Showing posts with label Njombe. Show all posts
Showing posts with label Njombe. Show all posts
IGP Sirro Awapuuza wanasiasa wanao sema sema 'Kazi ndio Msingi'
WANASIASA nchini wametakiwa kuliacha jeshi la polisi lifanyekazi yake na kuwacha kulishinikiza kufanya kazi na kuombwa kutoa ushirikiano pindilinapo hitaji ushirikiano.
Kauli hiyo inatolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro jana, wakati akizungumza na waandishi wa hapari mkoani njombe ambapo amekuwa kwenye ziara ya kutembelea jeshi hilo kwa siku moja, na kusema kuwa wanasiasa wasilifundishe kazi jeshi hilo wakati akizungumzia kile wanacho endelea kuhusiana na tukio alilofanyiwa Tundu Lissu Mbunge wa Singida magraribu.
IGP Sirro alisema kuwa jeshi hilo linaendelea na kufanya uchunguzi wa tukio hilo na watawaambia watanzania walipo fikia kwa kuwa Jarada la tukio hilo badi wanalo na Wanasiasa hawawezi kuwafundisha watu wa kuwahiji wakati wao wanajua kazi yao.
“Wanasiasa kazi yao ni kuzungumza na wapiga kura wao wanataka kuwaona wanazungumza hiyo hawezi kuzuia wao kuzungumza kwa kuwa yeye anafanya kazi ya uchunguzi,” alisema IGP Sirro
Aidha Sirro alisema kuwa wanasiasa wanazungumza ili kuonekana na wapiga kula wao na wanakula posho kwa kuongea hivyo hata weza kuwazuia kuzingunza.
Alisema kuwa wanasiasa wanafanya siasa kwa kuwa kuna amani hivyo wamuache aendelee kufanya kazi yake ya kuhakikisha watanzania wanakuwa na amani, na kuwa amani iliyopo ikitoweka wanasiasa hawata fanya siasa wanazi fanya sasa.
“Wanasiasa wanazungumza kwa kuwa hapa nchini kuna amani waniache niendelee kufanya kazi yangu ya kuhakikisha kuna amani na wanasiasa wafanye siasa zao,” Alisema Sirro.
Pamoja na kupuuza maneno ya wanasiasa IGP Sirro amewataka wanajamii kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo hapa nchini kwa kutoa taarifa pale wanapo ona kuna uhitaji wa taarifa hizo na kwa watu wanao watilia shaka ili kukabiliana na watu wasio julikana wanao fanya matukio ya kinyama hapa nchini na kutokomea kusiko julikana.
Kauli hiyo ya Sirro inakuja baada ya kuwepo kwa maneo ya Ndugu wa Mbunge Tundu Lissu kulitaka jeshi hilo kuhakikisha uchunguzi juu ya tukio la kupigwa lisasi kwa Ndugu yao mjini Dodoma na kwenda kulazwa Nchini Kenya kwa matibabu.
Pamoja na sakata la Lissu Sirro ameataka wananchi mkoani njombe kuachanna na matukio ya kushirikia ambayo yanasababisha vifi kwa wanajamii wa mkoani humo huku akimuagiza kamanda wa Polisi mkoani humo hufanya vipindi vya kutoa elimu kwa wakazi wa mkoa huo juu ya madhara ya mauaji kwa imani hizo.
Alisema kuwa elimu ndio kitu pekee kinaweza kuondoa masuala ya mauaji ya imani za kishirikima bila imani jamii haiwezi kubadilika na kuachana na masuala hayo.
WATOTO 2000 WAAZA KUNYWA MAZIWA SHULENI NJOMBE
.
Mkuu wa wilaya ya njombe Ruth Msafiri akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Nundu kulikofanyika uzinduzi wa unywaji wa maziwa kwa watoto wa shule ya msingi.
KATIKA hatua za kupambana na Udumavu mkoani Njombe wadau mbalimbali wameanzisha miradi ya kupunguza udumavu kwa watoto kwa kuanzisha unywaji wa maziwa kwanye shule za msingi halmashauri tatu za mkoa huo.
Mradi wa unjwaji maziwa kwa watoto wa chini ya miaka kumi walioko shule kwa mkoa wa Njombe unazinduliwa kwa kuanza kwa unywaji wa maziwa kwa wototo 2000 huku malengo yakia ni kufikiwa watoto 10,000 mwezi September mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa ya mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri akizindua mradi huo mkoa wa Njombe unaasilimia 49.4 ya udumavu ikiwa ni mkoa wa pili kitaifa, ukitanguliwa na mkoa wa Rukwa ambao unazaidi ya asilimia 50 ya udumavu licha ya mikoa hii kuwa ya kwanza kwa uzalishaji wa vyakula kitaifa.
Msafiri anasema kuwa unywaji wa maziwa kwa watoto hao 2000 mpaka 10,000 ni sawa na asilimia chini ya mbili kwa watoto wote walioko shule wenye umri wa miaka chini ya 10.
Alisema kuwa watu wasitegemea kunyweshewa maziwa na miradi nao wajipembe kuchangia kwaajili ya unywaji maziwa kwa watoto walipo shule.
