Showing posts with label June 04. Show all posts
Showing posts with label June 04. Show all posts
Daktari atuhumiwa kuwapa mimba wanawake 60 bila wenyewe kujua

Daktari atuhumiwa kuwapa mimba wanawake 60 bila wenyewe kujua

Mahakama moja nchini Uholanzi imeidhinisha ombi la familia zinazotaka vipimo vya vinasaba DNA vichukuliwe juu ya mmiliki wa kliniki ya uzazi ya daktari anayeshutumiwa kutumia mbegu zake za kiume katika makumi kadhaa ya kesi.
Jan Karbaat anatuhumiwa kuwa baba wa watoto wapatao 60 katika kituo cha afya alichomiliki katika eneo la Bijdorp, karibu na Rotterdam.
Vipimo sasa vitafanyika juu ya vifaa vilivyochukuliwa kutoka kwenye nyumba yake baada ya kifo chake mwezi Aprili, akiwa na umri wa miaka 89.
Wakili wa familia yake anasema hakuna ushahidi wa kuthibitisha madai hayo.
Jan Karbaat alijiita “Muasisi wa fani ya uzazi wa kusaidiwa”.
Kliniki yake ilifungwa mwaka 2009 wakati kulikuwa na taarifa kwamba alidaiwa kugushi data, uchunguzi na maelezo ya watoaji wa mbegu za kiumena kuzidisha idadi inayoruhusiwa ya idadi ya watoto sita kwa kila anayejitolea kutoa mbegu za uzazi.
Katika kesi ya mahakamani mwezi uliopita, wakili wa wazazi 22 na watoto walisema kwamba visa vinavyoshukiwa vinajumuisha mtoto wa mteja wao mwenye macho ya hudhurungi wakati alikuwa na macho ya blu na mvulana wa mteja wakeambaye anasura inayofanana na daktari.
Taarifa za vinasaba DNA zitasalia kuwa siri hadi pale watoto watakapoonyesha kuwa kuna sababu za kuamini daktari alikuwa baba yao, kulingana na mwandishi wa BBC Anna Holligan, ambaye alikuwa katika mahakama ya wilaya ya Rotterdam.
Hatimae, kama taarifa za vinasaba-DNA zitawiana na watoto hao ambao wengi wao walizaliwa miaka ya 1980s, kutakuwa na tumaini la kumshitaki daktari, labda kwa misingi ya kwamba hawangepaswa kuwepo, ameongeza Anna Holligan.
Joey, ambaye anaamini Jan Karbaat huenda ni baba yake ameiambia BBC: ” Ina maana kubwa kwangu … Tunatumai kupata majibu .”
Wakili wa familia ya Karbaat anapinga kufanyika kwa vipimo vyovyote vya vinasaba DNA.
Wakati wa uhai wake, daktari mwenyewe alikataa kufanya vipimo hivyo.
Hata hivyo, mwezi uliopita,kijana yake Jan Karbaat alitoa vinasaba vyake DNA vipimwe ambavyo vilionyesha kuwa daktari anaweza kuwa baba wa watoto 19, waliozaliwa kwa njia ya uzazi wa kutungishwa mbegu kwa lugha ya kitaaamu IVF, kulingana na ripoti ya shirika la habari la AFP.

