Showing posts with label 2017 at 06:32PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 06:32PM. Show all posts
TUNDU LISSU KUMPELEKA NDUGAI MAHAKAMA KUU
Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu amesema kuwa watakwenda mahakamani kupinga maamuzi ya kusimamishwa kwa wabunge wa CHADEMA, Esther Bulaya (Bunda) na Halima Mdee (Kawe) baada ya kupewa adhabu hiyo mwanzoni mwa wiki walipopatikana na hatia ya kudharau Mamlaka ya Spika wa Bunge.
Lissu amesema kuwa atakutana na wabunge hao waliosimamishwa na kuandaa hoja watakazopeleka Mahakama Kuu na kwamba uamuzi aliochukua Spika wa kuwafungia wabunge hao wa kutohudhuria vikao vya Bunge kwa miezi kumi ni makosa makubwa.
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai.
“Tunataka Mahakama ituambie kwenye ‘Judicial review’ je, Bunge linaweza kufuta ubunge wa Mbunge wake, kama wanavyotafsiri hawa akina Ndugai? Je, Bunge linaweza likatoa adhabu hata nje ya adhabu iliyopo kwenye kanuni? Je, Bunge lina uwezo wa kumuadhibu Mbunge bila kumpa fursa ya kujitetea kwenye Kamati na Bunge lenyewe?
Tutaomba Mahakama Kuu itupe tafsiri. Kwa vyovyote vile utaratibu huu hatutakubaliana nao. Tukienda hivi, hawa CCM wa Bungeni kuna siku wataamua Mbunge asiingie Bungeni kwa miaka mitano halafu wanasema Bunge lina mamlaka lisiingiliwe. Bunge haina mamlaka hayo.
Kuna kanuni za kutoa adhabu kwa Mbunge yeyote anayefanya kosa. Adhabu ya kumfungia Mbunge kwa miezi 10 haipo kwenye Kanuni za Bunge la Tanzania. Lakini kumekuwa na tabia na utamaduni, sasa inapofika wabunge wa upinzani wanapewa adhabu kubwa kubwa ambazo zipo nje kabisa ya utaratibu wa kanuni zilizopo,” alisema Lissu.
Amesema kuwa Sheria na kanuni za Bunge zinasema adhabu ya Mbunge ni kumfungia vikao 20 kwa maana ya siku na kwamba adhabu nyinginezo haiwezi ikawa kifungo cha siku 100 au miezi kumi. Pia alisema kuwa tafsiri nyengine ya kanuni hizo si kumzuia Mbunge kuhudhuria vikao 20, bali inaweza ikawa kumnyima Mbunge huyo mshahara wake, kuzuia bima yake ya afya na kumfutia posho ya jimbo.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!
from Blogger http://ift.tt/2rFqAn3
via IFTTT
BAD NEWS : Mzee A⸗a Kwenye Dirisha la Benki Baada ya Kukuta Hakuna Mshahara.
Mwanamume mmoja alifariki nje ya benki moja katika kaunti ya Garissa wakati akingojea pesa za malipo ya wazee, masikini na walemavu. Familia ya Hassan Haji Keinan 70 ilisema marehemu alikuwa amesafiri kutoka kijiji cha Mataarba kilichoko Hulugho ili kupokea malipo yake kutoka kwa benki. Mzee huyo anasemekana alipatwa na mshituko baada ya kuambiwa kuwa hakuwa katika orodha ya waliostahili kupokea fedha hizo ambazo zimekuwa zikitolewa na serikali ya Kenya.
Aidha, mzee huyo alikuwa akitarajia kupokea KSh 8,000 ambazo zilikuwa zimejilimbikiza kwa muda wa miezi minne. “ Wakati wake wa kuhudumiwa ulipotoka, keshia alimwambia kuwa jina lake halikuwa katika orodha ya waliostahili kupokea fedha hizo. Mzee huyo alianza kutokwa na jasho, akazirai na kuaga dunia alipokuwa akipelekwa hospitali kuu ya Garissa,” alisema mwanawe, Gurshed Hassan
from Blogger http://ift.tt/2sJpTa6
via IFTTT
Mghwira – Nimechoka ..2020 Namimi Nagombea Zangu Ubunge Tu..!!!
Aliyekuwa mgombea wa kiti cha Urais kupitia chama cha siasa ACT – Wazalendo, Anna Mghwira amedai Tanzania bado haina uchaguzi wa demokrasia huku akiweka wazi mpango wake wa kugombea ubunge katika uchaguzi ujao wa mwaka 2020 jimbo la Singida.
Mwanamama huyo ambaye alionyesha ujasiri mkubwa katika mbio za kuwania kiti cha Urais katika uchaguzi wa mwaka 2015, amesema hayo Jumatatu hii wakati akizungumza kupitia kipindi Cha Dakika 45 cha ITV.
“Siwazi siioni Tanzania ya uchaguzi ya mwaka 2020. Hatuna chaguzi za demokrasia bado. Pengine naweza kugombea nafasi ya ubunge jimbo la Singida mjini mwaka 2020,” alijibu Mama Anna Mghwira wakati akieleza mipango yake katika uchaguzi ujao.
Katika hatua nyingine Mama Anna aliishauri serikali kuwekeza katika kilimo ili kuiandaa Tanzania ya Viwanda.
