Showing posts with label 2017 at 11:24AM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 11:24AM. Show all posts
ALIEIGIZA KAMA BABA KWENYE MOVE ZA HOME ALONE AFARIKI DUNIA

ALIEIGIZA KAMA BABA KWENYE MOVE ZA HOME ALONE AFARIKI DUNIA

California, Marekani. Mwigizaji John Heard aliyejizolea umaarufu kwa kuigiza kama baba katika filamu za Home Alone, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 72.
Mwili wake aligundulika na mhudumu wa hoteli aliyofikuwa amefikia kwa ajili ya mapumziko baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo wa mgongo jijini California, Marekani.
Heard alikuwa akiigiza kama Peter McCallister katika filamu za Home Alone akiwa baba wa Macaulay Culkin maarufu Kelvin.
Ameigiza katika filamu mbili kati ya hizo ambazo ni Home Alone na Home Alone 2: Lost in New York

from Blogger http://ift.tt/2uUIdC7
via IFTTT


Taarifa kuhusu utata wa Biashara ya Gesi Tanzania na Kenya

Taarifa kuhusu utata wa Biashara ya Gesi Tanzania na Kenya

Taarifa iliyotumwa kwa umma kutoka Wizara ya Biashara na Uwekezaji inasema kwamba Tanzania itaendelea kuheshimiwa kwenye mikataba ya Kibishara na Nchi Kenya.
Tarehe 24 Aprili, 2017 magazeti nchini Kenya yalitoa taarifa ya kwamba Serikali ya Kenya itapiga marufuku uingizwaji wa gesi ya kupikia
Liquefied Petrolium Gas, LPG ) nchini humo kutokea Tanzania, na kwamba gesi itakayoruhusiwa kuingia Kenya ni ile itakayokuwa imepitia kwenye Bandari ya Mombasa peke yake. Baada ya kusoma taarifa hizi Serikali ya Tanzania iliwasiliana na Serikali ya Kenya ili kupata maelezo kuhusu hatua hii ambayo ni kinyume cha taratibu za kibiashara katika Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. 
Tarehe 18 Mei, 2017 Serikali ya Kenya ilitekeleza uamuzi wake kwa kuzuia shehena ya gesi isiingie Kenya kutokea Tanzania. Hatua hii ina athari kubwa kwa wafanyabiashara wa gesi ya kupikia hapa nchini pamoja na watu wote ambao ajira zao zinategemea biashara hii. Wakati hatua hizi zinachukuliwa bado Serikali ya Kenya ilikuwa haijatoa maelezo rasmi kwa Tanzania kuhusu uamuzi wake huo. Katika kikao cha Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kilichofanyika tarehe 2 Juni, 2017,
 suala la hatua ya Kenya kupiga marufuku uingizwaji wa gesi kutokea Tanzania lilizungumzwa kwa kirefu na kufanyiwa maamuzi. Kimsingi Serikali ya Kenya ilikubali kuondoa katazo la uingizaji wa gesi kupitia Tanzania mara moja, na makubaliano haya yaliingizwa kwenye kumbukumbu za Mkutano ambazo ziliafikiwa na nchi zote wanachama wa Jumuiya kwa kuweka sahihi. 
Pamoja na makubaliano haya, Kenya imeendelea kuzuia gesi isiingie nchini mwao kutokea Tanzania. Serikali ya Tanzania imewasilisha rasmi malalamiko yake Kenya kuhusu suala hili.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2sjE1uW
via IFTTT


Tahadhari..Kuwa Makini na Kofia za Helment za Bodaboda..Wanazipaka Dawa Zitakazokupoteza Fahamu Ili Wakuibie..Sambaza Ujumbe Huu kwa Mwezako..!!!

Tahadhari..Kuwa Makini na Kofia za Helment za Bodaboda..Wanazipaka Dawa Zitakazokupoteza Fahamu Ili Wakuibie..Sambaza Ujumbe Huu kwa Mwezako..!!!

