Showing posts with label burudani. Show all posts
Showing posts with label burudani. Show all posts
Muimbaji Janet Jackson,athibitisha ni mja mzito akiwa miaka 50

Muimbaji Janet Jackson,athibitisha ni mja mzito akiwa miaka 50



Janet Jackson na Wissam Al ManaImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionJanet Jackson ana mumewe, Wissam al-Mana wanatarajia kujifungua mtoto wao wa kwanza

Muimbaji Janet Jackson amethibitisha rasmi kwamba anatarajia kujifungua mtoto wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 50.
Ameliambia jarida la People: "Tunashukuru Mungu kwa baraka tuliyonayo", na akapigwa picha na tumbo lake linalozidi kuwa kubwa kudhihirisha uja uzito.
Fununu kuhusu uja uzito wake zilizuka Aprili alipojitokeza kuahirisha shughuli zake na tamasha la kimataifa 'Unbreakable' akisema anataka kupanga uzazi na mumewe Wissam al-Mana.
Ameonekana hivi karibuni London akinunua vitu katika duka la watoto.
Jarida la The People limenukuu duru iliyo karibu na familia ya Jackson aliyesema: "Ana furaha sana kuhusu uja uzito wake na anedelea vizuri sana. Ana raha kuhusu kila kitu."
Katika video iliowekwa kwenye Twitter mwezi April, amewaambia mashabiki wake kuwa ana ahirisha shughuli zake, kwasababu "kumekuwa na mabadiliko ya ghafla".

Janet Jacket katika video ya TwitterImage copyrightJANET JACKSON/@TWITTER
Image captionJanet Jackson alitangaza Aprili anaahirisha shughuli zake kupanga familia

"Nilidhani ni muhimu mujue kwanza. Mimi na mumewangu tunapanga familia yetu," alisema, na kuongeza: "Tafadhali iwapo munaweza, jaribu muelewa kuwa ni muhimu nifanye hivi kwa sasa."
Aliendelea kusema: "Ni lazima nipumzike, ni agizo la daktari."
Janet Jackson ni nani:

Janet Jackson (Mei 2010)Image copyrightPA

  • Janet Damita Jo Jackson alizaliwa Mei 16 1966 Gary, Indiana Marekani
  • Ni mdogo katika ndugu tisa na ni dadake muimbaji nyota Michael Jackson
  • Alitoa albamu yake ya kwanza Janet Jackson mnamo 1982
  • Ana albamu 11 ya hivi karibuni ikiwa ni Unbreakable, iliotolewa 2015
  • Ni mshindi mara 7 wa tuzo ya Grammy
  • Alianza taaluma yake kwa kushiriki katika kipindi cha televisheni The Jacksons mnamo 1976 na ameshiriki katika filamu kadhaa ikiwemo ya Tyler Perry 'Why Did I Get Married'
  • Muimbaji huyu ameolewa na mumewe wa tatu, Bilionea raia wa Qatari Wissam al-Mana, 2012.
Janet Jackson sio mwanamke maarufu wa kipekee kuzaa katika umri mkubwa.
Mshindi wa tuzo ya Oscar Halle Berry amezaa mtoto wake wa pili akiwa na miaka 47, miaka mitatu iliyopita.
Mkewe John Travolta, Kelly Preston amezaa mtoto wake wa tatu akiwa na miaka 48.

DIAMOND PLATINUMS AFICHUA MWIMBAJI WA BONGO AMBAYE ALIKUWA AKIMUIGA KABLA HAJATOKA


Diamond amesema wakati anaanza muziki, alikuwa anamuigiza Barnaba lakini baadaye akaja kupata njia yake mwenyewe.Alisema hivyo kujibu swali la anaonaje pale anapomsikia Harmonize akiimba kama yeye.
Akiongea kwenye kipindi cha The Base cha ITV, Diamond alisema, “Unajua katika muziki kila mtu ana role model wake. Mimi wakati naanza nilikuwa nawaangalia sana Ne-Yo na Usher Raymond na kwa hapa nyumbani nilikuwa namkopi sana Barnaba maAna ndIo msanii ambaye nilikuwa nampenda. Lakini baadaye nikaja kuwa kama mimi. Kwahiyo Harmonize naye ndio hivyo atakuja kuwa kama yeye tu na sidhani kama anaimba kama mimi,” alisisitiza.

Kwa muda mrefu, Harmonize amekuwa akilalamikiwa kwa kumgeza sana bosi wake huyo.