from Blogger http://ift.tt/2rGfgaG
via IFTTT


Jinsi ya Kumtambua Anayekupigia Kwenye Simu yako Kwa Jina na Mahali Alipo

Jinsi ya Kumtambua Anayekupigia Kwenye Simu yako Kwa Jina na Mahali Alipo

Leo nitakuonesha hatua ambazo zitakusaidia wewe kumfahamu nani anayekupigia kwenye simu yako na wapi anapotokea. Utaweza kufahamu kama simu hiyo inatoka kwenye kampuni au ni watu wanaosumbua. Nimeandalia njia mbili ambazo zitakusaidia kufuatilia namba ya simu kwa jina na mahala inapotokea.
Namba ngeni na binafsi ni moja kati ya vitu vinavyotisha katika maisha yetu ya kila siku unakutana na namba binafsi ambayo siyo ya kawaida tofauti kabisa na tulizozizoea.
Namba nyingi ambazo zinakuwa tofauti mara nyingi hutoka kwa makampuni ya kutafuta masoko kwa njia ya simu ili kutangaza bidhaa au huduma za wateja wao mbali mbali ambazo unaweza ukazipenda au usizipende. au namba ya mtu ambaye haipo katika simu.
Zifuatazo ni njia ambazo zinatumika kutambua namba ya simu ambayo imeingia kwenye simu yako ambapo utaweza kutambua jina na mahala alipo mtu anayekupigia.
Kutumia tovuti ya Truecaller
Hatua ya 1. Fungua tovuti ya Truecaller kwenye pc.
Tovuti ya Truecaller
Hatua ya 2. Chagua nchi ambayo unatokea kwenye orodha kama unatokea Tanzania chagua hapo kisha andika namba ya simu ya mtu ambaye unataka kumfahamu halafu bonyeza search.
tovuti ya Truecaller
Hatua ya 3. Kitatokea kiboksi ambacho kinakutaka ujiunge na true caller ili kuweza kupata taarifa za namba uliyo andika. Kama una account ya Gmail unaweza ukaitumia, au unaweza ukajiunganisha nao kwa kupitia account yako ya facebook kwa urahisi zaidi chagua kisha endelea.
Chagua njia za kujisajili ili kupata matokeo unayotafuta
Baada ya kumaliza usajili utapewa taarifa zote za namba uliyoandika ikiwa ni jina pamoja na mahali alipo. Taarifa hizo zinakuwa ni kweli kwa 90%.
Truecaller itakuletea taarifa za namba ya mhusika kama jina na mahala alipo
Hiyo ndiyo ilikuwa njia rahisi ya kufahamu namba ngeni kwa kutumia tovuti ya True caller. Nadhani kuanzia sasa hakuna namba ngeni mpya tena shikamoo Truecaller.
Kutumia App ya Truecaller kwenye simu yako
Unachotakiwa kufanya fungua playstore kisha pakua app ya Truecaller halafu install kwenye simu yako.
Hatua ya 1. Pakua app ya Truecaller moja kwa moja kwenye simu yako kwa kubonyeza hapa hiyo link inayofuata >> Truecaller pakua hapa
Hatua ya 2. Baada ya kupakua Truecaller kwenye playstore fanya installation ya app hiyo kwenye simu yako kisha ifungue.
Muonekano wa app ya Truecaller
Hatua ya 3. Utaona sehemu ya kutafuta jina au namba, tofauti na uzuri wa hii app haihitaji ujisajiri ili kuweza kupata taarifa za mtu unayetaka kumfahamu kama ilivyokuwa kwenye tovuti yake, kwa hiyo unaweza ukaandika namba yake hapo kisha utaona jina na mahali alipo.

from Blogger http://ift.tt/2rFjBLc
via IFTTT


Mwanzilishi wa kampuni ya Alibaba Jack Ma aliwahi kuomba kazi katika makampuni 30 na kukataliwa kabla ya kuwa mtu tajiri zaidi China.

Mwanzilishi wa kampuni ya Alibaba Jack Ma aliwahi kuomba kazi katika makampuni 30 na kukataliwa kabla ya kuwa mtu tajiri zaidi China.

Jack Ma ni moja kati ya watu matajiri zaidi duniani akiwa na utajiri unaofikia dola bilioni 20.4, mtandao wake wa Alibaba kwa siku unaingiza watu milioni 100, ambapo unaunganisha wauzaji na wanunuzi kutoka sehemu mbali mbali duniani.
Ila kabla ya kuwa mtu tajiri zaidi China, Ma alipitia vikwazo vingi sana maishani mwake.
Katika mahojiano ya hivi karibuni na Charlie Rose, mfanyabiashara huyo alisema alishafeli mitihani ya kujiunga na vyuo mara tatu mfululizo.
Baada ya kuachana na chuo, Ma aliomba kazi kwenye makampuni 30 tofauti na kukataliwa.
“Niliwahi kwenda kuomba kazi ya kuwa askari polisi; waliniambia, ‘we haufahi,'”.”Pia niliwahi kwenda kuomba kazi katika mgahawa wa KFC walipofungua tawi lao karibu na mtaa wetu. Watu ishirini na nne tuliomba kazi pale. Kati ya watu hao ishirini na nne tulioomba kazi mimi peke yangu ndiye niliyekataliwa.” Alimwambia Rose.
Wakati anaanzisha mtandao wa Alibaba mwaka 1998, Ma alikutana na vikwazo vingi sana.
Mtandao wake huo haukuweza kumuingizia kipato kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo kutokana na mabenki kutokuwa tayari kufanya kazi na Ma hivyo njia za malipo katika mtandao huo zilikuwa ni ngumu.
Ma aliamua kuja na njia mbadala ya malipo katika mtandao wake huo iliyoitwa Alipay. Programu hiyo ilikuwa inawezesha wauzaji na wanunuzi kutoka mataifa mbali mbali kuweza kutumiana pesa kwa njia nyepesi zaidi.
“Watu wengi nilikuwa nikiwaambia kuhusu Alipay, waliniambia, “Hilo ni wazo la kijinga kuwahi kufikiriwa na wewe,'”alisema Ma.”Mimi sikujari kama wao walisema ni wazo la kijinga cha msingi ni kwamba watu wataweza kutumia mfumo huo basi.”
Leo hii, watu milioni 800 wanatumia mfumo wa Alipay kufanya manunuzi katika mtandao wa Alibaba.

