Showing posts with label Pole na Pongezi. Show all posts
Showing posts with label Pole na Pongezi. Show all posts

IBADA YA KUMBUKUMBU YA MPENDWA BABA YETU GODFREY MNGODO COLUMBUS. OHIO





Familia ya Michael na Teddy pamoja na Mngodo wote, tunapenda kuwakaribisha ndugu, jamaa na marafiki zetu kwenye ibada maalumu ya shukurani, na kusherehekea maisha ya Marehemu Baba yetu Mzee GODFREY MBIU MNGODO, (pichani) itakayofanyika siku ya Jumamosi 10/31/2015 kuanzia saa kumi jioni hadi saa tatu usiku ..




Mahali ni:

35 E.STANTON AVE, 

COLUMBUS OH 43214. 




Karibuni sana na Mungu awabariki.




Kwa maelezo zaidi na maelekezo

Michael Godfrey Mngodo: 614 446 5565. Teresia Teddy Ngeleja Mngodo: 614 772 1591. Kwetukia Joseph Mngodo: 614 316 5092   Vickie Tungaraza: 614 288 8103
News Alert; Waziri Kigoda afariki dunia nchini India

News Alert; Waziri Kigoda afariki dunia nchini India


kigoda
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh Abdallah Kigoda (pichani) amefariki dunia jioni hii nchini India alikokuwa anapatiwa matibabu.
Taarifa za kifo cha Mh Kigoda ambaye pia alikuwa mbunge wa Handeni mkoani Tanga zimethibitishwa na ofisi ya Bunge jijini Dar es Salaam.
Mhe. Dkt. Kigoda alikwenda nchini India kwa matibabu tarehe 18 Septemba, 2015, kupata matibabu katika hospitali Hiyo ya Apollo. Taarifa zaidi kutolewa baadaye.
Modewji Blog inaungana na Familia ya Marehemu pamoja na Watanzania kwa ujumla katika kuomboleza kifo cha Dkt. Kigoda, Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Amen.

Mazishi ya Mch. Mtikila Mkoani Njombe, Tazama picha kumi za Mashada







Mgombea wa jimbo wa Ludewa mkoa wa Njombe Deo Filikunjombe, akiweka
taji la maua katika nyumba ya milele ya mch. Christopher Mtikila, jana
katika eneo la Milo wilayani Ludewa alikoziwa.


Mke wa Marehemu, Mch. Christopher Mtikila, Geogea Mtikila
akiweka taji la maua katika nyumba ya milele ya mch. Christopher
Mtikila, jana katika eneo la Milo wilayani Ludewa alikoziwa.


Mkuu wa mkoa wa Njombe, Dr. Rehema Nchimbi akiweka taji la maua katika
nyumba ya milele ya mch. Christopher Mtikila, jana katika eneo la Milo
wilayani Ludewa alikoziwa.


Msajili wa vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi akiweka taji la maua
katika nyumba ya milele ya mch. Christopher Mtikila, jana katika eneo
la Milo wilayani Ludewa alikoziwa.

TAMKO KUTOKA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA NCHINI NA VIDEO KIFO CHA MCHUNGAJI MTIKILA



Kufwatia kifo cha mwanasiasa mkongwe na mwanaharakati wa siasa za Tanzania ,Mwenyekiti wa chama cha DP mchungaji Cristopher Mtikila kilichotokea juzi kwa ajali ya Gari,baraza la vyama vya siasa nchini wametangaza kuahirishwa kwa kikao cha baraza kuu la vyama vya siasa nchini kilichokuwa kifanyike tarehe 6 na 7 mwezi wa kumi visiwani Zanzibar hadi  tarehe itakayopangwa tena baada ya maziko ya marehemu mchungaji MTIKILA.

Akizungumza na wanahabari Jijini Dar es salaam leo Mwenyekiti wa baraza la vyama vya siasa nchini Tanzania PETER KUGA MZIRAY amesema kuwa kamati ya uongozi ya baraza la vyama vya siasa kwa niaba ya baraza hilo wameshtushwa sana na kifo cha mwanasiasa huyo na wamekutana kwa dharura na kuamua kusogeza mbele kikao hicho ambacho kinatajwa kujadili mambo muhimu na nyeti kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

“Kifo cha mchungaji MTIKILA ni pengo kubwa sana katika siasa na democrasia ya vyama vingi nchini kwani amekuwa mdau mkubwa katika kudumisha na kuboresha mfumo wa siasa za nchi yetu na democrasia ya vyama vingi hapa nchini”amesema mziray.

