WAKANDARASI wa ujenzi wa umeme kutoka Makambako hadi Songea
wametakiwa na serikali kukamilisha mapema ujenzi huo ili kuondoa tatizo la kukatika
mara kwa mara kwa umeme wilaya za mkoa wa Ruvuma.
Umeme huo unatarajiwa kufikia vijiji 120 vya mkoa wa Ruvuma
chini ya mradi wa REA awamu ya tatu ambapo lengo la serikali ni kufikia
wananchi wote mwaka 2025.
Akizungumza na wakandarasi wa mradi wa umeme wa REA kutoka
Makambako Mpaka songea Naibu waziri wa nishati na madini Medard Kalemani amesema
kuwa serikali inataka umeme huo kufikia Septemba mradi uwe umekamilika.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mrati mbele ya naibu waziri
Meneja wa mradi Mhandisi. Didas Lyamuya amesema kuwa utekelezaji wa mradi
umekuwa ukikumbana na changamoto mbalimbali ikiwepo kucheleweshwa kwa fedha
kutoka serikali kuu.
Mradi huo sehemu ya kwanza ni ujenzi wa njia ya umeme kwa
kilomita 250 kutoka Makambako mpaka Songea kwa msongo wa kilovoti 220 upanuzi wa kituo cha Makambako kilovoti 220 na
ujenzi wa kituo kipya Madaba na Songea kwa kilovoti 220 ili kuwezesha
usambazaji wa umeme.