Watoto hao wananyeshwa maziwa bure mradi ambao tayari umeripiwa kila kitu na Bill and Merenda Gate chini cha taasisi ya uendelezaji wa sekta ya maziwa Afrika Masharaki (East Africa Daily Development) (EADD)
Meneja wa mradi huo Mark Tsoxo baada ya uzinduzi huo alisema kuwa sasa watoto watapata maziwa kila siku za masomo ambapo watoto watakao pata maziwa ni wakle wa shule za msingi wenye miaka chini ya 10 kwa shule za halmashauri za Njombe mji, Njombe wilaya na halmashauri ya wilaya ya Wanging’ombe na watoto 10,000 wanatarajiwa kunywa maziwa kufiakia mwezi Septemba.
Alisema kuwa mradi huo unampango wa kuboresha afya za watoto hao kwa kuwa muda mwingi wanatumia wakiwa shule, na vilevile ni kuboresha unjwaji wa maziwa kwa mikoa ya njanda za juu kusini na kuwafanya wananchi kunjwa maziwa yaliyo sindikwa.
Maziwa yakatayonyewa wan a watoto mashuleni yatatoka kkiwanda cha maziwa Njombe ambao wananunua maziwa kutoka kwa wananchi, Meneja wa kiwanda hicho Edwin Kidehele anasema kuwa kiwanda kimejipamba kunywesha maziwa kwa watoto hao.
BIDHAA ZISIZOFAA ZA MAMILIONI ZATEKETEZWA
BIDHAA zilizo kwisha muda wake zenye thamani ya zaidi ya milioni 7 na zile ambazo hazijasajiliwa kutumika hapa nchini zimeteketezwa mkoani Njombe baada ya kufanyika msako wa duka kwa duka na mamlaka ya chakula na dawa TFDA kanda ya nyanda za juu kusini.
Mkaguzi wa mamlaka hiyo kanda ya nyanda za juu Kusini, Dr. syrivester Mwidunda, akizungumza baada ya zoezi la uteketezaji, alisema kuwa malmaka hiyo imekuwa ikifanya ugaguzi wa kawaida katika maduka mbalimbali ili kubaini bidhaa ambazo hazijasajiliwa kutumika hapa nchini.
Alisema kuwa katika ukaguzi wao huwa wamekuwa pia wakiangalia bidhaa aambazo zina viambata sumu ambapo pia hutazamwa na zile zilizo kusha muda wake ikiwa na lengo la kuhakikisha kuwa watanzania wanatumia bidhaa bora zisizo na madhara kiafya.
Alisema kuwa wakiwa na ukaguzi huo mkoa wa njombe katika wilaya zake zote wamebaini kuwapo kwa didhaa zenye uzito wa kilo 882 zenye thamani ya shilingi milioni 7.4 (7,447,000) ambazo ni vinywaji, vipodozi na bidhaa ambazo muda wake wa matumizi umekwisha.
Hata hivyo wito umetolewa kwa jamii ya watanzania kuhakikisha kuwa wanakuwa makini wanapo nunua bidhaa madukani na kuangalia muda wa kuisha matumizi yake (Expire date) ili kuto tumia vitu hivyo huku wakihakikisha kuwa hawatumii mafuta ya kupaka yenye viambata sumu.
Aidha mratibu wa TFDA mkoa wa Njombe Inosensia Mtega alisema kwa magonjwa ya kasa sasa yamekuwa mengi ni kutokana na matumizi ya bidhaa hizo ambazo muda wa matumizi yake umekwisha na wale wanao tumia vipodozi vyenye viambata sumu.
Alisema kuwa madhara ya matumizi ya vipodozi vyenye viambata sumu huwa ni baada ya muda mrefu na kuwa baada ya hapo mtu huugua Kansa.
Alisema kuwa ni rahisi kuacha matumizi ya vipodozi kuliko kutibu kansa ambayo matibabu yake ni kukata kiungo ama kuchomwa na mionzi ambako ni gharama na hatimaye ni kifo.
Mtega amesema kuwa baada ya kutolewa sana elimu sasa wauzaji wa vipodozi na watumiaji wamepungua tofauti na miaka ya hapo nyuma ambapo watumiaji walikuwa ni wengi na katika maduka vipodozo vilikuwa vikipatikana kwa wingi.

WAMILIKI WA VIBANDA STENDI MAKAMBAKO WAHOFIA KUKUTWA NA YA MWANZA
WAFANYABIASHARA na wamiliki wa vibanda kuzunguka stendi ya Makambako,
wamepata hofu ya kufungiwa vibanda vyao baada ya halmashauri tya mji wa
Makambako mkoani Njombe kuwapa taarifa
za kufanya uhakiki wa vibada vyote katika stendi hiyo.
Wafanyabiashara hao waliambiwa na halmashauri katika mkutano
wao na afisa biashara kuwa wanahitajika kufanyiwa uhakiki wa kila kibanda
katika stendi hiyo na kuwapa mkataba wa malipo ya kodi ya ardhi katika eneo
hilo.
Wakizungumza na afisa biashara wa halmashauri ya mji Makambako
wafanyabiashara hao walisema kuwa wanawasiwasi wa kuja kufungiwa vibanda vyao
baada ya uhakiki huo.
Chesco Ngweta alisema kuwa wanavyo jadili kuhusu mkataba
unaotarajiwa kuwekwa baina yao na halmashauri inawajia kumbukumbu ya kile
kilicho fanyika halmashauri za moja mkoani Mara.
Alisema kuwa serikali inatakuwa kuwatambua na mkataba huo upakapo
letwa kwao usainiwe baada ya kuupitia na kuuelewa.
