Showing posts with label KUSINI. Show all posts
Showing posts with label KUSINI. Show all posts

Mtwara yapiga hatua upatikanaji wa maji safi na salama

 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendegu akiwakaribisha wajumbe wa Kamati Ndogo ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji iliyowasili mkoani humo kukagua miradi ya maji.
 Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Amina Makilagi akieleza lengo la ziara ya kamati hiyo mkoani Mtwara.
 Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Amina Makilagi, akizungumza na wanahabari kuhusu ziara ya kamati hiyo ambayo inahitimishwa leo wilayani Masasi mkoni Mtwara.
 Mhandisi wa Maji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara John Msengi akiwasilisha taarifa ya mradi wa maji wa Nanyamba kwa wajumbe wa Kamati Ndogo ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji iliyotembelea kukagua mradi huo.
 Mwenyekiti wa kijiji cha  Kibaoni kinachohudumiwa na Mradi wa Maji wa Nanyamba, Issa Bakari     akieleza jambo kwa wajumbe wa Kamati Ndogo ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji iliyotembelea kukagua mradi huo.
 Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Amina Makilagi akipanda ngazi za tanki la maji la mradi wa Maji wa Nanyamba.
 Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Amina Makilagi akivuka kidaraja kuelekea kukagua tanki lingine la maji la mradi wa Maji wa Nanyamba.
 Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Amina Makilagi akikagua kisima cha maji ya mradi wa Maji wa Nanyamba.
 Afisa Mtendaji wa Mamlaka ya Mji wa Nanyamba, akitoa ufafanuzi kuhusu kisima cha mradi wa Maji wa Nanyamba.
 Msafara wa Kamati Ndogo ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ukiwasili kwenye ofisi za wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara kukagua mradi wa Maji wa Matogoro.

 Mhandisi wa Maji Peter Malekia (katikati) akieleza jambo kwa Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Amina Makilagi na wataalamu wa Wizara ya Maji wakiwa chini ya tanki la maji la Mradi wa Maji wa Matogoro linaloweza kuhifadhi maji lita 100,000.
 Mhandisi wa Maji Peter Malekia, akieleza jambo kuhusu bomba la Mradi wa Maji wa Mteogoro wakati Kamati Ndogo ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ilipokuwa ikikagua miundombinu ya mradi huo.
 Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Amina Makilagi akionja maji ya bomba la maji ya Mradi wa Maji wa Matogoro.
 Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Amina Makilagi akimpongeza mwenyekiti wa Kamati ya Maji ya Mradi wa Maji wa Matogoro Mzee Mwanya Natanga Bwanaheri.

 Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Amina Makilagi akizungumza na viongozi wa kijiji cha Matogoro na Mradi wa maji baada ya kukagua mradi huo.
Bibi Rukia Maulana mkazi wa Matogoro, akieleza jambo kwa Kamati Ndogo ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji iliyotembelea mradi wa Maji wa Matogoro. Picha zote na Hussein Makame, MAELEZO
Mtwara, Wazazi waaswa kuendelea kujiandaa kuwapeleka watoto nshule

Mtwara, Wazazi waaswa kuendelea kujiandaa kuwapeleka watoto nshule

Wazazi na walezi wa wanafunzi waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2015 wilayani Tandahimba mkoani mtwara ambao kwasasa wamekosa vituo wametakiwa kuendelea na maandalizi ya watoto wao huku halmashauri ikijizatiti kujenga shule mbili za sekondari kwa ajili ya uchaguzi wa pili ifikapo mwezi februari mwakani.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa halmashauri ya Tandahimba Abdallah Njovu wakati wa maandalizi ya ujenzi wa shule mbili za mwaminaki iliyopo kata ya kitama na nandonde kata ya tandahimba kufuatia ufaulu mzuri uliyopelekea wilaya yake kushika nafasi ya kwanza kimkoa ambapo kati ya wanafunzi 3504 waliyofaulu wanafunzi 280 wamekosa vituo.