VIDEO: STAA WA NIGERIA, YCEE AUNGANA NA DJ MAPHORISA WA AFRIKA KUSINI KWENYE REMIX YA OMO ALHAJI

Msanii wa Hip-hop wa Nigeria, Ycee ameungana na mtayarishaji wa muziki na muimbaji wa Afrika Kusini, DJ Maphorisa kwenye remix ya wimbo wake unaofanya vizuri barani, ‘Omo Alhaji’.

Ikifanyika jijini Johannesburg, na kuongozwa na La Dupont Productions, remix ya wimbo huo inahusisha rap iliyoshiba na inayohitaji usikivu.

DJ Maphorisa amechanganya ladha ya kipekee ya Kusini kwenye mrindimo unaoungana vyema na mtindo wa Ycee na kuzalisha wimbo utakaofanya vizuri kwenye klabu, mtaani na hata kwenye redio. Remix hii ya Omo Alhaji, haina shaka itateka tena mawimbi ya redio na TV barani Afrika.

Ycee anasema, “Limekuwa jambo kubwa kufanya remix hii, kama msanii ninafurahi kujaribu muziki tofauti. Ulikuwa uzoefu mkubwa na wa kufurahia kufanya kazi na DJ Maphorisa. Ninaamini mashabiki watafurahia remix hii.”

KUHUSU YCEE

Akizaliwa kwa jina la Alejo Martin Oludemilade, tarehe 29, January 1993, Ycee ni msanii wa hip hop wa Nigeria na mshindi wa tuzo.  Amesainishwa kwenye lebo ya muziki ya TINNY ENTERTAINMENT. Alianza rasmi muziki Disemba 2012 kwa kuachia wimbo 'Smile on Me' uliotayarishwa na Jay Sleek, na zingine kama 'Pass Me' na 'Amen' akimshirikisha Mbryo.

Alikuja kujipatia umaarufu zaidi July 2015 baada ya kuachia wimbo 'Jagaban.' Jagaban ukaja kuwa miongoni mwa nyimbo kubwa zaidi kwa mwaka 2015/16 na kuja kuwa na remix nzito aliyomshirikisha staa wa YBNL, Olamide na video yake ikiongozwa na Director Q.

Wimbo huo ulimweka sehemu nzuri Ycee kama kinara wa hip hop ya kizazi kipya nchini Nigeria na hatimaye kumpa tuzo ya “Rookie Of The Year” kwenye tuzo za Headies, mwaka 2015.

Kutoka kwa wimbo ‘Omo Alhaji’, Disemba 2015, kulimpandisha zaidi Ycee kama mmoja wa wasanii wakali kabisa wa hip hop nchini Nigeria. Alikuja kuachia video ya wimbo huo iliyoongozwa na Director Q iliyofanyika Uingereza. Wimbo huo pamoja na video yake viligeuka wimbo wa taifa kwenye chati za redio za TV za Nigeria, kwenye klabu na hata mtaani huku ukiipa umaarufu sentesi: 'Who's your Daddy?

EP yake ya kwanza iliyopewa jina The First Wave itatoka Oktoba, 2016.

KUTAZAMA VIDEO HIYO FUATA LINK HIYO CHINI:


MITANDAO YA KIJAMII

NAPE AFUNGA RASMI TAMASHA LA NGOMA ZA UTAMADUNI LA TULIA 2016 RUNGWE LEO

 Kikundi cha Utamaduni cha Ikama kikitoa burudani wakati wa kufunga Tamasha la Utamaduni la Tulia Tradition Festival 2016 lililofanyika wilayani Rungwe mkoani Mbeya na kushirikisha vikundi vya ngoma 62.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ( wa pili kulia) akifurahia jambo na Naibu Spika Mhe. Tulia Ackson (kulia) wakati wa KUFUNGA Tamasha la Utamaduni la Tulia Tradition Festival 2016 liliofanyika wilayani Rungwe mkoani Mbeya  leo Oktoba 08,2016.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ( katikati) akicheza moja ya ngoma za kiutamaduni Wwakati wa kufunga Tamasha la Utamaduni la Tulia Tradition Festival 2016 liliofanyika wilayani Rungwe mkoani Mbeya  leo Oktoba 08,2016 kulia ni Naibu Spika Mhe. Tulia Ackson na kushoto ni Katibu Mtendaji BASATA Geodfrey Mngereza.


Na Kitengo cha Mawasiliano WHUSM -Mbeya

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye  amewashauri vijana kutumia ngoma za asili kujiajiri kwani ni fursa mojawapo ya ajira kwa sasa.

Ametoa ushauri huo leo Mjini Mbeya alipokuwa akifunga Tamasha la Utamaduni la Tulia Tradition Festival 2016 na kuwahimiza vijana kutosubiri kuajiriwa ikiwa wanaona wana uwezo wa kufanya kitu ambacho kitawasaidia kupata kipato na kuendesha maisha yao.

