Showing posts with label June 11. Show all posts
Showing posts with label June 11. Show all posts
Vincent Bossou: Timu 4 zimempa Ofa,Ikiwemo Hii Moja kutoka Tanzania

Vincent Bossou: Timu 4 zimempa Ofa,Ikiwemo Hii Moja kutoka Tanzania

Bossou ambaye anatarajia kwenda Dubai kwa mapumziko ya Siku 10, amethibitisha kuwa kuna Timu 4 zinamwitaji ikiwemo Singida United na Timu 3 Ulaya.
“Nimepata ofa nchi tatu, kama mambo yataenda vizuri nikitoka Dubai nitaunganisha kwenda Uturuki kufanya mazungumzo ila kwa sasa siwezi kukutajia kwa sababu bado mapema sana,” alisema Bossou.
“Kwa Tanzania nimepata ofa Singida United, wenyewe wako tayari kunipa fedha nzuri, ikiwemo dau la usajili na mshahara mnono, hivyo mambo yakiwa magumu nitarudi kuwasikiliza,”
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2sheGBs
via IFTTT


Bajeti 2017/18 inaenda kuwagusa wengi -Dkt Kigwangalla

Bajeti 2017/18 inaenda kuwagusa wengi -Dkt Kigwangalla

Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na watoto, Dkt Hamisi Kigwangalla amesema katika miaka yake 7 ya uwakilishi bungeni hajawahi kushuhudia bajeti ikishangiliwa kama ya Wizara ya Fedha huku akisema bajeti hiyo inaenda kuwagusa watu wengi.
Dkt Kigwangalla ametumia ukurasa wake wa Instagram kuisifia bajeti hiyo.
Katika miaka yangu saba ya uwakilishi #Bungeni sijawahi kushuhudia bajeti ikishangiliwa na wabunge kama ya jana. Kwa hakika bajeti ya 2017/18 inaenda kuwagusa watu wengi, kuanzia wakulima wetu wadogo wadogo hadi wakubwa hadi wenye viwanda vyenye fungamanisho na kilimo; wachimbaji wadogo hadi wakubwa. Kila mtu ameguswa. Dr. Mpango amekuja akiwa amejipanga haswa, kwa niaba ya Serikali yetu nzima. Michango mingi ya Wabunge na Mawaziri ameizingatia sana. Naamini huu usikivu ndiyo sababu ya bajeti kupendwa na kushangiliwa kiasi hicho. Kwa hakika itapita bila shida. Tutabaki na kazi ya kufanya kazi kwa bidii kuitekeleza. #bajeti #Bajeti2017 #HK #HamisiKigwangalla #Dr_Kigwangalla #SiasaNiVitendo
Juzi Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango aliwasilisha bungeni mapendekezo ya makadirio ya bajeti ya serikali kwa mwaka 2017/18.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2rZZJAU
via IFTTT


Mtoto naye akawa kwenye hali mbaya, tukamkimbiza kituoni, akafa siku tunazika akaanza mama naye akafa

Mtoto naye akawa kwenye hali mbaya, tukamkimbiza kituoni, akafa siku tunazika akaanza mama naye akafa

