Mtangazaji maarufu wa kipindi cha
Mboni Show kinachorushwa na kituo EATV Bi Mboni A .Masimba anataraji
kula sikukuu ya Krismas na mwaka mpya na watoto yatima mkoani
Iringa .
Akizungumza na mtandao huu wa
www.francisgodwin.blogspot.com ,Mboni amesema kuwa akiwa kama mtanzania
na mwanahabari ameamua kuandaa chakula cha pamoja na watoto
yatima wa vituo vitatu vya mkoa wa Iringa .
Alisema kuwa hafla hiyo ya kula
chakula na yatima itafanyika siku ya Desemba 25 mwaka huu ambayo
itakuwa ni sikukuu ya Krismas .
Bi Mboni alisema kuwa mbali ya
kuendesha vipindi vyake katika kipindi chake cha Mboni Show bado
ameguswa kula pamoja na watoto hao 230 pamoja na wageni mbali
mbali watakaofikisha idadi ya watu 300.
Alisema kuwa hafla hiyo itafanyika
katika ukumbi wa Hihglands mjini Iringa na kuwa vituo ambavyo
vimealikwa ni pamoja na TOSAMAGANGA , Upendo Centre Sabasaba na YATIMA MOYO KWA MOYO kilichopo Mufindi kata ya Bumilayinga
Hata hivyo alisema mbali ya chakula hicho pia watoto hao yatima watapata zawadi mbali mbali kutoka kwake.
Mboni amesema kuwa amekuwa bega kwa
bega na watoto yatima na kuwa mbali ya kula na watoto hao pia
amekuwa akifanya hivyo wakati wa sherehe za Ramadhan pia kutokana na
kipindi chake kutazamwa na watanzania wote .
Hivyo alisema lengo kuu ni
kuwakumbusha watanzania juu ya kuwakumbuka watoto yatima kama
ambavyo wamekuwa wakichangia sherehe mbali mbali .
Na Kamanda wa matukio