“Ngoma za asili ni chanzo cha ajira kwa vijana na sisi kama Serikali tutashirikiana na wadau wa Sanaa na Utamaduni ili kutengeneza ajira na kudumisha mila na desturi za nchi yetu” alisistiza Mhe. Nnauye.

Aidha kwa upande wake Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson amesema kuwa fursa pekee kwa vijana kujiajiri kupitia shughuli za Sanaa na Utamaduni kwani ndio sekta ambazo zimetoa ajira kwa vijana wengi duniani kwa sasa.

“Nawashauri vijana wa kitanzania kuangalia na upande huu wa Sanaa na Utamaduni kuna ajira pia na sisi tupo pamoja nao na tutawapa  ushirikiano ili wafikie malengo” alisema Mhe. Tulia.

Tamasha hili liliondaliwa na Naibu Spika Mhe.Tulia Ackson linafanyika kwa siku mbili na limeshirikisha vikundi vya ngoma za asili vipatavyo 62 kutoka mikoa mbalimbali nchini.

Rajab na Kithara Taarab Zanzibar walivyotumbuiza Jijini Washington

Kundi zima la Rajab and Kithara Taarab lenye kupiga mziki wa mahadhi ya mwambao kutoka Zanzibar, walipotumbuiza siku ya Jumanne Sept 6. ndani ya ukumbi wa The John F. Kennedy Center for the Performing Arts Jijini Washington.  Rajab and Kithara watakua hapa Marekani mwezi mzima wakitumbuiza States mbali mbali hapa Marekani. kwa ratiba zao bofya hapa  centerstageus.org
Mmoja wa waimbaji wa kundi zima la Rajab and Kithara,  Saada Nassor, akitumbuiza wimbo wa Chungu,  ndani ya ukumbi wa The John F. Kennedy Center for the Performing Arts  iliopo Jijini Washington. (Picha zote na swahilivilla.blogspot.com)
Saada Nassor, akionyesha pozi wakati anawatumbuzia Wamarekani.

Makame Faki  akitumbuiza wimbo wa "Salaam Aleikum"  
Makame Faki  akiimbaa wimbo wa "Salaam Aleikum"
Wataalamu wa upigaji wa vyombo vya mahadhi ya mwambao,  mpiga ngoma Foum Faki, (kushoto) akiwa na  mpiga bass kitaa,  Daudi Shahil, wakitumbuiza  wageni waalikwa 
Kundi zima la Rajab and Kithara Taarab,  Zanzibar walivyotumbuiza Jijini Washington 
 Mtaatam wa wa quanun Zanzibar ambae pia ni kiongozi wa kundi zima la  Rajab and Kithara, Rajab Suleiman akitambulisha kundi zima la Rajab and Kithara.  Picha  zaidi Bofya hapa

Baraka Da Prince afanya maamuzi ya kiutu uzima

Habari za uhakika zilizotufikia ni kwamba mwanamuziki wa bongo flava hapa nchini Baraka De Prince amemtambulisha rasmi mke wake mtarajiwa Najma kwa wazazi wake huko jiji Mwanza.

Hongera Baraka kwa maamuzi ya kiutu uzima.

MSANII PAM D ASTUKIA WANAUME KUMLEMAZA


 
Pam D


Binti ambaye sasa hakamatiki kwenye ulimwengu wa muziki Bongo, Pam D amefunguka kuwa, sasa hivi anasitisha kolabo na wasanii wa kiume akiwemo yule aliyemtoa, Mesen Selekta akidai kuwa amegundua wanamlemaza.
Akifungukia muziki anaofanya kwa sasa, Pam D alisema, anajua anacho kipaji na anaweza kusimama yeye kama yeye hivyo ni wakati wake sasa wa kutoa ngoma zake kali.

“Siwezi kukataa, Mesen kanipa sapoti kubwa sana mpaka kufikia hapa lakini sasa nimeona nisimame mimi kama mimi nione nitafika wapi, unajua wakati mwingine ukishirikisha sana wasanii waliokutangulia, hasa wanaume unajilemaza, kipaji chako kinashindwa kuonekana vizuri,” alisema Pam D.
Kwa sasa mwanadada huyo anaandaa ngoma yake mpya baada ya kufanya poa na traki zake zilizotangulia kama vile Popolipopo na Nimempata.

TBF yamtimua Zonga, Maluwe arithi mikoba


DAR ES SALAAM, TANZANIA
KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Salehe Zonga aliyekuwa amesimamishwa kwa madai ya kutumia madaraka vibaya mali za shirikisho hilo zikiwamo Sh. Milioni 15, ametoswa rasmi hivyo si kiongozi tena wa shirikisho hilo.

