Showing posts with label July 04. Show all posts
Showing posts with label July 04. Show all posts
MADUKA ya Supermarkets za Nakumatt Hali Tete..

MADUKA ya Supermarkets za Nakumatt Hali Tete..

Mamia ya wafanyakazi huenda wakakosa ajira Afrika Mashariki baada ya maduka ya jumla ya Nakumatt kuonekana kuwa hatarini.
Nakumatt iliyo na maduka nchini Kenya, Uganda, Tanzania na Rwanda inakabiliwa na changamoto za kulipa madeni yake, na sasa wadeni wake wanatishia kuweka mali ya Nakumatt kwenye mnada.
Kwa miaka kadhaa Nakumatt imejivunia kukidhi mahitaji yote ya wateja na kauli mbiu ya ‘You need it, we’ve got it’ (Unahitaji, Tunacho), lakini hivi karibuni hata bidhaa muhimu kama mkate zimekuwa nadra kupatikana kwenye rafu zake.
Wateja wa duka hilo la Jumla walitaka kutambua yanayojiri kwenye duka hilo kupitia mtandao baada ya kukosa bidhaa muhimu lakini wasimamizi wa maduka hayo wamekanusha madai kwamba huenda biashara yake ikaporomoka.
Pindu tu baada ya habari kuanza kuenea mitandaoni, ilianza kubainika wazi kuwa maduka hilo haliwezi tena kuwalipa wanaoyauzia bidhaa.
Nakumatt pia inadaiwa kushindwa kulipa kodi ya majumba ambayo yanatumiwa kwa maduka yake.
Wiki moja tu baada ya kufunga maduka matatu nchini Uganda, madalali wametwaa mali ya Nakumatt kwenye jumba moja la kibiashara viunganimwa jiji la Nairobi, kwa madai ya kutolipwa kodi ya takriban dola nusu milioni.
Aidha kampuni hiyo inakabiliwa na kesi nyingine ya kufilisika kwa kutolipa deni la zaidi ya dola laki saba, na kwa kuandika cheki hewa.
Serikali ya Kenya imeingilia kati majadiliano baina ya duka hilo na wadeni wake, ili kupata suluhisho litakalozuia kampuni hiyo kusambaratika, haswa kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika nchini Kenya mwezi Agosti.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2uldgn4
via IFTTT


Chid Benz Ageukia Kilimo

Chid Benz Ageukia Kilimo

Baada ya kukaa nje ya game la bongo fleva kwa muda, Rapa Chidi Benz amefunguka na kusema ameamua kujikita kwenye killimo akishirikiana na mama yake mzazi ili kuweza kujikimu kimaisha.
Leo akiwa kwenye dakika 10 za maangamizi kipindi cha Planet Bongo ndani ya East Afrca Radio Chidi amesema kwamba mama yake ni mtu wake wa kwanza kwenye kumpatia sapoti ndiyo maana anashirikiana naye katika kuwajibika kiuchumi.
“Kwa sasa najishughulisha na kilimo kwa sana. Mimi na mama yangu tuna mashamba huko Chanika kwa hiyo hichi kipindi nilichokaa nje ya ‘game’ kilimo kinaendeleza maisha yetu japokuwa mimi mkulima wa mjini’, alisema Chidi.
Aidha Chidi ameongeza kwamba :
“Lakini nina familia niliyoitengeneza kipindi nafanya vizuri kwenye game kwa hiyo siwezi nikafa na njaa wakati mimi nilikuwa nawalea na kuwasaidia pale walipokuwa wakinihitaji. Wasanii wengi wapo upande wangu hawakumbuki mabaya yangu wengi wanarudisha mawazo yao nyuma kwa mazuri yangu”,Chidi Benz aliongeza.
Hata hivyo rapa huyo kwa sasa amerudi na ngoma aliyomshirikisha Mkongwe Q- Chillah inayokwenda kwa jina la ‘muda’.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2uFD3pr
via IFTTT


