Showing posts with label YALIYOJIRI HIVIKARIBUNI NYANDA ZA JU KUSINI 2. Show all posts
Showing posts with label YALIYOJIRI HIVIKARIBUNI NYANDA ZA JU KUSINI 2. Show all posts

Mgombea Mwenza wa Urais CCM Aahidi Umeme Kila Kijiji Ruvuma



MGOMBEA mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu ameanza ziara yake mkoani Ruvuma akiinadi ilani ya chama hicho huku akiahidi neema kwa wakulima wa kahawa na mahindi wa mkoa huo.

Bi. Samia Suluhu ambaye amehutubia mikutano mitatu katika majimbo mawili ya mkoa wa Ruvuma yaani Jimbo la Nyasa na Mbiga Vijijini, akizungumza katika mikutano yake amesema serikali itakayoundwa na CCM endapo itashinda itahakikisha inashusha umeme katika vijiji vyote vya mkoa huo kwa awamu ili kuchochea maendeleo ya wananchi.

Alisema kwa kuwa mkoa huo unazalisha mazao ya mahindi na kahawa serikali itahakikisha inaanzisha viwanda eneo hilo vya kusaga na kuandaa unga wa mahindi kwa wakulima na kuwawezesha ili wauze unga na kunufaika zaidi tofauti na ilivyo kwa sasa ambapo wamekuwa wakilanguliwa.

Alisema viwanda vingine ambavyo Serikali ya CCM itavianzisha ni pamoja na viwanda vya kubangua kahawa na kuiandaa kikamilifu tayari kwa kutumika, jambo ambalo alisema licha ya kuongeza thamani ya zao hilo itaongeza ajira kwa vijana na kuchochea uchumi wa wakulima eneo hilo.
 
Akizungumzia miundombinu ya barabara ambayo bado ni changamoto kwa mkoa huo hasa vijijini alisema serikali itakayoundwa na CCM chini ya uongozi wa Dk. John Pombe Magufuli pamoja na yeye watahakikisha wanajenga na kuboresha barabara za maeneo hayo ili ziweze kupitika kwa uhakika.

Hata hivyo kiongozi huyo amesema Serikali itakayoundwa na CCM endapo itashinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2015 imejipanga kuboresha vizuri huduma za afya kuondoa ukiritimba na rushwa, elimu kwa kutoa elimu bure toka darasa la kwanza hadi kidato cha nne pamoja na ujenzi wa mabweni na uwezeshaji vijana na akinamama kiuchumi popote walipo mjini na vijijini.

Ziara ya mikutano ya kampeni ya mgombea mwenza huyo wa urais tiketi ya CCM, inaendelea leo katika Mkoa wa Ruvuma na ataingia Jimbo la Tunduru kuendelea kuinadi ilaya ya chama hicho kuomba ridhaa kwa wananchi ili waweze kurejeshwa madarakani na kuunda dola.
Mpekuzi blog
Vijana watakiwa kujiandikisha kwa wingi

Vijana watakiwa kujiandikisha kwa wingi

VIJANA nchini wametakiwa kuendeleza kujiandikisha katika Daftari la kudumu la mpiga kura Kwa mfumo wa Kielekroniki (Bvr) na kutimiza wajibu wao kwa kuchagua kiongozi kama watu wenye hekima.

Wito huo umetolewa mbele ya maelfu ya vijana kutoka sehemu mbalimbali nchini katika kongamano la vijana wa Katoriki Tanzania la kila mwaka linalofanyika Mkoani Njombe na Askofu wa jimbo la Mpanda, Gervas Nyaisonga mjini hapa jana.

Askofu Nyaisonga amesema kuwa vijana wanaotakiwa watumie wajibu wao wa kupiga kura na wajiazari kutumika katika kipindi hiki cha uchaguzi.