Januari mwaka huu, TBF ilitangaza kumsimamisha kiongozi huyo ili kupisha uchunguzi wa matumizi ya Sh. Milioni 38 zilizokuwamo kwenye akaunti ya shirikisho hilo.

Ilibainika kuwa Zonga alikuwa akizitumia kinyemela kwa matumizi binafsi, madai ambayo hadi sasa katibu huyo wa zamani ameyakana.

Makamu wa Rais wa TBF, Jaffar Hamisi, alisema bodi ilikutana juzi kujadili suala hilo na kufikia uamuzi wa kumsimamisha moja kwa moja na kumpa miezi mitatu kurejesha Sh. Milioni 15.6.

“Bodi imekaa juzi na kumtaka Zonga kurudisha Sh. Milioni 15.6 ndani ya miezi mitatu. Katika kikao hicho alikuwapo na aliendelea kukataa kuwa fedha hizo hakuzitumia,” alisema Jaffar.

Jaffar, aliongeza kuwa ikipita miezi mitatu bila kufanya hivyo, TBF itamfungulia mashtaka ya ubadhirifu wa fedha za shirikisho hilo.

Aidha, Bodi ilimteua Michael Maluwe kuwa Katibu Mkuu wa shirikisho hilo huku nafasi ya Katibu Msaidizi ikishikiliwa na Mwenze Kabinda, ambao majina yao yatapelekwa katika mkutano mkuu kupata baraka.


Tuesday, March 8, 2016

Mkwasa atangaza wachezaji 25 kuivaa Chad

DAR ES SALAAM, TANZANIA
Charles Boniface Mkwasa na Baraka Kizuguto Machi 8, 2016 
TIMU ya taifa ‘Taifa Stars’ imetangaza kikosi cha wachezaji 25 kitakachoivaa Chad katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza Michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON), jijini N’Djamena Machi 23 mwaka huu bila kuweka kambi kama ilivyozoeleka.

Aidha Taifa Stars itawakosa Mrisho Ngassa (Free State Stars, Afrika Kusini), Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (Yanga) na Aggrey Morris (Azam FC) kutokana na kuwa majeruhi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, kocha wa Taifa Stars Boniface Mkwasa, alisema amewaita kutokana na kuwa sawasawa kiakili na kimwili kwa ajili ya kuwakabili Chad wanaonolewa na nyota wa zamani wa Cameroon, Rigobert Song.

“Nimewaita kwa kuwa hatuna muda wa kufanya mazoezi, ni kupanda ndege tu kwenda kuivaa Chad, mchezaji majeruhi hana nafasi kwa sasa, isipokuwa uwezo tu na utayari wa kucheza mechi hii ambayo tunataka ushindi,” alisema Mkwasa.

Mkwasa alisisitiza, “Ligi Kuu ya Vodacom, michuano ya CAF (CL, CC) inachezwa wikiendi ya tarehe 18-20 Machi, hivyo wachezaji wote watakua na majukumu katika timu zao, muda wa kufanya mazoezi kwa pamoja kwa ajili ya mchezo huo hautakuwapo, ndio maana nasisitiza wachezaji niliowachagua wahakikishe wanajilinda wenyewe kwa kuwa fit wanapokuja kwenye safari ya mchezo huo wa Machi 23.”

Wachezaji walioitwa ni magolikipa Aishi Manula (Azam FC), Ally Mustapha (Yanga) na Shaban Kado (Mwadui FC), walinzi ni Juma Abdul, Haji Mwinyi, Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, David Mwantika (Azam FC) na Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ (Simba SC).

Viungo Himid Mao (Azam FC), Ismail Juma (JKU), Jonas Mkude, Said Ndemla, Mwinyi Kazimoto (Simba SC), Mohamed Ibrahim, Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar), Farid Mussa (Azam FC), Deus Kaseke (Young Africans).

Washambuliaji ni Nahodha Mbwana Samatta (KRC Genk), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe), John Bocco (Azam FC), Elias Maguri (Stand United), Jeremia Mgunda (Tanzania Prisons) na Ibrahim Hajibu (Simba SC).


Katika kundi G Tanzania ipo nafasi ya tatu ikiwa na alama moja huku Misri ikiwa na alama sita ikifuatiwa na Nigeria yenye alama nne huku Chad ikiwa haina alama. 
Baraka Kizuguto akizungumza jambo kabla ya Charles Mkwasa (kulia) hajatangaza kikosi Machi 8, 2016
Charles Mkwasa akitangaza kikosi cha wachezaji kuikabili Chad.

Kategori

Kategori