Showing posts with label 2017 at 10:23AM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 10:23AM. Show all posts
SHETTA AMPIGA DONGO DIAMOND KIAINA KIAINA KUHUSU KUTOA NGOMA MFULULIZO

SHETTA AMPIGA DONGO DIAMOND KIAINA KIAINA KUHUSU KUTOA NGOMA MFULULIZO

Msanii wa Bongo Flava, Shetta amesema haamini kutoa nyimbo nyingi kwa wakati mmoja ni sababu ya kufanya vizuri.
Shetta ambaye amekaa kipindi kirefu bila kutoa ngoma, ameiambia EA Radio kuwa yeye anaamini katika kujipanga zaidi na kutoa ngoma kali.
“Mimi siamini kwenye kutoa nyimbo nyingi ndio ku-trend, nafikiri kujipanga kwangu ndio huwa kuna sababisha kukaa muda mrefu bila kutoa wimbo, ningekuwa naweza kujipanga haraka ningeweza kutoa madude haraka lakini so far so good ngoja tutaibadilisha, ngoja tuone system yetu tufaifanyaje,” amesema Shetta.
Ameongeza kuwa, “naamini ukitoa kazi ambayo umejipanga nayo watu wanaweza wakaenyoy mwaka mzima au miaka miwili, kukaa kimya haijawahi kunihadhiri kwa chochote sana sana watu wananimisi lakini ninapokuja watu wanakuwa wananipokea, so am happy katika kitu ninachokifanya,” amesisitiza.

from Blogger http://ift.tt/2tvXLfn
via IFTTT


Dodoma: Upinzani Wampeleka Spika Ndugai Mahakamani

Upinzani wamefungua shauri Mahakama Kuu Dodoma wakiiomba mahakama itamke kuwa Spika ataliongoza Bunge kwa kufuata kanuni za kudumu tu.
Hii ni baada ya Spika kumzuia John Mnyika kuhudhuria bunge kwa wiki moja ambapo upinzani wamedai hakuna adhabu kama hiyo kwenye kanuni. 
Wabunge Watatu Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo Chadema Wamemfungua Mashitaka Mahakama Kuu Ya Dodoma Kupinga Uamuzi Wa Bunge Kuwapa Adhabu Halima Mdee, Estar Bulaya Na John Mnyika Mdee, Mnyika Na Bulaya Wawashitaki Spika Na Mwanasheria Mkuu Hakuna kanuni inayosema Spika anao owezo wa kumfungia Mbunge siku saba. Haipo, bali anaingiza kanuni zake mwenyewe kutoka kichwani mwake.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2sOSjTt
via IFTTT


Mkude yuko tayari kujiunga na Yanga ikiwa watafika dau hiliโ€ฆ

Mkude yuko tayari kujiunga na Yanga ikiwa watafika dau hili…

UNAWEZA ukashituka kidogo ila habari ndiyo hivyo anaweza kusaini Yanga kwa milioni 70 tu, Mkude ambaye mara kadhaa amewahi kuhusishwa kuwaniwa na Yanga ameamua kuweka wazi kuwa atatua ndani ya kikosi cha Yanga kwa ajili ya kukitumikia msimu ujao kwa kutoa sharti moja kubwa ambalo ni klabu hiyo kumpatia shilingi milioni 70.
Mkude kwa sasa yuko huru kujiunga na timu yoyote baada ya mkataba wake na Simba kudaiwa kumalizika hivi karibuni, ikiwa ni mwisho wa mkataba wake wa shilingi milioni 60 aliosaini kuitumikia Simba miaka miwili iliyopita.
Akizungumza na Shaffihdauda.co.tz., kiungo huyo amesema atakuwa tayari kusaini mkataba na klabu ya Yanga kwa dau la kuanzia milioni 70 kwenda juu kutokana na kiwango alichonacho kwa sasa. Simba wamempa ofa ya milioni 40-50 ila yeye amekataa kwa kigezo kwamba mkataba unaoisha walimpa milioni 60 kwa sasa lazima dau lipande.
“Kwa upande wangu nipo tayari kutua Yanga kwa dau la kuanzia milioni 70 na kuendelea hadi shilingi milioni 150 na siwezi kusaini chini ya hapo, nipo tayari kutua katika timu yoyote kwa kiasi ambacho tutakubaliana kwa kuwa kiwango changu kipo vizuri.
Nahodha huyo wa Simba amesema lolote linaweza kutokea kuanzia sasa: “Tusubiri kila kitu kitakuwa wazi muda si mrefu na wadau watajua nitasaini wapi kwa ajili ya msimu ujao, wasiwe na hofu.”
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2sqnc0L
via IFTTT


Kwa mara ya kwanza, bosi wa PSG azungumzia kuhusu taarifa za kumtaka Wenger

Kwa mara ya kwanza, bosi wa PSG azungumzia kuhusu taarifa za kumtaka Wenger

Hali ya kocha Arsene Wenger pamoja na kuipandisha timu hiyo hadi nafasi ya tano lakini bado si nzuri, huenda siku za mwisho za Wenger zimekaribia hata isiwe ndani ya mwezi huu au ujao lakini mwisho umekaribia.
Tayari imeelezwa vilabu mbali mbali vimeanza kufuatilia sakata la Wenger na Arsenal kwa ukaribu zaidi. PSG, Real Madrid, Barcelona na baadhi ya timu za nchini China zimekuwa zikimtaka Mfaransa huyo.
Lakini PSG wamekuwa wakitajwa sana na kupewa nafasi kubwa kutoka na kwamba Wenger ni mzaliwa wa Ufaransa huenda angevutiwa na kurudi nyumbani kufundisha soka.
Sasa mkurugenzi wa PSG ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa Barcelona Patrick Kluivert ameibuka na kuongelea suala hilo, Kluivert amesema habari hizo sio za kweli na zipuuzwe.
“Wenger kuja PSG?huo ni uongo na kuna asilimia sifuri ya hilo kutokea” alisema Kluivert, hiyo itakuwa imevunja minong’ono kuhush kocha huyo na PSG na sasa Real Madrid na Barcelona watakuwa ndio wanaoongelewa tu.
Keleleza kumpinga Wenger bado zinaendelea, japo ushindi wa bao 3 kwa 0 dhidi ya West Ham kidoogo.umeshusha presha kwa mashabiki wa klabu hiyo.

from Blogger http://ift.tt/2oPWXw6
via IFTTT


Kategori

Kategori