ya shinikizo la Urusi. Makubaliano haya ya leo na Georgia na Moldova nayo yanahitaji kusainiwa ili kuanza kazi rasmi, hatua inayotarajiwa mwakani. 
Rais wa Lithuania, Dalia Grybauskaite amesema mwenzake wa Ukraine, Viktor Yanukovych, haonekani kuwa tayari kuendelea na mafungamano na Umoja wa Ulaya. 
Rais wa Umoja huo, Herman Van Rompuy, amezipongeza Georgia na Moldova kwa ushujaa na dhamira zao za kisiasa.

Kategori

Kategori