Showing posts with label 2017 at 11:40AM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 11:40AM. Show all posts
MAENEO YOTE MAPYA YA UTAWALA KUJENGWA NYUMBA MPYA NA NHC

MAENEO YOTE MAPYA YA UTAWALA KUJENGWA NYUMBA MPYA NA NHC

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameliagiza Shirika la nyumba Nchini kwenda kujenga nyumba bora za makazi katika maeneo yote mapya ya utawala ikiwemo mikoa na wilaya ili kusaidia kutatua changamoto ya makazi kwa watumishi.
Pia ameweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa nyumba 20 za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba mkoani Songwe zinazojengwa katika kijiji cha Tindingoma, unaojengwa na Shirika la Nyumba Nchini.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Julai 21, 2017) wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Naming’ongo wilaya ya Momba akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Songwe.
“Nalipongeza Shirika la Nyumba kwa mikakati waliyonayo ndani ya shirika hilo na kwamba waendelee na utekelezaji wa mipango hiyo ya ujenzi wa nyumba ili maeneo yote mapya ya utawala yaweze kuwa na makazi bora ya kuishi watumishi.”
Pia aliwataka wakazi wa kata ya Chitete yaliko makao makuu ya wilaya ya Momba kuhakikisha wanachangamkia fursa ya uwepo wa makao makuu wa wilaya kwenye kata yao kwa kujenga nyumba za kisasa kwa ajili ya kupangisha watumishi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Bw. Nehemia Mchechu amesema mradi huo wenye thamani ya sh bilioni 2.2 ulianza kujengwa Machi 2016 na unatarajiwa kukamilika Septemba mwaka huu.
Amesema mradi huo ulibuniwa baada kupokea maombi kutoka Halmashauri ya wilaya ya Momba na kwamba unatekelezwa kwa awamu mbili ya kwanza ni ujenzi nyumba nane na tayari zimekamilika.
Ameongeza kwamba ujenzi wa awamu ya pili unajumuisha nyumba tisa ambapo gharama ya ujenzi wa nyumba itatumika kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya ofisi za Halmashauri hiyo.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya NHC , Bi. Blandina Nyoni amesema shirika hilo lilianzisha mpango wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu katika maeneo mbalimbali nchini ili kuwawezesha wananchi kuwa na makazi bora.
Amesema katika miradi 54 ya ujenzi wa nyumba inayotekelezwa na shirika hilo katika maeneo mbalimbali nchini kati yake miradi 24 imekamilika ikiwemo 14 ya nyumba za gharama nafuu.
Pia Mbunge wa jimbo la Momba (CHADEMA), David Silinde amesema anashukuru Serikali kwa ujenzi wa nyumba hizo na kumueleza Waziri Mkuu kwamba wananchi wa Momba wanaridhishwa na utendaji wa Serikali na kwamba maendeleo hayana chama.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, JULAI 21, 2017