Idris Sultan Apata Shavu la Kucheza Movie Hollywood Marekani

Idris Sultan Apata Shavu la Kucheza Movie Hollywood Marekani

Baada ya wiki ya mchakato wa usahili, Mshindi wa Big Brother Africa-Hotshots wa 2014, Idris Sultan ataonekana katika filamu ya ‘Ballin …On the Other Side of the World,’ itayoandaliwa nchini Marekani chini ya muongozaji Harvey White.
Muongozaji wa filamu hiyo aliwahi kufanya kazi na wasanii wenye majina makubwa akiwemo Chris Brown, Mariah Carey, Lady Gaga na Tamia.
Akiwa kama mhariri wa filamu, amehariri baadhi ya filamu kama vile ‘Think Like A Man 2,’ ‘The Wedding Ringer,’ na ‘King of the Dance Hall’ akishirikiana na Whoopi Goldberg.
Hadithi ya filamu hiyo imetungwa na Torino Von Jones, ambapo hadithi hiyo inamhusu kijana mdogo wa Kenya (Kunjani), ambaye wazazi wake ni waathirika wa uhalifu uliojaa vurugu.
Siku moja katika maeneo ya ya shule, kijana huyo aliye na umri wa miaka kumi na tatu aligunduliwa na padri wa Kimarekani ambaye alimwona akicheza mpira wa kikapu na akaamini ana uwezo mkubwa na anaweza kushirikia ligi ya NBA.
Wote wawili waliendelea na urafiki wao na padri huyo alianza kumpatia ushauri. (King) itaigizwa na Sultan, ana haiba kubwa,lakini ni mhalifu mkubwa na hatari sana ambaye ana wazo jingine na anataka Kunjani kujiunga na kundi lake la wahalifu na atafanya kila liwezekanalo ili mpango huo ufanikiwe.
Mara ya mwisho Sultan alionekana katika filamu ya Tanzania ‘Kiumeni,’ ambayo itaoneshwa katika tamasha lijalo la wiki ya filamu la Zanzibar (ZIFF) ambapo ‘Kiumeni’ itaoneshwa wakati wa Siku ya tamasha ya filamu za Kiswahili ya ZIFF Julai 14, na mtayarishaji na nyota wa filamu Ernest Napoleon.
Mapema mwaka huu, Napoleon aliweka historia wakati alipochaguliwa kuwa rais wa kampuni ya uzalishaji na usambazaji wa filamu ya Marekani ya D Street Media Group yenye makao yake jijini New York, pamoja na ofisi katika miji ya Berlin, Buenos Aires na Cape Town.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa D Street na mtayarishaji mtendaji Dexter Davis walimtambua Idris kutokana na kuiangalia filamu ya “Kiumeni’.
“Idris Sultan has what it takes to become an international star and our upcoming film ‘Ballin… On the Other Side of the World’ is a perfect fit. We’re considering Mr. Sultan for other movies as well, alisema Davis.
Kampuni hiyo ya filamu inaazimia kupiga picha sehemu za Marekani na Kenya na haitachelea kutafuta vipaji vingine kwa waigizaji wa Kenya na nchi nyingine za Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania pale inapolazimu.
Filamu hiyo imeandaliwa kwa bajeti ya Dola za Marekani milioni tano.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2ukTQ1P
via IFTTT