Aidha baraza hilo limetoa salamu za rambi rambi na pole nyingi kwa wanafamilia ya marehemu wanachamawa DEMPCRATIC PARTY (DP) na ndugu na jamaa wote,na kuwataka wawe na moyo wa uvumilivu kwani kila mtu anaondoka duniani kwa namna na siku yake.
Mchungaji mtikila alifariki siku ya jumapili alfajiri katika ajali ya gari iliyoacha njia na kupinduka mkoani pwani wakati akiwa safarini kuelekea jijini Dar es salaam
Siku za mwisho za Mtikila.

Siku za mwisho za Mtikila.

Mchungaji Christopher Mtikila.
Mchungaji Christopher Mtikila, ambaye ni Mwenyekiti wa Democratic Party (DP), amefariki dunia baada ya gari lake alilokuwa akisafiria kupinduka eneo la Msolwa, Chalinze Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.
 
Kufikia jana asubuhi wakati taarifa za kifo cha Mtikila zikisambazwa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii, tayari Mchungaji huyo wa Kanisa la Salvation Army, alishafichua jambo zito alilokuwa nalo moyoni kuhusiana na uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu. Alifariki dunia baada ya gari alilokuwa akisafiria aina ya Toyota Corolla, T 189 AGM, kuacha njia na kupinduka saa 11:45 alfajiri jana.
 
Mtikila alifichua ya moyoni siku moja kabla ya kifo chake wakati akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea ubunge wa chama chake Jimbo la Njombe Kusini, William Myegeta.
 
Katika mkutano huo uliofanyika kwenye viwanja vya National Housing mjini Njombe, Mtikila aliwaambia wananchi kuwa anaamini atashinda rufaa dhidi ya kuenguliwa kwake na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa sababu hiyo, aliwataka Watanzania wasijisumbue kufikiria kuwapigia kura wagombea wa vyama vingine kwani hawana sifa na badala yake, wajiandae kumchagua yeye ili awe kinara wa ukombozi wa kweli wa Tanzania.   
 
Mtikila alisema kuwa ukiondoa yeye ambaye ana uhakika atarudishwa kugombea licha ya Nec kumuengua kutokana na kasoro zilizodaiwa kufanywa na mgombea mwenza wake, wagombea wote kutoka vyama vingine hawana sifa, wakiwamo Dk. John Magufuli anayepeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Edward Lowassa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) anayewakilisha pia vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vya NCCR-Mageuzi, NLD na Chama cha Wananchi (CUF).
 
“Wote waliosimamishwa kutaka kutuongoza hawataikomboa nchi yetu. Mniombee nifanikiwe rufaa yangu na nishinde... vinginevyo msipige kura ya urais. Pigeni kura za wabunge ambao mnawaamini ili baadaye uchaguzi urudiwe na mimi nikichukua fomu nina imani lazima nitashinda tu,” alisema marehemu Mtikila, siku moja kabla ya kifo chake.
 
Alisisitiza kuwa kwa namna yoyote ile, akishashinda rufaa yake siku ya uchaguzi itaahirishwa ili kutoa nafasi kwa yeye na chama chake kuwamo kwenye kinyang’anyiro hicho na hivyo, akawataka wajiandae kuwapigia kura wabunge na madiwani na kwamba, siku itakayopangwa kwa uchaguzi wa rais, yeye apigiwe kura nyingi ili asjinde kwa klishindo na kuleta ukombozi wa kweli kwa Watanganyika.
 
Kadhalika, Mtikila alizungumzia umuhimu wa kupimwa afya kwa kila mgombea wa nafasi ya urais kwani kufanya hivyo, ni utaratibu ulizoeleka kwa kila kazi inayoombwa na mtu na jambo hilo ni kwa manufaa ya taifa.
 
