Showing posts with label 2017 at 11:28AM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 11:28AM. Show all posts
AGIZO LA RAIS MAGUFULI LASAIDIA DAWA NA VIFAA TIBA KUPUNGUA BEI

AGIZO LA RAIS MAGUFULI LASAIDIA DAWA NA VIFAA TIBA KUPUNGUA BEI

WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema bei za dawa, vifaa tiba na Vitendanishi vya maabara zinazonunuliwa na kusambazwa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) zimepungua bei kwa asilimia 15 hadi 80 ukulinganisha na mwaka jana kutokana na hatua ya MSD kuanza utaratibu wa kununua moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji, kama alivyo agiza Rais Dk.John Magufuli.
Waziri huyo ameyasema hayo kwenye mkutano wake na waandishi wa habari, alioufanya ofisi za Makao Makuu ya Bohari ya Dawa MSD, Keko, Dar es Salaam leo huku akizielekeza Halmashauri, Hospitali na Vituo vya Afya kutumia bei elekezi ya dawa iliyotolewa ma Wizara ya Afya ambayo ipo kwenye kitabu ya orodha ya bei cha MSD.
MSD kwasasa inaagiza dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji wanchizipatazo 20 ambazonipamojana Kenya, Uganda, Afrika Kusini, India, Bangladesh, Pakistan, Jamuhuri ya Watu wa Korea, China, Ujerumani, Uingereza, Uswisi, Denmark, Ufaransa, Ubelgiji, Italia, Romania, Marekani, Cyprus, Falme za Kiarabu, na Tanzania.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Bwanakunu amesema tayari wametoa mikataba 73 kwa wazalishaji ambapo kati ya hiyo 46 ni ya wazalishaji wa dawa ambao wanatoka nchi za Uganda, Denmark, Ufaransa, Ujerumani, China, Afrika Kusini, Nchi za Falme za Kiarabu,Bangladesh, India, Kenya na Tanzania ambao wanazalishia aina 178 za dawa.
Baadhi ya dawa hizo ni pamoja na dawa ya chanjo ya homa ya ini (hepatitis B Vaccine ) awali ilikuwa ikiuzwa shilingi 22,000 sasa inauzwa shilingi 5,300, Dawa ya sindano ya Diclofenac kwa ajili ya maumivu (vichupa 10) awali ilikuwa ikiuzwa shilingi 2,000 sasa inauzwa shilingi 800 na Dawa ya kupambana na maambukizi ya bacteria (Amoxicillin/Clavulanic Acid Potassium 625mg) yenye Vidonge 15 awali iliuzwa shilingi 9,800 sasa inauzwa shilingi 4,000.
Kwa upande wa vifaa tiba amesema jumla ya wazalishaji 18 wamepata mikataba ambao wanatoka Uingereza, Ujerumani, India, Kenya na Tanzania, kwa ajili ya aina 195 za vifaa tiba.Aidha, kwa upande wa vitendanishi vya maabara, jumla ya wazalishaji 9 kutoka nchi za Uingereza, Ujerumani, Ubelgiji, Romania, China, India na Kenya wamepata mikataba kwa ajili ya aina 178 za vitendanishi vya maabara.
Kwa mujibu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Serikali ya awamu ya tano imeboresha kwa kiasi kikubwa hali ya upatikanaji wa dawa nchini ambapo bajeti ya dawa,vifaa tiba, vitendanishi vya maabara na chanjo kwa mwaka huu wa fedha 2017/2018 ni shilingi Bilioni 269 kutoka Bilioni 251 ya mwaka jana wa fedha 92016/2017).
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu akisisitiza jambo katika mkutano huo.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa taarifa ya kupungua kwa bei za dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kutokana na uamuzi wa serikali wa kununua moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu.
Viongozi wakiwa meza kuu kwenye mkutano huo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa MSD, Victoria Elangwa, Mkurugenzi Mkuu MSD, Laurian Bwanakunu, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, Kaimu Mfamasia Mkuu wa Serikali kutoka Wizara ya Afya, Siana Mapunjo na Mfamasia kutoka Wizara hiyo, Mercy Masuki.

from Blogger http://ift.tt/2uBvfpO
via IFTTT


PAUL Makonda Kikaangoni Sakata la Kudaiwa Ana Vyeti Feki..

PAUL Makonda Kikaangoni Sakata la Kudaiwa Ana Vyeti Feki..