Alisema “Vijana mmekuwa mkitumika katika mambo mbalimbali hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi kwa namna ya maandamano na wengine kufanywa uraghai ili kupitisha kiongozi asiyefaa, angalieni na epukeni watu wa aina hiyo ili kupata viongozi bora,”

Alisema anajua kwa mkoa wa Njombe zoezi limeshapita lakini kwa mikoa ambayo zoezi linaendelea wajitokeze kujiandikisha ili kutumia hakiyao ya msingi na kiimani kumchagua kiongozi bora na kuwa katika sarafu inapande mbili za upande wa Kaisali na upande wa dini.

“Najua tu uchaguzi utakuwa jumapili na vijana wengi najua mnapenda kusali lakini siku hiyo muhakikishe mnawahi kanisani katika misa ya asubuhi na kwenda kupiga kura hatakama foleni itakuwa ndefu mvumilie si mshawahi kufunga siku hiyo mtafunga,” alisema Askofu Nyaisonga.

Alisema kuwa vijana wanawajibu mkubwa wa kupigia kura kiongozi wanae mtaka lakini kwa kujiandikisha wanaweza kufanya hivyo kama hawata jiandikisha ni sawa na kazi bure hivyo amewataka kwa ambao zoezi la uandikishaji unaendelea wajiandikishe katika dafdari hilo ili kupata fulsa ya kupiga kura.

Aliwataka vijana kutumia uchaguzi huo kama watu wenye hekima na watu wenye macho na kutumia hekima ya Mungu kufanya uchaguzi wa mtu wanaye mtaka bila kupenda pesa za mgombea yeyote.

Aliongeza kuwa ameisikia tume imesema imefanikiwa katika uandikishaji wa Daftari la kudumu la mpiga kula lakini anashangaa haijasema imefanikiwa kwa kuwaandikisha watu wangapi na kuwa angefurahi kusikia imefanikiwa kuwandikisha watu 45 milioni.


“Vijana kama hamtajiandikisha unatumika katika maandamano kwa hiyo jiandikisheni na mkapige kura, suala la Katiba Pendekezwa lilikuwa zinazungumziwa sana lakini sasa limesubilishwa wote tupo kimya wote wanazungumzia na walio kuwa hawazungumzii wote tupo sawa” alisema Askofu Nyaisongo


Kwa ufupi; Halumashauri ya mji Mpanda yaongeza siku uandaishaji BVR

Kwa ufupi; Halumashauri ya mji Mpanda yaongeza siku uandaishaji BVR

Halmashauri ya mji Mpanda Mkoani Katavi imeongeza siku katika zoezi la uandikishwaji katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa kata zilizoanza zoezi hilo mapema wiki jana mkoani humo. Zoezi linalo kosolewa vikali na wananchi kutokana na kasoro za wazi pamoja na kushindwa kudhibiti wimbi la kujiandikisha kiholela. BY Alinanuswe on fb

MKUU WA MKOA WA RUKWA ENG. STELLA MANYANYA AONGOZA KIKAO CHA DHARURA CHA KAMATI YA USHAURI YA MKOA RCC NA KUPITISHA MAPENDEKEZO YA KUANZISHA MAJIMBO MAWILI MAPYA YA UCHAGUZI KATIKA WILAYA ZA SUMBAWANGA NA KALAMBO


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya kulia akizungumza wakati akiongoza kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kujadili na kufanya uamuzi wa kuanzisha majimbo mapya ya uchaguzi katika wilaya ya Sumbawanga na Kalambo leo tarehe 23 Mei 2015. Kikao hicho kimeridhia mapendekezo hayo ya Halmashauuri husika baada ya kukidhi vigezo ambapo yatapelekwa ngazi za juu kwa uamiuzi zaidi. 