MAITI yaokotwa Bwawani

MAITI yaokotwa Bwawani

Mwili wa mtu ambaye hajafahamika umeokotwa katika bwawa la maji lililopo Mtaa wa Nkende Shuleni katika Halmashauri ya Mji wa Tarime.
Hili ni tukio la tatu la watu kuuawa kisha miili yao kutupwa kwenye mabwawa ya maji katika kipindi cha miezi sita iliyopita. Hivi karibuni, mwili wa kijana ambaye alikuwa dereva wa bodaboda ulikutwa ukiwa umetupwa katika eneo hilo hilo.
Kamanda wa Mkoa wa Polisi Tarime/Rorya, Henry Mwaibambe, amethibitisha kuokotwa kwa mwili huo na kubainisha kuwa Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi ili kuwabaini watu wanafanya mauaji hayo.
Chareles Kisege, ambaye ni mwenyekiti wa mtaa wa Nkende Shuleni na James Nyangai mwenyekiti wa mtaa wa Kimusi, wamesema matukio hayo yamezusha hofu miongoni mwa wananchi wanaoishi katika maeneo hayo.
Wamitaka serikali kuchukua hatua za haraka kuwadhibiti wauaji hao.
Licha juhudi za wananchi kutaka kuuopoa mwili huo, zoezi hilo limekuwa zito na gumu kutokana na kukosa zana.
Hata hivyo, mwenyekiti wa chama cha waendesha bodaboda wilayani hapa, Samwel Kegoye, amesema ingawa taarifa zinaonyesha kuwa mtu huyo aliyeuawa ni dereva wa bodaboda, wao badoi hawajapata taarifa hizo rasmi.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2tEZdvr
via IFTTT


Ni rahisi sana Sana Kwa Mwanandoa Aliyeajiriwa Hapa Mjini Kuchepuka, Hivi Ndivyo Wanavyofanya

Ni rahisi sana Sana Kwa Mwanandoa Aliyeajiriwa Hapa Mjini Kuchepuka, Hivi Ndivyo Wanavyofanya

Nina uzoefu kidogo na mambo ya kazi za ajira maofisini, nimefanya hivi kwa muda mrefu. Wakati flani nilifanya kazi katika ofisi zilizo katikati ya jiji, kule mitaa ya Posta jijini Dar es Salaam.
Ofisi nyingi za serikali na watu binafsi zinapatikana mitaa ile. Kutokana na sababu hiyo, kuna idadi kubwa pia ya migahawa, hoteli, mama ntilie, pub na kadhalika.
Kuna mambo mawili makubwa yenye ushawishi mkubwa wa usaliti. Ofa za chakula au vinywaji na usafiri. Kwa kawaida, wafanyakazi wa ofisi moja hupenda kutoka pamoja wakati wa chakula cha mchana, wenyewe tunapendelea zaidi kusema lunch!
Kila mmoja ana sehemu yake anayokula kulingana na kipato chake, wapo wanaokwenda Southern Sun kupata chakula cha mchana, na wapo wanaowafuata mama ntilie wanaojibanza kwenye vichochoro vingi vilivyopo mjini.
Huko ndiko tunakokutana na akina dada waliovalia vizuri na kupendeza, wakitokea katika maofisi mbalimbali, huwezi kujua yupi ni mhudumu wa chai, yupi ni bosi, wote wanang’ara. Na hapa ndipo ofa za misosi zinapoanza kushawishi ngono.
Kijana mmoja mwenye kipato kikubwa ofisini kwake, atavutiwa na msichana mrembo mwenye mshahara wa wastani. Ili kumsogeza karibu, atalipia chakula cha siku hiyo na kumualika kwa kesho yake. Kulipiwa chakula ni jambo dogo, lakini lenye thamani kubwa sana. Si rahisi mtu aliyekulipia chakula kwa nia njema, ukaacha kumshukuru na hata kumwelekeza unapofanya kazi.
“Mimi nipo pale Oj Traders,” msichana anaweza kujita mbulisha jina na kusema anapofanyia kazi huku mkaka akimweleza kuwa yeye ni mhasibu katika ofisi flani. Watakapo
kutana mara ya pili, wataachiana namba za simu.
Baada ya hapo, mkaka atafanya mbwembwe za kuhamahama maeneo ya lunch ili mradi tu mdada wa watu aingie kwenye laini. 
Ukimaliza suala la lunch, kuna hii kitu foleni, hasa kwa wakazi wa Dar es Salaam. Raha ya kufanya kazi katikati ya jiji inaingia shubiri kadiri jioni inavyozidi kusogea. Kuanzia saa kumi, ni vurugu katika vituo vya daladala na hasa wakati kama huu ambao bodaboda zimezuiliwa kuingia mjini.
Wenye magari binafsi ndiyo wakati wao wa kujidai, ingawa foleni inawakumba wote. Lakini ni afadhali ukiwa kwenye foleni ndani ya gari dogo, mko wawili kuliko foleni, umeshika bomba kwenye daladala.
Siyo rahisi kwa mdada kukataa lifti ya kijana mwenye gari. Na katika foleni ndefu, ni wazi kwamba hadi mwisho wa safari, watakuwa wameshabadilishana namba. Kwa msichana, kuwa na uhakika wa usafiri kila siku ni ukombozi.
Tusidanganyane, hakuna msichana ambaye hatajua kuwa lunch au usafiri anaopewa unahitaji malipo maalum, ambayo ni penzi. Hali hii haiko Dar tu, bali nchi nzima na pengine duniani kote.
Mwanamke aliyeajiriwa anakuwa katika mitihani mikubwa zaidi ya kusaliti ndoa au uhusiano wake, kwa sababu hata kama haitakuwa kwenye chakula au usafiri, bado watu anaokutana nao katika utendaji wake, wanaweza kumghasi. Fikiria anakutana na mabosi, marafiki wa mabosi wake, wafanya biashara, atapona kweli?
Hata hivyo, simaanishi kama tabia hii inawakumba waajiriwa wote, isipokuwa nadhani ni sehemu kubwa wanahusika!
By Mike Tee
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2uFRaeu
via IFTTT