Aidha afisa biashara Carros Mwenga alisema kuwa baada ya
uhakiki huo halmashauri inatarajia kuanza kujipatia ushuru wa ardhi na kuongeza
kwa vibanda ambavyo havija endelezwa vinandelezwa.
Alisema kupitia uhakiki huo vibanda hivyo vitatambuliwa
ambavyo vinawatu na ambavyo bado havina watu na kupatiwa watu kwaajili ya
kuviendeleza.
Alisema kuwa wafanyabiashara wakikubaliana kuto kubaliana
yaliyo tokea katika mikoa ya Mwanza na Mara yatatokea lakini wakikubaliana
kukubaliana hakuna atakaye fungiwa katika stendi hiyo.
Wamiliki hao wanawasiwasi wa kutokea yale yaliyo tokea Kwenye
stendi za mikoani ya Mwanza na Mara halmashauri kufunga baadhi ya vibanda.
Wafugaji njombe kuelimishwa ufugaji wa kisasa
WAFUGAJI
wa ng’ombe mkoani Njombe wamepewa changamoto kufanya ufugaji kilimo kibiashara
ili kuongeza uzalishaji na ubora wa maziwa utakaoweza kuinua kipato chao
imeelezwa mkoani humo jana.
Wito
huo umetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji ya Mfuko Kichocheo wa Kilimo
Nyanda za Juu Kusini (SAGCOT CTF), Dr Rosebud Kurwijila, wakati akizungumza na
baadhi ya wafugaji wa mkoa huo kwenye semina ya siku tano ya Kilimo Ufugaji
Biashara (FAAB) iliyoandaliwa na SAGCOT
CTF kwa kushirikiana na Kiwanda cha Maziwa Njombe pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo na
Biashara, (UNCTAD ikiwa na lengo la kuinua kipato kutokana na ufugaji wa ng’ombe wa maziwa
kibiashara.
Alisema
hii ni semina ya nne kutolewa nchini Tanzania kwa uratibu wa Mfuko wa SAGCOT
CTF na UNCTAD mara ya kwanza ikiwa ni
mkoani Tanga 2015 mafunzo yakitolewa kwa awamu tatu yakiwa na madhumuni ya
kuwafanya wafugaji wakulima wanaondokana na kilimo cha kujikimu.
“Mfuko
Kichocheo wa SAGCOT CTF unatoa ufadhili kwa wafugaji hao kupitia kiwanda cha
kusindika maziwa cha Njombe ambapo mfuko ulifanya utafiti wa kujua nini mfugaji
anahitaji kuinuka kiuchumi,” alisema.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa semina hiyo, Katibu Mtendaji wa Mfuko Kichocheo wa SAGCOT
CTF, John Kyaruzi amesema kuwa sasa ni wakati wa wafugaji kutajirika kutokana
na ufugaji na ndio maana ufadhili wa elimu hiyo utasaidia wafugaji kufuga
kibiashara ambapo mahitaji makubwa ni kupata ng’ombe mwenye uwezo wa kutoa maziwa kwa
wingi.
“Wafugaji
wengi wapo vizuri katika hatua ya kulisha mifugo yao lakini wanachokikosa ni
elimu ya uchaguzi wa ng’ombe wazuri wa maziwa na hivyo Mfuko Kichocheo wa
SAGCOT CTF hautatoa mkopo wa pesa pekee
kwa wakulima bali kuwawezesha kutoka na kile mfugaji atakacho,” alisema.
Katibu
Mtendaji huyo wa SAGCOT CTF aliongeza kuwa elimu hiyo ni muhimu kwani itasaidia
wakulima wafugaji kutambua kuwa kilimo ni biashara huku pia wakipewa mbinu ya
kupunguza gharama katika ufugaji wa ngo’mbe wa maziwa kibiashara na kwa matumizi
yao hivyo kukuza uchumi wa mkulima mmoja mmoja, jamii na pia kujenga afya zao kutokana na
kutumia maziwa bora.
Naye
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe, Iluminata Mwenda alisema kuwa wafugaji
hao watumie vizuri fursa hiyo kwa kuwa wanaletewa elimu ya kuwa na uchumi mzuri
na kuwa wafugaji wakifanya vizuri halmashauri nayo itaongeza kipato chake kwa
kuwa na kiwanda cha maziwa kinachozalisha kwa wingi.
Nao
baadhi ya wafugaji wameishukuru SAGCOT CTF, UNCTAD pamoja na washirika wengine
waliofanikisha semina hiyo kwani kupitia mafunzo hayo wanaweza kuwa ufugaji
wenye tija kwa ajili ya kuinua kipato na kuboresha afya zao.
Mfuko
wa SAGCOT CTF ulianzishwa Mei 2011 chini ya sheria ya wadhamini ya Mwaka 2002
chini ya Mpango Shirikishi wa Uchumi nchini (PPP), kuchochea maendeleo katika
sekta ya kilimo nchini. Katika kufikia malengo mfuko ulitafuta wabia muhimu
kufikia azma hiyo hivyo Shirika la UNCTAD ni mshirika wake katika kutoa
utaalamu elekezi. (technical assistance)
Mratubu wa biashara wa Mfuko Kichocheo SAGCOT, Abdala Msambachi akitoa ekelimu kwa wagugaji wa ng’ombe wa maziwa mkoani Njombe ili kufanya ufugajiwa kisasa na uinua uchumiwao elimu hiyo inayo tolewa na Mfuko Kichocheo SAGCOT.