Majimbo hayo yatazaliwa katika majimbo yaliyopo hivi sasa ambapo kwa jimbo la Kwela ambalo lipo katika Wilaya ya Sumbawanga litazaa jimbo la Ziwa Rukwa baada ya kukidhi vigezo vyote vilivyowekwa na tume ya taifa ya uchaguzi ikiwemo ya idadi ya watu na ukubwa wa jografia. Kwa upande wa jimbo la Kalambo ambalo lipo katika Wilaya ya Kalambo linatarajiwa kuzaa Jimbo jingine la Mambwe. Kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa.
 Sehemu ya wajumbe na waalikwa katika kikao hicho.
 Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa akitoa taarifa iliyopokelewa na ofisi yake kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi juu ya maelekezo ya kuchunguza mipaka na kugawa Majimbo ya Uchaguzi kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya na Kushoto ni muwakilishi wa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa Ndugu Clemence Bakuli ambaye ni Katibu Mwenezi wa Chama hicho Mkoa.
 Sehemu ya wajumbe na waalikwa katika kikao hicho.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akifafanua jambo katika kikao hicho. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mhe. Iddi Hassan Kimanta.
 Sehemu ya wajumbe na waalikwa wa kikao hicho.
 Sehemu ya wajumbe na waalikwa katika kikao hicho.

ASKARI WALIOKAMATA WAHARIFU WATUZWA SIMIYU


Jeshi la Polisi mkoani Simiyu limewazawadia vyeti na fedha askari Polisi wa vitengo mbalimbali wapatao 22 kutokana na utendaji wao mzuri uliofanya jeshi hilo kukamata wahalifu mbalimbali na kupunguza makosa ya ajali za barabarani katika mkoa huo.

Sherehe za kuwatunuku vyeti askari hao zilianza kwa gwaride ambapo mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya bariadi, Erasto Sima ambaye alimuwakilisha mkuu wa mkoa huo alikagua gwaride hilo.
 
Akizungumza kabla ya kukabidhi vyeti hivyo kwa niaba ya insepekita wa polisi nchini, kamanda wa polisi wa mkoa wa Simiyu, kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Charles Mkumbo amesema mkuu wa wilaya ya Bariadi Erasto Sima amewataka wananchi wa mkoa huo kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi hususani katika kufichuwa vitendo mbalimbali vya uharifu ambapo pia amewataka kuacha kujichukulia sheria mikononi kwa kutumia mabaraza ya kimila maarufu kama ndaga shida.
 
Kwa upande wao askari waliotunukiwa vyeti hivyo wamesema wataendelea kufanya kazi yao kwa weledi na kuzingatia maadili ya jeshi la polisi.

BOMU LILOTEGWA TBC SONGEA LATEGULIWA NA JWTZ


  • LILIKUWA LA KIENYEJI
  • LIMETEKEZWA PAPA HAPO
Bomu lililotengenezwa kienyeji  kama linavoonekana katika picha.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela akipata maelekezo kutoka kwa mtaaram wa mabomu ambaye ni kamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) kabla ya kulitegua bomu hili.

Hili ni eneo la tukio ambalo limezungushiwa mkanda huu wa pilisi uliandikwa hairuhusiwi kupita eneo hili,Lakini chini ya huo mti kama inavoonekana katika picha kukiwa na udongo umetifuliwa ndipo mahara ambapo lilitegwa bomu hili la kutengenezwa kienyeji pia hapo ndipo huwa wanakaa askari wa Usalama barabarani kwa kujikinga na jua ama kupumzika pindi wanapokuwa kazini
Bomu lililotengenezwa kienyeji
Mtaaramu toka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania akiweka vifaa vyake vya kutegulia bomu hilo lililo tengenezwa kienyeji.
Mtaaramu toka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania akiwa anaonyesha umahili wake alionao aweze kulitegua bila kuleta madhara yoyote yale katika jamii(Picha na demasho.com)
-------------------------
 Jeshi la polisi kwa kushirikiana na Jeshi la Ulinzi la wananchi Tanzania(JWTZ) wamefanikiwa kulipua bomu lililotegwa katika eneo la kituo cha kurushia matangazo kilichopo mshangano cha shirika la utangazaji Tanzania (TBC) Songea Mkoani Ruvuma siku ya jana majira ya saa moja jioni.

