from Blogger http://ift.tt/2wyc0Bq
via IFTTT
UKITAKA KUSTAAFU MAPEMA ZINGATIA MAMBO HAYA.
- Watu wengi sana wanatamani kuwa na uwezo na uhakika wa kustaafu mapema, lakini ni wachache sana wanachukua hatua mahususi kuhakikisha wanalitimiza jambo hilo.
- Ili uweze kustaafu mapema, mambo matatu yanahitajika: kipato cha uhakika, kuweka akiba na kuwekeza akiba yako.
- Jambo la kuzingatia ili utimize lengo hili ni kufanya mambo hayo matatu yawe ndio kipaumbele chako maishani.
-
Vijana wanajulikana kwa kuwa na tabia ya kutopenda kufata sheria, na linapokuja swala la matumizi ya pesa zao wanazozipata kwa jasho lao – wengi zaidi huwa hawataki hata ushauri kabisa.
Lakini uwezekano wa kustaafu mapema unaweza kuwafanya wengi washawishike kuachana na ubishi wao na kufikiria uhakika wa maisha yao ya uzeeni na kuanza kuchukua hatua za uhakika kuyanyoosha wangali bado vijana na wenye nguvu za kufanya kazi.
Zifuatazo ni njia hizo na jinsi ya kufanya:
1. Tengeneza chanzo imara cha mapato
Kama huna chanzo cha mapato, hutakuwa na nafasi hata ya kuanza kujenga utajiri. Hatua ya kwanza kabisa ya kuhakikisha unapata uhuru wa kipato ni kuwa na chanzo cha uhakika cha kipato ili uwe na uhakika kwamba kutokana na kipato hicho, unaweza kuweka akiba pamoja na kuwekeza kwa ajili ya maisha ya baadaye.Kwa baadhi ya watu, hii yaweza kumaanisha ufanye kazi kwa ufanisi kwenye ajira yako ya sasa ili uweze kutimiza lengo hili. Ukiwa na chanzo cha uhakika cha mapato, hata ikiwa ni kutokana na kazi za mkataba au tenda za kulipwa kwa siku, bado unaweza kuweka mipango ya baadaye na kuanza kuitekeleza, japo kidogo kidogo.
2. Weka akiba sehemu kubwa ya kipato hicho
Ukishakuwa na kipato cha uhakika, jambo muhimu ni kuhakikisha kuwa hutumii pesa yote unayopata. Kujifunza jinsi ya kuishi maisha ya gharama nafuu chini ya kipato chako ni muhimu ili uweze kubaki na pesa (hasa ukianzia ujanani mwako) na uweze kujiwekea akiba itakayokusaidia kwa maisha yako yote yaliyobaki.kwanza, miongoni mwa njia rahisi zaidi za kuhakikisha utakuwa na fedha uzeeni mwako ni kujiunga na mfuko wa hifadhi za kijamii. Mifuko hii itakusaidia kutoa michango yako kila mwisho wa mwezi au kwa muda maalum na kuja kuipata utakapotimiza umri wako wa kustaafu. Kwa waajiriwa, michango hii huwa inakatwa moja kwa moja kutoka kwenye mshahara wako – kwahiyo huna haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu hilo – lakini kwa ambao hawajaajiriwa, unaweza kujiunga kwenye mifuko hii kama mtu binafsi, kwakuwa inaruhusiwa kufanya hivyo pia. Michango unayoiweka ni kiasi kidogo sana cha pesa kwa mwezi, lakini faida yake uzeeni ni kubwa.
Pia, unaweza kupunguza matumizi yako ya pesa kwa kupunguza gharama za nyumba (kama umepanga) ili kodi yako kwa mwezi isizidi asilimia 30 ya kipato chako.
3. Wekeza akiba yako kwenye vitega uchumi vitakavyoongezeka au kutopungua thamani
Kuwa na pesa nyingi kwenye akiba yako ni jambo zuri, lakini unapoiwekeza pesa hiyo yaweza kusababisha tofauti kubwa sana kwenye safari yako ya kustaafu mapema.Kuna wanaoamua kuwekeza kwenye sekta ya majumba, na inaweza ukunufaisha kwakuwa una uwezekano wa kuingiza kipato cha kila mwezi kutokana na kodi za pango.