“Kazi yoyote unayoomba huwa ni lazima uende hospitalini kuchunguzwa afya kwa kuwa mtu ukiwa na ugonjwa wowote mwilini mwako huwezi kuongoza vizuri,” alisema. Aidha, alidai kuwa yeye hajazi watu katika mikutano yake kwa kuwa hawanunulii pombe aina ya viroba, lakini anaamini Watanzania waliopo katika mkutano wake wa Njombe ndiyo watakaosambaza taarifa za ukombozi kwa wale ambao hawakubahatika kuhudhuria mkutano huo.
 
Alisema mbali na kumpigia kampeni ubunge wa chama chake katika Jimbo la Njombe Kusini, pia atazunguka nchi nzima kufanya kazi hiyo kwani wamesimamisha wagombea wengi wa nafasi ya ubunge na udiwani, karibu katika kila upande wa nchi.
 
POLISI WAZUNGUMZIA AJALI 
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani, Ibrahim Jafarry, alisema gari alilokuwa akisafiria Mtikila lilikuwa katika mwendo wa kasi kubwa na kwamba baada ya kufika katika eneo la ajali liliacha njia na kupinduka. Alisema Mtikila alikuwa na abiria wengine wawili ndani ya gari hiyo pamoja na dereva. 
 
Hata hivyo, alisema wenzake wote walijeruhiwa na kukimbiziwa katika Hospitali Teule ya Tumbi, Kibaha. Kamanda Ibrahim aliwataja majeruhi kuwa ni dereva George Steven maarufu kama Ponera (31), mkazi wa Mbezi jijini Dar es Salaam na abiria wengine ni Mchungaji Patrick Mgaya (57), mkazi wa Dar es Salaam na Ally Mohamed (42), mkazi wa Mbezi Dar es Salaam.
 
Ilielezwa zaidi kuwa Mchungaji Mtikila alianza safari kutokea Njombe juzi saa 3:00 usiku baada ya kumalizika kwa mkutano wa kampeni.
 
Wakati huo huo, Mganga Mkuu wa Hospitali Teule ya Tumbi, Dk. Peter Dastan, aliiambia Nipashe kuwa hadi kufikia jana alasiri walikuwa bado wakiufanyia uchunguzi zaidi mwili wa marehemu Mtikila ili kubaini kwa kina sababu za kifo chake.
 
ENEO LA AJALI
Katika hatua nyingine, Kamanda Ibrahim alieleza kuwa kabla ya kifo chake, Mtikila alikuwa amekaa katika kiti cha mbele na kwamba gari hilo alilokuwa akisafiria halionyeshi kuwa ni la kwake bali alilikodi na mmiliki wake ni mkazi wa jijini Dar es Salaam.
 
Taarifa zaidi zimeeleza kuwa eneo la Msolwa alilopata ajali Mchungaji Mtikila na kufariki dunia siyo mara ya kwanza kushuhudiwa ajali mbaya kama ya jana na kusababisha vifo au majeruhi. 
 
Taarifa iliyothibitishwa na Kamanda Ibrahim ilieleza kuwa Februari 2013, eneo hilo liliwahi kukumbwa na ajali iliyohusisha vifo vya wanafunzi watatu wa shule ya sekondari na raia wengine waliokuwa wameomba msaada wa ‘lifti’ kwenye gari dogo aina ya Toyota Mark II kabla gari hilo lililowapakia kugongana uso kwa uso na lori aina ya Fuso na kusababisha vifo vya wanafunzi hao.
 
SALAMU ZA RAMBIRAMBI
Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazelendo, Samson Mwigamba, alisema wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mchungaji Mtikila kwani anaamini kuwa mchango wake ulikuwa unahitajika zaidi sasa katika wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu.
 
Mgombea ubunge wa DP Jimbo la Njombe Kusini, William Myegeta, amesema amepokea kwa masikitiko makubwa msiba huo na kuwa Chama na Taifa vimempoteza mtu muhimu kisiasa.
 
Katibu Mwenezi Taifa wa DP, Msambichaka Feruz, alisema chama kimepata pigo kwa kuondokewa na Mchungaji Mtikila na kwamba mambo yote aliyokuwa akiyapigania yataendelezwa.
 
Katibu wa NCCR-Mageuzi, Mosena Nyambabe, alisema kuwa chama chake kitamkumbuka Mchungaji Mtikila kutokana na harakati zake za mageuzi nchini tangu miaka ya 1990.
 