Mkuu wa wilaya Makete akutana na maagumu, mkutano wa kwanza na wananchi
WAKAZI jijiji cha Utweve kata ya Ukwama wilayani Makete mbele ya mkuu wa wilaya hiyo Veronica Kessi wanaapa kuto endelea na shughuli za maendeleo kutokana na watuhumiwa wa mauaji ya mtoto Fedy Sanga (17) May 31 kurejea kijijini kwao na kutamba.
Marehemu kabla ya kifo chake alituhumiwa na wanafamilia hao kuwa ni mwizi kitu kilicho wafanya wakazi hao kutokubaliana nacho kwa kuwa wanafahamu mtuhumiwa wa wizi hapashwi kuuwawa badala yake alipaswa kupelekwa polisi.
Katika mkutano wa kwanza wa mkuu wa wilaya ya Makete kukutana na wananchi anakutana na makubwa ambapo wananchi wanamueleza kelo yao na kumtaka ashughulikie watuhumia wanao tamba mtaani sheria itende haki na wao kuanza kufanya maendeleo.
Mama wa mtoto aliye uwawa alisema kuwa baada ya watuhumiw akurejea kijijiji hapo alitambiwa kuwa zinafungwa pesa na kuwa hawataweza kufungwa masikini ndio wanafungwa.
Atu Sanga ni mama wa marehemu aliangua kilio mbele ya mkuu wa wilaya kutokana na kauli alizo kuwa akizisikia kutoka kwa watuhumiwa na kuwa ni siku chache tangu kuzikw akwa mwanae.
Wananchi hao wakiwa na uchungu wa mtoto wa kijijini kwao kudaiwa kuuwawa na watuhumiwa watatu wanafamilia na kukaa ndani kwa wiki mbili na kurejea kijijini hapo wanataapa kuto fanya shughuli za maendele.
Abraham Tete alisema kuwa kijijini hapo hawata fanya maendeleo mpaka ufafanuzi wa watuhumiwa hao kupatikana kijijini hapo na kuwa ujenzi wa Zahanatu sasa umesimama kutokana na tatizo hilo.
Alisema kuwa mkutano wa mapato na matumizi uliokuwa ufanyike kijijini hapo ulivurugika kwa kuwa ufafanuzi wa jamo hilo ulikuwa haujapatikana kijijini hapo.
Mwanasheria wa halmashauri Godfrey Masunga baada ya kuwasikia wananchi anawataka waache mahakama ifanye kazi yake na kuwa wananchi hao wabadilishe mtazamo na kuelekea katika shuguli zao za kimaendeleo za kila siku.
“Kisheria polisi ndio wanafanya uchunguzi wa kesi na kupeleka maelezo mahakamani na anaye amua kesi hii iwe ya aina gani ni askali kulingana na upelelezi alio ufanya” alisema Masunga.
Hata hivyo mkurugenzi wa halmashauri ya makete Francis Namaumbo anawataka wananchi hao kuendele na shughuli za kimaendeleo na kuwaomba suala hilo waiachie mahakama ifanye kazi yake.
Baada ya kusikia kero hizo kutoka kwa wananchi mkuu wa wilaya Kesi anawaomba wananchi hao kuendelea na shughuli za kimaendeleo kijijini hapo na kuwa suala lao linashugulikiwa.
Aidha mwenyekiti wa kijiji hicho Rauteli Sanga alisem akuwa sasa suala lao litashughulikia na kuwaomba atakapo waita katika shughuli za maendeleo kuhakikisha kuwa wanajitokeza na kuendelea kukiletea maendeleo kijiji chao na kuwa kijiji cha mfano kwa wilaya ya makeni.
RC. DR NCHIMBI: USAFI UWE NI TABIA NJOMBE
Mkuu wa mkoa wa Njombe Dr. Rehema Nchimbi aliye vaa kofia ngumu mda mfupi baada ya kukabidhi pikipiki kwa washindi wa usafi kitaifa.
MKUU wa mkoa wa Njombe Dr. Rehema Nchimbi amepinga wakazi wa mkoa huo kufanya usafi wa mazingira wakati wa kampeni za usafi mazingira kitaifa badara yake usafi kuwa ni tabia.
Dr. Nchimbi anawataka wakazi wa mkoa huo kujijengea tabia ya
kufanya usafi mara kwa mara kwenye mazingira yao.
Wito huo aliutoa juzi wakati akikabidhi zawadi kwa
halmashauri ya wilaya Njombe, Mji Njombe na vijiji vilivyo ongoza kitaifa mpaka
nafasi ya tatu vilivyotoka halmashauri ya wilaya ya Njombe.
Dr. Nchimbi aliwataka wakazi hao kutofanya usafi kwa mazoea
na kufanya usafi kama tabia ya wakazi wa Njombe na kusiwe na haja ya watu
kuwashindanisha.
Alisema kuwa haiwezekani watu wakawa wanafanya usafi mpaka
kuwe na mashindano kitu hicho ni cha hatari kwa kuwa wanaweza kuugua kama
hakuta kuwa na mashindano.
