Showing posts with label 2017 at 02:12PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 02:12PM. Show all posts
TABORA: MUUGUZI AMCHOMA BINTI SINDANO YA USINGIZI NA KUMBAKA

TABORA: MUUGUZI AMCHOMA BINTI SINDANO YA USINGIZI NA KUMBAKA

MUUGUZI anayefanya kazi Kituo cha Afya Kata ya Igurubi Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Damian Mgaya (26) anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma ya kumbaka binti wa miaka 18 mkazi wa Kitongoji cha Mwagala B, Kijiji cha Mwagala.
Mtendaji wa Kata ya Igurubi, Ntemi James alisema uhalifu huo umefanyika Julai 14, mwaka huu saa 8 hadi alfajiri wakati binti huyo akimuuguza mama yake, Tatu Simbi ambaye amelazwa katika kituo hicho cha afya baada ya kushambuliwa kwa kipigo na mume wake. James alidai mtuhumiwa alimpokea mama wa binti huyo akiwa hoi na ndipo alimpatia matibabu kisha kumlaza katika kituo hicho cha afya huku akimchoma sindano ya usingizi ambayo ilisababisha mama huyo kupitiwa na usingizi.
Mtendaji huyo alidai kuwa muuguzi Damian alipoona mama wa binti huyo amelala, alimwambia waende wote chumba kingine ili akachukue dawa ya mama yake; lakini hata hivyo hakumpa dawa na badala yake alimwambia amchome sindano ili asipate maradhi kwa kuwa mazingira ya hospitali sio mazuri. Baada ya kuambiwa hivyo, binti huyo alikubali kuchomwa sindano mbili na alipochomwa sindano ya kwanza aliishiwa nguvu na alipochomwa sindano ya pili alianguka na kupitiwa na usingizi hadi asubuhi.
Alisema baada ya kuona amelala pasipokuwa na fahamu, muuguzi huyo alianza kumbaka hadi alfajiri alipoamshwa na mama yake huku yeye akiwa hajitambui kutokana na maumivu aliyokuwa akiyasikia sehemu zake za siri na mwili wote. Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Bonaventura Kalumbete alithibitisha kubakwa kwa binti huyo na muuguzi huyo na kueleza kuwa baada ya kupata taarifa hiyo, alituma timu ya wataalamu ambayo ilibaini binti huyo kubakwa na amelazwa kwenye kituo hicho na hali yake ni mbaya kwani hawezi kutembea.
Aidha, Dk Kalumbete alisema uchunguzi wa awali unaonesha binti huyo alichomwa sindano wakati alikuwa hata haumwi na hizo dawa nazo zimechangia kumsababishia kushindwa kutembea huku akiahidi kuwa baada ya uchunguzi, muuguzi huyo atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Mkuu wa Wilaya ya Igunga ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, John Mwaipopo alikiri kukamatwa kwa muuguzi baada ya kupokea taarifa ya kubakwa kwa binti huyo, alimwagiza Mkuu wa Polisi Igunga kumkamata muuguzi huyo Damian Mgaya ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria.
Chanzo: HabariLEO

from Blogger http://ift.tt/2uqYDlj
via IFTTT


Baada ya Roma Kupatikana ..Msanii Mwingine Bongo Ahukumiwa Kifungo cha Miezi 6..!!!

Baada ya Roma Kupatikana ..Msanii Mwingine Bongo Ahukumiwa Kifungo cha Miezi 6..!!!

Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, imemuhukumu kifungo cha nje cha miezi sita na kulipa faini ya Sh1 milioni, Aman Mwasote baada ya kutiwa hatiani kwa kumwita mtoto wa miaka tisa kuwa mchawi.
Mwasote, ambaye ni mwimbaji wa nyimbo za Injili alishtakiwa kwa kutoa kauli kuwa mtoto huyo huwaloga wanafunzi na walimu alipokuwa kwenye mkutano wa injili.
Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Mkazi, Venance Mlingi aliyesema mahakama imeridhishwa na ushahidi uliotolewa na mashahidi wanne wa upande wa Jamhuri kwamba, Mwasote alitenda kosa hilo.
Awali, Wakili wa Serikali, Xaveria Makombe alidai mshtakiwa alitenda kosa hilo Septemba 20, mwaka jana eneo la Shule ya Msingi Kalobe, akiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Injili.
Hakimu Mlingi alisema mshtakiwa atatumikia kifungo cha nje kwa kufanya shughuli za kijamii na Aprili 20 atatakiwa kufika mahakamani ili apangiwe shughuli ya kufanya.

from Blogger http://ift.tt/2ohwK7X
via IFTTT


Narudi Mtama Kuwaeleza Wapiga Kura Wangu Ukweli Wote โ€“ Nape

Narudi Mtama Kuwaeleza Wapiga Kura Wangu Ukweli Wote – Nape

Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye ametoa shukrani kwa wote waliomuunga mkono katika kusimamia haki huku akisema kuwa ataenda kuwaeleza wananchi wake ukweli wote.
“Shukrani kwa wote mlioniunga mkono katika kusimamia haki. Narudi Mtama kuwaeleza wapiga kura wangu UKWELI WOTE. Ni Jmosi hii tar 8/4/17,” ameandika Nape kupitia Twitter.
Marchi 23, Rais Magufuli alimuondoa Nape kama Waziri wa Habari,Sanaa na Michezo na nafasi hiyo kuchukuliwa na Dkt Harrison Mwakyembe aliyekuwa waziri wa Katiba na Sheria.

from Blogger http://ift.tt/2nfwcUB
via IFTTT


Kategori

Kategori