Mwenyekiti wa Chama cha Kijamii (CCK), Costantine Akitanda, alisema kuwa taifa limempoteza mzalendo wa kweli aliyesimamia kauli zake bila ya woga.
 
Alisema, marehemu Mchungaji Mtikila alikuwa na misimamo isiyoyumba hata pale wengine walipompinga na aliweza kuwasemea vyema Watanzania wenzako na kuonyesha uzalendo wa kweli.
 
Jana, majonzi yalitawala nyumbani kwa marehemu Mtikila, eneo la Mikocheni B jijini Dar es Salaam. 
 
Viongozi na watu kadhaa walionekana wakiwa na huzuni kubwa kutokana na taarifa za kifo cha kiongozi huyo.
 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, alisema amepokea kwa masikitiko na majonzi makubwa taarifa za kifo cha Mchungaji Mtikila.
 
Mbowe alisema kifo cha Mchungaji Mtikila kimeacha pengo kubwa katika siasa za mageuzi nchini hasa katika kupigania Tanganyika na suala la mgombea huru kuwa haki ya kikatiba nchini.
 
lImeandikwa na Magreth Malisa, Yasmine Protace, Furaha Eliab na Christina Mwakangale na Thobias Mwanakatwa.
SOURCE: NIPASHE

Marehemu.Mch. Mtikila Akiwa katika mkutano wake wa mwisho kabla ya Umauti na kuwataka Watanganyika kuto pigia kura Rais


Wakazi wa mkoa wa Njombe wakimsikiliza Mchungaji Mtikila Jana kabla hajaondoka mkoani humo na kupaja ajali leo Alfajili na kusababisha kifo chake. 

Mch. Christopher Mtikila Akizungumza wakazi wa mkoa wa njombe Jana kabla ya kukutwa na umauti Leo alfajili katika ajali mkoa wa Pwani baada ya gari aliyo kuwa akisafilia kupinduka

Mgombea ubunge kupitia DP William Myegeta Akinadiwa katika mkutano wa hadhara ulio kuwa na watu haba kabla ya Mwenyekiti wa chama hicho Mchungaji Mtikila Achafariki dunia Leo alfajili.(Picha na Mwandishi wa Elimtaa Njombe)
MWENYEKITI wa chama cha DP Mch. Christoper Mtikila siku moja kabla ya kifo chake aliwataka wakazi wa mkoa wa Njombe kuto chagua rais baada ya kuingia katika chuma cha Uchaguzi Octaba 25 mwaka huu kwa kuwa yeye wagombea uraisi wote walio simamishwa na vyama vingine hapa nchini anaona wanadosari.

Marehemu Mtikila Aliyasema hayo katika viwanja vya National Housing vya mjini Njombe wakati akizungumza na wakazi wa Njombe katika mkutano wa Kampeni za kuwanadi wagombea wa Chama chake cha Dp kwa ngazi za Ubunge na Udiwani.

 Mtikila alisema kuwa wagombea wote walio simamishwa kumpokea Rais Jakaya Kimwete wote anaona hawafai kuipokea Tanzania na kuwa hawana ukombozi wa kweli kwa watanzania.

"Wote walio simamishwa kutaka kutuongoza hata weza kuikomoa nchi yetu mniombee nifanikiwe rufaa yangu na mishine msipidge kura ya Rais pigeni kura za wabunge ambao mnawaamini ili uchaguzi urudiwe na mimi nikichukua fomu ninaimani nitashinda," alisema Marehemu Mtikila.

Aliwataka wakazi wa Njombe kuto pigia kura Rais Yoyote siku ya uchaguzi kitu kitakacho sababisha uchaguzi kuahirishwa na mchakato kuanza upya na yeye kuingia katika kinyanganyilo cha kuusaka Urais na akishinda ataleta ukombozi wa kweli kwa watanganyika.

Alisema kazi yoyote mtu anayomba anaenda kuchunguwa kama ni mzima lakini fomu za mwaka huu hakuna aliyeenda kuchunguzwa nashangaa, miaka ya nyuma wakati anenda kuchukua formu ya Uraisi niliambiwa niende Muhimbili kuchunguzwa afya yangu.

