Showing posts with label 2017 at 01:56PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 01:56PM. Show all posts
Nyepesi Nyepesi….John Boko Atua Simba

Nyepesi Nyepesi….John Boko Atua Simba

Klabu ya Simba imemsainisha John Boko Mkataba wa Miaka miwili
Taarifa zinaeleza mkataba huo ni wa awali na inaonekana Bocco ameamua kutua Simba baada ya makubaliano yake na Azam baada ya mkataba wake kwisha, kuonekana unakwenda kombo.
Hata hivyo, Bocco amekuwa hapokei simu ili kulithibitisha hilo suala ingawa hivi karibuni alikanusha kila kilichoandikwa kwenye akaunti yake ya Instagram kuhusiana na kwamba ana mpango wa kuondoka Azam.
Alidai akaunti yake ilikuwa imetekwa lakini hali halisi ilionyesha kwamba hakuwa amezungumza lolote.
Afisa Habari wa Azam FC, Jaffar Iddi yeye alisema walikuwa katika mazungumzo na Bocco baada ya mkataba wake kufikia tamati.

from Blogger http://ift.tt/2rCnmSe
via IFTTT


TANZIA Mbunge Viti Maalum CHADEMA afariki dunia

Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Viti Maalum (CHADEMA) akiwakilisha walemavu Dkt. Elly Macha amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Image result for Dkt. Elly Macha
Dkt Elly Macha (Enzi za uhai wake)
Msemaji wa CHADEMA Tumaini Makene amethibitisha kutokea kwa kifo hicho, ambapo amesema mbunge huyo alikuwa akipatiwa matibabu mkoani Arusha.
“Taarifa ni za kweli, mbunge Viti Maalum Dkt. Elly Macha amefariki, lakini sijapata bado taarifa za kina, lakini ninachojua ni kwamba amekuwa akipatiwa matibabu kwa muda mrefu Arusha” Amesema Makene.
Tazama video Mtoto amvua kofia
 Papa Francis

from Blogger http://ift.tt/2nqzmAO
via IFTTT


Kategori

Kategori