Bomu hili linalosadikiwa kutengenezwa kienyeji nawatu wasiojulikana lilitegwa hatua  zinazokadiliwa thelathini kutoka kitika kituo kilipo katika eneo ambalo askari wa usalama barabarani wanakaa kwa ajili kufanya kazi zao za kila siku.

 Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela amesema kwamujibu wa wataalamu wa milipuko kutoka jeshi la Ulinmzi la wananchi wa Tanzania bomu hili linaonekakana limetengenezwa kienyeji.
ameitaka jamii kutoa ushrikiano kwa jeshi la polisi ili liweze kuwabaini watu waliowalipua kwa bomu lililotengenezwa kienyeji askari polisi watatu  wakiwa katika doria katika kata ya misufini manispaa ya songea.

Msikhela amesema Jeshi la polisi linafanya jitihada za kuwapata watu hawa wanaohusika na mtandao huu wa utegaji wa mabomu na ulipuaji, Aidha ameitaka jamii kutoa ushrikiano kwa Jeshi la Polisi ili liweze kuwabaini watu wanaousika na matukio ya namana hii.

Na hii ni mara ya pili katika manispaa ya songea kutokea kwa matukio haya ambapo tarehe Oktoba 16 mwaka huu askari watatu wa jeshi la polisi katika wilaya ya Songea mkoani Ruvuma,  walijeruhiwa kwa kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu la kutupwa kwa mkono ambalo lilisadikiwa kutengenezwa kienyeji, katika eneo la matarawe mjini songea mkoani Ruvuma.

Askari hao walikutwa na mkasa huo saa moja na nusu usiku wakati wakiwa katika doria ambao ni WP Felista Abel, PC John Kaduma na PC Ramadhani Ally

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Joseph Mkirikiti akizungumza na mtandao huu wa demasho  kwa njia ya simu amesikitishwa na kitendo hicho cha utegeji wa Mabomu ikiwa nikutaka kuhatarisha amani iliyopo katika mkoa huu wa Ruvuma.
Aidha amesema serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama watahakikisha wanawasaka na kuwakamata walewote wanaohusika na vitendo hivi.

