Showing posts with label 2017 at 03:24PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 03:24PM. Show all posts
ZIARA YA KIKAZI YA RAIS MAGUFULI YAKAMILIKA NDANI YA SIKU 7 KATIKA MIKOA MINNE

ZIARA YA KIKAZI YA RAIS MAGUFULI YAKAMILIKA NDANI YA SIKU 7 KATIKA MIKOA MINNE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 25 Julai, 2017 amekamilisha ziara yake ya kikazi ya siku 7 katika Mikoa ya Kagera, Kigoma, Tabora na Singida kwa kufungua barabara ya Itigi – Manyoni Mkoani Singida.
Barabara hiyo inayounganisha Mikoa ya Singida, Tabora na Kigoma ina urefu wa kilometa 89.3 na imejengwa gharama ya Shilingi Bilioni 114.692, fedha ambazo zimetolewa na Serikali ya Tanzania.
Akizungumza na wananchi wa Itigi katika sherehe za ufunguzi wa barabara hiyo Mhe. Rais Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli, amesema Watanzania wana kila sababu ya kutembea kifua mbele kwa kuwa barabara hiyo pamoja na nyingine saba alizozifungua katika ziara hii zenye urefu wa jumla ya kilometa 707 zimejengwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 806, fedha zote zikiwa zimetolewa na Serikali ya Tanzania.
Mhe. Rais Magufuli amebainisha kuwa miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara imetekelezwa na inaendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini na kwamba Serikali imeamua kuanzisha Wakala wa Barabara Vijijini kwa lengo la kuhakikisha barabara za vijijini zinajengwa kwa kiwango cha lami.
Kwa barabara ya Mkiwa – Itigi yenye urefu wa kilometa 57 na ambayo tayari zabuni ya ujenzi ilishatolewa kwa mkandarasi ili aijenge kwa kiwango cha lami kwa gharama ya Shilingi Bilioni 104, Mhe. Rais Magufuli ameiagiza Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuupitia upya mkataba wa ujenzi wa barabara hiyo kwa kuwa kiwango cha fedha kilichopangwa ni kikubwa ikilinganishwa na gharama halisi.
Pia amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa Mnyaa kujadiliana na Mkandarasi anayejenga barabara hiyo ili aweze kuendelea kujenga barabara kutoka Itigi kuelekea Chunya hadi Makongorosi Mkoani Mbeya.
Pamoja na wananchi wa Itigi Mkoani Singida, Mhe. Dkt. Magufuli aliyetokea Tabora amezungumza na wananchi waliosimamisha msafara wake katika vijiji vya Kigwa, Kizengi na Tura Wilayani Uyui na amewataka kuendelea kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa pamoja na kuzingatia uzalishaji mazao yanayostahimili ukame kama vile uwele, mtama, viazi na muhogo ili kuepuka tatizo la upungufu wa chakula.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewataka viongozi wote nchini kuhamasisha wananchi kufanya kazi hususani shughuli za kilimo ambacho ni uti wa mgongo wa Taifa, na ameonya kuwa kiongozi ambaye hatatekelezi agizo hilo atakuwa hafai na ataondolewa.
“Nawaagiza Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya hamasisheni watu kufanya kazi na kama kuna viongozi na watendaji wasiotekeleza wajibu huo katika maeneo yenu waondoeni mara moja” ameagiza Mhe. Rais Magufuli.
Viongozi wengine waliongozana na Mhe. Rais Magufuli katika ziara ya leo ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Prof. Norman Sigalla King na Wabunge wa Mkoa wa Singida.