“Hatuwezi kuwa na Tanzania ya viwanda bila ya kuboresha kilimo kwanza, Tunahitaji kuwa na Tanzania ya kilimo kwanza,” alimema.
from Blogger http://ift.tt/2oJdt1b
via IFTTT
Kashfa Faru John Kuwasomba Vigogo Wawili..!!!
KAMATI iliyoundwa kuchunguza utaratibu uliotumika kumhamisha Faru John kutoka Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Sasakwa Black Rhino Sanctuary iliyoko kwenye Hifadhi ya Grumeti Serengeti, imependekeza hatua za kinidhamu dhidi ya maofisa wawili wa serikali.
Kamati haikufafanua aina ya hatua ambazo zinapaswa kuchukuliwa kwa maofisa hao, lakini umakini uliopo katika serikali ya awamu ya tano unaashiria upo uwezekano mkubwa kwa maofisa hao kutumbuliwa.
Ingawa kamati hiyo iligundua kuwa Faru John alikufa kifo cha asili, imependekeza hatua za kinidhamu kwa sababu hakukuwa na kibali rasmi cha kumhamisha kwenda mazingira ambayo yalisababisha kifo chake.
Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyelle alitoa pendekezo hilo jana wakati akikabidhi ripoti hiyo kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa juu ya uchunguzi walioufanya kuhusu uhamishwaji na kifo cha mnyama Faru John.
Kamati hiyo imependekeza hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi ya Mkurugenzi wa Wanyamapori wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Profesa Alexander Songorwa na Daktari wa Shirika la Hifadhi la Taifa (Tanapa), Dk. Moris Kileo.
TAZAMA HARMORAPA ALIVYO TIMUA MBIO BAADA YA KUIONA BASTOLA
from Blogger http://ift.tt/2njvJfX
via IFTTT
Bandarini Dar: Rais Magufuli akamata kontena lenye magari 3 na Makontena 20 yenye Mchanga wa Madini
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 23 Machi, 2017 amefanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya Dar es Salaam kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa kwa nyakati tofauti juu ya kudhibiti udanganyifu wa mizigo inayoingia na kutoka nchini kupitia bandari hiyo ikiwemo usafirishaji wa mchanga wa madini kwenda nje ya nchi.
Katika ziara hiyo Mhe. Rais Magufuli ameshuhudia makontena 20 ya mchanga wenye madini kutoka kwenye migodi iliyopo kanda ya ziwa ambayo yamezuiliwa kusafirishwa nje ya nchi tangu alipotoa agizo la kupiga marufuku usafirishaji wa mchanga nje ya nchi tarehe 02 Machi, 2017.
Pamoja na kushuhudia makontena hayo, Mhe. Rais Magufuli amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP – Ernest Mangu na vyombo vingine vya dola kuhakikisha mchanga wa madini unashikiliwa popote ulipo, mpaka hapo uchunguzi wa kina utakapofanyika kubaini ukweli.
“Nataka niwaambie nchi yetu inachezewa mno, nimekuja kuyaona haya makontena kama yapo, na kweli nimeyaona, sasa utaratibu utakapokamilika nataka Watanzania na dunia nzima ione kilichomo humu ndani kama ni mchanga kweli ama dhahabu” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Akiwa bandarini hapo Mhe. Dkt. Magufuli pia ameshuhudia udanganyifu mwingine unaofanywa na wafanyabiashara wanaoagiza mizigo kutoka nje ya nchi baada ya kuoneshwa makontena ambayo nyaraka zinaonesha yamebeba mitumba ya nguo na viatu wakati ndani yake kila kontena moja limebeba magari matatu ya kifahari.
Maafisa wa bandari ya Dar es Salaam na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wamemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa kufuatia maelekezo aliyoyatoa ya kuhakikisha mizigo yote inakaguliwa kwa mitambo ya mionzi (Scanning Machines) wamefanikiwa kubaini udanganyifu mwingi unaofanywa na wafanyabiashara wanaoingiza nchini na kusafirisha nje ya nchi mizigo mbalimbali yakiwemo makontena 10 ambayo yamepatikana yakiwa na magari ya kifahari ilihali nyaraka zake zikionesha yana mitumba ya nguo na viatu.
Mhe. Rais Magufuli amewapongeza maafisa na wafanyakazi wa bandari ya Dar es Salaam na TRA kwa kazi nzuri wanayofanya kudhibiti upotevu wa fedha za umma bandarini hapo na amewataka kuendelea kutekeleza wajibu wao kwa uzalendo na kujiepusha na rushwa.
“Leo mmenifurahisha sana, ninawatia moyo endeleeni kuwakamata wote wanaofanya udanganyifu huu na muwachukulie hatua kali za kisheria, lakini msimuonee mtu na msipokee rushwa, tunataka watu wajifunze kuwa hapa sio shamba la bibi” amesisitiza Rais Magufuli.
Aidha, ametoa wito kwa vyombo vyote vinavyoshughulikia udhibiti wa mizigo inayoingia na kutoka kupitia bandari ya Dar es Salaam na bandari nyingine hapa nchini, kuendelea kushirikiana ili kukomesha vitendo vyote vya udanganyifu ambavyo vinasababisha nchi kupoteza mapato mengi.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
23 Machi, 2017
TAZAMA JAMAA HUYU ALIVYOKOSWA KOSWA NA KIFO KWA AJARI MTONI
from Blogger http://ift.tt/2nHkeT9
via IFTTT
Subscribe to:
Posts (Atom)