Mashindano hayo kitaifa ya usafi wa mazingira na ujenzi wa
vyoo bora mkoa wa Njombe umetwaa ushindi kwa halmashauri zake mbili za Njombe
Mji ambayo imepata Pikipiki ambayo imeongoza kwa halmashauri zote za miji
nchini.
Halmashauri ya wilaya ya Njombe ikiibuka mshindi kwa
halmashauri zote za wilaya nchini na kupata zawadi ya Pikipiki, na Gari moja
aina ya Landcruise Hadtop.
Hata hivyo vijiji hapa nchini ushindi uliangukia katika
vijiji vya halmashauri ya wilaya ya Njombe ambapo vijiji vitatu bora na kijiji
cha Wanginyi kikichukua nafasi ya kwanza kwa vijiji vyote Tanzania.
Emmanuel Mwenda ni Mwenyekiti wa kijiji cha Wanginyi mshindi
wa kwaza kitaifa anabainisha changamoto walizopitia kuupata ushindi huo.
“Katika mashindano haya tulikumbana na changamoto ya maji na
tatizo hili mpaka sasa lipo katika vijiji ninakotoka na vyoo vya masinki bila
kuwapo kwa maji usafi wake ni mgumu naomba serikali kutusaidia maji
yakapatikana” alisema Mwenda
Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri mbali na kuwapongeza
washindi kitaifa alisema changamoto ya maji kweye wilaya yake ishughurikiwe na
wakirugenzi ili wananchi wafanye shughuli zao na kuachana na mahangaiko ya
kutafuta maji.
ELIMU BURE WAALIMU WAOMBA MADARASA NA WAALIM KUONGEZWA
MIEZI sita baada ya sera ya elimu bure kuanzia shule ya msingi mpaka kidato cha nne hapa nchini waalimu wamebaini changamoto mbalimbali ambapo wanaomba serikali kuzishugulikia ili elimu bora itolewa kwa wanafunzi wengi walio jitokeza kupata elimu.
Baada ya sera hiyo kuanza wanafunzi wengi wamejitokeza kupata elimu, huku changamoto ya awali ya uchache wa madawati imetatuliwa tayari sasa wanafuzi wanakaa kwenye madawati lakini shida inakuja katika suala ya vyumba vya madarasa.
Waalimu mkoani Njombe pamoja na kumshukuru Rais wa jamuhuri ya Tanzania Dokta John Magufuli kuhakikisha kuwa wanafunzi wanakaa katika madawati wamemuomba Rais kutatua tatizo la uchache wa waalimu, vitendea kazi pamoja na madarasa kwa baadhi ya shule.
Victoria Kiwale, ni mwalimu wa wanafunzi viziwi kwenye shule wa watu hao mkoani Njombe anaomba serikali kuhakikisha kuwa watoto wanapatiwa wanafunzi wa kutosha hasa kuweka sawa uwiano kati ya wanafunzi na waalimu.
Tatizo hili linaenda sambana na uhutaji wa vitendea kazi kwa waalimu wanao fundisha watoto wenye uhitaji maalumu kama wale wenye uoni hafifu.
Mwalimu Subula Mligo anasema kuwa waalimu wanaofundisha watu wenye ulemavu wanauhaba wa vitu vya kufundishia hasa vile vya nukta nundu.
“Ombi langu kwa serikali ni kuwasaidia waalimu wenzangu kuwapatia vitendea kazi vya kufundishia tunashukuru sasa wanafunzi wanafundishwa wakiwa kwenye madawati,”alisema Mligo.
Viongozi wa chama cha waalimu CWT mkoa wa Njombe wanaona umuhimu wa kutoa elimu kwa waalimu wanawake na walemavu huku wakiwaelimisha juu ya sera ya elimu bure na mwenyekiti CWT Kitengo ke taifa anaomba uwiano urekebishwe.
Katibu wa chama cha waalimu mkoa wa Njombe Fratern Kwahison anasema kuwa waalimu baada ya kupatiwa maada mbalimbali kuhusiana na elimu bure wameibua changamoto mbalimbali na kuomba serikali kukaa na wadau hao ili kuangalia namna ya kuzitatua.
Aidha mwenyekiti wa CWT kitengo cha wanawake Sherida Mtaki, anaomba serikali kuhakikisha kuwa inatafuta ufumbuzi wa tatizo la uchache wa waalimu baada ya kuanza elimu ya bure wanafunzi wengi wamejiandishisha na kuwazidia waalimu.
“Sasa serikali ifanye jitihada za kuongeza waalimu na madarasa ili kuweka sawa uwiano wa waalimu na wanafuzi nashukuru wazazi wamepokea vizuri suala la kuwapo kwa elimu bure wamepeleka watoto wao shule,”alisema Mtaki.
Victoria Kiwale, ni mwalimu wa wanafunzi viziwi
Katibu wa chama cha waalimu mkoa wa Njombe Fratern Kwahison

Makambako shule ya msingi yapata madawati na vyumba viwili kutoka benki ya Posta
SHULE ya
msingi Makambako ya halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe, wamekabiziwa
madarasa mawili na ofisi kukiwa na madawati 50 katika madarasa hayo huku shule
hiyo ikikabiliwa na upungufu madarasa na kusababisa wanafunzi kujazana katika
madarasa.
Shule hiyo
inamlundikano wa wanafunzi ukitofautisha na madarasa yaliyopo katika shule hiyo
ambayo ipo katikati ya mji mkubwa kuliko yote mkoani Njombe.