Alisema kuwa watu wanaenda kuchunguzwa kwa kuwa ugonjwa wowote unaleta itirafu katika kichwa na kushindwa kufanya kazi vizuri.


"Kazi yopyote unavyoomba unaenda Hospitalini Kuchunguzwa kwa kuwa mtu ukiwa na ugomjwa wowote Mwilini mwako unasababisha madhara katika kichwa kwa sababu hata ukiganyaga kipisi cha sigala kama mvutaji alikitupa vibaya akili inapiga simu haraka katika mguu wako na kukutaka uondoe hiyo mtu akiwa anaumwa hataweza kuwa vizuri kutokana na madhara ya ugonjwa,"

Alisema kuwa mtu akiwa anasumbuliwa na ugonjwa wowote Nyaya hugusana na hivyo mtu kama hakuenda kupima na kama anaumwa anaogopwa kuajiliwa kwa kuwa atasababisha hasara kwa kuwa nyaya zitakuwa zinagusana.

Alisema kuwa watu wanao jaza watu wanawajaza kwa kuwanunulia viroba na kuwa haita wezekana kumpata raisi mweye ukombozi wa taifa hili kama kutakuwa na watu anawanunulia viroba ili waje kwenye mikutano yake.

Alisema kuwa yeye hajajaza watu katika mikutano yake kwa kuwa hawanunulii viroba, lakini alijipo moyo kwa kusema kuwa watanzania waliopo katika mkutano wake ndio watakao sambaza taarifa za ukombozi kwa wale ambao hawapo katika mkutano huo.

Marehemu Mtikija Jana Kabla ya kifo chake leo Alfajiri alimnadi mgombea wa Ubunge kupitia chama chake Cha DP jimbo la Njombe Kusini William Myegeta na kuwataka wananchi kumchagua mhombea huyo kwa lengo la kiigomboa Njombe na Tanzania kwa ujumla.

Alisema kuwa Chama hicho kimesimamisha wagombea katika majimbo mengi na sio Njombe Pekee na kuahidi kuwa atazunguka nchi nzima kuwanadi wagombea hao.

Mungu ailaze mahara pema Roho ya Marehemu Mch. Mtikila Amen

Breaking News: Mchungaji Christopher Mtikila afariki dunia leo alfajiri

Breaking News: Mchungaji Christopher Mtikila afariki dunia leo alfajiri


ChristopherMtikila
Taarifa zilizotufikia hivi punde katika chumba chetu cha habari, Mwenyekiti wa Chama cha Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila (pichani) amepata ajali na kufariki dunia alfajiri ya leo eneo la Msolwa-Chalinze.
Elimtaa Blog inaungana na wanachama wa DP pamoja na watanzania wote katika kuomboleza kifo cha Mchungaji Mtikila, Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Mchungaji Mtikila Amen.
mtikila
Pichani ni gari iliyopinduka na kumuua Mchungaji Mtikila.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Naibu Katibu Mkuu wa chama cha DP, Abdul Mluya.
Elimtaa Media inaendelea kukusanya taarifa zaidi na tutawajuza wasomaji wetu hapo baadae.
By MoDewijBlog
TAJIRI AFA, MALI ZAZUA BALAA

TAJIRI AFA, MALI ZAZUA BALAA

ALI za aliyekuwa tajiri maarufu Dar, marehemu Charles John Mallya zimezua balaa baada ya mke mkubwa, Philomena Masechu ambaye anadai kuchuma naye kiasi kikubwa cha mali hizo kusema amedhulumiwa na mke mdogo, akimtaja Mariana kwa kushirikiana na watoto wa wake wengine wa marehemu.


Marehemu Charles John Mallya enzi za uhai wake.

Akizungumza na gazeti hili kwa masikitiko, Philomena alisema uchochezi mkubwa ulifanywa na watoto wa nyumba zingine ndogo (wake wenzake).“Tangu ujana tulihangaika na marehemu na kufanikiwa kupata mali nyingi, nikiwa kama mshauri wake lakini sasa watoto wa wake zake wengine wawili waliyokuwa katika mikono yangu wamefikia hatua ya kunidhulumu kila kitu. Hivi sasa naishi kwenye kijumba kidogo nilichojengewa na ndugu zangu,” alisema mwanamke huyo huku akilia.