Tume ya Maadili ya Utumishi wa Viongozi wa Umma yakubali mashtaka dhidi ya RC Makonda yaliyopelekwa na Meya wa Manispaa ya Ubungo.
Moja ya mashtaka yaliyowasilishwa ni tuhuma ya RC wa Dar, Kugushi vyeti vya kitaaluma kulikofanywa na RC makonda huku akijua fika kuwa vyeti anavyotumia vya taaluma si vyake wala si muhusika hivyo kujiita PAUL CHRISTIAN MAKONDA huku akijua fika kuwa yeye ni DAUDI ALBERT BASHITE, amekiuka sheria za nji nakutenda jinai.
Pili ni Kula kiapo cha utii na uaminifu mbele ya Mheshimiwa Rais kwa kutumia jina la kugushi.
Tatu ni kujipatia mali kama magari na vinginevyo kinyume na maadili ya viongozi wa umma, ambapo zawadi zote unazopokea unapaswa kutangaza hadharani, ikiwemo kupata mali hizo kwa wahusika ambao amekuwa akiwatangaza hadharani na kuwatuhumu kujihusisha na uuzaji wa madawa ya kulevya.
Nne ni kukiuka Misingi ya utawala bora haki za binadamu na utawala wa sheria kwa kutuhumu watu ovyo hadharani kuwa walijihusisha na biashara ya madawa ya kulevya kabla ya kukutwa na hatia na kisha wengine kuachiwa huru baada ya kubainika hawakutenda makosa hayo; kinyume kabisa na sheria ambapo mtu anatakiwa kutangazwa hadharani anapokutwa ametenda makosa.
Na tano ni uvamizi wa kituo cha kirusha matangazo ya redio na runinga cha Clouds media, ambapo akijua kuwa maadili ya viongozi wa umma, hayaruhusu kiongozi kushurutisha au kulazimisha jambo lolote kwakutumia madaraka yake kama kiongozi, ambapo mtuhumiwa alitenda kosa la kutaka kutumia nguvu kurusha kipindi.

from Blogger http://ift.tt/2oxJ47F
via IFTTT


Makonda โ€“ Sitishiki Ngโ€™ooโ€ฆ!!!

Makonda – Sitishiki Ng’oo…!!!

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ameadhimisha mwaka mmoja wa kuwa kwenye kiti hicho kwa kula chakula cha mchana na waathirika wa dawa za kulevya, huku akizungumzia mafanikio aliyopata katika uongozi wake.
Licha ya kueleza mafanikio aliyopata, hakugusia kuhusu tuhuma mbalimbali zilizoelekezwa kwake na watu mbalimbali, badala yake alisema hakuna wa kumtisha wala kumnyamazisha na kwamba sasa ndiyo amepata nguvu mpya baada ya kupata mashambulizi mbalimbali.
Pia mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Maofisa wa Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam, ulihudhuriwa na watu wachache wakiwamo waandishi kutoka vyombo vichache vya habari, tofauti na mikutano yake mingine ambayo alikuwa akialika vyombo vingi vya habari.
“Mwaka wangu wa pili katika uongozi ambao unaanza kesho (leo), speed (kasi) ya hali ya utumishi wangu itaongezeka mara mbili zaidi kwa sababu nimeshakomaa, lazima Dar es Salaam iwe kwenye mazingira salama.
“Eti mtu anataka nikae kimya wakati wananchi wangu wa Dar es Salaam wanateseka kwa matumizi ya dawa za kulevya… nauliza wewe ni nani uninyamazishe na umetoka wapi?” alihoji Makonda.
Alisema pamoja na changamoto nyingi anazopitia, hajawahi kutetereka wala kutingishwa na kwamba yuko tayari idadi ya wanaomchukia iongezeke kwa sababu hahitaji kupendwa.
“Sijawahi kutetereka wala sijawahi kutingishwa. Kazi hii nimepewa na Mungu, acha idadi ya wanaonichukia iongezeke kwa sababu sihitaji kupendwa, lakini niwe na uhakika na Mungu wangu.
“Mara nyingi ninapochapwa na mawimbi makali, mke wangu amekuwa akizama kwenye sala na kuniombea,” alisema.
Alisema anafanya kazi hiyo kwa upendo na kwamba hana kisasi na yeyote.
“Tunayafanya haya kwa upendo, hatuna kisasi na yeyote, ndiyo maana sisi tunafurahi, lakini upande wa pili wanapambana, kazi yetu ni kumulika watu,” alisema Makonda.
Aidha alisema wameamua kupigana vita ya dawa za kulevya hadharani kwa sababu hataki kupokea rushwa wala fedha haramu.
Makonda alisema kupitia fedha za dawa za kulevya, wengi wamejenga maghorofa na wamesababisha hata bei ya viwanja ipande, hivyo atahakikisha fedha hizo zinakauka ili kila mtu ale kwa jasho lake.
Alisema lengo lake ni kupambana kupigania ndoto za vijana na matumaini ya wazazi wao na haijalishi kama amechelewa, lakini hataacha.
Makonda alisema hababaishwi na watu wanaomchukia wakati akitekeleza majukumu aliyopewa na Rais Dk. John Magufuli kama Mkuu wa Mkoa.
Alisema wakiwaita wengine Kituo cha Polisi kwa vipimo, wamekuwa wakitumia dawa ya meno aina ya Colgate na chumvi, lakini sasa wamekuja na mbinu mpya ya vipimo.
“Wengine tukiwaita kwa ajili ya vipimo, kwa wale ambao wanapimwa kwa njia ya mdomo wanameza Colgate, wale wanaopimwa kwa njia ya mkojo wanaweka chumvi.
“Mnakumbuka wengine tulipowaita walikuwa wanachelewa kuja kumbe wanatumia vitu hivyo ili wasigundulike, sasa tuna mbinu mpya za kuwapima,” alisema Makonda.

from Blogger http://ift.tt/2ngqm4C
via IFTTT


Kategori

Kategori