MWANAMUZIKI Chid Benz Amshushia Mkwala Mzito Chin Beesโ€ฆ

MWANAMUZIKI Chid Benz Amshushia Mkwala Mzito Chin Bees…

Msanii wa hip hop Bongo, Chid Benz amemtaka msanii mwenzake Chin Bees kutafuta jina lingine.
Sababu ya Chid Benz kusema hivyo imetokana na majina yao kufanana, na kuongeza kuwa wote wanafanya muziki wa aina tofauti hivyo kulikuwa hakuna ulazima wa ufanya hivyo.
“Siku moja nimeona Shetta anamuangalia instagram nikamuuliza huyo ni nini?, akaniambia ni Chin Bees, nikamuuliza anafanya muziki gani, akaniambia Bongo Fleva!. Sisemi kwa ubaya ila sikuelewa ile style anayofanya yeye ni tofauti sana na mimi mtu mzima mwenye hit kama 32 najua nikiingia kwenye stage nachapa tu,” Chid Benz ameiambia Planet Bongo ya EA Radio na kuhoji.
“Huyo Chin Bees ana single hata saba kweli?, atafute jina lingine,” amemaliza kwa kusema.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2sI7dan
via IFTTT


Tuache siasa za kipuuzi puuzi- Zitto

Tuache siasa za kipuuzi puuzi- Zitto

Niseme jambo moja muhimu Sana. Miswada ya sheria za madini tunazopitisha wiki hii ni hatua za kimapinduzi na kiokombozi. Sio hatua ndogo. Ni hatua zenye maumivu. Hata hivyo tukiweka mikakati ya kukabili changamoto zitakazoanza kutukabili maumivu yatakuwa ya muda mfupi tu.
Hivyo, tusijidanganye kuwa kila kitu kitakuwa ‘ mswano ‘, la hasha. Kampuni za nje zinazoweka mitaji yao hapa Tanzania zitaacha kuweka mitaji na zingine zitaondoa mitaji yao. Uzalishaji wa Dhahabu utashuka na Kwa kuwa dhahabu inachangia 30% ya Fedha za kigeni tutatetereka kidogo upande wa urari wa biashara na hata shilingi yetu kushuka thamani.
Serikali inapaswa kuweka mikakati ya muda wa kati kukabiliana na changamoto hizi. Moja ya njia muhimu na yenye maana kubwa ni kuongeza mauzo nje kwenye sekta ya kilimo ( Korosho, Katani, Kahawa, Chai, Pamba). Pia mauzo nje ya bidhaa za viwanda. Uzalishaji wa Sukari na Mawese ghafi unapaswa kuongezeka ndani ya wa kati ili kuokoa matumizi ya fedha za kigeni kununua bidhaa hizo nje.
Tutashambuliwa Sana na propaganda za magazeti ya ubepari mamboleo ( neo liberal right wing media). Hivyo, viongozi wetu wa kisiasa WANAPASWA kuwa WAMOJA kwenye shabaha hata kama wanapingana kwenye njia. Vyombo vya habari vya ndani vinapaswa kuandaliwa kuelewa hali yetu na kuelewesha dunia.
Huu sio wakati wa siasa za kipuuzi puuzi, ni wakati wa Siasa za kiuongozi.
Tukisimama imara na pamoja Kwa ushirikiano tutavuka katika kujenga Uchumi shirikishi wenye kuzalisha ajira nyingi. Tukiendekeza kuzodoana, kutukanana, kugandamiza demokrasia na kukomoana, ninawaapia tutashindwa vita Hii.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2uFQ56p
via IFTTT


