Showing posts with label Habari ya Mbeya. Show all posts
Showing posts with label Habari ya Mbeya. Show all posts

MAKALA ATAKA SUALA LA UGONJWA WA KIPINDUPINDU LIWE HISTORIA MKOANI MBEYA


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya mstaafu Abasi Kandoro (kulia) akimkabidhi rasmi ofisi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala katika hafla fupi iliyofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Machi 17 mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala akizungumza na watumishi  waliohudhuria hafla ya makabidhiano ya ofisi na Mkuu wa Mkoa mstaafu Abaas Kandoro Machi 17 mwaka huu .

MBWA 70 WAPIGWA RISASI MBARALI


ZAIDI YA Mbwa na paka 70 wameuwawa katika mamlaka ya mji mdogo wa Rujewa wilayani Mbarali mkoani Mbeya ikiwa ni jitihada za kupambana na kichaa cha Mbwa kwa wakazi wa halmashauri hiyo.

Mbwa hao na paka wameuwawa wakati kukiendelea na kutolewa kwa elimu kwa wakazi wa mji huo na kuhakikisha kuwa wananchi wanawachanja mbwa pamoja na paka wao ili kuto leta magonjwa ya kichaa cha mbwa kwa wakazi.

Akisoma taarifa ya utekelezaji wa kamati ya Ujenzi na uchumi kwenye baraza la mamlaka ya mji mdogo wa Rujewa Daniel Myuki alisema kuwa jumla ya mbwa 70 na paka mmoja ameuwawa kwa kupigwa risasi na mlenga shabaha wa mamlaka hiyo kwa kushirikiana na wataalamu wa idara ya kilimo, na afya.

Myuki alisema kuwa zeozi hilo liliendeshwa kwa siku mbili ndani ya mitaa ya Ibara Rujewa, Isisi, Uhamira, Ihanga, Igomelo, na Lugelele, ndani ya mamlaka hiyo huku waklio kuwa wakilengwa ni mbwa na paka wa mitaani na huku wananchi endelea kupatiwa elimu juu ya kuwachanja mbuwa wao.

Alisema kuwa licha ya kutoaelimu pia amewataka wananchi kuhakikisha kuwa watatii amri ya kufungulia mbwa nap aka wao majira ya saa 4:00 usiku na kuwafungia majira ya saa 12:00 asubuhi.

Hata hivyo alisema kuwa wananchi wanatakiwa kuhakikisha kuwa mbwa na paka wao wanawafungi katika mabanda ama kuwafunga kwa minyororo ili wasizagae mitaani.
 
“Wananchi tunaendelea kuwapa elimu juu ya kuwafuga vizuri mbwa na paka wao na kuwafundisha jinsi ya kuwarisha na madhara ya kuto wapa chanjo mara kwa mara,” alisema Myuki.

Hata hivyo baadhi ya wajumbe walitaka kujua udadi ya mbwa nap aka katika mji huo wa ili kufanya tathimini ya mbwa nap aka wangapi watakuwa wametibiwa na wangapi wabebaki kitu kilicho kuwa ni kigumu kwa kamadi hiyo huku ikisema kuwa mbwa nap aka wanaongezeka kila kikicha hivyo haiwezekani kupatikana idadi yake kamili.

MBEYA KILA JUMAMOSI SIKU YA USAFI NI KUTOKANA NA AGIZO LA RAIS DR. MAGUFULI


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa maagizo ya Rais.


Afisa maendeleo ya jamii Mkoa wa Mbeya, Stellah Kategile akisoma taarifa ya utekelezaji wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani kwa Mkoa wa Mbeya
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akimkabidhi boksi la dawa kwa ajili ya watu wanaoishi na maambukizi ya VVU Mganga mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dk. Seif Mhina kwa ajili ya kuzisambaza kwa watumiaji.


Baadhi ya madawa na vifaa mbali mbali vilivyonunuliwa kutokana na gharama za maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani zilizokuwa zifanyike kimkoa Wilaya ya Mbarali zikiwa kuokolewa

Waandishi wa habari wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya


KATIKA kutekeleza agizo la Rais kuhusu maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani na Uhuru wa Tanzania Bara, Mkoa wa Mbeya umetenga siku ya kila jumamosi kuwa siku ya usafi endelevu na kununuamadawa  ya magonjwa nyemelezi.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika ofisini kwake, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro alisema katika maadhimisho yaliyofanyika Disemba mosi mwaka huu kuna shughuli nyingi zimeshafanyika ikiwa ni pamoja na ununzi wa madawa, utoaji wa elimu na shughuli za kijamii.