from Blogger http://ift.tt/2uk7B2O
via IFTTT


MAKALA: JINSI YA KUTAMBUA TAIRI YA GARI ILITENGENEZWA LINI NA MUDA WA MATUMIZI

MAKALA: JINSI YA KUTAMBUA TAIRI YA GARI ILITENGENEZWA LINI NA MUDA WA MATUMIZI

Watu wengi hupata wakati mgumu wanapokwenda kununua tairi au matairi kwa ajili ya gari au magari yake kwa sababu hajui ni lini tairi lile lilitengenezwa. Watu wengi huangalia kama tairi ni chakavu (kipara) au la ili kuweza kuamua kama wanunue au wasinunue.
Wengine wakienda kununua tairi, kwa vile tu wanaona tairi ni mpya basi wanajua itafaa kutumika kwenye gari lake bila kujua anahatarisha maisha yake, kwani tairi inaweza ikawa inaonekana mpya lakini kiuhalisia ilitengenezwa miaka mingi nyuma, na hivyo kuwa imeisha muda wake wa matumizi.
Kabla hujanunua tairi au matairi kwa ajili ya matumizi ya gari lako, hakikisha unazichunguza kwa makini tarakimu nne ambazo huandikwa pembeni mwa tairi hiyo.
Matairi ya gari huandikwa muda yalipotengenezwa. Hivyo ni muhimu kuzingatia hili ili kuepuka kupata ajali kwa matairi gari lako kupasuka licha ya kuwa ni mapya.
Jinsi ya kutambua tairi lilitengenezwa lini tafuta alama kwenye tairi iliyoandikwa kwa mfumo huu (1516) wa namba nne zilizokaa pamoja. Katika namba hizo nne, namba mbili za mwanzo zinaonyesha tairi lilitengenezwa wiki ya ngapi katika wiki 52 za mwaka, na namba mbili za mwisho zinaonyesha mwaka tairi lilipotengenezwa. Kwa mfano tairi ikiwa na na namba 1516, inamaanisha kuwa ilitengenezwa wiki ya 15 ya mwaka 2016, au 2309 inamaanisha ni wiki ya 23 ya mwaka 2009.
Kabla ya mwaka 2000, tairi za magari zilikuwa zikiandikwa tarakimu tatu (168) kutambua muda tairi iliyotengenezwa. Lakini walibadilisha na kuweka tarakimu nne kwa sababu tarakimu tatu zilikuwa zinasumbua kujua mwaka halisi. Mfano 168 ni wiki ya 16, lakini unashindwa kujua ni mwaka 1998, au 1988 au 1968. Hivyo kuwekwa tarakimu nne (2001) inaondoa utata kuwa ni wiki ya 20 mwaka 2001.
Aidha, unashauriwa usinunue tairi lililokaa muda mrefu sana dukani kwani linakuwa si salama kwa matumizi yako. Hakuna muda maalum ambao unaweza kutajwa kuwa ndio mwisho wa matumizi ya tairi tangu siku ilipotengenezwa kwa sababu kuisha muda wa matumizi ya tairi kunategemea na sababu nyingi.
Miongoni mwa sababu zinazochangia kuisha kwa tairi ni namna unavyotumia tairi zako, barabara unayopitisha gari lako, sehemu unapohifadhi, hali ya hewa ya nchi uliyopo. Tairi za gari kwenye nchi zenye joto huharibika mapema zaidi kutokana na jua kuharibu mpira. Hapa ni sawa na ruber band ukiiweka kwenye jua kwa muda mrefu, ukija kuivuta utaona inaanza kukatika.
Katika makala ijayo tutazungumza jinsi ya kutambua uwezo wa spidi ya tairi. Kila tairi inauwezo wake wake wa spidi, hii inamaana ukiendesha gari zaidi ya spidi ya tairi, utakuwa kwenye hatari kubwa. Endelea kuwa nasi.

from Blogger http://ift.tt/2rrYOKD
via IFTTT


Waliovunjiwa Nyumba Mkwajuni na Mkunguni Dar Kulipwa

Waliovunjiwa Nyumba Mkwajuni na Mkunguni Dar Kulipwa

BUNGE limeelezwa kuwa wananchi waliovunjiwa nyumba katika eneo la Mkwajuni wilayani Kinondoni ambao wana hati watalipwa fidia.
Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula, wakati akijibu swali la Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia (CUF) aliyetaka kujua hatima ya watu waliovunjiwa nyumba katika eneo hilo.
Naibu Waziri alisema, ni kweli watu walivunjiwa nyumba katika eneo la Mkwajuni na Mkunguni, hivyo wapeleke hati zao wizarani walipwe fidia.
Akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalumu, Salma Mwassa (CUF) aliyetaka kujua kuna umuhimu gani kusarisimisha nyumba alisema, kunapunguza migogoro ya ardhi.
Mabula alisema urasimishaji wa ardhi maana yake ni kutambua miliki ya wananchi kwenye maeneo yaliyoendelezwa bila kupimwa kisheria.
Matokeo ya urasimishaji ni kutoa hati miliki na kuweka miundombinu ya msingi kama vile barabara, maji, mifereji ya maji ya mvua na ikiwezekana majina ya mitaa.


“Urasimashaji ni mpango shirikishi unaowezesha wananchi kukubaliana na mipaka ya viwanja, kufungua njia na kutoa maeneo ya huduma za jamii kama vile shule, vituo vidogo vya polis, makaburi, zahanati na maeneo ya wazi,” alisema.

from Blogger http://ift.tt/2nM3z1t
via IFTTT


Hii Hapa Taarifa ya Maendeleo ya Kiafya ta James Mbatia..Bado Anaโ€ฆ!!!

Hii Hapa Taarifa ya Maendeleo ya Kiafya ta James Mbatia..Bado Ana…!!!

