Showing posts with label michezo. Show all posts
Showing posts with label michezo. Show all posts

NJOMBE MJI YAPATA KOCHA MPYA



BAADA ya kupata matokeo mabovu kwa muda mrefu timu ya Njombe mji imeamua kutafuta mwalimu mkuu wa timi ambaye amewasili hii leo na kuahidi matokeo ya kuwepo kwake kuanza kuonekana katika mechi ya kesho baina ya timu ya Njombe mji na Mbeya city.
Kocha Mkuu wa Njombe Mji  Ally Bushiri amesema kuwa mashabiki wa timu ya Njombe mji waanze kutaraji matokeo katika mchezo wake wa kwanza kuwa na timu hiyo na kuwa kwa michezo iliyo baki ni lazima ataifikisha timu hiyo sehemu mzuri.
Mwenyekiti wa timu hiyo Erasto Mpete amesema kuwa wakati huu mgumu ndio wa mashabiki kuonyesha kwa timu hiyo kwa kuwa matokeo inayo pitia wanataraji mabadiliko kama watakuwa na ushirikiano.
Pamoja na uongozi kuwa na matumaini hata kwa mashabiki huku kuhusu wakati wa ujio wa kocha ikiwa ni wakati wake muafaka.
Timu ya Njombe mji sasa ipo katika nafasi ya mkiani lakini bado wanamichezo mingi ambayo kama wakifanya vizuri watakuwa katika nafasi nzuri.

Elimtaa Tv: Njombe mji kukipiga na Tanzania Prison, Prison wanamajeruhi mmoja mfahamu hapa....

TIMU za Njombe Mji na Tanzania Prison ya Jijiji Mbeya zinazo tarajiwa kucheza Jumamosi wiki hii zinaendelea na mazoezi huku waalimu wake wakisema kuwa wamejipanga vizuri kuingia katika mchezo huo Prison wakisema wanamajeruhi mmoja ambaye wanawasiwasi wa kukosa mchezo huo.

Meneja wa timu ya Tanzania Prison ya Jijini Mbeya amesema kuwa timu yake imejipanga vizuri kupambana na timu ya Njombe Mji na ina majeruhi mmoja ambaye ni Beki yao na inadaiwa mchezo huo anaukosa.

Waalimu wa timu zote mbili wakizungumza kwa nyakati tofauti wanasema kuwa wachezaji wao wapo vizuri kuingia katika mechi hiyo ya ligi kuu.

Kuhusu uwanja wa Sabasaba Meneja wa uwanja huo anasema uwaja upo vizuri na wamemaliza mapungufu waliyo yaona wakati wa majaribio.


Timu ya Njombe mji inacheza mechi ya ligi kuu ukiwa ni mchezo wake wa kwanza na timu ya Prison ilikuwa Mjini Zanzibar kwa kujipanga na ligi kuu Tanzania bara.

Elimtaa Tv Njombe Mji Kukipiga na Singina United uzinduzi uwanja wa sabasaba Njombe

Uwanja umekamilika ni ule wa sabasaba wa nyumbani kwa Njombe Mji FC
UWANJA WA SABASABA NJOMBE

UWANJA wa sabasaba wa mjini Njombe unatarajiwa kufanyiwa majaribio Jumapili wiki hii kwa kucheza mechi ya kujipima uwezo kati ya timu ya Njombe Mji wenyeji na Timu ya Singida United ya mkoani singida zote zikiwa zinaingia ligi kuu Tanzania bara msimu huu.
Meneja wa uwanja wa Sabasaba anasema kuwa mechi hiyo itakuwa ni yakwanza kuzikanjaka nyasi hizo na kuwa kama uzinduzi wa uwanja huo na kuangalia mapungufu katika miundombinu yake.
Katibu wa CCM wamiliki wa uwanja huo anasema kuwa uwanja huo umekamilika kwa asilimia kubwa na mechi hiyo itasaidia kuona mapungufu yaliyo salia na kuyakamilisha kabla ya kuingia Ligi kuu.
Mashabiki nao wanasema wamefurahishwa na uwaja kufikia hatua hiyo na kusema kuwa hamu yao ni kuona wachezaji wakubwa wakicheza mkoani Njombe.

Timu hizo mbili zote zimepada dalaja msimu uliopita na kuingia ligi kuu mwaka huu pamoja na timu Lipuli ya mkoani Iringa.