Mhe. Rais Magufuli amewasili katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia Wananchi Kijiji Cha Tula Uyui Mkoani Tabora waliojitokeza Barabarani Kumsalimia akiwa njiani kuelekea Mkoani Dodoma akitokea kwenye Ziara ya siku tatu Mkoni Tabora Julai 25,2017Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo akiawa njiani katika moja ya mikutano ya barabarani kwa waliojitokeza Kumsalimia akiwa njiani kuelekea Mkoani Dodoma akitokea kwenye Ziara ya siku tatu Mkoni Tabora Julai 25,2017.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikaribishwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi wakati Rais alipowasili Mkoani Singida eneo la Itigi ili kufungua Barabara ya Itigi -Manyoni -Chaya yenye urefu wa kilometa 89.5 iliyojengwa na Serikali kwa asilimia mia moja,Mheshimiwa Rais alikuwa akitokea kwenye Ziara ya siku tatu Mkoni Tabora Julai 25,2017.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Itigi na Manyoni wakati wa Ufunguzi wa Barabara ya Itigi -Manyoni -Chaya yenye urefu wa kilometa 89.5 iliyojengwa kwa fedha za Serikali kwa asilimia mia moja,Mheshimiwa Rais alikuwa akitokea kwenye Ziara ya siku tatu Mkoni Tabora kwa Kupitia Singida hadi Makao Makuu ya Nchi Mkoani Dodoma Julai 25,2017.Wananchi wa Itigi na Manyoni wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwatubia kwenye Ufunguzi wa Barabara ya Itigi -Manyoni -Chaya yenye urefu wa kilometa 89.5 iliyojengwa kwa fedha za Serikali kwa asilimia mia moja,Mheshimiwa Rais alikuwa akitokea kwenye Ziara ya siku tatu Mkoni Tabora kwa Kupitia Singida hadi Makao Makuu ya Nchi Mkoani Dodoma Julai 25,2017Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wapili kushoto na Viongozi wengine wa Mkoa wa Singida,wakiondoa kitambaa kuashiria Kufunguliwa Rasmi kwa Barabara ya Itigi -Manyoni -Chaya yenye urefu wa kilometa 89.5 iliyojengwa kwa fedha za Serikali kwa asilimia mia moja,Mheshimiwa Rais alikuwa akitokea kwenye Ziara ya siku tatu Mkoni Tabora kwa Kupitia Singida hadi Makao Makuu ya Nchi Mkoani Dodoma Julai 25,2017.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Viongozi wengine wa Mkoa wa Singida na Tabora Wakikata Utepe kama ishara ya kufunguliwa Rasmi kwa Barabara ya Itigi -Manyoni -Chaya yenye urefu wa kilometa 89.5 iliyojengwa kwa fedha za Serikali kwa asilimia mia moja,Mheshimiwa Rais alikuwa akitokea kwenye Ziara ya siku tatu Mkoni Tabora kwa Kupitia Singida hadi Makao Makuu ya Nchi Mkoani Dodoma Julai 25,2017Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kulia akiteta jambo na Wang Chao mwakilishi wa Pawer China Internatinal Group Limited wakati wa Ufunguzi wa Barabara ya Itigi -Manyoni -Chaya yenye urefu wa kilometa 89.5 iliyojengwa kwa fedha za Serikali kwa asilimia mia moja,Mheshimiwa Rais alikuwa akitokea kwenye Ziara ya siku tatu Mkoni Tabora kwa Kupitia Singida hadi Makao Makuu ya Nchi Mkoani Dodoma Julai 25,2017Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwashukuru na kuwasalimia kwa kupunga mikono kwa wananchi wa Itigi na Manyoni walioshiriki na Kushuhudia Ufunguzi wa Barabara ya Itigi -Manyoni -Chaya yenye urefu wa kilometa 89.5 iliyojengwa kwa fedha za Serikali kwa asilimia mia moja,Mheshimiwa Rais alikuwa akitokea kwenye Ziara ya siku tatu Mkoni Tabora kwa Kupitia Singida hadi Makao Makuu ya Nchi Mkoani Dodoma Julai 25,2017