Philomena aliendelea kusema kuwa, hitaji lake kubwa ni kupewa nyumba moja ya ghorofa iliyoko Sinza na nyumba ambayo haijaisha iliyoko Moshi, Kilimanjoro.Naye mmoja wa watoto wa mama huyo, Brighton Mallya akisimulia hali hiyo, alisema: “Baba aliacha mali nyingi na kutamka kuwa ni aseti ambayo kila mtu akipata shida ataweza kutatuliwa kupitia mali hizo kwa utaratibu na makubaliano, lakini sasa zimetekwa na baadhi ya ndugu.”

Kwa mujibu wa nyaraka zenye mali za marehemu Mallya, sehemu ya mali alizoziacha ni kampuni ilitwayo Mti Mmoja Enterprises, jina linalotumika katika baadhi ya miradi. Pia aliacha maduka 2, mashamba, biashara ya magari, viwanja zaidi ya 4, nyumba za kawaida, nyumba 3 za biashara ambazo ni ghorofa (zina vyumba 105) pia kuna nyumba zingine za biashara ikiwemo Mariana Bar, Mti Mmoja Annex na Mti Mmoja Guest ambazo ziko Sinza Mugabe, Dar.


Baadhi ya mali alizoacha marehemu.

Aidha, kwa mujibu wa nyaraka hizo thamani ya mali hizo ni zaidi ya shilingi bilioni moja na milioni mia tano (kwa mwaka 2010) ambapo walalamikaji hao wanasema ilitakiwa kila mtu apate haki yake kama inavyostahili na kusingekuwa na malalamiko.

Baada ya kupata tuhuma hizo timu ya Uwazi iliamua kumtafuta mke huyo mdogo ambapo aliposomewa mashtaka aliliambia Uwazi:“Siwezi kuzungumza, naumwa, ongea na mtoto wangu.”
Akampa simu mwanaye wa kiume ambaye aliposomewa madai ya Philomena, alijibu: Iwe mwanzo na mwisho kupiga simu hii.”

Uwazi lilipohitaji ufafanunuzi zaidi alijibu yeye si mwalimu wa kufafanua.
Dawati letu lilifanikiwa kupata baadhi ya nyaraka zinazoonesha marehemu Mallya alizaliwa mwaka 1934, mwaka 1959 alioa mke mkubwa (Philomena) na walifanikiwa kupata watoto 6 na kuwa na biashara ya bar na hotel mjini Moshi.
Mwaka 1956 alimuoa Salome Gasper wakajaliwa kupata watoto wanne.

Mwaka 1963 alimuoa Joyce Mowo na kufanikiwa kupata naye mtoto mmoja. Mwaka 1977, Solome aliaga dunia na mwaka huohuo alimuoa Mariana ambapo mwaka 2010, mwezi Machi, ndipo mzee huyo alikumbwa na mauti kwa maradhi ambayo hayakutajwa
WAZIRI CELINA KOMBANI KUZIKWA SIKU YA JUMATATU MKOANI MOROGORO

WAZIRI CELINA KOMBANI KUZIKWA SIKU YA JUMATATU MKOANI MOROGORO







Wananchi wa mkoa wa Morogoro wamepokea kwa majonzi msiba wa aliyekuwa waziri wa nchi ofisi ya rais menejimenti ya utumishi wa umma na mbunge wa jimbo la Ulanga Bi, Celina Kombani mazishi yanatarajiwa kufanyika Jumatatu wiki ijayo katika eneo la shamba lake lililopo Lukobe manispaa ya Morogoro.



Wakizungumza nyumbani kwa marehemu wakazi wa Morogoro wameeleza kusikitishwa na msiba huo ambapo wamesema marehemu alikuwa kipenzi cha watu, mchapa kazi na kuwataka wakazi wa Morogoro hususani wa jimbo la Ulanga kuwa wavumilivu kwa kupotelewa na kipenzi chao ambapo waziri huyo alikuwa anagombea ubunge kwa awamu ya tatu kwa tiketi ya CCM katika jimbo la Ulanga.

