Showing posts with label August 23. Show all posts
Showing posts with label August 23. Show all posts
SHULE 18 ZAFUNGIWA NA SERIKALI KIGAMBONI

SHULE 18 ZAFUNGIWA NA SERIKALI KIGAMBONI

Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni imeendesha zoezi la kufunga shule za msingi na awali ambazo hazina usajili katika manispaa hiyo.
Zoezi hilo limesimamiwa na Kaimu Afisa Elimu wa Manispaa ya Kigamboni, Mwalimu Mathew Komba pamoja na Wakaguzi wa Elimu katika manispaa hiyo.
Image result for WANAFUNZI
Katika zoezi la ukaguzi katika shule mbalimbali, mapungufu mbalimbali yalipatikana ambayo ni pamoja na shule kutokuwa na usajili,
madarasa machache, kutokuwa na vyoo kwa ajili ya wanafunzi na walimu ambapo baadhi ya shule zinatumia vyoo vya misikiti au wanafunzi kujisaidia kwenye vyoo vya jirani .
Katika siku ya kwanza ya ukaguzi huo, timu hiyo imezifunga shule 18 kati ya 58 zilizobainishwa kutokuwa na usajili katika kata za Kigamboni, Vijibweni na Tungu.
Kati ya shule zilizofungwa ni Malaika Nursery School, Kigamboni English Medium School, Patmos, Montecarlos, Riziki, Taqwa, Firdaus na Meck.
Aidha, uongozi wa Manispaa ya Kigamboni imewataka wazazi kutowapeleka watoto wao kwenye shule hizo mpaka hapo watakapokimilisha taratibu walizowekewa pamoja na kupata usajili.

from Blogger http://ift.tt/2wyc0Bq
via IFTTT


UKITAKA KUSTAAFU MAPEMA ZINGATIA MAMBO HAYA.

UKITAKA KUSTAAFU MAPEMA ZINGATIA MAMBO HAYA.

  • Watu wengi sana wanatamani kuwa na uwezo na uhakika wa kustaafu mapema, lakini ni wachache sana wanachukua hatua mahususi kuhakikisha wanalitimiza jambo hilo.
  • Ili uweze kustaafu mapema, mambo matatu yanahitajika: kipato cha uhakika, kuweka akiba na kuwekeza akiba yako.
  • Jambo la kuzingatia ili utimize lengo hili ni kufanya mambo hayo matatu yawe ndio kipaumbele chako maishani.
  • Vijana wanajulikana kwa kuwa na tabia ya kutopenda kufata sheria, na linapokuja swala la matumizi ya pesa zao wanazozipata kwa jasho lao – wengi zaidi huwa hawataki hata ushauri kabisa.

    Lakini uwezekano wa kustaafu mapema unaweza kuwafanya wengi washawishike kuachana na ubishi wao na kufikiria uhakika wa maisha yao ya uzeeni na kuanza kuchukua hatua za uhakika kuyanyoosha wangali bado vijana na wenye nguvu za kufanya kazi.

    Image result for GRAND PARENTS

    Zifuatazo ni njia hizo na jinsi ya kufanya:

    1. Tengeneza chanzo imara cha mapato
    Kama huna chanzo cha mapato, hutakuwa na nafasi hata ya kuanza kujenga utajiri. Hatua ya kwanza kabisa ya kuhakikisha unapata uhuru wa kipato ni kuwa na chanzo cha uhakika cha kipato ili uwe na uhakika kwamba kutokana na kipato hicho, unaweza kuweka akiba pamoja na kuwekeza kwa ajili ya maisha ya baadaye.

    Kwa baadhi ya watu, hii yaweza kumaanisha ufanye kazi kwa ufanisi kwenye ajira yako ya sasa ili uweze kutimiza lengo hili. Ukiwa na chanzo cha uhakika cha mapato, hata ikiwa ni kutokana na kazi za mkataba au tenda za kulipwa kwa siku, bado unaweza kuweka mipango ya baadaye na kuanza kuitekeleza, japo kidogo kidogo.

    2. Weka akiba sehemu kubwa ya kipato hicho
    Ukishakuwa na kipato cha uhakika, jambo muhimu ni kuhakikisha kuwa hutumii pesa yote unayopata. Kujifunza jinsi ya kuishi maisha ya gharama nafuu chini ya kipato chako ni muhimu ili uweze kubaki na pesa (hasa ukianzia ujanani mwako) na uweze kujiwekea akiba itakayokusaidia kwa maisha yako yote yaliyobaki.

    kwanza, miongoni mwa njia rahisi zaidi za kuhakikisha utakuwa na fedha uzeeni mwako ni kujiunga na mfuko wa hifadhi za kijamii. Mifuko hii itakusaidia kutoa michango yako kila mwisho wa mwezi au kwa muda maalum na kuja kuipata utakapotimiza umri wako wa kustaafu. Kwa waajiriwa, michango hii huwa inakatwa moja kwa moja kutoka kwenye mshahara wako – kwahiyo huna haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu hilo – lakini kwa ambao hawajaajiriwa, unaweza kujiunga kwenye mifuko hii kama mtu binafsi, kwakuwa inaruhusiwa kufanya hivyo pia. Michango unayoiweka ni kiasi kidogo sana cha pesa kwa mwezi, lakini faida yake uzeeni ni kubwa.