from Blogger http://ift.tt/2rxviSs
via IFTTT


Jeshi la polisi Dubai kuanza kutumia gari za umeme kutoka BMW

Jeshi la polisi Dubai kuanza kutumia gari za umeme kutoka BMW

Jeshi la polisi jijini Dubai wameongeza gari mpya za BMW i3 ambazo zinatumia umeme kwenye orodha ya gari zao, Jeshi la polisi Dubai linafahamika ulimwenguni kwa kuwa na gari za kisasa na zenye gharama kubwa sana.
Gari kama Ferrari, Mercedes Benz, Bugatti Veyron, Aston Martin, Bentley, McLaren ni aina ya magari ambayo yanamilikiwa na jeshi la polisi jijini Dubai, ila idadi kubwa ya magari hayo hayatumiki kwa kufukuzia wahalifu bali ni kwa maonesho.
Gari hiyo ya BMW i3 ambayo inatumia umeme ilioneshwa kwa mara ya kwanza kwenye maonesho ya magari jijini humo, ambapo wazili wa nishati wa jiji hilo Al-Mazrouei alisema wanampango wa kuongeza magari mengi zaidi yanayotumia umeme katika jeshi la polisi la Dubai kwa asilimia 10 ya magari yote ya serikali ambapo matumizi ya magari hayo ya umeme yatasaidia kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa unaosababishwa na gari zinazotumia mafuta kwa asilimia 15 ndani ya miaka 4 ijayo.
Jeshi la polisi nchini Marekani, Ujerumani, Italia, Australia na Uingereza tayari nao wameshaanza kutumia gari hizo za BMW i3 kwenye majeshi yao ya polisi.

from Blogger http://ift.tt/2sDdPaw
via IFTTT


Maajabu..Namba ya Simu ya Ben Saanane (Msaidizi wa Mbowe) Aliyetoweka Yatumika Whats App

Maajabu..Namba ya Simu ya Ben Saanane (Msaidizi wa Mbowe) Aliyetoweka Yatumika Whats App

