Showing posts with label 2017 at 11:07AM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 11:07AM. Show all posts
Klabu ya zamani ya Haruna Moshi yamtimua Mghana kwa kesi ya kubaka

Klabu ya zamani ya Haruna Moshi yamtimua Mghana kwa kesi ya kubaka

Mahakama moja nchini Sweden imemhukumu mwanasoka wa ligi daraja la pili kwenda jela miaka 2 kwa kosa la kumbaka na kumpiga mkewe. 
Baada ya kumaliza adhabu yake, Kwame Bonsu mwenye umri wa miaka 22, ambaye kabla ya kesi alikuwa akiitumikia klabu ya zamani ya mchezaji wa soka wa Tanzania Haruna Moshi Boban – Gefle IF Club, atafukuzwa katika nchi hiyo ya Scandanavia, ambapo amekuwa akiishi tangu miaka 4 iliyopita, mahakama ya Gavle District imeamua.
Klabu ya Gefle imesema Bonsu amefukuzwa kwenye klabu hiyo mara moja baada ya kupatikana na hatia ya mashtaka yake. 
Mchezaji huyo pia ametakiwa kulipwa kiasi cha 245,000 kronor zaidi ya million 50 za kitanzania – ikiwa ni fidia kwa mkewe, ambaye ni raia wa Sweden. 
Bonsu alikutana na mkewe mnamo mwaka 2014 wakati akiitumikia klabu ya Mjolby na wakaoana mwaka uliofuatia. Miezi kadhaa baada ya ndoa alisaini kwenda klabu ya Gafle – kilomita zaidi ya 300 kutoka Mjolby.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2s7oFIR
via IFTTT


Diamond Platnumz – Ili Uwe na Sifa ya Kujiunga na WCB Lazima Uwe na Uwezo wa Jambo Hili

Diamond Platnumz – Ili Uwe na Sifa ya Kujiunga na WCB Lazima Uwe na Uwezo wa Jambo Hili

Rais wa lebo ya WCB Diamond Platnumz amefunguka na kusema ni vigumu kwa msanii kujiunga na lebo yake hiyo kama hajui kuandika nyimbo.
Diamond amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds Fm kuwa wimbo unapoandikwa ndani ya lebo hiyo mara zote unakaguliwa na watu wote ili kubaini kama kuna makosa na kuelekezana.
“Kwanza Rich Mavoko ndiye mgumu kwenye kupitisha nyimbo, ikitoka hapo Ravvanny aipitishe, Queen Darleen aipitishe, ikitoka hapo niipitishe mimi, iende kwa Mkubwa Fella na Babu Tale waipitishe na Sallam aipitishe, ukitoka hapo wewe ni mwanaume haswa,” amesema Rich Mavoko na kuongeza.
“Kwa hiyo wengi wanakuwa na uwezo mkubwa. Labda unaweza ukaja ukasikia kitu kidogo, ukasema ukiweka hapa kitu flani itakuwa poa zaidi, yaani ukiandika unaandika haswa,” ameeleza Diamond.

from Blogger http://ift.tt/2qUSObq
via IFTTT


Matajiri Wajenga Mahandaki Kujiandaa na Mwisho wa Dunia..!!!