Waziri Mwijage azindua mashine ya kusaga na kukoboa nafaka kijijini Maisha Plus

Waziri Mwijage azindua mashine ya kusaga na kukoboa nafaka kijijini Maisha Plus


2016-10-30-PHOTO-00000145 “Hii mashine ni njia mbadala ya kumuwezesha mtu kufanya mazoezi badala ya kwenda gym kufanya mazoezi utaweza kutumia mashine hii ukiwa unasaga nafaka huku unafanya mazoezi,” alisema Mwijage. 2016-10-30-PHOTO-00000148 Alisema ni vyema kwa washiriki kutumia njia hiyo kuweza kubuni mashine nyingine zaidi ili kuweza kuongeza soko la Afrika Mashariki.
Alitoa wito kwa mshiriki atakayeshinda Tzshs. Milioni 30 za Maisha Plus aziwekeze katika uchumi wa viwanda. 2016-10-30-PHOTO-00000147 Grace PEMBA kutoka Mtwara aula Katika hatua nyingine, Waziri Mwijage ameahidi kumpatia mshiriki Grace Pemba kutoka Mtwara mashine ya kubangua korosho yenye thamani ya shilingi milioni nane. "Ukienda ripoti SIDO Mtwara, waambie Waziri amesema mnipe mashine ya kubangua korosho."
Grace aliyekua anafanya kazi katika saluni za kutengeneza nywele ameshauriwa kutumia mashine hiyo kujikwamua kiuchumi. Vipindi vya Maisha Plus vinarushwa na kituo cha Televisheni cha Azam Two na pia kupitia akaunti ya Youtube ya Maisha Plus. Taarifa zaidi kuhusu mashindano hayo zinapatikana katika tovuti rasmi ya www.maishaplus.tv na kupitia mitandao ya Maisha Plus ya Facebook, Instagram na Twitter.
Bob Dylan ashinda Tuzo ya Fasihi ya Nobel

Bob Dylan ashinda Tuzo ya Fasihi ya Nobel



Dylan alichukua jina lake la usanii kutoka kwa mshairi Dylan ThomasImage copyrightAFP
Image captionDylan alichukua jina lake la usanii kutoka kwa mshairi Dylan Thomas

Mwanamuziki wa nyimbo za asili wa Marekani Bob Dylan ametunukiwa Tuzo ya Fasihi ya Nobel.
Mwanamuziki huyo wa miaka 75 ametunukiwa tuzo hiyo kwa "kuunda aina mpya ya kujieleza kishairi kupitia utamaduni maarufu wa nyimbo Marekani".
Dylan alizaliwa Robert Allen Zimmerman mwaka 1941 na alianza uimbaji 1959, akicheza katika migahawa Minnesota.
Nyimbo zake maarufu aliziimba miaka ya 1960, ambapo alikuwa maarufu kwa kusimulia matatizo ya Marekani katika historia.
Nyimbo zake kama vile Blowin' in the Wind na The Times They are A-Changin'zilitumiwa sana na wanaharakati wa kupinga vita na watetezi wa haki za raia.
Aliachana na nyimbo asili, na akaamua kuingilia muziki wa rock na ala za kutumia umeme baadaye.

WAZIRI NAPE NNAUYE ASHIRIKI SIKU YA KITAIFA YA HISPANIA JIJINI DAR ES SALAAM


 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape  Nnauye akipiga kitaa wakati wa hafla fupi ya Siku ya Kitaifa ya Hispania alipoalikwa kama mgeni rasmi na Balozi wa Hispania hapa nchini.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape  Nnauye (kulia) akigonga glasi na Balozi wa Hispania nchini Ndg. Felix Costale Artieda(kushoto) ikiwa ishara ya kutakiana kheri  wakati wa hafla fupi ya Siku ya Kitaifa ya Hispania alipoalikwa kama mgeni rasmi nyumbani kwa Balozi huyo Jijjini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape  Nnauye akijadiliana jambo na Balozi wa Hispania nchini Ndg.Felix Costale Artieda(katikati) wakati wa hafla fupi ya Siku ya Kitaifa ya Hispania alipoalikwa kama mgeni rasmi na Balozi wa Hispania hapa nchini.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape  Nnauye akibadilishana mawazo na baadhi ya waalikwa wa hafla fupi ya Siku ya Kitaifa ya Hispania alipoalikwa kama mgeni rasmi na Balozi wa Hispania hapa nchini Jijini Dar es Salaam.Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WHUSM.
Jerry Muro leo aibuka na haya hapa

Jerry Muro leo aibuka na haya hapa

Tokeo la picha la jerry muroMTAZAMO WANGU


Nimesoma hoja za wadau tangu juzi na jana, nimeona na kujifunza mengi sana kutoka kwa waliokuwa viongozi wa yanga na wadau wa yanga kuwepo kwa tofauti ya mitazamo ni jambo la afya katika uhai na maendeleo ya Yanga hilo kwanza lazima tukubaliane.