Wakati hofu ikiwa imetenda baada ya jumla ya miezi minane kupita tangu alipopotea kwenye mazingira ya kutatanisha, matumaini mapya yameanza kuibuka baada ya simu yake kuonekana imetumika kwenye mitandao ya kijamii.
Ben Saanane ambaye alikuwa msaidizi wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe alitoweka mwaka jana na kumekuwapo na hisia nyingi kuwa huenda alishafariki dunia kutokana na kuwa, hakuna yeyote anayefahamu alipo kijana huyo aliyekuwa akichipukia katika siasa nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa gazeti la TanzaniaDaima, simu ya Ben jana alitumika majira ya saa tatu asubuhi ambapo ilionekana namba yake ikijitoa kwenye makundi ya WhatsApp. Imeelezwa kuwa namba yake ilijitoa kwenye makundi mengi huku ikiwaacha na mshangao mkubwa wajumbe (members) wa makundi hayo.
Hofu ya kuwa kijana huyo hayupo hai ilichangiwa na jibu alilolitoa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa bungeni ambapo alisema, “familia ya mtajwa (Ben Saanane) aliyetangulia mbele za haki au vinginevyo, uchunguzi wa suala lake utakapokamilika, taarifa rasmi itatolewa.”
Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo alipokuwa akijibu swali la Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe Aprili 20 mwaka huu aliyetaka kujua kwanini serikali imekuwa kimya sana kwenye suala la kupotea kwa msaidizi wake.
Namba ya Ben Saanane iliyotoka kwenye makundi ya whatsapp ni 0768078523 ambayo imesajiliwa kwa jina lake na amekuwa akiitumia kabla ya kutoweka.
Makundi ambayo namba hiyo inadaiwa kujitoa ni pamoja na Jukwaa la Siasa, Chadema Tanzania, Friends of Bavicha, Tanzania nchi yetu sote na Bantu Politics Tz Kwanza.
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema alisema kuwa tukio hilo limewashtua sana kuona mtu ambaye ametoweka simu yake ikitumika kujitoa kwenye makundi ya whatsapp. Aidha, alihoji Polisi wanachukua hatua gani kujua alipo au simu yake ilipo.
Kwa upande wa familia yake, Erasto Saanane ambaye ni mdogo wake Ben alisema kuwa hawajui kama ni yeye au ni nani anatumia simu hiyo kwani hata kwenye kundi la familia amejitoa.
Ndugu huyo alisema hata rafiki zake Ben walisema kwenye makundi mengine amejiondoa pia, na kuwa Jumatano iliyopita ukurasa wake wa Facebook ulitumika ukimuonyesha yupo Tengeru, Arusha.
Aidha baada ya kuona kaka yake amejitoa kwenye makundi hayo, alitoa taarifa katika kituo cha polisi Tabata, na kuwa uchunguzi wa suala hilo umeanza.

from Blogger http://ift.tt/2qOIbug
via IFTTT


Mimi Mars Amkana Dada Ake Vanessa Mdee

Mimi Mars Amkana Dada Ake Vanessa Mdee

Msanii anayechipukia kutoka ‘Mdee Music’ Mimi mars amefunguka na kuweka wazi kwamba hataweza kushirikiana na dada yake Vanessa Mdee katika kuandaa kazi ya pamoja kwa kipindi hiki kwa sababu ya mashabiki zake bado wanashindwa kutofautisha sauti zao
Mars ambaye anafanya vizuri na wimbo mpya unaokwenda kwa jina la ‘Dedee’ amesema kwa sasa yupo kwe wakati mgumu wa kujitofautisha na dada yake huyo kwai sauti zao zimekuwa zikiwachanganya mashabiki zao kiasi cha kuonekana kama Vanessa.
Akizungumza na eNewz ya EATV Mars amesema kwamba “Mission yangu ni kujitahidi kubadilisha suala la kufanana na Vanessa, kwani mashabiki na watu wengine wamekuwa wakisema tunafanana uimbaji . Nadhani kwa sababu bado ni mapema hawajazoea kwani mimi ni mgeni lakini
niyahakikisha nakuwa tofauti ila ikishindikana kubadilika, nadhani watakuwa wameshazoea na hata kututofautisha wao wenyewe. Lakini niwe mkweli Vanessa siwezi kufanya naye kazi sahivi mpaka watu waweze kututofautisha ili isije ikaonekana yeye ndo kaimba wimbo wote peke yake, pia hatuwezi kuunda kundi moja la muziki bali tutaendelea kusaidiana na kuachia kazi huko mbeleni”- Mimi Mars.

from Blogger http://ift.tt/2rF6s4Z
via IFTTT


Ronaldo Aweka Rokodi Mpya UEFA..Atwaa Ufungaji Bora kwa Miaka Mitano Mfululizo..!!!

Ronaldo Aweka Rokodi Mpya UEFA..Atwaa Ufungaji Bora kwa Miaka Mitano Mfululizo..!!!

Cristiano Ronaldo ameithibitishia dunia yeye ni mchezaji wa aina yake baada ya kuweka rekodi ya kuwa mfungaji Bora wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa misimu mitano mfululizo.
Ronaldo amefunga mabao mawili wakati Real Madrid ikiitwanga Juventus kwa mabao 4-1 na kube ubingwa wa Ulaya.
Mabao hayo mawili yamemfanya amfikie na kumvuka mpinzani wake, Lionel Messi wa Barcelona ambaye alikuwa na mabao 11.
MISIMU
2017- Mabao 12
2016- Mabao 16
2015-Mabao 10
2014- Mabao 17
2013-Mabao 13.

from Blogger http://ift.tt/2sD0GOL
via IFTTT


Mamia Wachangamkia Ofa ya Kuingia Hifadhini Bure..!!!

