Showing posts with label 2017 at 02:17PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 02:17PM. Show all posts
FAIDA SITA ZA KUOA MWANAMKE KAMA ZARI HASSAN

FAIDA SITA ZA KUOA MWANAMKE KAMA ZARI HASSAN

Mwanadada maarufu nchini Uganda, Zari Hassan, ambaye pia ni mfanyabiashara mkubwa na mzazi mwenza wa mwanamuziki Diamond Platnumz amekuwa akitajwa sana kwenye vyombo vya habari kuliko wanawake wengi, na mara nyingi kati ya hizo amekuwa akitajwa kwa ubaya.
Mwanadada huyu mwenye taswira ya utata amekuwa akitajwa kwenye vyombo vya habari vya nchini Uganda vikimuelezea kwa taswira kadhaa kama mrembo wa Uganda mwenye watoto watano, mtalaka wa milionea – Ivan Don Ssemwanga na sasa mzazi mwenza wa mmoja wa wanamuziki wanaolipwa pesa nyingi zaidi hapa Tanzania, Diamond Platnumz.
Shutuma nyingi anazopewa kwenye vyombo vya habari zimesababisha achukiwe na baadhi ya mashabiki zake na wakati huohuo kumuongezea mashabiki wapya wengi zaidi ya wanaomchukia. Japokuwa wengi, hasa mahasimu wake hawatakubali, Zari ni mwanamke ambaye kila mwanaume angependa kuwa naye.
Zifuatazo ni sababu 6 za kumfanya mwanaume atake kumuoa Zari wakati wowote:
1. Anajua kupika
Tunaanza na hili kwakuwa tofauti na wengi ambao wanaotengeneza kucha na kuosha mikono kwa bei ghali kama yeye wasingekubali kuingia jikoni kupika na badala yake wangetumua wafanyakazi wa ndani kwa ajili ya kazi hiyo. Mara mbili ameonekana kwenye mitandao ya kijamii akiwa jikoni akipika na hilo huwezi kuliona kwenye akaunti nyingi za ‘wanawake wa mjini.’
2. Ana uhusiano mzuri sana na wanae
Ingawa inaonekana anapitia mengi akiwa na mzazi mwenzie (Diamond), Zari amekuwa na uhusiano mzuri sana kati yake na watoto wake. Muda mwingi anakuwa nao na moja kati ya nyakati zilizodhihirisha hili ni katika mazishi ya mtalaka wake, Ivan. Hata wakati ambao Diamond alikuwa hajafika, alibaki kuwa imara kwa ajili ya wanae wakubwa.
3. Tukiongelea uimara alionao, tazama jinsi anavyokabiliana na maneno mengi yanayosemwa na mahasimu wa mapenzi kati yake na Diamond Platnumz
Hakumshambulia wala kumkosoa mpenzi wake huyo Diamond aliposema kwamba huwa anamtafuta akiwa na hamu ya kufanya mapenzi kwakuwa Zari si muaminifu. Pamoja na utoto huu aliofanya Diamond, ambao bila shaka Zari haupendi, bado ameweza kumsamehe na kuendelea maisha yao ya pamoja.
Kwa wengi, hili halikuchukuliwa kama ni uamuzi wa busara uliofanywa na mwanamke huyo, bali lilitafsiriwa kama anang’ang’ania mapenzi na Diamond, hata kama ananyanyaswa. Mbali na tafsiri zote zitazotolewa na mashabiki, uwezo wa mwanamke kusamehe jambo kama hilo kutoka kwa baba wa wanae linaonesha ungangari wa hali ya juu kabisa, hasa ukizingatia kwamba mambo mengi maishani mwake yalikuwa yanamuendea kombo, ikiwemo kifo cha mtalaka wake mwezi Mei.
4. Anajiweka kwenye mvuto wa hali ya juu siku zote, muda wote
Akiwa na umri wa miaka 35 na watoto watano, Zari bado ana muonekano wa kuvutia sana kana kwamba ni binti wa miaka ishirini. Amekuwa akiwatoa udenda wanaume wengi akiposti picha akiwa amevaa kivazi cha kuogelea kinachoweka wazi maumbile yake akiwa mapumzikoni, ikiwemo ya hivi karibuni alipokuwa mapumzikoni jijini Mombasa na mpenzi wake Diamond. Anafanya mazoezi, anakula vyakula sahihi na pia anawaambia mashabiki zake wa Instagram siri za urembo wake. Tuweke kando nguo za bei ghali anazovaa.
5. Kuhusu watoto, hajali kuhusu kujiwekea idadi wala uzazi wa mpango
Ukiacha watu maarufu nchini Kenya kama Julie Gichuru mwenye watoto wanne na Akothee mwenye watoto watano, Zari ni mtu pekee maarufu anayejulikana kwa kuzaa watoto wengi kwa urahisi. Kwa kuangalia picha zake tu, mtu yeyote anaweza kukubali kwamba Zari anapenda kuwa mama na jambo hilo ni nadra sana kulipata kwa wanawake kwenye tasnia ya sanaa na burudani.
6. Anaweza kusimamia vizuri biashara na miradi ya familia
Zari hapati tabu kabisa kubadili muonekano wake wa mvuto wa kimapenzi na kuvaa suti kuwa tayari kibiashara. Mtalaka wake Ivan Don alipofariki, Zari amepewa mamlaka yote kuhusu usimamizi wa mali za watoto wake na ameachiwa kuendesha biashara nyingi ambazo walikuwa wakizifanya kwa ubia. Kwa upande mwingine, Zari ameshaanza kuwekeza kwa ajili ya watoto wake wadogo kwani mpaka sasa mtoto wa mwisho ni balozi wa kampuni ya nguo za watoto. the difference: Zari is one of the few who chose not to let them define her.