Kandoro alisema jumla ya madawa yenye thamani ya shilingi Milion 3,550,000 yamenunuliwa na kukabidhiwa kwa Mganga mkuu wa Mkoa ambaye atasambaza katika Zahanati, Vituo vya Afya na Mahospitali yanayotoa huduma.

Alisema maandalizi ya maadhimisho hayo ambayo yalikuwa yafanyike Wilayani Mbarali kimkoa yalianza Novemba 13 mwaka huu kabla ya maagizo ya Rais kutolewa ambapo wadau zaidi ya 50 walijitokeza na kuchangia fedha pamoja na vifaa mbali mbali vyenye thamani ya shilingi Milioni 32.

Alisema vifaa vilivyotolewa kuwa ni pamoja na Mipira, sare za mpira, mafuta ya gari, vipeperushi,Kondomu, vikombe, kofia, T shirt, Ndoo na Kanga ambavyo vyote watapewa walingwa ambao ni Watu wanaoishi na Maambukizi ya Virusi vya ukimwi.

Alisema shughuli zilizofanyika ni pamoja na kuendesha midahalo ya wazi katika jamii kuhusu kujikinga na maambukizi mapya ya Ukimwi katika Kata za Igulusi, Chimala, Mapogoro,Rujewa na Ubaruku katika Wilaya ya Mbarali.

Aliongeza kuwa shughuli zingine ni pamoja na kuendesha mashindano mbali mbali ya mpira wa miguu, kutoa mafunzo kwa waelimisha rika, Semina, Ushauri nasaha na upimaji pamoja na kutembelea klabu za watoto wanaoishi na VVU.

Kuhusu maadhimisho ya sherehe ya miaka 54 ya Tanzania Bara Kandoro alisema Mkoa wa Mbeya umeanza kutekeleza agizo la Rais la kuitumia siku hiyo kufanya usafi ambapo katika kikao cha viongozi wa Wilaya zote walikubaliana kuanza utekelezaji Disema 2 mwaka huu kwa kila Halmashauri kutenga siku ya kufanya usafi.

Alisema mbali na kuanza tarehe mbili pia waliazimia kutenga siku ya Jumamosi ya kila wiki kuwa ni siku ya usafi ili kujenga tabia ya wananchi kuuchukia uchafu na kupenda usafi ili zoezi hilo kuwa endelevu.

Alisema siku ya kilele ya Disemba 9 kila mwananchi kuanzia ngazi ya Kaya hadi Halmashauri bila kujali nafasi aliyonayo anapaswa kujitokeza kufanya usafi katika maeneo yanayowazunguka kwa kuhakikisha mifereji na mitaro inazibuliwa.

Alisema kuna changamoto ya vifaa vya kuzibulia mifereji pamoja na usombaji wa taka ambapo ameziagiza Halmashauri zote kuhakikisha wanapata vifaa hivyo ikiwa ni kwa kukodi ama kuazima ili mradi zoezi lifanyika kwa kiwango kizuri.

PROF. MJEAMA 'WAHITIMU BIASHARA WASIKATE TAMBAA'

PROFESA EMMANUEL MJEMA AWAFUNDA WAHITIMU WA CBE KAMPASI YA MBEYA.


Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara(CBE) Profesa Emmanuel Mjema,akizungumza na Wahitimu wa mafunzo ya ujasiliamali alipokuwa mgeni wakati wa kufunga semina ya Ujasiliamali kwa Wahitimu wa CBE Kampasi ya Mbeya


Mwenyekiti wa Umoja wa Wahitimu waliosoma CBE Kanda ya Nyanda za juu kusini (ALUMNI) Boyd Mwakyusa, akitoa neno la utangulizi katika hafla ya kufunga mafunzo ya ujasiliamali kwa wahitimu wa CBE Kampasiya Mbeya

Katibu wa Alumni, Graciano Kunzugala, akiwashukuru washiriki wa Mafunzo ya Ujasiliamali waliyoyapata wahitimu wa Chuo cha CBE Kampasi ya Mbeya

Profesa Mjema akiwa meza kuu pamoja na viongozi wengine wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya ujasiliamali kwa wahitimu wa CBE Kampasi ya Mbeya.