Mamia Wachangamkia Ofa ya Kuingia Hifadhini Bure..!!!

Mamia ya watu wamejitoza kutembelea Hifadhi ya Manyara na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kutokana na ofa ya kuingia bure hifadhini, iliyotolewa na Serikali.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kutembelea hifadhi hizo jana (Jumamosi), wameipongeza Serikali kwa ofa hiyo iliyowawezesha kushuhudia vivutio vya utalii.
Cecilia Magandila, mkazi wa Mto wa Mbu wilayani Monduli, amesema ameshuhudia vivutio vingi katika hifadhi ya Manyara ambavyo hakuwahi kuviona.
“Nimeona wanyama, chemchem za maji ya moto na mazingira mazuri ambayo sikuwahi kuyaona,” amesema.
Mpishi mkuu wa hoteli ya Serena Manyara, Gervas Mhina na wafanyakazi wenzake kwa nyakati tofauti wakiwa katika lango la kuingia Hifadhi ya Ngorongoro na Serengeti wamesema uamuzi wa Serikali utasaidia kuwafanya Watanzania kupenda uhifadhi.
Mhina amesema ni jambo la aibu kwa watalii kutoka Ulaya kuja kutembelea hifadhi na Watanzania hata wanaoishi jirani, hawajawahi kuingia hifadhini kushuhudia vivutio vya utalii.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Manyara, Dk Noelia Myonga amesema kumekuwa na mwitikio mkubwa ambao kwa siku mbili zaidi ya Watanzania 300 wametembelea hifadhi hiyo.
Myonga amesema kujitokeza kwa watu hao kutasaidia kujua umuhimu wa kutunza mazingira na kutembelea vivutio vya utalii.
Ofisa wa Idara ya Uhusiano ya Hifadhi ya Ngorongoro, Nickson Nyange amesema zaidi ya watalii 400 wametembelea hifadhi hiyo kwa siku mbili na hifadhi imeandaa waongoza watalii kusaidia wanaofika.
Nyange ametoa wito kwa Watanzania kutumia fursa ya ofa ya bure kutembelea hifadhi za Taifa ili kuona umuhimu wa kutunza mazingira na kujionea vivutio vya utalii

from Blogger http://ift.tt/2sD9VhK
via IFTTT


Hata Miezi Haijaisha..Yanga Waanza Kuikaba Koo Spot Pesa..Yataka Milioni 400 Ili Kieleweke..!!

Hata Miezi Haijaisha..Yanga Waanza Kuikaba Koo Spot Pesa..Yataka Milioni 400 Ili Kieleweke..!!

YANGA juzi ilipiga hodi kwa wadhamni wao Kampuni ya SportPesa kuomba watanguliziwe Sh milioni 400 kwa ajili ya mishahara ya wachezaji wake. Timu hiyo, inadaiwa mishahara ya miezi mitatu na wachezaji wake walioiwezesha kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara tatu mfululizo ikiwemo msimu uliopita.
SportPesa hivi karibuni iliingia mkataba waudhamini wa miaka mitano na Yanga ambapo kila mwaka itakuwa ikipata Sh milioni 995.
Bosi mmoja wa Yanga aliliambia Championi Jumamosi kuwa, wameifuata SportPesa ili wawape fedha hizo kwa ajili ya kuwalipa mishahara wachezaji ili waanze haraka kambi ya mazoezi kujiandaa na michuano ya SportPesa Super Cup.
Alisema nusu ya wachezaji wamegomea kambi ya timu hiyo ila wameahidi kujiunga nayo endapo watalipwa malimbikizo yao ya mishahara ya miezi mitatu, miongoni mwao ni straika Amissi Tambwe.
“Kama mmoja wa viongozi wa Yanga, nilitoa mapendekezo kwa wenzangu na kamati yetu ya utendaji kwenda kuwaomba SportPesa watutangulizie shilingi milioni 400 kwa ajili ya kuwapa wachezaji wetu madai ya mishahara yao ya miezi mitatu.
“Mambo yanaenda vizuri na hivi karibuni tunatarajia kumaliza kila kitu.
“Ilikuwa lazima twende SportPesa kuomba fedha hizo, kama unavyojua wao ndiyo waandaaji wa michuano hiyo mipya tutakayoshiriki, hivyo tumekutana na kuahidi kulifanyia kazi hilo na mara litakapomalizika basi tutaanza kambi haraka,” alisema mtoa taarifa huyo.
Alipotafutwa Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa kuzungumzia ishu hiyo, alisema: “Wachezaji wanaidai timu mishahara ya miezi mitatu, na viongozi tunatafuta fedha na muda wowote tutawalipa.”

