Showing posts with label usa. Show all posts
Showing posts with label usa. Show all posts

TAMCO YASISITIZA MSHIKAMAO WA KIJAMII


Tanzanian Muslim Community Washington DC na vitongoji vyake nchini Marekani (TAMCO) imesisitiza umuhimu wa umoja na mshikamao wa kijamii miongoni mwa wanajumuiya hiyo na Watanzania kwa ujumla wanaoishi katika maeneo hayo. 

Mwenyekiti wa Tanzanian Muslim Community Ndugu Ali Muhammed Shafi (Picha zote na Abou Shatry)
Hayo yameeelezwa na Mwenyekiti wa TAMCO Ndugu Ali Muhammed Shafi alipokuwa akizungumza na Swahilivilla pembezoni mwa "Siku Ya Familia" iliyoandaliwa na Jumuiya hiyo, Siku ya Jumamosi June 6,  jijini Washington DC.

"Lengo kubwa la siku hii ni kuwakusanya pamoja wanachama wa jumuiya yetu na Watanzania wengine wanaoishi katika eneo hili hata kama si wanachama wa jumuiya yetu, kwa lengo la kusisitiza umuhimu wa Familia na mshikamano wa kijamii", alisema Ndugu Shafi, na kuongeza kuwa ni nafasi nzuri ya kujuana khususan kwa watoto.

Aliendelea kusema kuwa mkusanyiko huu ambao hufanyika mara moja kila mwaka una lengo pia la kufanya matayarisho ya mwezi Mtukufu wa Ramadhan, ambapo wanajumuiya huchangisha fedha kwa jili ya futari ya pamoja kwa mwezi mzima wa Ramadhani.

"Tayari TAMCO imeshaandaa kumbi maalum kwa ajili ya futari ya pamoja kwa muda wa mwezi mzima wa Ramadhani na matayarisho yote yameshakamilika, tunachosubiri ni kumkaribisha mgeni huyo Mtukufu" alisema Bwana Shafi, na kuwatolea wito wanajumuiya ambao bado hawajatoa ada zao za uanachama kufanya hivyo, ili kurahisisha na kufanikisha malengo ya jumuiya hiyo.

Akizungumzia malengo ya baadaye ya jumuiya hiyo, Bwana Shafi alisema kuwa wana lengo la kufungua madras kwa ajili ya watoto wanaoish Washington na maeneo ya karibu, ili kuhakikisha kuwa watoto wanapata elimu,malezi na mafunzo halisi ya Kiislamu.

Aliwatolea wito wanajumuiya kuitumia fursa ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa ajili ya kuongeza Ibada na Imani ndani ya mwezi huo na katika maisha kwa ujumla.

Siku Ya Familia ya TAMCO (TAMCO Family Day), hufanyika kila mwaka ambapo wanajumuiya hiyo na wengineo hukutanika pamoja kwa siku nzima, ambapo pamoja na mambo mengine, hutoa nafasi kwa watoto kucheza, kufurahi kujuana na kujenga urafiki tangu wakiwa wadogo.

Baadhi ya waumini wa  Tanzanian Muslim Community wakiwa katika mkusanyiko wa siku ya familia, ilioandaliwa rasmi na jumuiya hiyo,  Siku ya Jumapili June 6, waIslamu Washington DC


Nyuma kabisa aliekuwa muasisi wa zamani wa Tanzanian Muslim Community in Washington DC (TAMCO) Bwana Yusuf Kalala akiwa na Shamis Alhatry, kushoto, Kulia ni Mwenyekiti wa ZADIA, pa moja na Mganga  katika sharehe ya familia Day Siku ya Jumamosi June 6, waIslamu Washington DC

Baadhi ya waumini wa  Tanzanian Muslim Community wakiwa katika mkusanyiko wa siku ya familia, ilioandaliwa rasmi na jumuiya hiyo,  Siku ya Jumapili June 6, waIslamu Washington DC

Mwenyekiti wa Zanzibar Diaspora Association (ZADIA) Omar Haji Ally (kulia) akibadilishana mawazo na aliekuwa muasisi wa Tanzanian Muslim Community in Washington DC (TAMCO) Bwana Yusuf Kalala, kwenye sharehe ya familia Day Siku ya Jumapili June 6, waIslamu Washington DC

Hapa ikifika Muda wa Pambano la MANNY PACQUIAO NA FROYD MAYWEATHER UTATAZAMA LIVU HAPA kRIBU ELIMTAA!!!!!!!!