Baadhi ya washiriki wa semina ya ujasiliamali wakisubiri kutunukiwa vyeti vya ushiriki wa mafunzo waliyopata

Mkurugenzi wa CBE Kampasi ya Mbeya, Dionise Lwanga akimwelekeza jambo Mwenyekiti na Katibu wa ALUMNI Kanda ya Mbeya

Profesa Mjema akimtunuku Cheti cha ushiriki wa mafunzo ya ujasiliamali mmoja wa Wahitimu wa Chuo cha CBE Kampasi ya Mbeya.

Mhitimu wa CBE akipongezwa na Mkurugenzi wa Kampasi ya Dodoma

Mkurugenzi wa Kampasi ya Mbeya, Dionise Lwanga akimpongeza mmoja wa wahitimu wa CBE Mbeya baada ya kutunukiwa cheti cha ushiriki wa mafunzo ya ujasiliamali

Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi na baadhi ya Watumishi wa CBE baada ya kufungwa kwa mafunzo ya ujasiliamali

Baadhi ya Washiriki wa mafunzo ya ujasiliamali wakionesha vyeti vyao katika picha ya pamoja na viongozi wa CBE na waandaaji wa mafunzo


MKUU wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Profesa Emmanuel Mjema,ametoa wito kwa wahitimu wa vyuo kutokata tama katika utafutaji wa maisha.

Profesa Mjema ametoa wito huo alipokuwa akifunga mafunzo ya siku mbili ya Ujasiliamali kwa Wahitimu wa CBE Kampasi ya Mbeya yaliyomalizika katika ukumbi wa Hoteli ya Livingstone.

Profesa Mjema ambaye pia aliwatunuku vyeti vya kuhudhuria mafunzo hayo wahitimu alisema katika utafutaji wanapaswa kuwa na uvumilivu hivyo hawatakiwi kukata tama mapema.

Aidha aliwataka wahitimu hao kuitumia kwa vitendo elimu ya ujasiliamali walioipata kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo katika jamii.

Mkuu huyo wa Chuo pia aliwapongeza waandaaji wa mafunzo hayo ambao ni umoja wa wahitimu waliosoma zamani CBE(ALUMNI) kanda ya Nyanda za juu kusini.

Alisema kitendo walichokifanya ni uzalendo wa kukipenda Chuo kwa kurudisha fadhila ambayo wameitoa kwa wahitimu.

Alisema jukumu la wahitimu ni kukishauri Chuo juu ya mabadiliko mbali mbali na kukijulisha juu ya mambo yanayokuwa yakiendelea nje ya Chuo.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Mwenyekiti wa ALUMNI Kanda ya Nyanda za juu kusini, Boyd Mwakyusa alisema mafunzo hayo yamehudhuriwa na washiriki 88.

Alisema lengo la mafunzo ni kuwafanya wahitimu kutohangaika pindi wanaporudi uraiani badala yake wajue fursa za kuzitumia ikiwa ni pamoja na kujishughulisha na ujasiliamali.

by Mbeya Yetu Blog

SUGU 'MADIWANI FANYENI KAZI KWA KASI YA MAGUFULI'

Sugu Akiteta Jambo
Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu amewataka madiwani wa jimbo hilo waliochaguliwa kwa tiketi ya Chadema kuhakikisha wanafanya kazi kubwa kushindana na kazi ya rais John Magufuli.

Sugu alitoa kauli hiyo hivi karibuni katika kikao cha kumchagua diwani atakayewania nafasi ya Umeya kwa tiketi ya chama hicho.

Aliwataka madiwani hao kuchapa kazi na kuwafanya wananchi kujivunia kasi ya maendeleo inayoletwa na Mbunge na Meya wa jiji hilo ili wasitamani jimbo hilo lingeongozwa na wapinzani wao wa CCM.