Hii imenitokea tarehe 28/05/2017 maeneo ya ubungo 
Iko hivi hawa jamaa waendesha bodaboda wamebuni mbinu mpya za kuwaibia wateja wao.
Niipanda Boda Boda pale ubungo river side baada ya kumweleza naelekea wapi nikapewa kofia (helmet) nikavaa ,baada ya kuivaa mara moja dereva alianza safari na akawa anaendesha mbio ilikuwa jioni ya saa 1:30 kwenda saa mbili usiku.
Kitendo cha kusogea mbele kidogo nilianza kuishiwa nguvu huku Dereva naye akianza kupotelea machochoroni baada ya muda mfupi nilipoteza fahamu sikuwa najitambua tena .
Ilinichukua masaa kama matatu hivi kuja kuzinduka kutoka usingizini,wakati huo nilijikuta vitu vyangu vyote nilivyobeba sikuwa navyo ikiwa ni pamoja na pesa kiasi cha shs 180,000 pamoja na laptop yangu na vitu vingine .
Hivyo nawaonya mnaopanda bodaboda muwe makini hasa nyakati za usiku helmet Inapakwa madawa yanayosababisha kuishiwa nguvu kabisa na hii haijalishi mwanamke ,mwanaume kuweni makini na madereva msiowajua.

from Blogger http://ift.tt/2rVDKhe
via IFTTT


Ujue Ugonjwa Hatari wa Homa ya Matumbo (Typhoid fever) na Matibabu Yake..!!!

TYPHOID FEVER
Homa ya matumbo
Homa ya matumbo husababishwa na bakteria anayeitwa Salmonella Typhoid. Ugonjwa huu huambukizwa kwa mtu kula au kunywa chakula au maji yalio na kinyesi cha mu aliyambukizwa. Bakteria hawa hutoboa na kunyonya chakula kwenye matumbo ya binadamu.
Dalili ya Maradhi:
Homa kali
Kutoka kwa majasho mengi
Kuharisha (bila ya kutoa damu)
Mara nyingine, vitone vyekundu huonekana kwenye mwili.
Kwa kawaida, homa ya matumbo isipotibiwa hugawanyika katika hatua nne, kila hatua ikichukua takriban wiki moja.
Katika wiki ya kwanza:
Joto la mwili huongezeka
Kichwa huuma
Kukohoa
Damu kutoka kwa pua, ingawa tukio hili huwa ni nadra kutokea.
Maumivu ya tumbo pia huweza kutokea
Katika wiki ya pili:
Homa huongezeka
Mgonjwa huanza kupagawa, kama mwenda wazimu
Vitone vyekundu huanza kutokea kwenye kifua
Mgonjwa huharisha, takriban mara sita au nane kwa siku.
Kutapika kwa mgonjwa
Ini la mgonjwa huvimba
Homa ya mgonjwa huongezeka katika wakati wa alasiri kwenye wiki ya kwanza na ya pili.
Wiki ya tatu:
Matumbo hutoa damu.
Matumbo hutoboka
Wiki ya Matibabu[hariri | hariri chanzo]
tatu ikimalizika, homa huanza`kutilia. Hii huendelea hadi wiki ya nne.
Matibabu kwa dawa za kizungu
Mara nyingi, homa ya matumbo haiuwi binadamu. Dawa kama ampicillin, chloramphenicol, trimethoprim-sulfamethoxazole, Amoxicillin and ciprofloxacin hutumika kutibu wagonjwa katika nchi zilizoendelea.
DAWA YA KUTIBU HOMA YA MATUMBO DAWA YA TIBA ASILIA
FANYA HIVI: Chukuwa Glasi 4 za Maji tia ndani ya jagi la maji changanya na nusu kijiko kidogo cha chumvi ya unga. Kisha tia ndani yake vijiko 6 vidogo vya sukari, kisha koroga vizuri hayo maji.
Matumizi yake: kunywa asubuhi kabla ya kula kitu glasi 1 mchana glasi 1 Jioni Glasi 1na usiku glasi 1 kila siku dawa ikiisha tengeneza dawa ingine utumie hiyo dawa kwa siku 30 utaweza kupona.
Hatua za kuzuia kupata homa hii
Usafi wa mazingara na wa kibinafsi ni hatua bora ya kujikina kutokamana na ugonjwa huu.
Homa ya matumbo haiathiri wanyama kwa hivyo maambukizi ni kutoka kwa binadamu mmoja hadi mwingine.
Homa hii hueza kuenea kwenye mazingara ambayo kinyesi cha binadamu hutangamana na vyakula vyao. Upishi wa makini na uoshaji mikono ni kingo bora zaidi kwa kuzuia maradhi haya kuenea.
Chanjo ni za aina mbili: moja inayotiwa kwa njia ya mdomo iitwayo Ty21a (au Vivotif Berna) na nyingine ya sindano kwa majina Typhim Vi iliyotengenezwa na Sanofi Pasteur au Typherix iliyotengenezwa na GlaxoSmithKline.
Ukitumia Dawa hujapona unaweza kunitafuta nikupe Dawa ya kuweza kukutibu ukapona kwa haraka zaidi.
Ukiwa na Shida yoyote ile
Usipo pona kwa Dawa za Hospitali nitafute mimi nipate kukutibia upate kupona ukihitaji matibabu yangu.
TAZAMA HARMORAPA ALIVYO TIMUA MBIO BAADA YA KUIONA BASTOLA