MKUTANO WA WAHITIMU WA CHUO CHA ELIMU YA BIASHARA (CBE) WANAOISHI NYANDA ZA JUU KUSINI


Mkuu wa Mkoa Mstaafu wa Mbeya Mh. Johm Mwakangale ambaye ndiye Mgeni Rasmi katika Mkutano wa wahitimu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE)  wanaoishi nyanda za Juu kusini waliowahi kusoma katika chuo hicho kuanzia mwaka 1965-2014 na yeye akiwa ni mmoja wa wanafunzi ambaye alisoma katika chuo hicho mwaka 1967 na ambaye pia alikuwa ni Mkufunzi katika chuo hiki na Mlezi wa Umoja wa wana CBE waishio nyanda za juu kusini akitoa hotuba yake ambapo, alikishukuru chuo cha CBE kwa kufanya mkutano huu muhimu wa kuwaalika wahitimu wote kukutana pamoja pia aliongeza kuwa CBE ni chuo cha Kuigwa kwa sababu hata Viongozi baadhi yao Tanzania wamesoma katika Chuo hicho mfano Omar Kingi Mhasibu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Stagomena Tax Katibu Mtendaji SADC, Harry Katillya aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Suzan Kaganda-RPC Tabora, Dkt. Ramadhani Dau Mkurugenzi Mtendaji NSSF na Graciano Kanzugala Mwenyekiti wa TCCIA kanda za nyanda za juu Kusini , Alimalizia kwa Kuzindua umoja huo wa wanafunzi na kusema CBE ni chuo ambacho kimezalisha wataalam wengi . Mwisho alizindua Rasmi Umoja wa wana CBE waishio nyanda za Juu kusini mkutano uliofanyika Tarehe 4.10.2014
 Mkuu wa Mkoa Mstaafu wa Mbeya Mh. John Mwakipesile akisaini kitabu cha wageni wakati akiingia katika Mkutano huo
Meza kuu
 Muongozaji wa Mkutano MC Bwana Ben akiwa anatoa Muongozo wakati wa Mkutano huo 
 Mkuu  wa Chuo Cha Elimu ya Biashara Kampasi ya Mbeya Ndugu Deonise Lwanga akitoa utambulisho pamoja na Kumkaribisha Mkuu wa Vyuo vyote vya CBE Tanzania.
 Mkuu wa Vyuo vyote vya Elimu ya Biashara (CBE ) Profesa Emmanuel Mjema akitoa nasaha zake na kueleza malengo makuu ya Mkutano huo, alieleza kuwa wanafunzi waliowahi kusoma katika Chuo cha CBE kuwa ni Mabalozi wazuri ambao ndio wanaweza kukitangaza vyema chuo hicho kwa kuwa wao ndio wanajua vyema chuo hicho, aliongeza kuwa wanafunzi waliowahi kusoma katika Chuo cha CBE wanasaidia chuo kwa kutoa mrejesho wa chuo hicho,pia inasadia katika Elimu, na aliongeza kuwa Alumni ni muhimu katika maswala ya kuandaa Semina, Makongamano na mambo kama hayo, Mwisho Alimshukuru Mgeni Rasmi kwa kukubali mwaliko na kujumuika katika Mkutano huo pamoja na wanachuo wote waliowahi kusoma katika chuo cha CBE
Makamu Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) , Mipango, Fredha na Utawala Dkt. Peter Msami akitoa Salamu za Shukurani kwa niaba ya chuo cha CBE
 Mkurugenzi wa Fedha wa Chuo cha CBE Bwana John Mwangobola akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa Mkutano huo.
Mwenyekiti wa kwanza wa Umoja wa wana CBE waishio Nyanda za juu Kusini ambao umezinduliwa Rasmi Tarehe 04.10.2014 Bwana Boyd Faustin Mwakyusa akitoa neno la Shukurani Baada ya uteuzi huo
Msimamizi wa Taaluma kutoka Chuo cha CBE Kampasi ya Mbeya Bwana Kayombo akizungumza jambo wakati wa Mkutano huo
 Viongozi wa kwanza wa Umoja wa wana CBE waishio nyanda za Juu Kusini wakiwa pamoja na Mlezi wao Mkuu wa Mkoa Mstaafu wa Mbeya Mh. John Mwakipesile wa nne Kutoka Kushoto Mara baada ya Uchaguzi huo
 Washiriki wakiwa wanafuatilia Mkutano kwa umakini
Picha ya Pamoja
 Picha za ajali iliyoua wanafunzi watano Mtwara leo Jan 22 pamoja na taarifa kamili.

Picha za ajali iliyoua wanafunzi watano Mtwara leo Jan 22 pamoja na taarifa kamili.


