Jeshi la polisi Dubai kuanza kutumia gari za umeme kutoka BMW

Jeshi la polisi jijini Dubai wameongeza gari mpya za BMW i3 ambazo zinatumia umeme kwenye orodha ya gari zao, Jeshi la polisi Dubai linafahamika ulimwenguni kwa kuwa na gari za kisasa na zenye gharama kubwa sana.
Gari kama Ferrari, Mercedes Benz, Bugatti Veyron, Aston Martin, Bentley, McLaren ni aina ya magari ambayo yanamilikiwa na jeshi la polisi jijini Dubai, ila idadi kubwa ya magari hayo hayatumiki kwa kufukuzia wahalifu bali ni kwa maonesho.
Gari hiyo ya BMW i3 ambayo inatumia umeme ilioneshwa kwa mara ya kwanza kwenye maonesho ya magari jijini humo, ambapo wazili wa nishati wa jiji hilo Al-Mazrouei alisema wanampango wa kuongeza magari mengi zaidi yanayotumia umeme katika jeshi la polisi la Dubai kwa asilimia 10 ya magari yote ya serikali ambapo matumizi ya magari hayo ya umeme yatasaidia kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa unaosababishwa na gari zinazotumia mafuta kwa asilimia 15 ndani ya miaka 4 ijayo.
Jeshi la polisi nchini Marekani, Ujerumani, Italia, Australia na Uingereza tayari nao wameshaanza kutumia gari hizo za BMW i3 kwenye majeshi yao ya polisi.

from Blogger http://ift.tt/2sDdPaw
via IFTTT