from Blogger http://ift.tt/2rSkIIp
via IFTTT


Mbunge Wema Kaumbika Jamani! Ammwagia Sifa Kedekede

Mbunge Wema Kaumbika Jamani! Ammwagia Sifa Kedekede

ACHANA na umahiri wake awapo bungeni. Weka pembeni sauti yake ya mamlaka na wala usijishughulishe hata kidogo na ujasiri wake wa kumnaga yeyote. Joseph Kasheku ‘King Msukuma’ ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini ametoa ya moyoni na kukiri urembo na ‘figa’ ya msanii Wema Sepetu haupishani na uzuri wa samaki aina ya Nguva, Ijumaa bwana teh…teh… teh…teheeeeee. Jumatatu ya wiki hii, saa saba na dakika zake mchana, mwandishi wetu akiamini King Msukuma atakuwa nje ya viunga vya bunge akiifaidi posho yake, aliamua kumtafuta kupitia simu yake ya mkononi kwa lengo la kubadilishana naye mawazo juu ya mambo mbalimbali ya kimaendeleo ndipo suala la uhusiano wake na Wema Sepetu likaibukia katikati ya mazungumzo na mbunge huyo kulitolea ufafanuzi.
TULIANZIA HAPA
Siku nne mfululizo za wiki iliyopita, mwandishi wa habari hii alimtafuta mbunge huyo kwa lengo la kufanya naye mahojiano juu ya mambo mbalimbali, ambapo alipokea simu na kusikiliza huku akimuomba mwandishi ampigie baada ya dakika tano kwa kile alichodai… “kuna kitu naweka sawa hapa…”
ATAFUTWA TENA
Baada ya muda huo, mwandishi wetu akiwa na shauku kubwa ya kufanya mahojiano na mbunge huyo machachari ikiwa ni mara yake ya kwanza kuingia bungeni akiwakilisha jimbo jipya, alimpigia simu tena lakini hakupokea, lakini alipotafutwa saa moja usiku siku hiyohiyo, alipokea na kumsikiliza mwandishi wetu kwa kirefu.
AKUBALI KUFANYIWA MAHOJIANO
Muda huo wa saa moja, King Msukuma alikubali ombi la mwandishi ambapo alimuomba ampigie siku iliyofuata (Ijumaa) saa nne asubuhi.
ATAFUTWA, ATOA UDHURU TENA!
Gazeti la Ijumaa huwa halikati tamaa. Siku iliyofuata alitafutwa lakini alimtaka mwandishi wetu amuache kwani alikuwa hospitali akidai kusumbuliwa na tumbo, jambo lililomfanya mwandishi kumpa muda wa kupumzika.
JUMAMOSI NA JUMAPILI ZIII…!
Jitihada za kumtafuta mbunge huyu ziliendelea kwa siku za Jumamosi na Jumapili lakini hakuwa akipokea simu jambo lililoacha maswali mengi kwa mwandishi wetu.
HATIMAYE JUMATATU TIII…!
Sisi nao! Jumatatu ya wiki hii, kama ilivyoelezwa kwenye aya ya pili ndipo mheshimiwa huyo aliweza kuzungumza kwa kirefu na mwandishi wetu ambapo bila kuremba alimtaka aeleze alichofanya jimboni kwake ikiwa ni pamoja na kufungukia madai ya muda mrefu ya kuwahi kuwa ‘close’ sana na msanii Wema Sepetu. Kuhusu mambo ya maendeleo jimboni kwake alimtaka mwandishi wetu avute subira hadi Bunge la Bajeti lipite ndipo atapata muda mzuri wa kukusanya data kamili za utendaji na utimizaji wa ahadi zake jimboni, lakini suala la Wema akalifafanua.
MSIKILIZE MWENYEWE
“Hayo mambo hayawezi kuwa na maana yoyote ya kimaendeleo, muhimu ni kuzingatia utendaji kazi wa mtu na si kutazama mambo ya namna hiyo. Wewe mwenyewe unamuona jinsi huyo mwanamke (Wema) alivyo, mtoto kaumbika kama nguva (aina ya samaki, yaani mtoto ni mashallah na, tena kaumbika namna hiyo, kawaida sana katika maisha,” alisema mheshimiwa huyo.
WEMA ATAFUTWA
Mwandishi wetu pia alifanya jitihada za kumtafuta Wema ili kuzungumzia sifa alizopewa na mheshimiwa huyo lakini kila simu yake ilipopigwa ilikuwa ikiita bila kupokelewa. Hata hivyo, kwa wanawake wengi wamekuwa wakijisikia poa sana wanaposifiwa na wanaume na pia si jambo baya kwa mwanaume kumsifia mwanamke. Kwa maana hiyo alichokifanya Mheshimiwa Msukuma ni kueleza hisia zake, jambo ambalo siyo dhambi hata kidogo.

