Showing posts with label UCHAGUZI MDOGO. Show all posts
Showing posts with label UCHAGUZI MDOGO. Show all posts

UCHAGUZI LUDEWA MWANZO MWISHO


 Baadhi ya wananchi walio jitokeza kupiga kura Siku ya Jumapili jimbo la Ludewa licha ya kuwa wachache
 Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Ludewa William Waziri akitangaza matokeo ya uchaguzi jimbo la Ludewa na kumtangaza mbunge mteuliwa Deo Ngalawa kuwa mbunge mteuliwa
 Deo Ngalawa akishangilia ushindi alioupata pembeni kulia ni mama wa Ngalawa akiungana na mwanae kushangilia ushindi
 Ilikuwa ni majira ya saa Mbili matokeo yakitangazwa cheti kinaonyeshwa kwa walio shuhutia matokeo yakitangazwa
Ngalawa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutangazwa na kuwataka wakazi wa jimbo hilo kuona makubwa kutoka kwake.
(picha ni kutoka Ludewa na Mnyalu)
stori yake tafadhari BOFYA HAPA

WANANCHI WA KATA YA SARANGA KUPIGA KURA JUMAPILI


 Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 
WANANCHI wa Kata ya Saranga Manispaa ya Kinondoni wametakiwa kujitokeza kupiga kura ya Diwani Novemba 15 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Mhandisi Mussa Natty amesema kuwa kufanya uchaguzi huo kunatokana na kuharibika kwa uchaguzi wa Oktoba 25 ulisababishwa na vurugu.

Amesema wananchi wanaotakiwa kupiga kura kwa kata hiyo ni wale waliojiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura.
Natty amesema waliojiandikisha katika daftari la wapiga kura  ni 58,611 ambao ndio wataoruhusiwa kutimiza haki yao ya kikatiba ya kupiga kura kwa diwani wanayemtaka kuongoza kata hiyo.

Amesema vituo vya kupiga vitafunguliwa majira ya saa moja asubuhi na kufungwa saa 10 jioni na baada ya hapo zoezi likiwa limekamilika la uhesabiaji kura atatangazwa mshindi katika uchaguzi huo.

Uchaguzi wa diwani katika kata hiyo ilitokana na vurugu kubwa ambazo zilianza majira ya 11:000 asubuhi ilifanywa na baadhi ya wasimamizi wa vituo na watu wasiojulikana katika cha kugawa vifaa eneo TANROAD Temboni.

Kura za maoni Ludewa Masanja aanguka awa wa sita kati ya saba

Matokeo ni kama ifuatavyo.

Wapigakura wakiopigakura   walikuwa 1193

Kura zilizoharibika ni 2
Kura halali ni 1991

Matokeo

Deogratius Ngalawa 537.

Philip Filikunjombe 501

James MGAYA 62

Zephania  chaula 38

Evaristo Mtitu  21

Jacob mpangala 3

Emanuel MGAYA  19

Wagombea watatu walijitoa Na hayo ndio matokeo halali  na msimamizi wa uchaguzi kwa siku hii ya Leo alikuwa ni Mh. Lucas nyanda katibu wa wazazi ccm mkoa wa njombe ambae amemtangaza MH, Deogratius Ngalawa kuwa ndiye aliyeongoza katika uchaguzi huu kwakupata jumla ya kura 537.

ZANZIBAR: MKUTANO WA KAMPENI CHAMA CHA ADC KISIMAMBAAZI KIEMBESAMAKIsamaki

CONTACT WITH ELIMTAA BLOG BY: CALL :+255 788 056115 EMAIL: furahanews1@gmail.com Facebook: www.facebook.com/elimtaa Twitter: www.twitter.com/@elimtaa "ANY TIME CALL US FOR ADVERTISEMENT, OR ANY NEWS YOU WANT APPEAR TO Elimtaa Blog" Elimtaa 'more news update your mind'




Mwenyekiti wa Chama cha ADC Mhe. Said Miraj akimnadi Mgombea wake kwa Wananchi wa Jimbo la Kiembesamaki wakati wa mkutano wao wa Kampeni ya Uchaguzi Mdogo wa jimbo hilo unaotarajiwa kufanyika mwazoni mwa mwezi wa Febuari. 
Mwenyekiti wa Chama cha ADC Taifa mHE. Said Miraj, akitowa Sera za Chama chake kwa Wananchi wa Kiembesamaki katika mkutano wake wa Kampeni katika viwanja vya Kisimambaazi. 
Kazi mojo tu, kumpigia Kura mgombea wa ADC  Mhe. Amani Ismail Rashid mgombea wa ADC ndivyo inavyoonekana Mwenyekiti wa ADC Taifa Mhe. Said Miraj akihutubia katika mkutano wa kampeni
.
Mgombea wa ADC jimbo la kiembesamaki akinadi sera za Chama chake wakati wa kuomba kura kwa Wananchi wa jimbo la kiembesamaki, akiwa katika mikutano yake ya kampeni ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki.  

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha ADC Mhe, Juma Sanani, akihutubia katika mkutano wa kampeni katika viwanja vya kisimambaazi kiembesamaki Zanzibar. 
MWENYEKITI wa Taifa wa Wanawake ADC, Ndg. Khadija Abdallah, akimuombea Kura mgombea wake kwa Wananchi wa Jimbo la Kiembesamaki, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya kisimambaazi kiembesamaki.
VIONGOZI wa Chama cha ADC, wakimsikiliza Mgombea wao Amani Ismail Rashid, akihutubia katika mkutano wa Kampeni ya Uchaguzi Mdogo wa jimbo la kiembesamaki mkutano uliofanyika katika viwanja vya Kisimambaazi   
WANACHAMA wa Chama cha ADC wakimshangilia Mgombea wao akiwahutubia na kuomba Kura kwa Wananchi wa kiembesamaki katika mkutano wa kampeni  uliofanyika katika viwanja vya kisimambaazi 










Na ZanziNews

Kategori

Kategori