    Pia, unaweza kupunguza matumizi yako ya pesa kwa kupunguza gharama za nyumba (kama umepanga) ili kodi yako kwa mwezi isizidi asilimia 30 ya kipato chako.

    3. Wekeza akiba yako kwenye vitega uchumi vitakavyoongezeka au kutopungua thamani
    Kuwa na pesa nyingi kwenye akiba yako ni jambo zuri, lakini unapoiwekeza pesa hiyo yaweza kusababisha tofauti kubwa sana kwenye safari yako ya kustaafu mapema.

    Kuna wanaoamua kuwekeza kwenye sekta ya majumba, na inaweza ukunufaisha kwakuwa una uwezekano wa kuingiza kipato cha kila mwezi kutokana na kodi za pango.

    Kwa wale wasiovutiwa na biashara ya majumba, unaweza kujifunza na kuwekeza kwa kununua hisa za makampuni mbalimbali ambayo yana rekodi nzuri ya ukuaji.

    Mwanzo wa safari ya mafanikio ya kuwa na uhuru wa kipato unaanza kwa uamuzi wako kwamba kufanya hivyo ni muhimu sana kwako. Kisha ukiwa unazingatia malengo yako, basi unaweza kutimiza kila unachokitaka bila wasiwasi.

from Blogger http://ift.tt/2vYuBW9
via IFTTT


ULIPAJI KODI YA ARDHI KWA SIMU ZA MKONONI WAANZISHWA NA SERIKALI

ULIPAJI KODI YA ARDHI KWA SIMU ZA MKONONI WAANZISHWA NA SERIKALI

Ili kujua unadaiwa kiasi gani cha kodi ya pango la ardhi kwa kutumia simu ya mkononi bonyeza *152*00# au kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi yaani SMS halafu unatuma kwenda namba 15200 na baada hapo unaweza kulipia kwa njia ya Mpesa, Tigo Pesa au kulipia tawi lolote la benki ya NMB na CRDB.
Image result for i phone
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ikishirikiana na Wizara ya Fedha, imesambaza maafisa wake katika Halmashauri 169 kote nchini kutoa mafunzo katika vituo vyote vya makusanyo ya kodi ya ardhi na tozo nyingine kwa kutumia simu ya mkononi ili kuondoa kabisa mfumo wa zamani wa malipo.
Zaidi ya maafisa 170 kutoka makao makuu ya Wizara ya Ardhi, Wizara ya Fedha na kutoka kanda nane za ardhi wameanza kutoa elimu hiyo katika Halmashauri na vituo vyote vya makusanyo ya kodi ya ardhi ili kurahisisha ulipaji kodi ya ardhi kwa wananchi kwa kutumia simu zao na kuondoa usumbufu.
Mfumo wa ulipaji kodi ya pango la ardhi kwa njia ya simu ya mkononi ni mfumo wa kielektroniki wa Government electronic Payment Gateway (GePG) katika makusanyo ya kodi ya pango la ardhi ambao utamrahisishia wananchi kulipia popote walipo kwa kutumia simu zao kwa urahisi zaidi.
Mwananchi yeyote anayemiliki kiwanja au shamba lililopimwa na kupatiwa hati, ataweza kutumia simu yake ya mkononi kujua kiasi cha kodi ya pango la ardhi anachodaiwa na kulipa kwa kutumia simu yake ya mkononi.
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanza rasmi kutumia mfumo huu wa kielektroniki wa GePG katika makusanyo ya kodi ya pango la ardhi pamoja na tozo nyingine zinazotokana na sekta ya ardhi nchini na kuondoa kabisa mfumo wa zamani.
Mfumo huu utamrahisishia mwananchi kulipa kodi ya pango la ardhi popote alipo, ikiwa ni pamoja na kulipia tozo nyingine mbalimbali za sekta ya ardhi. Mmiliki wa kipande cha ardhi ataweza kujua anadaiwa kiasi gani cha kodi ya pango la ardhi na kulipia popote alipo bila kusumbuka kufuata huduma hizo katika vituo vya makusanyo.
Kwa majaribio ya ukusanyaji kodi ya pango la ardhi kwa kutumia mfumo wa kielektroniki yalifanywa katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani na baada ya mafanikio makubwa kuonekana elimu ikatolewa kwa watendaji wote wa sekta ya ardhi katika Halmashauri zote za mkoa wa Dar es salaam kabla ya zoezi hilo kuhamishiwa mikoani.
Kwa zile huduma nyingine za sekta ya ardhi ambazo zinahusisha malipo kama vile upekuzi katika daftari la msajili (official search), mwananchi atapaswa kutembelea ofisi za Wizara ya ardhi zilizo katika eneo lake na kupatiwa makadirio ya kulipia huduma husika pamoja na namba ya malipo itakayomuwezesha kulipia aidha kwa njia ya benki au simu ya mkononi.
Kwa sasa kikosi kazi kinachotoa mafunzo juu ya matumizi ya mfumo huu kimeshaanza kuelemisha mikoa mingine baada ya kupata mafanikio mazuri katika mkoa wa Dar es Salaam. Lengo kubwa la kutumia mfumo huu ni kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa maduhuli ya serikali pamoja na kurahisisha ulipaji kodi ya pango la ardhi nchini.