“Hata CCM wenyewe wamebadilika, Magufuli anakwenda jalamba. Hakutakuwa na vitu kama ambavyo mnaviwaza, tunaenda kufanya kazi za wananchi ili wananchi wasitamani kwamba afadhali na hapa pangekuwa CCM. Waseme hata kama Magufuli anaenda spidi na sisi Mbeya yetu Meya na Mbunge wanakwenda spidi.”

JIJI LA MBEYA HATARI KUKUMBWA NA UGONJWA WA KIPINDUPINDU


 
Wafanyabiashara ndogo ndogo katika eneo la Makunguru jijini Mbeya wakiendelea na shughuli zao kama kawaida.

Na Mwandishi wetu,Mbeya
 
Halmashauri ya jiji la Mbeya limewataka wafanyabiashara ndogondogo hususani wa chakula  kujijengea tabia ya kuchoma taka nyakati za jioni mara wamalizapo kuuza biashara zao na si kusubili gari ya taka kuja kuzoa.
 
Aidha imewataka  wakazi hao kuondokana na fikra duni  ya kuamini kuwa kazi ya uzoaji wa taka na kusafisha mazingira ni ya halmashauri ya Jiji na sio mali ya mtu
 
Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji la Mbeya, Dkt. Samweli Lazaro, amesema, wananchi wanatakiwa kujenga tabia ya usafi na sio kusubili kupigizana kelele na serikali kwa kuwahimiza kufanya usafi kwani adui mkubwa wa afya ni uchafu hivyo kila mmoja anapaswa kuwa mlinzi wa mwezake katika kutunza mazingira.
 
Hali hiyo imesababisha kuwepo kwa malimbikizo mengi ya taka  kwenye sehemu zisizorasmi  ndani ya JIji la Mbeya na kupelekea jiji hilo kuwa chafu hususani katika maeneo ya  sokoni.
 
Amesema, hivi sasa halmashauri ilianzisha mpango wa uzoaji wa taka barabarani ambapo mpango huo umeonekana  kupokelewa na wananchi kwa asilimia 100 changamoto inakuja kwa upande wa halmashauri kuonekana kuzidiwa kutokana na ukosefu wa vitendea kazi.
 
“Halmashauri ilianzisha zoezi la kupitia taka zinazozalishwa na wananchi ambazo huziweka barabarani na magari yanapitia lakini mapango huu umeonekana kuzaa matunda kwa jamii kuupokea lakini tatizo ni uhaba wa vitendea kazi,”alisema.
 
Alisema, ili zoezi hilo lifanikiwe halmashauri inahitaji zaidi ya gari saba za ubebaji taka na kontena 80 lakini mpaka sasa magari yaliyopo ni manne na kontena 30 .
 
Hata hivyo kutokana na changamoto hiyo, Lazaro anawasihi wananchi kujenga tabia ya kuweka mazingira safi hasa kipindi hiki cha mvua kwani ndipo magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu yanapoibuka na kusababisha vifo vya watu.
 

 
JAMIIMOJABLOG MBEYA

UNICEF YAKABIDHI MAGARI KUMI YA KUBEBEA WAGONJWA MBEYA

Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Unicef Dkt Jama Gulaid akitoa hotuba katika sherehe ya makabidhiano ya magari ya kubebea  wagonjwa Mkoa wa Mbeya15 Octobar  2015

Mratibu wa Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto Ndugu Prisca Butuyuyu akitoa taarifa ya huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto katika Mkoa wa Mbeya kwenye hafla fupi ya makabidhiano ya magari ya kubebea wagonjwa 15 Octobar 2015.

Mwakilishi UNICEF Dkt Jama Gulaid kulia akimkabidhi Kaimu katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Ndugu Kastro Msigala taarifa muhimu za magari hayo yenye thamani ya shilingi mil 700 .

Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Mbeya pamoja na wageni waalikwa wakishiriki kikamilifu tukio la makabidhiano ya magari ya wagonjwa  Mkoa wa Mbeya 15 Octobar 2015 kutoka kwa shirika la kimataifa la UNICEF.

Timu ya Uendeshaji wa huduma za za Afya Mkoa wa Mbeya

Kastro Msigala Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo za makabidhiano ya magari kumi ya kubebea wagonjwa ambayo yametolewa na shirika la kimataifa la UNICEF Octobar 15 mwaka huu.