from Blogger http://ift.tt/2hu9QMv
via IFTTT


Tukio Hili Linaweza Kuwa Ushahidi Kwamba Tukifa Tunarudi Duniani kwa Miili Mingine…!!!?

Tukio Hili Linaweza Kuwa Ushahidi Kwamba Tukifa Tunarudi Duniani kwa Miili Mingine…!!!?

Mtoto mmoja wa kiume huko India aliwahi kuwaacha hoi wazazi wake baada ya kuanza kudai aliwahi kuishi kabla ya kizaliwa
Mtoto huyo wa kiume, Taranjijt Singh anasema aliwahi kuishi miaka michache nyuma, ambapo alifariki kwa ajali ya pikipiki akiwa bado mdogo.
Mtoto huyo akiwa na umri wa miaka miwili alianza kusema kuhusu maisha yake ya nyuma na alikuwa akitoroka sana nyumbani . Alikuwa akiwaambia wazazi wake kwamba anakumbuka kijiji alichokuwa akiishi na hata jina la shule aliyokuwa akisoma.
Alikumbuka pia jina la baba yake wa zamani {kabla hajafa}. Awali ilionekana kama aina fulani ya kisirani cha mtoto, lakini ilibidi wazazi wake waanze kuwa na wasiwasi kwa kadiri alivyokuwa akiongezeka kiumri.
Mtoto huyo alikumbuka pia siku aliyokufa . Aliwaambia wazazi wake kwamba, alikufa September 10,1992. Alikufa baada ya kugongwa na pikipiki wakati akiwa kwenye baiskeli akiwa anakwenda shuleni asubuhi. Baada ya ajali hiyo alipata majeraha kichwani na alifariki siku ya pili baada ya ajali.
Baba yake wa sasa hivi, Ranjit Singh, anasema, mtoto wake alipozidi kusisitiza kuhusu maisha yake ya zamani, waliamua na mkewe kumpeleka huko kijijini anakodai kwamba, ndiko alikoishi kabla hajafa. Awali hawakuweza kumpata mtu ambaye alikuwa anafanana na maelezo ya mtoto huyu. Mkazi mmoja wa kijiji hicho aliwaomba waende kijiji cha jirani kinachofuata.
Kwenye kijiji hicho walikwenda kwenye shule ya kijiji ambapo mwalimu mkuu wa shule hiyo alithibitisha kamba, September 10, 1992 alikufa mwanafunzi wa shule hiyo kwa ajali ya pikipiki. Kupitia shuleni hapo, walibaini mahali wazazi wa mtoto yule aliyekufa kwa ajali ya pikipiki, walipokuwa wakiishi.
Ni kweli waliwakuta wazazi ambao walithibitisha kufiwa na mtoto katika tarehe na njia iliyoelezwa. Baba wa sasa wa mtoto huyu, Tanjit Singh alieleza kwamba, mtoto wao aliwaambia kwamba madaftari aliyokuwa nayo wakati wa ajali yalilowa damu baada ya ajali ile na alitaja kiwango cha fedha ambazo zilikuwa kwenye mkoba wake wa shule.
Mama wa zamani wa mtoto huyu ambaye kwa maana hiyo ni mama wa mtoto aliyefariki mwaka 1992 aliposikia hivyo aliangua kilio kikubwa , kwani maelezo hayo yalikuwa sahihi bila doa la kosa. Alisema vitabu na fedha hizo bado vipo, kwani aliviweka kwa kumbukumbu ya kifo cha mwanaye .
Baadae mtoto huyu alirudi na wazazi wake wa sasa nyumbani kukiwa na maswali yasiyo na majibu. Wazazi wake wa zamani pamoja na ndugu zake, walikwenda kumtembelea kwao baadae. Mtoto huyu aliibaini picha ya siku ya ndoa ya wazazi wake, ambayo walikuja nayo wakati walipokwenda kumtembelea kwa wazazi wake wapya.
Awali mwanasayansi, Vikram Chauhan, alikataa kukubaliana na maelezo kuhusu mtoto huyu , lakini baadae alijipa moyo wa kuanza uchunguzi. Alitembelea vijiji vyote viwili , cha zamani alikozaliwa na kufa na hiki cha sasa alipozaliwa.
Alizungumza na wazazi wote na kupata maelezo ambayo yalimfanya kuona kuna jambo la maana kuhusiana na kifo na ‘kufufuka’ kwa mtoto huyu. Kwenye kijiji alichozaliwa na kufa mtoto huyu, muuza duka mmoja alikiri kwamba ni kweli , mtoto kama huyo alikuwepo na yeye alimkopesha madaftari jana yake na alipogongwa alikuwa akielekea dukani kwake kumlipa madaftari hayo.
Chauhan alichukua sampuli ya mwandiko wa mtoto huyu na ule wa kwenye madaftari ya marehemu. Ilipokwenda kupimwa na wataalamu wa mwandiko, ilibainika kwamba, ilikuwa ni ya mtu mmoja.
Kumbuka kwamba mwandiko wangu hauwezi kuwa sawa na wa mtu yeyote, kama ilivyo alama za vidole. Kila mwandiko una sifa zake maalum ambazo haziwezi kupatikana kwenye mwandiko wa mtu mwingine.
Wataalamu wana uwezo wa kubaini mwandiko wa kughushi hata kama umefanywa na mtaalamu wa kiasi gani wa kughushi miandiko.
Kubwa zaidi ni kwamba mtoto huyu ambaye alishaanza kusoma kwenye maisha yake ya kabla ya kifo, hivi sasa hajapelekwa shule, kwa sababu familia yake ya sasa ni maskini. Hata hivyo katika jambo la kushangaza zaidi alipotakiwa kuandika alifabeti za kiingereza na ki-punjabi aliweza kufanya hivyo bila tatizo. Kama hajasoma ingewezekana vipi kufanya hivyo? Anatumia akili ya zamani ya kabla hajafa.
Familia yake ya zamani imeomba kukabidhiwa mtoto wao, lakini familia yake ya sasa imesema hapana, huyo ni mtoto wao. Kisheria, bila shaka, familia yake ya sasa ambayo ni maskini sana, wakati ile ya zamani ilikuwa na uwezo, ndiyo yenye uhalali wa kuishi na mtoto huyu.
Huenda baada ya sayansi kuthibitisha kwamba watu hufa na baadae kurudi wakiwa wanamiliki miilia tofauti, familia kama hii ya zamani ya mtoto huyu, ndipo itakapoweza kupata haki.
Hata hivyo, bila shaka kila familia kati ya hizo mbili, itakayoishi naye, itakuwa na mashaka ya aina fulani.
Ni vigumu kupingana na maelezo ya mtoto huyu, ambaye tangu akiwa na umri wa miaka miwili, alikuwa akizungumzia kuhusu kumbukumbu alizonazo juu ya maisha yake ya nyuma. Ugumu wa kupinga unatokana na ukweli kwamba, hatimaye maelezo yake yalithibika
Jambo hili linathibitisha maisha baada ya kifo
Lakini sio maisha baada ya kifo peke yake bali pia kukubali kwamba huenda binadamu ataendelea kuwepo, kwa sababu uwepo {being} haujapotea na hauwezi kupotea. Mwili wako utaharibika, lakini uwepo wa binadamu hauwezi kupotea.
Karibuni kwa maoni ndugu zangu woote!
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2rOFLuw
via IFTTT