Nichangie kidogo hapa mimi kama Jerry muro nachangia kama mdau wa kawaida tu kwa tulipofika sasa lazima tukiri kuwa tunaitaji club iongozwe na watu wenye mitaji mikubwa ya fedha iwe kwa kukodishwa au kuwekeza mana mfumo wa uendeshaji wa mpira duniani kote umebadilika kasoro Tanzania ambapo bado tuko kama vile kwenye soka la ridhaa wakati mfumo unaotawala ni soka la kimataifa na la kisasa.

Vilabu vya Tanzania vimekuwa kama vile ni vijiwe vya kufurahishana tu baada ya kazi na haswa kwa simba na y
Yanga vikishafungana vyenyewe kwa vyenyewe biashara imekwisha hakuna kifuatacho, na ndio mana tunapokwenda kwenye michuano ya kimataifa tunapata shida mana sisi mtazamo wetu ni yanga amfunge simba basi mtaani tushikishane adabu kwisha kazi.

Sasa tunachotakiwa ni kutoka hapa tulipo na kwenda mbele zaidi kwa kuwa na mfumo na muundo thabiti wa kimataifa.
Kwa Yanga tumeanza na tunashukuru Mungu tumeanzia pazuri kwa kuwa sasa muamko umekuwa mkubwa na umejenga mijada mingi sana ya kuonyesha dira ya tuendako, hilo kwangu mimi ni afya kubwa sana kwa maendeleo ya Klabu.

Tusiwabeze waliothubutu tuwasaidie kwa kuwaonyesha njia na kuwatia moyo mana tukumbuke kila jambo Kiowa linaloanza kwa mara ya kwanza lina changamoto kubwa zipo nyingine zinaweza kutatulika kwa sasa na haswa kwenye mikataba na yako mengine yatakuwa yanajitatua taratibu yenyewe wakati mfumo na muundo unaendelea cha msingi ni kuwa na SUBIRA.

Mwisho nimalize kwa kusema kuwa hizi ni zama mpya zenye maono mapya na mwamko mpya lazima tukubali kubadilika la sivyo tutabadilishwa kwa lazima(nature will change us)
Kwa wale wenye nia pia ya kusaidia yanga bado fursa zipo nyingi sana katika maeneo mengine makubwa mfano mali za yanga majengo, kuwekeza kwenye rasilimali watu ambao ni wanachama na mambo mengine, na tukiona hatuwezi uko basi tuvute subira tusubiri baada ya miaka 10 tujitokeze kuchangamkia fursa kutoka Yanga.

Niseme kutoka moyoni kabisa Yanga ni yetu sote tusaidiane kuijenga yanga na sio kuibomoa na katika yote lazima tukubali kuvumiliana katika madhaifu yetu hakuna mkamilifu chini ya mbingu na jua hivyo KUVUMILIANA NI JAMBO LA BUSARA SANA.

Jerry Cornel Muro
Mdau wa soka Yanga

VIDEO: STAA WA NIGERIA, YCEE AUNGANA NA DJ MAPHORISA WA AFRIKA KUSINI KWENYE REMIX YA OMO ALHAJI

​Msanii wa Hip-hop wa Nigeria, Ycee ameungana na mtayarishaji wa muziki na muimbaji wa Afrika Kusini, DJ Maphorisa kwenye remix ya wimbo wake unaofanya vizuri barani, ‘Omo Alhaji’.

Ikifanyika jijini Johannesburg, na kuongozwa na La Dupont Productions, remix ya wimbo huo inahusisha rap iliyoshiba na inayohitaji usikivu.

DJ Maphorisa amechanganya ladha ya kipekee ya Kusini kwenye mrindimo unaoungana vyema na mtindo wa Ycee na kuzalisha wimbo utakaofanya vizuri kwenye klabu, mtaani na hata kwenye redio. Remix hii ya Omo Alhaji, haina shaka itateka tena mawimbi ya redio na TV barani Afrika.