IMG-20140122-WA0006Wanafunzi watano wa shule ya sekondari Mustafa Sabodo iliyopo nje kidogo ya mji wa Mtwara wamefariki Dunia na wengine 47 kujeruhiwa baada ya kugongwa na gari wakati  wakikimbia mchakamchaka mapema leo asubuhi.
Taarifa inasema kuwa gari hilo lenye namba za usajili T174 AED aina ya Mercides Benz lilikuwa likiendeshwa na Dereva Baraka Mgwegwe ambapo likiwa kwenye mwendo kasi liliacha njia na kuwagonga wanafunzi hao ambao walikuwa kandokando ya barabara wakikimbia mchakamchaka kurejea shuleni.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara Zelothe Steven na Mganga Mkuu wa hospital hiyo wamethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na amewataja wanafunzi waliopoteza maisha kwa ajali hiyo ni pamoja na Khairati Mohamed Said, Mwanahamisi Mohamed,Nasma Salum Mpunja, Hilda Matias Nguli na Farida Ally ambao wote wanasoma kidato cha kwanza katika shule hiyo.
Mpaka sasa hali za majeruhi 21  waliolazwa hospitalini hapo zinaendelea vizuri ukiondoa mmoja ambaye amehamishiwa katika hospitali ya mission Nyangao mkoani Lindi kwa matibabu Zaidi huku dereva aliyesababisha ajali hiyo akishikiliwa na polisi kusubiri sheria kufuata mkondo wake.
Dereva Baraka Mgwegwe ameongea na millardayo.com na kusema>>’Nimetoka nyumbani kwangu sa 10 na nusu alfajiri naelekea kumpeleka Mgonjwa Lindi  Hospital nilikuwa na ndugu zangu wawili na mgonjwa kwenye gari,tulipofika maeneo ya Pacha ya kwenda Mchuchu mbele yangu kulikua na lori imesimama na nyuma ya lori ndio kunasadikiwa kuwa kulikuwa na hao wanafunzi’
‘mimi nilikuwa nimejiandaa kupishana na hiyo lori na wanafunzi na wanafunzi nao wanaingia barabarani sehemu ambayo mimi nilikuwa najiandaa kupita mimi sikumuona mwanafunzi hata mmoja kilichotokea pale nikutokea kwa hiyo ajali ya kuwagonga hao wanafunzi baada ya kuwagonga nikaenda kusimama kama mita 20 kutoka eneo la tukio nikatafuta usafiri wa piki piki nikaja kituoni hapa’.
Hizi ni picha za gari iliyosababisha ajali hiyo.2
1
Hizi ni picha za baadhi ya wanafunzi waliolazwa hospital ya mkoa wa Mtwara kufuatia ajali hiyo.
IMG-20140122-WA0007
IMG-20140122-WA0009
IMG-20140122-WA0004
IMG-20140122-WA0002
Hii ni taarifa ya Jeshi la polisi Mkoa wa Mtwara.
 press2
002
Na Millard Ayo

YALIYOJIRI 2013: SHEHENA ZA VIPODOZI FEKI ZAKAMATWA MKOANI IRINGA



 Baadhi ya shehena za vipodozi  zilizokamatwa na jeshi la polisi mkoa wa Iringa baada ya kushushwa katika roli katika makao makuu makuu ya jeshi mkoa wa Iringa.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi akionyesha shehena ya vipodozi vilivyokamatwa na jeshi hilo mkoani  Iringa katika makao makuu ya jeshi hilo jana.(picha na Denis Mlowe)


JESHI la polisi mkoa wa Iringa limefanikiwa kukamata shehena ya vipodozi vyenye thamani ya mamilioni ya shilingi iliyokuwa inasafirishwa kutoka nchini Zambia kwenda jijini Dar es Salaam vilivyopigwa marufuku kwa matumizi ya binadamu.

Shehena hizo zilikuwa zimebebwa na gari aina ya lori la mafuta lenye namba za usajili T 247 BHP na tela lenye namba usajili T 598 BMK mali ya World Oil Ltd ya jijini Dar es Salaam.

Waliokamatwa na shehena hiyo ya vipodozi ni  Dereva wa lori Mohamed Sadru(23) na Kassimu Kaifa anayesadikika ndio mwenye mali.

Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi  amethibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao na kusema kuwa walipata taarifa za kiitelejensia kutoka Tunduma kuwa kuna lori linasafirisha shehena hiyo kutoka nchini Zambia.

Mungi alisema walijiweka tayari kulikamata gari hilo kwa kukaa barabara kuu kuanzia saa moja jioni hadi ilipofika saa kumi alfajiri ndipo gari lilipofika na kukamatwa.

Anaongeza kuwa maafisa wa polisi mkoa wa Iringa walijipanga vizuri kuweza kulikagua gari hilo na waligundua kuna shehena kubwa ya vipodozi vilivyopigwa marufuku na TFDA na kuwaweka chini ya ulinzi dereva na roli hilo.