Wakizungumza na ITV kwa niaba ya familia kaka wa marehemu Martin Ombeshi na mkwe wa marehemu Bw, Jeradi Mlenge wamesema wameupokea msiba huo kwa masikitiko ambapo wameeleza mazishi yatafanyika mkoani Morogoro siku ya Jumatatu shambani kwake Lukobe na msiba utapelekwa nyumbani kwao Mahenge wilayani Ulanga mkoa wa Morogoro.
Duh!! MTOTO WA MIAKA MITANO ACHOMWA MOTO KISA KAIBA KIPANDE CHA NYAMA

Duh!! MTOTO WA MIAKA MITANO ACHOMWA MOTO KISA KAIBA KIPANDE CHA NYAMA




Mtoto Mary Emmanuel mwenye umri miaka mitano mkazi wa mtaa wa Kipika wilayani Mbinga mkoani Ruvuma amekuwa akinyanyaswa kwa kunyimwa chakula na sasa amechomwa moto kiganja cha mkono wake wa kushoto na shangazi yake aitwaye Anneth Nyoku kwa madai ya kuiba kipande cha nyama.

Afisa maendeleo ya jamii wa wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma Bi.Davina Maketa amesema mtoto huyo anadaiwa kunyanyaswa kwa kunyimwa chakula na kupigwa na shangazi yake anayeishi naye aitwaye Aneth Nyoku anayedaiwa kumchoma moto mtoto huyo huku wananchi wakilaani ukatili huo.

Naye mtuhumiwa wa ukatili huo Bi.Anneth Nyoku amesema hakuwa na nia mbaya kumchoma moto mtoto huyo bali lengo ilikuwa ni kumuonya kuacha tabia ya wizi.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma ACP Revocatus Malimi amesema taarifa za tukio hilo bado halijafika mezani kwake na atalifuatilia na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mtuhumiwa huyo.

Maafari shule ya Msingi Genius King’s jijini Dar Es Salaam


Wahitimu wa darasa la saba kutoka shule ya Msingi Genius King’s iliyopo jijini Dar es salaam wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi Mhandisi Michael Mrema kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo (hayupo pichani) wakati wa mahafali ya nne ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika hivi karibuni shuleni hapo.
Mgeni Rasmi Mhandisi Michael Mrema akitoa hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wakati wa mahafali ya nne ya kuwaaga wanafunzi wa shule ya Msingi Genius King’s iliyopo jijini Dar es salaam iliyofanyika hivi karibuni shuleni hapo. Waliopo meza kuu ni Wakurugenzi wa shule hiyo, kwanza kulia ni Mkurugenzi Imelda Philip akifuatiwa na Machage Kisyeri. Na wa kwanza kushoto ni Julius Rutabanja.
Mtimu wa darasa la saba wa shule ya Msingi Genius King’s iliyopo jijini Dar es salaam Deniol Msemwa akipokea cheti cha kuhitimu elimu ya shule ya msingi kutoka kwa Mgeni Rasmi Mhandisi Michael Mrema kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo.
Mgeni Rasmi Mhandisi Michael Mrema (katikati mstari wa mbele walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na Wahitimu wa darasa la saba kutoka shule ya Msingi Genius King’s iliyopo jijini Dar es salaam wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa wakionesha vyeti mara baada ya kukabidhiwa vyeti hivyo wakati wa mahafali ya nne ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika hivi karibuni shuleni hapo.
Mhitimu wa darasa la saba Emma Emily akiwa amepokea cheti cha kufanya vizuri katika somo la Hisabati pamoja na hati ya ufadhili wa kusomeshwa kidato cha kwanza hadi cha nne katika shule ya sekondari ya Bright Future Girls iliyopo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wazazi na walezi wakifuatilia hafla ya kuwaaga Wahitimu wa darasa la saba kutoka shule ya Msingi Genius King’s iliyopo jijini Dar es salaam hivi karibuni.