from Blogger http://ift.tt/2rSsOkD
via IFTTT


Utata Waibuka Juu ya Sehemu ya Kuuaga Mwili wa Ndesamburo..Lema Afunguka Haya Mazito Kuhusu Njama za Jeshi la Polisi Kuzuia Tukio Hilo..!!!

Utata Waibuka Juu ya Sehemu ya Kuuaga Mwili wa Ndesamburo..Lema Afunguka Haya Mazito Kuhusu Njama za Jeshi la Polisi Kuzuia Tukio Hilo..!!!

Mbunge wa Arusha mjini, Mh. Godbless Jonathan Lema amedai Vyombo vya usalama vimezuia kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Moshi mjini Mh. Philemon Ndesamburo kwenye uwanja wa Mashujaa.
Kupitia ukurasa wake wa twitter Mh. Lema amedai kuwa amezungumza na Diwani wa kata ya Sombetini Mh. Ally Bananga na kwamba wamezuiliwa na vyombo vya usalama kufanyia hapo shughuli ya kumuaga Mzee Ndesamburo.
“Nimeongea na Mh Bananga aliyeko uwanja wa mashujaa , vyombo vya usalama vinazuia kuaga mwili wa Ndesamburo kuagwa hapo. Hii ni mbaya sana” – Mh. Godbless Lema.

from Blogger http://ift.tt/2qTUQqJ
via IFTTT


Baada ya Kumwagana na Ali Kiba,,Jokate Aaamua Kuweka Wazi Vigezo kwa Kidume Mwingine Anayemtaka..!!!

Baada ya Kumwagana na Ali Kiba,,Jokate Aaamua Kuweka Wazi Vigezo kwa Kidume Mwingine Anayemtaka..!!!

Mrembo Jokate Mwegelo ameamua kuweka wazi juu ya mwanaume anayependa kuolewa naye na kuanzisha familia baada ya miaka mitano.
Akizungumza na gazeti la Mwanachi Jokate ambaye ametajwa kuwa katika orodha la jarida la Forbes Africa la kuwa miongoni mwa vijana walio na umri chini ya miaka 30 wenye mafanikio mbalimbali kwa mwaka 2017.
“Kusema kweli kitu ninachotamani awe nacho mume wangu ni hofu ya Mungu, pia awe mchapakazi na mwenye malengo ya mbele. Mwanaume wa aina hiyo ni rahisi sana kumthamini mke wake, kutambua mwanaume mwenye upendo wa dhati si ngumu kwani unaangalia maisha yake binafsi anaishije na ndugu ,jamaa na marafiki” amesema Joketi.
Pia mrembo huyo amesisitiza kuwa suala la dini si kikwazo kwake kwani amezungukwa na watu wa imani tofauti.
Kwa takribani mwaka mmoja Jokate amekuwa akihusishwa kuwa na mahusiano na mwanamuziki Alikiba ingawa hakuna kati yao aliyewahi kuthibitisha hilo.

from Blogger http://ift.tt/2qTOTKh
via IFTTT


Kategori

Kategori