Picha 5 za Mbunge wa CCM Alivyotaka Kupigana na Wabunge wa CHADEMA Jana Bungeni

Picha 5 za Mbunge wa CCM Alivyotaka Kupigana na Wabunge wa CHADEMA Jana Bungeni

MBUNGE wa Viti Maalum (CCM) Juliana Shonza, jana alizua timbwili nje ya viwanja vya bunge na kunusurika kupigwa na wabunge wa upinzani kutokana na kuwatambia kwamba atahakikisha Mbunge wa Kawe, Halima Mdee ambaye yuko kifungoni anaendelea kusota huko.
Wabunge hao wa Chadema waliitwa Polisi kuhojiwa usiku wa kuamkia leo
Hapo chini ni picha za tukio hilo 
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2uFDtfP
via IFTTT


Good News: Ali Kiba Atangazwa Kuwa Mmiliki wa Kampuni ya Rockstar4000

Good News: Ali Kiba Atangazwa Kuwa Mmiliki wa Kampuni ya Rockstar4000

GOOD NEWS: #DirectorKiba ; 
Baada ya kufanya kazi na kampuni ya usimamizi wa kazi zake ya #Rockstar4000 kwa takribani miaka 6, usiku wa jana King Kiba alitangazwa rasmi kuwa sehemu ya wamiliki wa kampuni ya #Rockstar4000 Music Entertainment Co & Rockstar Television. 
Alikiba sasa anakuwa sehemu ya wasanii waliochini ya Rockstar4000 pia anakuwa Director of Music n Talents. 
Rockstar Television inajishughulisha na utengenezaji wa vipindi vya mastar tofauti kutoka nchi mbalimbali na kuvisambaza katika vituo vya Television vya kimataifa.
#MkurugenziAli #DirectorKiba
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2slME40
via IFTTT


KAULI โ€˜Tataโ€™ zamponza Halima Mdeeโ€ฆ.

KAULI ‘Tata’ zamponza Halima Mdee….

Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh.Ally Happi amegiza jeshi la polisi kumuweka ndani kwa saa 48 Mbunge wa Kawe Mh. Halima Mdee kwa kutoa kauli za kumkashifu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli.
Agizo hilo la Mkuu wa wilaya limekuja leo ikiwa ni siku moja tangu mbunge huyo atoe kauli ya kupingana na Rais John Magufuli kuhusu watoto wanaobeba mimba wasirudi shule aliyoitoa siku chache akiwa mkoani Pwani, huku yeye akimtaka rais afuate sheria na katiba za nchi na kwamba siyo kila kauli yake ni sheria.
Mh. Happi amesema “Mh. Mdee amemtaja kwa jina rais kwamba ana tabia za hovyo, na kwamba tabia zake za hovyo zimempelekea kuona kwamba maneno yake ndiyo sheria ya nchi. Pia amesema kwamba ipo siku rais ataagiza watanzania watembee vifua wazi yaani wanawake kwa wanaume. Nimeshtushwa sana”, amesema Mh. Happi .
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2tLZ5e6
via IFTTT


Kategori

Kategori