JE UNA SMART PHONE AU KUMPYUTA BANDO YAKO TU WAWEZA TAZAMA LIVE MPAMBANO WA KARNE

Jinsi ya kutazama live mpambano huu Bonyeza Play hapo chini au juu ya picha na endelea kuzataza live mpambano huu wa Karne
Barack Obama ataka amani Nigeria

Barack Obama ataka amani Nigeria


Raisi wa Marekani Barack Obama
Raisi Barack Obama ametoa mwito kwa wa Nigeria kusitisha vurugu hasa kuelekea uchaguzi mkuu wa nchi hiyo mapema mwishoni mwa wiki hii.
Wasi wasi wa hali ya usalama umezidi kuongezeka nchini humo wakati siku ya kupiga kura kadiri inavyokaribia ambapo wananchi wa Naijeria wanatarajiwa kupiga kura jumamosi wiki hii baada uchaguzi huo kuhairishwa mwezi uliopita kutokana na mashambulio ya kundi la Boko Haram.
Rais Obama amesema kwamba Nigeria inapaswa kufanya uchaguzi ulio huru na wa haki.
wanaijeria wote wanapaswa kupiga kura zao bila ya vitisho ama wasi wasi .Hivyo natoa wito kwa viongozi wote pamoja na wagombea kuzungumza na wapiga kura wao kwamba vurugu hazina nafasi katika uchaguzi wa kidemokrasia,na hawapaswi kuchochea, wasaidie au kujihusisha na vurugu zozote kabla ama baada ya uchaguzi na wakati wa kuhesabu kura.
Nina waomba wanaigeria wote kueleza hisia zenu kwa amani na kuwapuuza wote wanaotoao wito wa kufanya vurugu .
Wakati Rais Obma akitoa wito huo Joto la uchaguzi linazidi kupamba moto nchini Nigeria.
Mvutano mkali upo kati ya rais Goodluck Jonathan wa chama tawala cha PDP na mgombea wa upinzani Jenerali Muhhamadu Buhari wa APC. Wananchi wa Nigeria watapiga kura siku ya Jumamosi kuchagua mtu atakayewaongioza kwa miaka minne ijayo.
SASA NI MIAKA 10 TOKA KUANZISHWA KWA FACEBOOK

SASA NI MIAKA 10 TOKA KUANZISHWA KWA FACEBOOK

CONTACT WITH ELIMTAA BLOG BY: CALL :+255 788 056115 EMAIL: furahanews1@gmail.com Facebook: www.facebook.com/elimtaa Twitter: www.twitter.com/@elimtaa "ANY TIME CALL US FOR ADVERTISEMENT, OR ANY NEWS YOU WANT APPEAR TO Elimtaa Blog" Elimtaa 'more news update your mind'


Wakuu wa Facebook wakisherehekea miaka 10
Facebook inasherehekea miaka kumi wiki hii tangu kuzinduliwa. Ina watumiaji bilioni 1.2. Lakini nani anatumia Facebook and wanaitumia kwa njia gani?
Mishumaa kwenye keki ya Facebook inaposherehekea miaka 10 haitazima kabla ya mtu kuwa na tashwishi ikiwa kampuni hiyo itadumu na kufikisha mwaka wake wa 11.
Katika utafiti uliofanywa hivi karibuni, ikiwa utaaminika , siku za mwisho za Facebook zinakaribia.
Taarifa mbali mbali zinapendekeza kuwa idadi kubwa ya watumiaji wa Facebook , vijana wakiwemo wengi, wanachoshwa na mtandao huo wa kijamii baadhi ya watafiti wakisema kuwa watumiaji wengi wanalinganisha Facebook na maradhi mabaya.
Utafiti kama huu ambao huambatanishwa na picha ya Mark Zuckerberg mwasisi wa mtandao huo akionekana mwenye huzuni huonyeshwa sana na vyombo vya habari na hata kusambazwa zaidi kwenye Facebook.
Kwa hivyo wakati watafiti waliposema kuwa kampuni hiyo itapoteza asilimia themanini ya watumiaji wake katika kipindi cha miaka mitatu, wakuu wake walijibu kwa ukali.
Facebook ina watumiaji wengi zaidi vijana kuliko mtandao mwingine wowote.
Imekuwa ikibadili sura yake tangu mwaka 2004.
Mark Zuckerberg
Hata hivyo baadhi ya watafiti wanasema kuwa karibu vijana milioni tatu waliondoka kwenye Facebook katika miaka mitatu iliyopita nchini Marekani.
Vijana wengi wanasema waliacha kutumia Facebook kwa sababu ya wazazi wao, ambao pia wamejiunga na mtandao huo wa kijamii.
Wazazi hutuma picha za watoto wao kwenye mtandao ambazo wao wenyewe wanahisi ni za kuchekesha.Jambo hili limewatia aibu vijana ambao wameamua kutumia mitandao kama WhatsApp au Snapchat badala ya kuwa kwenye mtandao mmoja na wazazi wao.
Licha ya vijana wanaotumia Facebook kupungua watu wenye umri zaidi ya 55 wameonekana kuongezeka.
 Na BBCSwahili
Kanisa Kuingia doa Chicago, makuhani waendesha unyanyasaji wa ngono

Kanisa Kuingia doa Chicago, makuhani waendesha unyanyasaji wa ngono

Kardinali Francis George wakati akizungunzia wazi wa nyaraka iliyo kuwa siri (Picha na AP)
Maelfu kwa maelfu ya kuraza zinazo onyesha kumbukumbu zilizo andikwa kwa mkono zinazo toa madai kwa viongozi wa kuhusu unyanya saji wa Ngono zimekutwa kwa wanashelia baada ya kuwasilishwa na waathirika na wa vitendo hivyo.

