Mwanamuziki wa nyimbo za asili wa Marekani Bob Dylan ametunukiwa Tuzo ya Fasihi ya Nobel.
Mwanamuziki huyo wa miaka 75 ametunukiwa tuzo hiyo kwa "kuunda aina mpya ya kujieleza kishairi kupitia utamaduni maarufu wa nyimbo Marekani".
Dylan alizaliwa Robert Allen Zimmerman mwaka 1941 na alianza uimbaji 1959, akicheza katika migahawa Minnesota.
Nyimbo zake maarufu aliziimba miaka ya 1960, ambapo alikuwa maarufu kwa kusimulia matatizo ya Marekani katika historia.
Nyimbo zake kama vile Blowin' in the Wind na The Times They are A-Changin'zilitumiwa sana na wanaharakati wa kupinga vita na watetezi wa haki za raia.
Aliachana na nyimbo asili, na akaamua kuingilia muziki wa rock na ala za kutumia umeme baadaye.