Akipokea
madawati hayo mkuu wa shule ya Makambako inaupungufu wa vyumba vya madarasa 24
ambapo watoto wa darasa la kwanza na lapili wamekuwa wakisoma kwa zam huku idadi
ya waalimu ikiwa ni ileile.
Mwalimu huyo
amepokea amepokea Madarasa na madawati kutoka Benki ya Posta Tanzania ambayo
imewajengea Madarasa hayo kwa thamani ya Milioni 19 pamoja na madawati.
Mkuu wa mkoa
wa Njombe Dr. Rehema Nchimbi anakuwa ni mgeni Rasimi wakati wa kupokea dawati
na vyumba hivyo vilivyo kabidhiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Posta, Letisia
Lutashobya.
Shule hiyo
inakabiliwa na upungufu wa vyumba hivyo kutokana na kuwapo kwa elimu bule
kunako sababisha wanafunzi wengi kujitokeza kusoma.

MADAWATI YANATOSHEREZA NJOMBE
MKUU wa Mkoa wa Njombe DR. Rehema Nchimbi amewaagiza
wakurugenzi kutoa maeneo kwa waalimu kwaajili ya kila shule kuwa na miti ya
mipatachichi ili kuwapunguzia waalimu ukali wa maisha huku waalim hao
wakimpatia pesa kwaajili ya madawati ikiwa ni kuunga mkono juhudi ya Rais ya
kuhakikisha kuwa watoto hawakai chini.
DR. Nchimbi amewataka waalimu hao kuomba maeneo kwa
wakurugezi wa halmashauri ili waalimu hao kupanda miti ya miparachichi na
kusema kuwa katika shule zake hakuna wanafuzi wanao kaa chini na kusema kuwa
halmashauri pekee ya Ludewa ndio kunashida ya madawati licha ya kuwa vifaa
vyote vinavyo hitajika kuwepo.
Mkuu wa mkoa huyo amewaambia waalimu hao kuwa wajikite katika
ujasiliamali na kujikwamua na ugumu wa maisha huku pesa walizotoa kwaajili ya
madawati zilizotolewa na CWT kitengo cha wanawake na walemavu kurejeshwa kwao.
Walimu hao wamesema kuwa wanaunga mkono juhudi za Rais Dr.
John Magufuli, kuhakikisha wanafunzi hawakai chini kwa kuchangia shilingi laki
saba kwaajili ya kununua madawati.
Waalimu kitengo cha wanawake na walemavu mkoa wa Njombe wapo
katika semina ya kujengeana uwezo na mafunzo ya ujasiliamali ili kujikwamua na
matumizi mabaya ya pesa za mishahara.

WAKANDARASI WATAKIWA KUHAKIKISHA UJENZI WA UMEME UNAKAMILIKA KWA WAKATI
WAKANDARASI wa ujenzi wa umeme kutoka Makambako hadi Songea
wametakiwa na serikali kukamilisha mapema ujenzi huo ili kuondoa tatizo la kukatika
mara kwa mara kwa umeme wilaya za mkoa wa Ruvuma.
Umeme huo unatarajiwa kufikia vijiji 120 vya mkoa wa Ruvuma
chini ya mradi wa REA awamu ya tatu ambapo lengo la serikali ni kufikia
wananchi wote mwaka 2025.
Akizungumza na wakandarasi wa mradi wa umeme wa REA kutoka
Makambako Mpaka songea Naibu waziri wa nishati na madini Medard Kalemani amesema
kuwa serikali inataka umeme huo kufikia Septemba mradi uwe umekamilika.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mrati mbele ya naibu waziri
Meneja wa mradi Mhandisi. Didas Lyamuya amesema kuwa utekelezaji wa mradi
umekuwa ukikumbana na changamoto mbalimbali ikiwepo kucheleweshwa kwa fedha
kutoka serikali kuu.
Mradi huo sehemu ya kwanza ni ujenzi wa njia ya umeme kwa
kilomita 250 kutoka Makambako mpaka Songea kwa msongo wa kilovoti 220 upanuzi wa kituo cha Makambako kilovoti 220 na
ujenzi wa kituo kipya Madaba na Songea kwa kilovoti 220 ili kuwezesha
usambazaji wa umeme.
Wadau wa Ukimwi wakaa Njombe
WADAU wa kupambana na
maambukizi mapya ya Ukimwi mkoa w anjombe wamesema kuwa kunachangamoto ya
baadhi ya watu kutoroka kupata dawa katika vituo vya kuchukulia dawa za
kupunguza makali ya Virusi vya Ukimwi.
Imedaiwa kuwa baadh ya watu wamekuwa wakitoroka kutoka katika
vituo vya kuchukulia dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi kwa
kushawishiwa na baadhi ya viongozi wa dini kuwa watawaombia na waache kuchukua
dawa hizo.
Wakizungumza katika mkutano wa wadau wa kupambana na virusi
vya ukimwi mkoa w anjombe unaojumuisha viongozi wa dini wa dini zote na
waratibu wa ukimwi mkoa na wilaya ya mkoa wa Njombe pamoja na wadau kutoka
asasi mbalimbali za kupambana na maambukizo ya virusi vya ukimwi.