Kwa wale wasiovutiwa na biashara ya majumba, unaweza kujifunza na kuwekeza kwa kununua hisa za makampuni mbalimbali ambayo yana rekodi nzuri ya ukuaji.
Mwanzo wa safari ya mafanikio ya kuwa na uhuru wa kipato unaanza kwa uamuzi wako kwamba kufanya hivyo ni muhimu sana kwako. Kisha ukiwa unazingatia malengo yako, basi unaweza kutimiza kila unachokitaka bila wasiwasi.
from Blogger http://ift.tt/2vYuBW9
via IFTTT
ULIPAJI KODI YA ARDHI KWA SIMU ZA MKONONI WAANZISHWA NA SERIKALI
from Blogger http://ift.tt/2xsNb6q
via IFTTT
MAABARA YA NYUKLIA YAANZA KUJENGWA NASERIKALI
from Blogger http://ift.tt/2wnr704
via IFTTT
MAMLAKA YA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA YAVUNJWA NA RAIS MAGUFULI
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amezungumza na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa Kulevya Bw. Rogers William Siyanga ambaye amemhakikishia kuwa kazi ya kukabiliana na tatizo la biashara na matumizi ya dawa za kulevya inaendelea vizuri.
Bw. Rogers William Siyanga amesema tatizo la dawa za kulevya lilikuwa kubwa na ametaja dawa za kulevya ambazo Mamlaka inapambana nazo kuwa ni bangi, heroine, cocaine, kemikali bashirifu na kwamba kwa sasa imeanza kukamata na kuharibu mashamba ya bangi na bangi iliyovunwa.
Amebainisha mikakati mitatu inayotumika katika mapambano dhidi ya tatizo hilo kuwa ni kuzuia dawa za kulevya zisiingie nchini, kutoa elimu kuanzia shule za msingi, sekondari, vyuo na kwenye jamii ili watu waache kutumia dawa za kulevya na kutoa tiba kwa watu walioathirika na dawa za kulevya, na pia ametoa wito kwa watu wenye waathirika wa dawa za kulevya kuwapeleka katika mamlaka hiyo ili watibiwe.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
23 Agosti, 2017
from Blogger http://ift.tt/2ipaI5F
via IFTTT
KISA CHA NDEGE NDOGO (DRONE) ILIYOPELEKEA MZEE WA GHANA KUHIJI MAKA
from Blogger http://ift.tt/2xkhXhI
via IFTTT
HII NDIYO KAULI YA SERIKALI KUHUSU WANAFUNZI KWENDA VYUO VIKUU BILA KUHITIMU KIDATO CHA SITA
from Blogger http://ift.tt/2vWsuAs
via IFTTT
DAR:MENO YA TEMBO YENYE KILO 376 YAKAMATWA NA SERIKALI
from Blogger http://ift.tt/2xhCLXd
via IFTTT
MAMBO MATATU TUNAYOJIDANGANYA ZAIDI KUHUSU FURAHA NA MAFANIKIO MAISHANI
from Blogger http://ift.tt/2iiC6Ca
via IFTTT
MAGHOROFA YA LUGUMI KUPIGWA MNADA NA SERIKALI
from Blogger http://ift.tt/2v5vAkj
via IFTTT
MAZAO MATANO YANAYOINGIZIA SERIKALI FEDHA ZA KIGENI ZAIDI
from Blogger http://ift.tt/2w0kws1
via IFTTT
RAIS MAGUFULI AKUTANA NA TAJIRI NAMBA MOJA DUNIA
from Blogger http://ift.tt/2vSW1h6
via IFTTT
MAJINA 7 YA WAHALIFU WALIOHUSIKA NA MAUAJI YA ASKARI 8 WILAYANI KIBITI
- Hassani Ali Njame
- Abdallah Abdallah Mbindimbi @ Abajani
- Saidi Abdallah Kilindo
- Abdulshakuru Mohamed Ubuguyu
- Issa Mohamed Mseketu @Mtawa
- Rajabu Thomas @Roja
- Mohamed Ally Kadude @Upolo
Ndugu Wanahabari
| S/N | KIELELEZO | UTAMBUZI |
| SILAHA, RISASI NA MABOMU | ||
| 1. | SMG = 5 | Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani |
| 2. | Anti Riot Gun 38mm = 2 | Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani |
| 3. | SAR = 1 | Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari Polisi huko Stakishari Jijini Dar es Salaam |
| 4. | MAGAZINI = 2 | Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani |
| 5. | Risasi za SMG 158 | Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani |
| 6. | Bomu la kurusha kwa mkono = 1 | Uchunguzi dhidi ya Bomu hilo unaendelea |
| 7. | Mabomu ya kutuliza ghasia = 4 | Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani |
| VIELELEZO VINGINE | ||
| 8. | Pikipiki = 2 | Pikipiki hizi zilitumika kuwasafirisha wahalifu hawa kwenye utekelezaji wa matukio ya uhalifu maeneo mbalimbali |
| 9. | Vitenge na Nguo mbalimbali | Vitenge na nguo mbalimbali viliporwa baada ya kufanya tukio la kumuua Diwani wa Zamani wa Kibwiwi |
| 10. | Begi = 1 | Liliporwa baada ya kumuua Mtendaji wa Kijiji cha Mangwe |
- Kuua OC CID na Watumishi 2 (Wawili) wa Idara ya Maliasili katika tukio la Jaribu Mpakani – Wilaya Kibiti
- Kuua Askari Polisi 8 (Nane) katika tukio la Mkengeni – Wilayani Kibiti
- Kuua Trafiki 2 (Wawili) katika tukio la Bungu “B” – Wilaya ya Kibiti
- Kumuua Diwani wa Zamani CCM katika tukio la Kibwibwi – Wilaya ya Kibiti
- Kuua Afisa Mtendaji, Mwenyekiti wa Mtaa na Mkulima katika tukio la Kijiji cha Mangwi – Wilaya ya Kibiti
- Wananchi wote nchini kuondoa hofu ya kwamba eneo hili si salama. Nawaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi na kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha nawaomba wananchi kutoa taarifa mara moja kwa Jeshi la Polisi wanapohisi kuna jambo lolote wanalolitilia mashaka.
- Natoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Pwani, hususani maeneo ya Mkuranga, Kibiti na Ikwiriri, kuendelea na shughuli zao mbalimbali za kujiletea maendeleo. Nawasihi kwa dhati kabisa waendelee kutupatia taarifa zitakazosaidia kumaliza kabisa uhalifu kwenye eneo hili. Nitumie fursa hii kuwashukuru sana wananchi wa maeneo ya Mkuranga, Kibiti na Ikwiriri kwa ushirikiano mnaotupatia ambao umesaidia sana kuwadhibiti wahalifu.
- Mamlaka za Hospitali, Zahanati, Vituo vya Afya, Maabara za Afya ya Binadamu na Maduka ya Kuuza Dawa za kutibu Binadamu zijiepushe na utaratibu wa kutoa matibabu kienyeji au kificho kwa watu waliojeruhiwa bila kufuata taratibu za kisheria ikiwemo kupata taarifa ya Polisi “kupitia Fomu maalum ya kuruhusu matibabu (maarufu kama PF. 3)”. Wahalifu wakijeruhiwa ni lazima watafute matibabu.
Ndugu Wanahabari
Natoa wito kwa wananchi ambao wanawafahamu watuhumiwa wafuatao kutoa taarifa katika kituo chochote cha Polisi ili waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
- Hassan Haruna Kyakalewa @ Abuu Salma @ Shujaa @ Dokta
- Shekhe Hassan Nasri Mzuzuri
- Rashid Mtutula
from Blogger http://ift.tt/2useYXE
via IFTTT
MASKINI…Mwanamke Aolewa Saa 10 Jioni, Afariki Saa 7 Usiku na Kichanga Tumboni…..
from Blogger http://ift.tt/2v3iC9e
via IFTTT