“Cha kushangaza gari la mafuta kuweza kubeba  vipodozi hivi vilivyopigwa marufuku hivyo tukaamua kuwashirikisha wadau wengine ambao ni TRA, TFDA na Tanroad kuweza kubaini makosa ambayo watuhumiwa hao wamefanya katika usafirishaji wa shehena hiyo.” Alisema Mungi

Mungi alisema uchunguzi wa awali unaonyesha shehena hiyo ina thamani kubwa na ndio maana watuhumiwa walikuwa wanasafirisha kwa njia ya magendo na wanaendelea kuchunguza kubaini thamani halisi ya mzigo huo.

Kwa upande wake Mratibu wa Mamlaka wa Chakula na Dawa (TFDA) mkoa wa Iringa, Deodata Rukupwa alisema shehena iliyokamatwa asilimia 100 ina kemikali iliyopigwa marufuku ya Hydroqunone na mamlaka hiyo.

Alisema vipodozi hivyo vitateketezwa kwa pamoja na jeshi la polisi na gari hilo kutaifishwa na serikali kutokana na kubeba mzigo wa magendo.

Rukupwa aliwataka wananchi kuwa makini katika kutumia vipodozi vilivyopigwa marufuku na serikali na kutoa taarifa wanapobaini kuna vipodozi vilivyopigwa marufuku vinauzwa.
Na Denis Mlowe,Iringa
kwa hisani ya Pamoja blog

YALIYOJIRI X-MASS:MBONI AJUMUIKA NA WATOTO YATIMA MKOANI IRINGA KUSHEREKEA SIKUKU YA CHRISMAS






Mtangazaji  maarufu  wa kipindi cha Mboni Show kinachorushwa na  kituo  EATV  Bi Mboni A .Masimba anataraji  kula  sikukuu ya Krismas na mwaka  mpya  na  watoto   yatima mkoani Iringa .
 Akizungumza na mtandao  huu wa www.francisgodwin.blogspot.com ,Mboni amesema  kuwa akiwa kama mtanzania na mwanahabari ameamua  kuandaa chakula  cha  pamoja  na  watoto  yatima  wa  vituo  vitatu vya mkoa wa  Iringa .
 
Alisema  kuwa  hafla  hiyo  ya  kula  chakula na yatima  itafanyika  siku  ya Desemba 25 mwaka  huu ambayo  itakuwa ni sikukuu ya Krismas .
Bi Mboni  alisema  kuwa  mbali ya  kuendesha  vipindi  vyake  katika kipindi  chake cha  Mboni Show bado ameguswa  kula pamoja na  watoto  hao 230  pamoja na wageni  mbali mbali  watakaofikisha idadi  ya watu 300.
Alisema  kuwa  hafla  hiyo  itafanyika katika ukumbi wa Hihglands mjini  Iringa  na  kuwa  vituo ambavyo vimealikwa ni pamoja na TOSAMAGANGA , Upendo Centre  Sabasaba na YATIMA MOYO KWA MOYO  kilichopo Mufindi kata ya  Bumilayinga

Hata  hivyo  alisema mbali ya  chakula  hicho   pia  watoto  hao  yatima  watapata  zawadi mbali mbali  kutoka kwake.
Mboni  amesema  kuwa  amekuwa  bega kwa bega na watoto  yatima  na  kuwa mbali  ya kula na  watoto  hao pia  amekuwa akifanya  hivyo wakati  wa sherehe  za Ramadhan pia  kutokana na kipindi  chake  kutazamwa na  watanzania  wote .
Hivyo  alisema  lengo  kuu ni kuwakumbusha  watanzania  juu ya  kuwakumbuka  watoto  yatima  kama  ambavyo  wamekuwa  wakichangia sherehe mbali mbali .
Na Kamanda wa matukio  

Kategori

Kategori