UKITAMKA “handaki la kujificha kwa ajili ya mwisho wa dunia” watu wengi watadhani kuwa ni chumba kilichojengwa kwa uimara wa hali ya juu kikiwa kimesheheni vyakula vilivyosindikwa na vitu vingine ili kuwezesha watu kuishi kwa muda mrefu.
Tishio la kuangamia kwa dunia kwa sasa ni kubwa kama ilivyokuwa wakati wa Vita Baridi, lakini mahandaki haya ya leo ni tofauti kabisa na zile za karne ya 20.
Kampuni nyingi duniani kote zimekuwa zikishughulikia kuongezeka kwa mahitaji ya majengo yenye uwezo wa kuwalinda watu dhidi ya hatari ya aina yoyote, iwe ni magonjwa hatari ya kuambukiza, dunia kugongana na sayari au kitu chochote kutoka anga za juu, Vita ya Tatu ya Dunia – lakini wakati huo huo jengo hilo liwe ni sehemu yenye starehe.
“Mahandaki wakati wa baba au babu yako hayakuwa yanakalika,” anasema Robert Vicino, mfanyabiashara wa majengo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Vivos, kampuni ambayo hujenga na kusimamia majumba ya kifahari duniani kote.
“Hayakuwa yanavutia. Yalikuwa yanajengwa kwa chuma, kama ilivyo meli au kifaa cha kijeshi. Na ukweli ni kwamba, binadamu hawezi kuishi kwa muda mrefu katika mazingira ya namna hiyo.
Mahitaji ya mwisho wa dunia
Matajiri wengi duniani, wakiwemo mameneja wa mifuko ya fedha, nyota wakubwa wa michezo mbalimbali na matajiri katika nyanja ya teknolojia (kuna uvumi kuwa Bill Gates amejenga handaki kwenye kila sehemu ambapo ana mali isiyohamishika kama ardhi) wamechagua kubuni makazi yao ya siri kwa ajili ya familia na wafanyakazi wao.
Gary Lynch, meneja mkuu wa kampuni ya Rising S Company ya huko Texas nchini Marekani, anasema kuwa mauzo kwa ajili ya majengo ya chini ya ardhi yameongezeka kwa asilimia 700 mwaka 2016, ukilinganisha yalivyokuwa mwaka 2015, wakati kwa ujumla mauzo hayo yameongezeka kwa asilimia 300 tangu uchaguzi mkuu wa Marekani Novemba mwaka jana.
Majengo ya chuma ya kampuni hiyo, ambayo yamebuniwa kwa ajili ya kudumu kwa vizazi kadhaa, yanaweza kuchukua chakula cha kutosha matumizi ya mwaka mzima kwa kila mkazi wa majengo hayo na pia yana uwezo wa kuhimili matetemeko makubwa ya ardhi.
Lakini wakati wengine wanataka kukaa kwenye majengo hayo peke yao, wengine wanataka kukaa huko na jamii zao ili kuwa na mfano wa maisha yanayofanana na yalivyo sasa.
Wabunifu wa majengo maalumu kwa ajili ya jamii mara nyingi hununua mahandaki ambayo hapo awali yalikuwa yakitumiwa kijeshi au mahandaki maalumu ambayo yalijengwa na serikali ya Marekani kwa ajili ya kuficha silaha kali – maeneo ambayo yanaweza kugharimu mamilioni ya dola kwa ajili ya kuyajenga leo hii.
Majengo hayo ambayo yameimarishwa, yamebuniwa kuweza kuhimili shambulio la kinyuklia na yamewekewa mifumo maalumu ya umeme, mifumo ya kusafisha maji, mifumo kwa ajili ya kuhimili matetemeko makubwa ya ardhi, na pia kuhimili mashambulizi ya silaha za kibiolojia na kikemikali. Lakini pia, majengo hayo yana mifumo kwa ajili ya kusafisha hewa.
Majengo hayo yanaweza kuchukua kiasi cha chakula cha kuweza kukaa kwa mwaka mzima au zaidi, na mengi ya majengo hayo yana bustani maalumu ambazo zinaweza kutumiwa kupanda mimea kwa kutumia madini fulani ambayo huwekwa kwenye maji, hivyo kuondoa umuhimu wa kutumia udongo, na hivyo kuweza kuwapatia wakazi wa majengo hayo virutubisho maalumu ambavyo vinapatikana kwenye mimea.
Wajenzi wa majengo hao pia wanafanya kazi ili kuhakikisha kuwa jumuiya ambazo zitakuwa zinaishi kwenye majengo wanakuwa na vipaji mbalimbali ili kuhakikisha kwamba watu wataweza kuishi katika majengo hayo kwa muda mrefu, kuanzia madaktari hadi walimu.
Vicino anasema Vivos imepokea maombi mengi kwa ajili ya majengo yake wakati wa uchaguzi nchini Marekani mwaka jana.
Safina ya mbunifu
Moja ya makazi hayo, Vivos xPoint, yapo karibu na Black Hills huko South Dakota nchini Marekani, na lina jumla ya mahandaki 75 ya kijeshi ambalo zamani lilikuwa ni sehemu maalumu kwa ajili ya kuhifadhi silaha za jeshi hadi mwaka 1967.
Sehemu hiyo sasa inabadilishwa ili kuwa ni sehemu yenye uwezo wa kuchukua jumla ya watu 5,000. Marekebisho ndani ya mahandaki hayo yanafanywa kwa gharama ya kazi ya dola 25,000 hadi 200,000 kwa kila moja. Bei ya handaki hutegemea ukubwa wake.
Jengo lenyewe litawekwa starehe zote ambazo hupatikana kwenye mji mdogo, zikiwemo ukumbi wa burudani, madarasa, bustani maalumu, kliniki na sehemu ya kufanya mazoezi ya mwili.
Kwa wateja ambao wanatafuta vitu adimu na vya starehe zaidi, kampuni hiyo inauza Vivos Europa One, ambayo imepewa jina la “safina ya kisasa ya Nuhu” katika ghala za zamani za kuhifadhi silaha wakati wa vita baridi nchini Ujerumani.
Jengo hilo, ambalo limejengwa kwenye jabali, lina makazi 34 binafsi, kila moja likiwa na ukubwa wa futi za mraba 2,500, na likiwa na uwezekano wa kuongeza ghorofa hivyo kufikia ukubwa wa futi za mraba 5,000.
Nyumba zilizoimarishwa kuhimili nyuklia
Majumba kwa ajili ya matajiri yaliyojengwa na Larry Hall zinazofahamika kama Survival Condo huko Texas nchini Marekani zinatumia maeneo mawili yaliyokuwa yanatumiwa kuhifadhi makombora ya masafa marefu, ambayo yalijengwa na mainjinia wa Jeshi la Marekani ili kuhifadhi vichwa vya mabomu ya nyuklia wakati wa miaka ya 1960.
“Wateja wetu wanapewa faida ya kuwa na nyumba ya kifahari na ambayo inakuwa imeimarishwa kuhimili shambulizi la kinyuklia,” anasema Hall, ambaye tayari amesjaanza kazi ya ujenzi wa nyumba nyingine ya aina hiyo sehemu nyingine.
TAZAMA HARMORAPA ALIVYO TIMUA MBIO BAADA YA KUIONA BASTOLA