Alichokisema Mwigulu Nchemba Baada ya Kufika Eneo Walipouawa Askari Nane na Majambazi..!!!

Alichokisema Mwigulu Nchemba Baada ya Kufika Eneo Walipouawa Askari Nane na Majambazi..!!!

WAZIRI wa mambo ya ndani ya nchi,Mwigulu Nchemba,amesema hawatokubaliana na mtandao,kundi ama mtu anaehusika na kugharimu maisha ya askari ama wananchi wasio na hatia.
Aidha amebainisha kwamba kilichombele kwa sasa ,wanaendelea kuhakikisha kuwa wanarudisha silaha zinazochukuliwa katika matukio mbalimbali ya mauaji ya askari na kuendelea na mapambano na wahalifu hao.
Nchemba ameyasema hayo jana ,wilayani Kibiti,mkoani Pwani,na kumtaka mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoani Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo kupambana na matukio ya mauaji yanayoendelea katika baadhi ya wilaya mkoani hapo.
Waziri huyo wa mambo ya ndani ,alieleza kwamba,amepokea taarifa ya kuuwawa kwa askari nane wilayani Kibiti kwa mshituko mkubwa .
Nchemba aliwaomba watanzania kwa kipindi hiki wawe watulivu wakati jeshi la polisi likiendelea kukabiliana na mambo hayo.
“Hii ni changamoto kwa wizara ya mambo ya ndani kuanza upya kuboresha mbinu zake za ki intelensia zinazoendana na mazingira ya sasa kwa mahitaji ya sasa”alisema.
Alibainisha kwamba,ni ngumu kuingia akili kwa watu wachache kuuwa hovyo askari ambao ndio walinzi wa raia na mali zao
“Kuna jambo lipo nyuma limejificha ambalo mwisho wake umefika kwani hatutoweza kulifumbia macho”alisisitiza.
Nchemba aliomba jamii iendelee kulinda amani ya nchi na kuheshimu askari polisi ambao wapo kwa ajili ya kuwalinda katika usalama wao

from Blogger http://ift.tt/2plNKvP
via IFTTT


Kategori

Kategori