Mmoja wa wadau hao kutoka taasisi za kidini Elias Msemwa wa
mkoani Njombe alisema kuwa kuna baadhi ya waumini wamekuwa wakikimbia dawa na
kwenda kwa baadhi wa viongozi wa dini kuombewa ambapo baada ya kuacha dawa hizo
asilimia kubwa ya hao hupotelea huko huko.
Alisema kuwa alifuatwa na muumini wake mmoja na kuambiwa kuwa
anataka kwenda katika kituo kimoja cha maombezi ambacho kina waambia wasinywe
dawa na watapona kitu ambacho hakukubaliana nachi na alimshauri muumini wake
kuhusiana na tukio hilo na kuomba watumishe wenzake kuto washawishi watu
kuachana na matumizi ya dawa.
Alisema kuwa baadhi ya watu wanao enda huko hupotelea huko
humo baada ya kuacha dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi, na
kusababisha watu hao kufa baada ya kuacha matumizi ya virusi vya Ukimwi.
Hata hivyo mratibu wa Ukimwi halmashauri ya Mji wa Njombe
(Chac), Daniel Mwasongwe, alisema kuwa katika halmashauri yake kuna watu ambao
wanakimbia katika vituo vya kuchukulia dawa na haijulikani kama wamefariki ama
bado wapo wanaishi.
“Halmshauri ya Njombe kuna watu 7662 wanatumia dawa, 3496
wamehama, 14 wamepotea, wamepotea, walio kimbia vituo vya kutolea dawa na
wameacha kunywa dawa hii ni hatari kwa kuwa haijulikani kama watu hao wamekufa
au wapo wanaishi,” alisema Mwasongwe.
Akiwasilisha tarifa ya halmashauri yake kuhusiana na
mapambano ya Ukimwi na utekelezaji wa mapambano ya ugongwa huo alisema kuwa
kuna watu, 18,460 Wanaoishi na virusi vya vya ukimwi halmashauri ya mji wa
Njombe na waliandishishwa katika vituo vya huduma, 7662 wanatumia dawa, 14
wamepotea, 3496 wamehama 1433 wamekufa.

UVCCM NJOMBE WAOMBA RAISI KUKAZA UZI
RAIS wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Rais Dr. John Magufuli ameombwa kuendelea na kasi hiyo ili kuwa wasaidia watu wa hali ya chini waliokuwa wakinyanyasika kutokana na vitendo vya ufisadi vilivyokuwa ukiendelea hapa nchini ikiwa ni pamoja na kuwafirisi wale wanao bainika kutafuna pesa za wananchi.
Ombi hilo limetolewa na umoja wa vijana wa chama cha Mapinduzi UVCCM mkoa wa Njombe baada ya kuona kasi anayoendanayo inaenda kuboresha maisha ya watanzania kwa kubana mianya ya rushwa na kutolewa kwa elimu bure.
Wakizungumza katika mkutano wa tathimini ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba mwaka jana vijana wa umoja huo walisema kuwa wanamuomba Rais kuhakikisha kuwa anakaza uzi na kasi aliyoanzanayo ili kuimarisha uchumi wa nchi.
Vijana hao walisema kuwa kile anacho kifanya Rais ni kuweka sawa masuala ya uchumi kuwapandisha wasio nacho na kukaribia wale walio nacho na kuw ana uchumi wa kati.
Sylvester Mgimba mkazi wa Ludewa alisema kuwa vijana wote Tanzania waungane na Rais kupambana na Ufisadi wa mali za umma na kuwasaidia walio kuwa wananyonywa na kumuunga mkono juhudi zake za kukusanya kodi.
Alisema kuwa kukiwapo na Rais wa aina hiyo kunakuwa na watua wanao mpingia wanaopinga ni moja kati ya watu ambao walikuwa na maslahi katika ubadhilifu.
“Nchi ilikokuwa inaenda ilikuwa inapotea sasa tumepata mkombozi wa watanzania na amekuwa kuinyoosha Tanzania katika njia sahihi maana nchi iliko kuwa inaenda ilikuwa inapotea” alisema Happy Mpete mkazi wa Makambako.
Alisema ukamuaji wa majipu anao ufanya Rais Magufuri watu wasichukie maana wananzania wa hali ya chini wamenyanyashwa vya kutosha na kuwa kutokana na ukamuaji huu watanania tunaelekea kwenye neema.
Mwenyekiti wa Uvccm mkoa, Iman Fute alisema kuwa mabadiliko anayo yafanya Rais nndio yalikuwa yanahitajika na watanzania wengi kwa kuwa vitendo vilivyo kuwa vinatpokea havikuwa vinakemewa sasa mkemeaji amepatikana na nchi inakuwa katika msitali na watumishi kuwatumikia wananchi sawasawa.
Alisema kuwa kama vijana wanampongea Rais kwa kuanzisha huduma ya elimu bure kwa watanzania na kuwa mpango huo umeongeza watoto wa kitanzania kuingia shuleni.
“Sasa inaonyesha ni jinsi gani watanzania walikuwa hawapati elimu kutokana na gharama za ada shuleni sasa vijana wengi wanakwenda shule kwaajili ya kupata elimu kwa hili tunapongeza sana kasi ya Rais Magufuli,” alisema Fute.
Aidha katibu wa CCM Hosea Mpagike aliwataka vijana hao kuhakikisha kuwa wanamsaidia Rais katika kasi yake na kufichua wale wanao fanya ubadhilifu mdogomdogo huko vijijini kwas kuwa nchi hii ni kubwa hivyo wawafichue.