Wahitimu Burongwa: Rushwa mahospitalini sio wanachofundishwa madaktari vyuoni




 Wahitimu wa taaluma ya udaktari wa meno na wauguzi katika chuo cha sayansi ya Afya Bulongwa wilayani Makete wakiingia katika ukumbi wa sherehe za mahafari ya kuhitimu elimu yao Septemba 5, 2015 

 Burudai kidogo ilifanyika babla ya mambo mengine kuendelea

 Waziri wa habari na michezo (Mwenye Nyekundu) katika chuo cha Bulongwa 
 Maabara ya kujifunza kwa vitendo


 Muhitimu kwa masomo ya udaktari wa meno akizunhumza na waandishi wahabari (hapapo pichani)



 Wanachuo wakiwa katika ukumbi wa sherehe za maafari ya kuhitimu elimu yao ya uuguzi na utaktari wa meno chuo cha Bulongwa Makete Mkoani Njombe


 Baadhi ya wazazi na ndugu za wahitimu walio kuja kusheherekea na nduguzao
 Mkuu wa chuo cha Bulongwa John Matala akizungumza na wahitimu
 Dmo wa wilaya ya Makete Mkoani Njombe
 Mgeni Rasmi Prof. Norman Sigalla (Kushoto) akikaribishwa na Mwakilishi wa askofu wa KKKT-Makete
 Wahitimu wakisoma Lisala mbele ya Ngeni Rasm 




 Wahitimu wakila kiapo cha kuuhakikishia uma kuwa watafanya kazi kwa utii na kufuata kanuni za utumishi wa taalkuma yao.

 Mwakilishi wa askofu wakitoa neno kwa wahitimi hao

 Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Songea na mgombea ubunge jimbo la Makete mkoani Njombe na mgeni rasimi katika Maafari hayo ya wahitimu wa Uuguzi na udaktari wa meno katika Chuo cha Bulongwa.
MC katika maafari hayo Sanga akiendesha shuguli hiyo


VITENDO vya Rushwa maneno machafu kwa baadhi wa watumishi wa hospitali wakiwemo wauguzi na madaktari vimedaiwa kuwa ni hulka ya mtu binafsi na sio maadili wanayofundishwa katika vyuo vya taaluma yao.
Hayo yamebainishwa na baadhi ya wanachuo na wahitimu wa chuo ya Sayansi ya afya Bulongwa cha wilayani Makete Mkoani Njombe, ambao wamesema kuwa vitendo vya Rushwa na Lugha chafu havifundishi chuoni na kuwa wanafundishwa kuwa wataratibu wanapo hudumia wagonjwa.

Mmoja wa wahitimu katika chou hicho Dr. Daniel Ngailo amesema kuwa miaka ya sasa maadili ya taaluma hiyo wamekuwa wakifundishwa na kuwa ndio maana katika vituo vya afya mpaka hospitali vitendo vya maneno machafu vimepungua kutokana na maadili kufundishwa sana.

Hata hivyo  Maulisia Mlowe anaye hitimu mafunzo ya uuguzi anasema kuwa vitendo vya rushwa na kashifa kwa wagonywa vinakuwa ni hulka ya mtu binafsi na tamaa huku akisema kuwa serikali iongeze kiwango cha mishahara ili kuhakikisha kuwa wauguzi wanafanya kazi bila kuwa na tamaa ya pesa kutoka kwa magonjwa na kuondoa vitendo vya Rushwa.


Kwa upande wake mkuu wa chuo cha Bulongwa, John Matala amesema kuwa serikali imekuwa ikiwatembelea mara kwa mara na kuhakikisha kuwa elimu inayotolewa inakuwa bora na kuwa katika chuo hicho wahitimu wanao toka wanaende kuwa wenye maadili kutokana na walivyo wafundisha.


Alisema kuwa chuo hicho wanamalengo ya kuwa chuo kikuu na kuanza kutoa elimu ya afya kwa hadhi ya chuo kikuu, na kuwa wanatarajia kuongeza vitengo vingine vya kutoa wahudumu wa afya.



Naye mgeni rasimi katika maafari hayo aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Songea kwa sasa ni mgombea wa ubunge jimbo la Makete Prof. Norman Sigalla  amesema kuwa chuo hicho kinatakiwa kuwa na wakuu wa bodi wenye uwezo wa kifedha na watu wenye ubunifu ili chuo hicho kufikia malengo yake kwa haraka ya kuwa chuo kikuu.


Alisema kuwa kuna watu wenyeuwezo ka kuandaa miradi katika wilaya hiyo na chuo kinatakiwa kuwatumia watu hao ili kiweze kufikia malengo yake mapemba ya kuwa chuo kikuu ya afya kama yalivyo malengo yao.

 

Kategori

Kategori