from Blogger http://ift.tt/2xsNb6q
via IFTTT


MAABARA YA NYUKLIA YAANZA KUJENGWA NASERIKALI

MAABARA YA NYUKLIA YAANZA KUJENGWA NASERIKALI

Serikali imetenga shilingi bilioni 2.3 kwa ajili ya ujenzi wa maabara ya kisasa ya nyuklia katika Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC). Lengo la maabara hiyo ni kutoa huduma bora za kisasa za masuala ya mionzi kwa nchi za Afrika.
Aidha, vifaa vyenye thamani ya shilingi bilioni 11.5 kwa ajili ya maabara hiyo vilivyotolewa na Umoja wa Ulaya (EU) vimeanza kuwasili nchini na kuhifadhiwa kwenye maabara za tume hiyo.
Akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa maabara hiyo jana, Waziri wa Elimu, Sayansi, na teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako alisema shilingi bilioni 2.3 hizo zimetolewa na Serikali na zimetokana na fedha za ndani.
Alisema Serikali imetoa kwanza shilingi bilioni moja kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo linalotarajiwa kukamilika Februari mwakani. Kiasi kilichobaki cha shilingi bilioni 1.3 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo kitafuatia ili maabara hiyo ya kisasa iweze kutumiwa na watu mbalimbali nchini na Afrika nzima.
“Tunamshukuru Rais John Magufuli kwa kuwezesha,” alisema Profesa Ndalichako. “Maendeleo ya nchi yanasongwa hasa katika kuhakikisha tume hii inapata maendeleo na kuchangia fedha katika mfuko huu wa Serikali.”
Akizungumza katika hafla hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAEC, Brigedia Jenerali Fulgence Msafiri, alisema maabara hiyo itatoa huduma mbalimbali za matumizi salama ya mionzi pamoja na kuwa msaada kwa wanafunzi wa vyuo vikuu katika ngazi ya shahada ya Uzamili na uzamivu.
HT @ Nipashe

from Blogger http://ift.tt/2wnr704
via IFTTT


MAMLAKA YA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA YAVUNJWA NA RAIS MAGUFULI

MAMLAKA YA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA YAVUNJWA NA RAIS MAGUFULI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 23 Agosti, 2017 amemteua Luteni Kanali Frederick Felix Milanzi kuwa Kamishna wa Operesheni wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya.
Luteni Kanali Frederick Felix Milanzi anachukua nafasi ya Bw. Mihayo Msikela ambaye amerejeshwa Makao Makuu ya Polisi.
Uteuzi wa Luteni Kanali Frederick Felix Milanzi unaanza mara moja.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amezungumza na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa Kulevya Bw. Rogers William Siyanga ambaye amemhakikishia kuwa kazi ya kukabiliana na tatizo la biashara na matumizi ya dawa za kulevya inaendelea vizuri.

Bw. Rogers William Siyanga amesema tatizo la dawa za kulevya lilikuwa kubwa na ametaja dawa za kulevya ambazo Mamlaka inapambana nazo kuwa ni bangi, heroine, cocaine, kemikali bashirifu na kwamba kwa sasa imeanza kukamata na kuharibu mashamba ya bangi na bangi iliyovunwa.

Amebainisha mikakati mitatu inayotumika katika mapambano dhidi ya tatizo hilo kuwa ni kuzuia dawa za kulevya zisiingie nchini, kutoa elimu kuanzia shule za msingi, sekondari, vyuo na kwenye jamii ili watu waache kutumia dawa za kulevya na kutoa tiba kwa watu walioathirika na dawa za kulevya, na pia ametoa wito kwa watu wenye waathirika wa dawa za kulevya kuwapeleka katika mamlaka hiyo ili watibiwe.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

23 Agosti, 2017

from Blogger http://ift.tt/2ipaI5F
via IFTTT


Kategori

Kategori