Kaimu Katibu tawala Mkoa wa Mbeya Kastro Msigala akikata utepe kuashiria kupokea rasmi msaada wa magari hayo kutoka kwa shirika la kimataifa la UNICEF msaada ambao umegharimu kiasi cha shilingi Mil 700.


Meza kuu katika  picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa wa Mbeya na wawakilishi wa Shirika la UNICEF.

Meza kuu katika picha ya pamoja na waganga wakuu wa Halmashauri za Mkoa wa mbeya .

Meza Kuu katika picha ya Pamoja na timu ya Uendeshaji wa Huduma za Afya Mkoa wa Mbeya .

Meza kuu katika picha ya pamoja na wafanyakazi shirika la UNICEF.


 
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa  linalo shughulikia watoto Duniani (UNICEF) limekabidhi msaada wa magari kumi  ya Kubebea wagonjwa yenye tahamni ya shilingi mil 700.7  kwa serikali ya Mkoa wa Mbeya .

Aidha shirika hilo lina mpango wa kuboresha vituo 184 vya kutolea huduma za afya katika mkoa huo wa mbeya ambavyo ni vituo afya na hospital 30 pamoja na zahanati 154  sanjali na kuvipatia vifaa muhimu vya kutolea mafunzo kwa watumishi wake.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Octobar 15 mwaka huu  Mwakilishi wa shirika la  UNICEF   nchini Tanzania Dkt Jama Gulaid  amesema shirika hilo limetenga kiasi cha shilingi bilioni 2 kwa ajili ya mradi huo.

Amesema mchango wa UNICEF katika sekta afya na lishe hapa mkoani mbeya imepanua wigo kutoka halmashauri mbili za mkoa huo hadi kufikia halmashauri zote katika kipindi cha miaka miwili .

Aidha Dtk, Jama amesema katika kukabiliana na magonjwa na vifo vya watoto na wanawake wajawazito ,UNICEF imechangia vifaa tiba muhimu ikiwa ni pamoja vile vya uchunguzi wa ujauzito ,upasuaji  sanjali na vifaa kuwasaidia watoto wachanga kupumua mara wanapo zaliwa na vifaa vingine vya utoaji wa huduma katika idara ya uangalizi maalumu  ICU.

Aidha  amewataka viongozi hao wa mkoa wa Mbeya kuhakikisha wanaweka juhudi kubwa zaidi katika kupunguza vifo vya akina mama na watoto wachanga kwa kuhakikisha kwamaba kina mama wajawazito wote wanapata huduma za afya bure kwa wakati.

Awali akisoma  taarifa ya huduma za afya ya uzazi na mtoto katika mkoa mbeya mratibu wa huduma za afya ya uzazi na mtoto Ndugu Prisca Butuyuyu amesema toka shirika hilo la UNICEF  lianze kufanya mwaka 2012 huduma za afya zimeimalika kwa kiasi kikubwa hususani kwa kuweza kuzuia vifo vya uzazi na vya watoto wachanga.

Amesema kwa ujumla hali ya vifo hususani vilivyokuwa  vinatokea katika vituo vya huduma vimepungua kutoka 140  kwa mwaka 2012 na kufikia vifo 94 kwa kwa mwaka 2014 pamoja na kupunguza vifo vya watoto wachanga kutoka 602 kwa mwaka 2012 hadi kufikia 568  mwaka 2014 ambapo punguzo hilo ni sawa na asilimia 33.9 na 5.7 kwa watoto wachanga.

Akipokea msaada huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Kaimu katibu Tawala Ndugu Kastro Msigala amelishukuru shirika hilo kwa msaada wa magari hayo sanjali na kutoa wito kwa viongozi  wa halmashauri ambao ni wakurugenzi na waganga wakuu kuhakikisha wanayatunza magari hayo ili yaweze kutoa huduma stahiki kwa wananchi.

Msaada huo wa magari imegawanywa katika halmashauri zote mkoa huo wa mbeya ambazo ni Ileje,Mbozi,Mbeya vijijini,Rungwe,Busokelo,Mbarali pamoja na Kyela na Momba .
Mwisho
(Imeandaliwa na Jamiimojablog Kanda ya Nyanda za juu kusini Mbeya  0759406070 )

Kategori

Kategori