Ycee anasema, “Limekuwa jambo kubwa kufanya remix hii, kama msanii ninafurahi kujaribu muziki tofauti. Ulikuwa uzoefu mkubwa na wa kufurahia kufanya kazi na DJ Maphorisa. Ninaamini mashabiki watafurahia remix hii.”

KUHUSU YCEE

Akizaliwa kwa jina la Alejo Martin Oludemilade, tarehe 29, January 1993, Ycee ni msanii wa hip hop wa Nigeria na mshindi wa tuzo.  Amesainishwa kwenye lebo ya muziki ya TINNY ENTERTAINMENT. Alianza rasmi muziki Disemba 2012 kwa kuachia wimbo 'Smile on Me' uliotayarishwa na Jay Sleek, na zingine kama 'Pass Me' na 'Amen' akimshirikisha Mbryo.

Alikuja kujipatia umaarufu zaidi July 2015 baada ya kuachia wimbo 'Jagaban.' Jagaban ukaja kuwa miongoni mwa nyimbo kubwa zaidi kwa mwaka 2015/16 na kuja kuwa na remix nzito aliyomshirikisha staa wa YBNL, Olamide na video yake ikiongozwa na Director Q.

Wimbo huo ulimweka sehemu nzuri Ycee kama kinara wa hip hop ya kizazi kipya nchini Nigeria na hatimaye kumpa tuzo ya “Rookie Of The Year” kwenye tuzo za Headies, mwaka 2015.

Kutoka kwa wimbo ‘Omo Alhaji’, Disemba 2015, kulimpandisha zaidi Ycee kama mmoja wa wasanii wakali kabisa wa hip hop nchini Nigeria. Alikuja kuachia video ya wimbo huo iliyoongozwa na Director Q iliyofanyika Uingereza. Wimbo huo pamoja na video yake viligeuka wimbo wa taifa kwenye chati za redio za TV za Nigeria, kwenye klabu na hata mtaani huku ukiipa umaarufu sentesi: 'Who's your Daddy?

EP yake ya kwanza iliyopewa jina The First Wave itatoka Oktoba, 2016.

KUTAZAMA VIDEO HIYO FUATA LINK HIYO CHINI:


MITANDAO YA KIJAMII

HUU HAPA MSIMAMO NA MATOKEO LIGI KUU PRIMUS LEAGGUE BURUNDI WIKI HII YA 5


Ligi Kuu ya Primus League Burundi imeingia kwenye wiki yake ya 5 huku kuna mabadiliko makubwa  katika msimamo wa ligi tofauti na wiki ya 4. Mjini Bujumbura Buja City inaendelea kupoteza kwa kuridhika kupigwa vikali bao tatu kwa moja dhidi ya Magara Star (1-3), LLB inaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa kupata ushindi wa bao moja bila dhidi ya Inter Star (1-0), timu kama Olympic Star na Flambeau zimeshindwa kujitetea mbele ya mashabiki zao kwa kupoteza pointi huku Les Lierres imecharazwa vikali kwa bao nne bila dhidi ya Musongati.

Matokeo ya wiki ya 5: 

Jumamossi, 08/10/2016:
-Buja City 1-3 Magara Star.
-LLB 1-0 Inter Stars
-Ngozi City 2-0 Rusizi FC
-Olympic Star 0-1 Muzinga
Flambeau de l'Est 1-2 Messager Ngozi.
-Musongati 4-0 Les Lierres.

Jumapili  09/10/2016:

-Messager Bujumbura 0-2 Athletico Olympic.
-Aigle Noir 0-0 Vital'o

Msimamo wa Ligi Kuu Primus League wiki ya 5:

1.LLB: Pointi 15 na bao 6
2.Athletico Olympic: pointi 13 na bao 14 
3.Inter Stars: pointi 12 na bao 3
4.Musongati FC: pointi 9 na bao 5
5.Messager Ngozi: pointi 9 na bao 1
6.Aigle Noir: pointi 8 na bao 2
7.Ngozi City: pointi 6 na bao 1 
8.Flambeau de l'Est: pointi 6 haina bao
9.Muzinga: pointi 6 na bao -4
10.Les Lierres: pointi 5 na bao -2
11.Rusizi FC: pointi 5 na bao -4
12.Vital'o: pointi 4 na bao -1
13.Magara Star: pointi 4 na bao -3
14.Olympic Star: pointi 4 na bao -7
15.Messager Bujumbura: pointi 2 bao -6
16.Bujumbura City: pointi 1 na bao -