MAMA SALMA KIKWETE AFANYA MIKUTANO YA KAMPENI KATA ZA NACHINGWEA NA MINGOYO MKOANI LINDI

 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi anayewakilisha Wilaya ya Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akisalimiana na viongozi wa CCM Kata ya Nachingwea iliyoko mjini Lindi wakati alipotembelea tawini hapo kwa ajili ya kikao na viongozi wa kata hiyo juu ya ushiriki wa Chama cha Mapinduzi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, vjiji na vitongoji unaotarajiwa kufanyika tarehe 14.12.2014.
  Viongozi wa CCM Kata ya Nachingwea pamoja na wagombea uongozi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa wakiwa katika kikao na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa Mama Salma Kikwete (hayupo pichani)
  Viongozi wa CCM Kata ya Nachingwea pamoja na wagombea uongozi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa wakiwa katika kikao na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa Mama Salma Kikwete (hayupo pichani)
  Mjumbe wa NEC Taifa wa CCM na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishiriki katika shamrashamra na viongozi wa CCM Kata ya Nachingwea muda mfupi kabla ya kuzungumza na viongozi hao tarehe 6.12.2014.
 Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa  Chama Cha Mapinduzi, Mama Salma Kikwete akiwahutubia viongozi wa CCM Kata ya Nachingwea na wagombea wa chama hicho kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 14.12.2014.
 Mjumbe wa NEC Taifa ya Chama cha Mapinduzi na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia viongozi wa CCM Kata ya Mingoyo pamoja na wagombea uongozi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika tarehe 14.12.2014.
 Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM, Mama Salma Kikwete akimjulia hali mtoto mdogo aliyebebwa na mama yake wakati Mama Salma akiingia kwenye sehemu ya mkutano wa kampeni katika Kata ya Mingoyo huko Lindi tarehe 6.12.2014.
 Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya Chama Cha Mapinduzi Mama Salma Kikwete  akijumuika na viongozi mbalimbali wa Mkoa na wilaya ya Lindi mjini pamoja na wananchi wa Kata ya Mingoyo kucheza wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Mnazi Mmoja tarehe 6.12.2014.

 Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi Mama Salma Kikwete  akiwahutubia viongozi wa Kata ya Mingoyo pamoja na wananchi wa Mnazi Mmoja wakati wa mkutano wa kampeni ya uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 14,12.2014

PICHA NA  JOHN  LUKUWI. 
 Picha za ajali iliyoua wanafunzi watano Mtwara leo Jan 22 pamoja na taarifa kamili.

Picha za ajali iliyoua wanafunzi watano Mtwara leo Jan 22 pamoja na taarifa kamili.

IMG-20140122-WA0006Wanafunzi watano wa shule ya sekondari Mustafa Sabodo iliyopo nje kidogo ya mji wa Mtwara wamefariki Dunia na wengine 47 kujeruhiwa baada ya kugongwa na gari wakati  wakikimbia mchakamchaka mapema leo asubuhi.
Taarifa inasema kuwa gari hilo lenye namba za usajili T174 AED aina ya Mercides Benz lilikuwa likiendeshwa na Dereva Baraka Mgwegwe ambapo likiwa kwenye mwendo kasi liliacha njia na kuwagonga wanafunzi hao ambao walikuwa kandokando ya barabara wakikimbia mchakamchaka kurejea shuleni.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara Zelothe Steven na Mganga Mkuu wa hospital hiyo wamethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na amewataja wanafunzi waliopoteza maisha kwa ajali hiyo ni pamoja na Khairati Mohamed Said, Mwanahamisi Mohamed,Nasma Salum Mpunja, Hilda Matias Nguli na Farida Ally ambao wote wanasoma kidato cha kwanza katika shule hiyo.
Mpaka sasa hali za majeruhi 21  waliolazwa hospitalini hapo zinaendelea vizuri ukiondoa mmoja ambaye amehamishiwa katika hospitali ya mission Nyangao mkoani Lindi kwa matibabu Zaidi huku dereva aliyesababisha ajali hiyo akishikiliwa na polisi kusubiri sheria kufuata mkondo wake.
Dereva Baraka Mgwegwe ameongea na millardayo.com na kusema>>’Nimetoka nyumbani kwangu sa 10 na nusu alfajiri naelekea kumpeleka Mgonjwa Lindi  Hospital nilikuwa na ndugu zangu wawili na mgonjwa kwenye gari,tulipofika maeneo ya Pacha ya kwenda Mchuchu mbele yangu kulikua na lori imesimama na nyuma ya lori ndio kunasadikiwa kuwa kulikuwa na hao wanafunzi’
‘mimi nilikuwa nimejiandaa kupishana na hiyo lori na wanafunzi na wanafunzi nao wanaingia barabarani sehemu ambayo mimi nilikuwa najiandaa kupita mimi sikumuona mwanafunzi hata mmoja kilichotokea pale nikutokea kwa hiyo ajali ya kuwagonga hao wanafunzi baada ya kuwagonga nikaenda kusimama kama mita 20 kutoka eneo la tukio nikatafuta usafiri wa piki piki nikaja kituoni hapa’.
Hizi ni picha za gari iliyosababisha ajali hiyo.2
1
Hizi ni picha za baadhi ya wanafunzi waliolazwa hospital ya mkoa wa Mtwara kufuatia ajali hiyo.
IMG-20140122-WA0007
IMG-20140122-WA0009
IMG-20140122-WA0004
IMG-20140122-WA0002
Hii ni taarifa ya Jeshi la polisi Mkoa wa Mtwara.
 press2
002
Na Millard Ayo

Kategori

Kategori