KATIBU Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Juju Danda amesema afya ya Mwenyekiti wa Chama hicho, James Mbatia inaendelea vizuri na matarajio yao ni kumwona akishiriki Bunge la Bajeti linaloanza leo, Dodoma.
Aidha, Danda amesema chama hicho hakirudi nyuma kujijenga na kuwa watu wanaofikiria kuwa kitaharibu malengo yake hawatafanikiwa.
Katibu huyo alisema hayo jana alipozungumza na kubainisha kuwa kwa matibabu anayopata Mwenyekiti wao yanamfanya aendelee vizuri na afya yake inazidi kuimarika.
“Tangu atoke kwenye matibabu amekuwa akiimarika na kwa sasa hata magongo hatumii kutembea na naamini atashiriki vikao vya Bunge,” alisema.
Alisema wamejiwekea mikakati ya kurejesha heshima ya chama, hivyo watu wanaotumika kuharibu mwelekeo wa chama hawatakubalika.
Katibu Mkuu alisema katika kuonesha dhamira ya kujenga chama wamemfukuza aliyekuwa mwanachama wao, Faustine Sungura baada ya kubaini kuwa hana nia njema na chama hicho.
Alisema Sungura amekuwa akishirikiana na watu kujaribu kuhuju chama, hivyo wasingeweza kumvumilia.
“Sungura amekuwa akitumika na bahati nzuri hakuwa na cheo hivyo hana madhara lakini katika kurejesha heshima ya chama Kamati Kuu ilivyokutana hivi karibuni iliamua kumfukuza NCCR-Mageuzi,” alisema.
Kwa upande mwingine alisema chama hicho hakina mpango wa kufungua kesi ya kupinga mchakato wa uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), kwa kuwa wagombea wa vyama vya CUF na Chadema ni wana Ukawa wenzao.

from Blogger http://ift.tt/2ox7HC9
via IFTTT


Haya Ndio Baadhi ya Madhara ya Kuvaa Chupi Kwa Wanawake

1. Magonjwa ya “Urinary tract infection” au UTI hayataisha kwako. Hii hasa ni kwa wanawake wanavaa nguo nyingi kwa wakati mmoja na kwa muda mrefu zaidi ya saa kumi. Unavaa chupi, lakini tight, suruali ya jeans, nk halafu unashinda na hizo nguo kuanzia asubuhi unapoenda kazini hadi saa mbili usiku unaporudi home. Hiyo ni hatari sana. Mwanamke anayefanya kazi zinazompasa kuwepo kazini zaidi ya masaa 8 namshauri asiwe anavaa chupi kabisa. Chupi ivaliwe nyakati za hedhi tu.
Kama hauko kwenye siku zako vaa suruali tu bila chupi. Au vaa underskirt pekee yake kwa ndani na ndoo uvae nguo yako ya kawaida. 
Hii itakuepusha na kuugua UTI. Ukiacha sababu za ngono UTI husababishwa na bacteria wanaopendelea mahali penye unyevu na joto. Kwa hiyo mwanamke akivaa nguo nyingi bacteria hao hujipatia joto la kutosha kuzaana. Mwanamke ni vyema ukaepuka kuvaa nguo za kubana mwili sana ili kuepukana na uwezekano wa kupafanya ukeni pawe na joto sana na ikitokea bacteria mmoja tu akaingia humo atazaa haraka sana na kujikuta UTI inakuwa rafiki yako. Vaa sketi bila chupi au kama kuvaa suruali ni lazima hakikisha unavaa suruali peke yake. Jizoeze tu utazoea. Na ukizoea kuvaa nguo bila chupi utainjoi sana.
2. Magonjwa ya kuvu au fungus hayatakoma kwako. Bado niko kwa wanawake, kama nilivyoeleza mwanzo hapo magonjwa ya fungus yanasababishwa pia na kuvaa chupi kwa muda mrefu. Chupi inayovaliwa kwa zaidi ya saa 8 lazima italeta ukungu au uvundo sehemu nyeti. Huo uvundo waweza kuleta fungus ukeni. Fungus za ukeni hazina tofauti na zile za miguuni kwa wanaume wanaovaa viatu kwa muda mrefu bila usafi miguuni wa kutosha. Chupi inakuwa kama socks za wanaume. Mwanamke avaae chupi muda mrefu bila kuruhusu upepo upite ndani ni watapata fungus ukeni sawa na mwanaume anayevaa socksi zisizofaa kiafya. 
Chupi au socks zinazofaa ni zile za pamba au cotton. Of course sababu za kupata ugonjwa wa fungus kwa mwanamke siyo tu kuvaa chupi inayobanaaaa kwa muda mrefu ni pamoja na kutawadha kwa kutumia maji. Wanawake wengi hawajui kutawadha kwa kutumia maji
Tazama video Mtoto amvua kofia 
Papa Francis

from Blogger http://ift.tt/2nlTljk
via IFTTT


Nape Baada ya Makonda Kuvamia Kituo cha Clouds Fm..!!!

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amefunguka kupitia mitandao ya kijamii juu ya madai ya kuvamiwa kwa kituo cha Redio Clouds FM majira ya saa nne usiku, siku ya Ijumaa kuamkia Jumamosi.
Aidha Nape amewataka wanahabari watulie mpaka pale jambo hili litakapo patiwa ufumbuzi.
“Litatolewa ufafanuzi”, aliandika Nape.

from Blogger http://ift.tt/2mZxzTP
via IFTTT


Kategori

Kategori