from Blogger http://ift.tt/2v7gUF7
via IFTTT


Wema Sepetu Amzimikia Rayvanny Amtabiria Makubwa Tuzo za BET

Wema Sepetu Amzimikia Rayvanny Amtabiria Makubwa Tuzo za BET

RayVanny ni msanii pekee kutoka Tanzania na Afrika Mashariki ambaye anatuwakilisha kwenye tuzo za BET zitakazofanyika Marekani baadaye mwezi huu akiwania Viewers Choice Awards ama (Pendekezo la Mashabiki ama watazamaji) huku BET wakitangaza namna ya kuwapigia kura wasanii ili washinde tuzo hizo.
Pamoja na baadhi ya mastaa kama Elizabeth Michael kumpigia na kumuombea kura RayVanny kwenye kurasa zao za Social media, Wema Sepetu naye ametumia ukurasa wake wa Instagram kumpigia kura RayVanny akiandika:

Umechaguliwa tu kuwania lakini kwangu wewe ni mshindi tayari …Unastahili kabisa! V-Vanny Boy. Na haiishii hapa Tuendelee kupiga kura.

 Wasanii wanaowania tuzo ya Viewers Choice Awards pamoja na RayVnanny ni pamoja na Dave (UK ) Jorja Smith (UK) Amanda Black (South Africa) Changmo (South Korea) Daniel Caesar (Canada) Remi (Australia) Skip Marley (Jamaica).
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2t1Uobm
via IFTTT


Nape Nnauye: Kitendo Kilichofanywa na Mkuu wa Mkoa kimenajisi Tasnia ya Habari

Waziri Nape: Kabla ya kuchukua hatua zozote, sisi kama Serikali tunataka kusikia kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda
Waziri Nape: Tumeunda timu ya watu 5 kufanya kazi katika saa 24 ili wapate maelezo ya RC Makonda na ripoti hiyo itasomwa wazi
Waziri Nape: Kitendo kilichofanywa na RC Makonda kinanajisi Uhuru wa Vyombo vya Habari katika Nchi Huru. Mamlaka zitajua cha kufanya
Kusaga: Kama RC Makonda ataomba radhi hatuna shida naye, ataendelea kuwa rafiki!
Reginald Mengi: Tuna Rais anayependa Vyombo vya Habari, lakini mapenzi haya ayaonyeshe kwa Vitendo!
Nape Nnauye(Waziri wa Habari): Wanahabari tutulie na tusubiri kusikia kutoka pande zote mbili kabla ya kuchukua uamuzi
Nape: Natoa pole kwa Clouds Media na kwakuwa tumejiridhisha kuwa jambo hili limetokea basi tutalishughulikia
Nape Nnauye: Ripoti itakayoletwa na Kamati ya Uchunguzi pamoja na hatua zitakazochukuliwa vitatangazwa hadharani baada ya saa 24\
Habari zaidi….
Waziri Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye amesema kuwa Tukio la Uvamizi wa Kituo cha Habari cha Clouds unaodaiwa kufanywa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paul makonda akiwa na askari kadhaa ni tukio la kupingwa huku akidai kuwa matukio kama hayo hutokea pindi nchi inapotaka kupinduliwa lakini kama Rais yupo, nchi haijapinduliwa.
Aidha amesema kuwa Vitendo hivyo ni kunajisi uhuru wa habari na kama akishindwa kusimamia hilo na yeye hafai kuwa katika nafasi aliyopo.
Chanzo : Mwananchi

from Blogger http://ift.tt/2nrK1hU
via IFTTT


Nisha: Sitamtambulisha mpenzi wangu tena

Msanii machachari wa bongo movie Nisha Bebe amesema hatorudia kosa la kumtambulisha mpenzi wake kwa sasa bali atamtambulisha mume wake akiwa tayari.
Akiongea kupitia eNewz ya EATV, Nisha amesema “Sirudii makosa kwa sasa hivi wasitarajie kumsikia mpenzi wangu wala kumtambulisha kwa jamii mtu nitakaye kuja kumtambulisha ni mume wangu ambaye tayari nishampata ila tunachunguzana tabia kwanza kwa sasa” aliongea Nisha
Hata hivyo Nisha aliendelea kusema kwamba hata kama itamchukua muda mrefu kujuana tabia na mume wake mtarajiwa haijalishi ili mradi waweze kujuana vizuri na
“Watu wasitarajie kuona dalili yeyote ya kumtambulisha mpenzi wangu kabla hatujaoana” Alimalizia Nisha.

from Blogger http://ift.tt/2mITz4x
via IFTTT


Kategori

Kategori