from Blogger http://ift.tt/2nPdPVZ
via IFTTT


Unatatizo la Kuchelewa Kuamka..? Tumia Njia Hizi 10 Zitakazokusaidi Kuwahi Kuamka Kila Siku…!!!

1.Kuna chakula/tunda unalolipenda zaidi? Jiwekee zawadi, kwamba ukiamka asubuhi tu cha kwanza ni kula chakula hicho/ tunda/ chokleti nk. Hii itakufanya Utoke kitandani pale tu utakaposhtuka!
2.Iwekee Kipaumbele kazi unayopenda kufanya zaidi iwe ya kwanza kutendeka asubuhi. Utajkuta unatamani kuamka mapema zaidi kuwahi kazi hiyo na siku yako itaenda vizuri
3.Andaa mapema nguo ya kuvaa siku inayofuatia, ili kuwahi jumatatu, andaa nguo ya kuvaa jumapili usiku. Utafiti unaonyesha kuwa asilimia 40 (40%) ya watu huchelewa kutoka kitandani kwa kuwa walitumia muda mwingi kupanga watavaa nguo gani.
4. Anza kupunguza dakika 20 kila siku Taratibu; Kama ulikua unaamka saa mbili kamili, amka saa moja na dakika arobaini, baada ya siku mbili punguza tena dakika ishirini mpaka utakaporidhika
5. Jiwekee Lengo na uwaambie watu. Hii itakufanya ufanye kazi kwa bidii kwa kutaka kuwaonyesha watu kwamba umetimiza lengo lako na utajikuta unawahi kuamka asubuhi
6. Tengeneza “appointment” (Miadi) ya kuonana na mtu asubuhi, utajikuta unawahi kuamka kwa kuogopa kumuangusha mtu huyo.
7. Kama una mtu unaishi nae, tengeneza ratiba ya pamoja kama kufanya mazoezi, maombi, kusoma nk! Itakusaidia kukuongeza morali ya Kuwahi kuamka.
8 Weka saa ya kukuamsha (alarm clock) mbali na kitanda ikiwa na sauti kubwa, ni vizuri ukitumia wimbo uupendao.
9. Muombe mpenzi wako akuamshe kila asubuhi, au jenga tabia ya kumpigia mpenzi wako simu asubuhi
10.Ondoa vitu Vinavyokufanya uchelewe Kuamka mfano; pombe, kahawa na kuwahi kulala usiku.
TAZAMA HARMORAPA ALIVYO TIMUA MBIO BAADA YA KUIONA BASTOLA

from Blogger http://ift.tt/2n1tGwa
via IFTTT


Kategori

Kategori