Showing posts with label Rais wa Nigeria augua. Show all posts
Showing posts with label Rais wa Nigeria augua. Show all posts

Boko Haram lateka kambi ya jeshi Nigeria

Wanajeshi wa serikali waliokuwa wakipiga doria katika mji wa Baga kabla ya Boko haram kuuteka pamoja na kambi ya kijeshi
Maafisa nchini Nigeria wanasema kuwa kundi la Boko Haram limeuteka mji na kambi moja ya kijeshi inayotumiwa na wanajeshi wa kimataifa wanaojaribu kukabiliana na wapiganaji hao.
Seneta wa Borno Kazkazini Maina Ma'aji Lawan,eneo la mji wa Baga amesema kuwa wanajeshi waliitoroka kambi yao baada ya kushambuliwa na Boko Haram jumamosi asubuhi.
Wakaazi wa Baga,ambao walitoroka kupitia maboti hadi taifa jirani la Chad,amesema kuwa raia wengi wameuawa na mji huo kuchomwa.
Wapiganaji wa Boko Haram tayari wanadhibiti eneo kubwa karibu na mji wa Baga,ambao hadi kufikia jumamosi ni miongoni mwa miji michache iliokuwa imesalia na serikali.
Nigeria: Soko la Nguo lashambuliwa

Nigeria: Soko la Nguo lashambuliwa

 

Wapiganaji wa Boko Haram ambao wamekuwa wakifanya mashambulizi ya mara kwa mara nchini Nigeria
Bomu limelipuka karibu na soko katika mji wa Kaskazini mjini mwa Nigeria.
Kwa mujibu wa maafisa wakuu wanasema bomu hilo lilipuka katika eneo ambako mizigo hupakiwa, katika soko la nguo la Kantini Kwari.
Taarifa za majeruhi bado hazijatolewa. Takriban watu 2,000 wameuawa katika mashambulizi yaliyofanywa na kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Boko Haram mwaka huu.
Mwezi jana zaidi ya watu 100 walifariki katika shambulizi lengine lililofanywa na kundi hilo wakati wa maombi katika msikiti mkubwa mjini Kano.
Mwandishi wa BBC Habiba Adamu anasema Kantin Kwari ni soko kubwa zaidi la nguo mjini Kano ambako watu kutoka nchi jirani na maeneo mengine ya nchi kuendeshea biashara zao.
Soko hilo daima huwa limejaa watu.
 Vijiji vyashambuliwa tena Nigeria

Vijiji vyashambuliwa tena Nigeria


Watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Boko Haram wameshambulia vijiji kadha na makanisa kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Shule ya Chibok ambapo wanafunzi wasichana walitekwa nyara ApriliWakaazi wa huko walisema kuwa watu wengi wameuwawa na nyumba nyingi zimeteketezwa.
Mashambulio yamefanywa karibu na mji wa Chibok, ambako wasichana wa shule zaidi ya 200 walitekwa nyara mwezi wa Aprili.
Mwandishi wa BBC Nigeria anasema katika kijiji kimoja cha Kautikari, wanamgambo wa kijiji walizidiwa nguvu walipojaribu kulinda kanisa.
Anasema jeshi halikuweza kufika katika vijiji hivyo vilioko mbali.
Rais wa Nigeria augua akiwa London

Rais wa Nigeria augua akiwa London

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan

Nigeria imesema rais Goodluck Jonathan ameugua akiwa London na ameshauriwa kupumzika kwa siku kadhaa.
Taarifa kutoka ofisi ya rais imesema bwana Jonathan alitakiwa kuhudhuria mkutano wa uwekezaji katika mji mkuu wa Uingereza Alhamis lakini hakuweza kushiriki.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa hali ya rais Jonathan si mbaya sana lakini imebidi tahadhari ichukuliwe na anapewa matibabu.

 Rais huyo wa Nigeria alifikisha umri wa miaka 56 wiki hii. Ameshika wadhifa wa urais wa Nigeria tangu mwaka 2010. Nchi hiyo ni maarufu kwa uzalishaji wa mafuta barani Afrika. 
Na VOAswahili

Kategori

Kategori