Kardinali Francis George alisema Jimbo Kuu la Chicago zimepatikana nyaraka zilizo andikwa kwa mkono maelfu ya kurasa zenye kumbukumbu na madai juu ya viongozi wa dini kuhusika na ngono za unyanyasaji ambazo zimekutwa kwa wanasheria zikiwa zimeletwa na waathirika.

Wanasheria hao walipigania kwa miaka mingi kuhakikisha kanisa katoriki linawajibika kwa ajili ya kushughulikia suala la madai hayo.

Nyalaka zilizo kutwa zina husisha taifa la tatu kwa ukubwa jimbo kuu ni pamoja na malalamiko, nyaraka hizo zilihusisha wafanyakazi na nyingine kwa ajili ya makuhani 30 wanaohusika na unyanyasaji uliotolewa kuhusiana na madai hayo.

Wanasheria walisema kuwa Waathirika  wiki ijayo watatoa maelezo ya kina kwa umma kuhusiana na nyaraka na madai ya uhalifu wa siri uliohusisha makuhani kwa ajili ya nafasi ya kuwa ruhusu watoto kuendelea Kutoa maudhui.

Na Aljazila
Imetoholewa na Elimtaa Blog
Uraibu wa sigara wawavutia wengi

Uraibu wa sigara wawavutia wengi


 
Athari za uvutaji sigara
Idadi ya wavutaji wa sigara duniani imeongezeka kwa karibu bilioni moja kwa mujibu wa takwimu mpya.
Watafiti walioandika katika jarida la Shirika la madaktari la Marekani wanasema hata hivyo kuwa idadi hiyo ni ndogo ikilinganishwa na ongezeko la watu kwa ujumla duniani na kuelezea haja ya juhudi zaidi kufanyika kuwazuia watu kuwa na tabia hiyo.
Idadi ya watu wanaovuta sigara kila siku duniani imepanda kwa kiwango cha watu takriban milioni 250 million kati ya mwaka 1980 na 2012, kwa mujibu wa ripoti .
Katika nchi kama vile Urusi ,Indonesia na Timor ya Mashariki , zaidi ya nusu ya wanaume wana tabia ya kuvuta sigara kila siku.
Baadhi ya maeneo yenye idadi ndogo ya wavutaji wa sigara ni katika visiwa vya Caribbean vya Antigua na Barbuda ambapo mtu mmoja kati ya 20 huvuta sigara kila siku.
Watafiti wanasema kuongezeka kwa kiwango cha wavutaji wa sigara kinatokana na ongezeko la watu duniani.
Lakini licha ya kuongezeka kwa kiwango cha uvutaji sigara , kiwango cha watu wanaovuta sigara duniani kimepungua. Idadi ya Wanaume wanaovuta sigara imepungua kwa asilimia 10 tangu mwaka 1980, na wanawake wamepunguza uraibu huo kwa asilimia 4.
Shirika la afya duniani linasema vifo vya mamilioni ya watu vinaweza kuepupika kwa nchi zaidi kuweka hatua kama vile kuongeza kodi ya sigara, kupiga marufuku uvutaji sigara katika maeneo ya umma na kuweka onyo kwenye paketi za sigara
Kerry aanza ziara ya siku tano katika Mashariki ya Kati

Kerry aanza ziara ya siku tano katika Mashariki ya Kati

Waziri wa Mambo ya Nchi za Kigeni wa Marekani John Kerry yuko katika Mashariki ya Kati kujaribu kuunga mkono mkakati wa makubaliano ya amani baina ya Israel na Palestina. 
Kerry amewasili leo mchana mjini Tel Aviv, Israel, na alitarajiwa kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Rais wa Palestina Mahmoud Abbas.
Mazungumzo hayo yaliyodumu miezi mitano na ambayo yanastahili kudumu miezi tisa, yanakaribia kutokota, kwa sababu ya hasira ya Wapalestina dhidi ya ujenzi wa makaazi unaoendelea kufanywa na Israel na mgogoro kuhusiana bonde la Jordan ,mashariki ya Ukingo wa Magharibi. Msemaji wa Ubalozi wa Marekani mjini Tel Aviv Geoff Anisman amesema mkakati unaotayarishwa na Kerry utayaangazia masuala yote ya msingi katika mgogoro huo baina ya pande hizo mbili, ikiwa ni pamoja na mji wa Jerusalem, mipaka, wakimbizi, makaazi pamoja na mipango ya usalama.

Kategori

Kategori