Mpagike alisema kuwa vijana wahakikishe kuwa taarifa wanazo zitoa za majipu madogo madogo kuwa yanatumbuliwa kwa kutolewa taafira za uhakika ili kuokoa pesa za miradi mbalimbali.
“Vijana toeni taarifa za kuwapo kwa ubadhirifu huko vijijini kwa kuwa nchi hii ni kubwa Rais hawezi kufika kila kona tumsaidie kuibua wabadhilifu katika kila kona za nchi yetu ili kuhakikisha kuwa miradi inasimamiwa ipasavyo,” alisema Mpagike.

HALMASHAURI YAKABILIWA NA CHANGAMOTO YA KUJIENDESHA
HALMASHAURI
ya Mji wa makambako mkoani Njombe, inakabiliwa na changamoto mbalimbali
ikiwemo za kiuendeshaji tangu kuanzishwa
kwake mwaka 2013.
Hayo
yamebainishwa katika kikao cha cha baraza la madiwani ambapo imebainika kuwa
imeshuka kimapato uwezo wa kujitegemea umepungua kutoka asilimia 18 kujitegemea
na sasa imeshuka hadi asilimia 15.
Akiwasilisha
taarifa katika kikao hicho Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Chesco Mfikwa,
amekiri kuwepo kwa changamoto katika uendeshaji na kwamba inatokana na baadhi
ya wafanyabiashara kugoma kutumia mashine za kielektroniki (EFD).
Akimwakilisha
mkuu wa Mkoa katika kikao hicho Katibu wa Tawala wa Mkoa Jacson Saitabahu
anatoa ushauri kwa madiwani kutoka hapo walipo
hivi sasa.
Deogtius
Peter Mkaguzi mkazi wan je wa mkoa wa Njombe, akatoa ushauri ili kukabiliana na changamoto hizo.
Angalizo
likatolewa kwa watendaji kuhakikisha elimu inatolewa kwa wafanya biashara
kuhakikisha watumia mashine za EFD ili kuepukana na ukwepaji wa kodi nakwamba
sio hiari ni amri ya serikali na hivyo linahitaji utekelezaji.
Madiwani waanza semina ya siku 4 kwaajili ya kuelimishwa Njombe
Baadhi ya madiwani na watendaji wa halimashauri za Makete na wanging'ombe wafuatilia jambo katika semina kwao inayo tolewa katika Mradi wa PS3
Kiongozi wa mradiwa wa PS3 akizungumza wakatiwa kumkaribisha mgeni tasimi katika semiana kwa madiwani na watendaji ya kuwa weka imara katika mifumo yao ya uterndaji na utoaji huduma kwa jamii.
Mgeni rasimi na kaimu mkuu wa mkoa wa njombe na mkuu wa wilaya ya Makeye Daud Yasini akifungua mkutano wa semiana kwa Madiwani ya siku 4 mkoani Njombe
Mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe Assumpta Mshama akizungumza na madiwani wa kata za Makete na Wangingombe.
IMEDAIWA kuwa bila kuwapo kwa ushirikiano mzuri baina ya
wananchi na serikali kufuatia kutambiliwa kwa kuwepo kwa ushirikiano huo
halmashauri za Wangingombe na Makete zimeanza kupatiwa elimu kwa madiwani wake
ambao ni wawakilishi mukumu wa wananchi.
Akifungua semina ya siku nne kwa madiwani, watendaji na
wenyeviti wa halmashauri za Makete na Wanging’ombe, yanayo tolewa chini ya
mradi wa uboreshaji ya huduma kwa umma kwa serikali za mitaa wa Public Sector
system Strengths (PS3) kaimu mkuu wa mkoa wa Njombe na mkuu wa wilaya ya Makete
Daudi Yasini.
Yasini alisema kuwa serikali haita weza kufanya shughuli za
maendeleo kama kutakuwa na mpasuko wa kiutendaji ma maelewano baina ya Madiwani
na watendaji wa halmashauri.
Alisema kuwa madiwani ni kiunga muhimu baina ya serikali na
watendaji wa serikali madiwani waasipo kuwa vizuri katika utendaji wao
watasabaisha shughuli za maendeleo kuwa ni ngumu kutekelezwa na serikali katika
kata zao.
Alisema kupitia elimu hiyo serikali itaenda kufanya shughuli
zake bila kuwapo kwa vikwazo kwa kuwa madiwani na watendaji wote watafanya kazi
kwa mipaka yao ya kiutendaji.
Aidha kwa niaba ya watendaji na madiwani akitoa shukrani
baada ya kufunguliwa kwa semina hiyo mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe Assumpta
Mshama alisema kuwa serikali inatoa elimu hiyo itasaidia kuhakikisha kuwa maendeleo
yanaonekana.
Alisema kuwa kupitia elimu hiyo madiwani hawata kuwa na tabia
ya kuazimia wetendaji kuondolewa nyazifa za watendaji na baada ya elimu
kutawasaidha kufanyakazi kila mtu kwa nafasi yake.
Aidha Kiongozi wa mradi huo wa PS3 Peter Kilima, alisema
kuwa ni kutokana na nafasi kubwa waliyonayo ya kuwasirisha matatizo ya wananchi
shirika la USAID limeonelea Kutoa mafunzo hayo kwa madiwani.
Subscribe to:
Posts (Atom)