from Blogger http://ift.tt/2n1DnLf
via IFTTT


Yusuph Manji Awekwa Chini ya Ulinzi Siku 20, Aiomba Mahakama Iingilie Kati…!!!

Yusuph Manji Awekwa Chini ya Ulinzi Siku 20, Aiomba Mahakama Iingilie Kati…!!!

Mfanyabiashara maarufu Yusuf Manji amewasilisha hati ya kuiomba Mahakama Kuu iwaagize maofisa Uhamiaji wamfikishe mahakamani ili kesi yake isikilizwe kwa mujibu wa sheria.
Manji yuko kwenye matibabu Hospitali ya Aga Khan jiji hapa akiwa chini ya ulinzi baada ya kuachiwa kwa dhamana.
Februari 20 mwaka huu, alipelekwa ofisi ya Uhamiaji mkoa na kuhojiwa kwa madai ya kuingia nchini kinyume cha sheria.
Katika kesi hiyo wajibu maombi hayo ni Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam,Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG) na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.
Wakili wa Manji, Hudson Ndusyepo aliyefungua kesi ya maombi hayo, anataka Mahakama iagize maofisa uhamiaji na polisi kumfikisha mahakamani ili iamue uhalali wa kushikiliwa kwake na kuagiza aachiwe.
Katika hati ya maombi hayo, Ndusyepo anadai kuwa alimtembelea mteja wake hospitali ya Aga Khan Februari 17 mwaka huu na kukuta maofisa wa Uhamiaji wakimsubiri mteja wake wampeleke kwa ofisa Uhamiaji wa mkoa kwa mahojiano dhidi ya tuhuma kuwa siyo raia wa Tanzania.
Kwa mujibu wa Ndusyepo, Manji ambaye ni Mwenyekiti wa Quality Group Limited na Diwani wa Mbagala Kuu, Amedai kuwa alitoa maelezo kwa maofisa Uhamiaji na alirudishwa Aga Khan ambako yupo chini ya ulinzi hadi leo.

from Blogger http://ift.tt/2ngoatR
via IFTTT


Mwanaume, Fanya Haya Ili Kumroga Mwanamke, Hata Kama Huna Kitu..!!!

Salam enyi watanzania wenzangu. 
Mungu kanituma niwaeleze haya mambo mazuri kwa ajili ya kudumisha mahusiano yetu, hasa mke na mume au wachumba nk.
Kwanza kabisa, wanawake wana akili sana katika kututawala sisi wanaume na wana uelewa na creativity kubwa sana ya kukusoma vizuri mwanaume kila unachofanya na kila unakokwenda na issues zako zote. Hata kama hakwambii, elewa anajua kila kitu, anakustahi tu.
Kujiamini ni nguzo muhimu sana kwa sisi wanaume kumkalisha mwanamke chini, awe billionea, awe professor, awe na cheo nk kwako si kitu kama mwanaume unayejiamini.

Asijue kitu fulani hujui, asijue kitu fulani huna, asijue kama umeshindwa mahali. Wanawake hutumia “failures” za mwanaume kuwa “opportunities” kwao. Atafanya ya ajabu kwakuwa anajua huwezi kitu fulani, huna kitu fulani, huna uwezo fulani.

Hata kama ikitokea ndani hakuna kitu, mwambie tu ‘kuna mtu nimemwelekeza ataleta hapa nyumbani’. Hata kama huna hela mwambie tu ‘kuna jamaa anatuma sasaivi kwenye mpesa’. 

Hata kama huyo mtu asipoleta, huyo mtu asipotuma kwenye simu, we kauka tu…endelea hivyohivyo kubadili visentensi ili aridhike, huku wewe unaplan/unastruggle kinyakimya kuhakikisha chochote kuhakikisha mambo yanakaa vyema.

Usirogwe ukamwambia mwanamke “siwezi, sijui, sina, nitaangalia, ngoja kwanza, “. Otherwise atafanya anachoweza kuhakikisha anapata kila kitu na hata kukulisha wewe.

Kujiamini, kujiamini, kujiamini ndo dawa ya ‘Eva’ huku duniani.

from Blogger http://ift.tt/2nyjWeb
via IFTTT


Kategori

Kategori