NAPE AFUNGA RASMI TAMASHA LA NGOMA ZA UTAMADUNI LA TULIA 2016 RUNGWE LEO

 Kikundi cha Utamaduni cha Ikama kikitoa burudani wakati wa kufunga Tamasha la Utamaduni la Tulia Tradition Festival 2016 lililofanyika wilayani Rungwe mkoani Mbeya na kushirikisha vikundi vya ngoma 62.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ( wa pili kulia) akifurahia jambo na Naibu Spika Mhe. Tulia Ackson (kulia) wakati wa KUFUNGA Tamasha la Utamaduni la Tulia Tradition Festival 2016 liliofanyika wilayani Rungwe mkoani Mbeya  leo Oktoba 08,2016.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ( katikati) akicheza moja ya ngoma za kiutamaduni Wwakati wa kufunga Tamasha la Utamaduni la Tulia Tradition Festival 2016 liliofanyika wilayani Rungwe mkoani Mbeya  leo Oktoba 08,2016 kulia ni Naibu Spika Mhe. Tulia Ackson na kushoto ni Katibu Mtendaji BASATA Geodfrey Mngereza.


Na Kitengo cha Mawasiliano WHUSM -Mbeya

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye  amewashauri vijana kutumia ngoma za asili kujiajiri kwani ni fursa mojawapo ya ajira kwa sasa.

Ametoa ushauri huo leo Mjini Mbeya alipokuwa akifunga Tamasha la Utamaduni la Tulia Tradition Festival 2016 na kuwahimiza vijana kutosubiri kuajiriwa ikiwa wanaona wana uwezo wa kufanya kitu ambacho kitawasaidia kupata kipato na kuendesha maisha yao.

“Ngoma za asili ni chanzo cha ajira kwa vijana na sisi kama Serikali tutashirikiana na wadau wa Sanaa na Utamaduni ili kutengeneza ajira na kudumisha mila na desturi za nchi yetu” alisistiza Mhe. Nnauye.

Aidha kwa upande wake Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson amesema kuwa fursa pekee kwa vijana kujiajiri kupitia shughuli za Sanaa na Utamaduni kwani ndio sekta ambazo zimetoa ajira kwa vijana wengi duniani kwa sasa.

“Nawashauri vijana wa kitanzania kuangalia na upande huu wa Sanaa na Utamaduni kuna ajira pia na sisi tupo pamoja nao na tutawapa  ushirikiano ili wafikie malengo” alisema Mhe. Tulia.

Tamasha hili liliondaliwa na Naibu Spika Mhe.Tulia Ackson linafanyika kwa siku mbili na limeshirikisha vikundi vya ngoma za asili vipatavyo 62 kutoka mikoa mbalimbali nchini.

Simba, Yanga Marufuku Uwanja wa Taifa

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amezifungia rasmi timu za Simba na Yanga kutumia uwanja wa Taifa mpaka pale zitakaporuhusiwa tena na Serikali.

Nape ametoa amri hiyo leo Jumapili ikiwa ni siku moja baada ya mashabiki wa klabu ya Simba, kung'oa viti vilivyopo kwenye majukwaa ya uwanja huo kwa kile walichokidai kupinga uamuzi wa Refa, Martin Saanya aliyechezesha mechi hiyo.

"Simba na Yanga hawatoutumia tena uwanja huu mpaka pale Serikali itakapoona kuwa mazingira yanaruhusu," alisema Nape.

Ndege mpya yatua Dar abiria zaidi ya 70


Ndege ya kwanza iliyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kutumiwa na Shirika la NdegeNdegeNdegeania (ATCL) imetua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam ikitokea nchini Canada ilikotengenezwa.

Ndege hiyo aina ya Bombadier Q400 Next Gen imetua majira ya saa 6:15 Mchana na kisha kupatiwa heshima maalum ambayo hutolewa kwa ndege yoyote mpya inayotua katika nchi yake (Water Salute).

Baada ya kupokea heshima hiyo, ndege imeegeshwa katika eneo la ndege za jeshi (Airwing Ukonga).

Akizungumza baada ya kuwasili kwa ndege hiyo Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt. Leonard Chamriho amesema ndege ya pili inatarajiwa kuwasili baada ya wiki moja na kwamba baada ya kuwasili ndege ya pili ndipo yatafanyika mapokezi rasmi, yatakayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa tarehe itakayotangazwa baadaye.

Kategori

Kategori