Watu watatu wa familia moja wakazi wa Kijiji cha Nyantira wilayani hapa mkoani Mara wanadaiwa kufariki katika mazingira ya kutatanisha huku wanannchi wakihusisha vifo hivyo na ulaji wa asali.
Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Polisi Tarime, Rorya, Sweetbert Njewike akizungumza kwa simu akiwa Shirati wilayani Rorya, amesema hana taarifa hiyo ofisini kwake.
Mwenyekiti wa kijiji cha Nyantira, James Chacha amesema tukio hilo lilitokea kati ya Juni 7, 8 na 9 na kuzua taharuki kijijini hapo kutokana na aina ya vifo vya wanafamilia hao watatu kufariki kwa kufuatana.
Amewataja waliofariki kuwa ni Kerato Nyangerela (70), Regina Kerato (50) na Samwel Kerato (12) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tatu Shule ya Msingi Nyantira.
Chacha amesema, “Juni 7 tulizika mzee baada ya kumkimbiza Kituo cha Afya, Muriba, baada ya saa 12 akafariki, tukamleta nyumbani kuzika, tulipomaliza maziko mtoto naye akawa kwenye hali mbaya, tukamkimbiza kituoni, akafa siku tunazika akaanza mama naye akafa pia,” alisema.
Ameongeza kuwa kufariki kwa watu hao kwa mfuatano kijiji kumeibua hali ya wasiwasi na huzuni hasa kwa kuwa wameacha watoto wadogo.
Akizungumzia vifo hivyo, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Tarime, Mkumbo Odari alisema,”asali kama asali haina madhara kwenye mwili wa binadamu isipokuwa pale inapokuwa imechanganyika na sumu ndipo inapoweza kuleta madhara, na ndiyo maana asali inatumiwa kama dawa, kwenye chakula na kupaka kwenye mikate,” alibainisha Odari.
Naye Diwani wa Kata ya Nyansicha, Sunday Magacha alisema hadi sasa chanzo cha vifo vya wanafamilia hao hakijajulikana na uchunguzi bado unaendelea ili kufahamu chanzo licha ya kuwa uchunguzi wa awali uliofanywa na kituo cha afya Muriba ulionyesha kuwa walikuwa wamekula sumu.
Alisema tukio hilo lilikuwa la kwanza na la aina yake ambalo limewaacha wananchi wakiwa wameathirika kisaikolojia.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2sbfWoQ
via IFTTT


Watuhumiwa wa kesi za udhalilishaji sasa kunyimwa dhamana

Watuhumiwa wa kesi za udhalilishaji sasa kunyimwa dhamana

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala bora Mhe. Haroun Ali Suleiman amesema kutokana na kuongezeka vitendo vya udhalilishaji Zanzibar kwa wanawake na watoto, endapo serikali kupitia taasisi zake zinazoshughulikia kesi za udhalilishaji itamkamata mtu yoyote na kesi za udhalilishaji haitampa dhamana mtuhumiwa wa vitendo vya udhalilishaji.
Akizungumza na Waandishi wa Habari huko ofisini kwake mazizini wakati akitaja vipaumbele vya wizara yake kwa mwaka 2017/2018 amesema jitihada mbalimbali zinachukuliwa kuhakikisha kesi za udhalilishaji zinapungua Zanzibar na moja wapo ni ya kuwanyima dhamana watuhumiwa ili kutoa fundisho kwa wengine na kuimarisha utowaji wa haki.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2r7zC9S
via IFTTT


IGP Sirro: Ni kosa Polisi Kudai Hela ya Mafuta kwa Raia

IGP Sirro: Ni kosa Polisi Kudai Hela ya Mafuta kwa Raia

Mkuu wa Jeshi la polisi nchini (IGP), Simon Sirro amewataka makamanda wa polisi mikoa kuhakikisha wanatumia vizuri mafuta ya magari wanayowekewa ili kuepuka malalamiko ya wananchi kwa magari ya polisi kukosa mafuta.
Pia amesema hataki kusikia polisi hawajafika katika tukio kutokana na kisingizio cha kutokuwa na mafuta.
IGP Sirro alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jana mkoani Morogoro na kuongeza kuwa ni kosa kwa mwananchi kudaiwa fedha za mafuta ya gari la polisi.
IGP Sirro yupo katika ziara ya kuangalia hali ya uhalifu katika mikoa akitokea mkoani Dodoma.
Alisema mafuta ya gari yapo katika bajeti ya Jeshi la Polisi kwa kila mkoa hivyo kinachotakiwa ni makamanda wa mikoa kuhakikisha kuwa wanayatumia vizuri.
“Ni jambo la kusikitisha mwananchi kutakiwa kuchangia mafuta ya gari la polisi,hili hatuliruhusu kabisa,” alisema Sirro
Hivi karibuni, wakazi wa Malinyi walimlalamikia Mkuu wa Wilaya hiyo Jacob Kassema kwa kuwachangisha Sh800,000 za mafuta ya gari lake. Hata hivyo, Kassema alikanusha suala hilo.
Mbali ya suala la mafuta, IGP Sirro aliwatoa hofu wananchi na kusema Serikali inaendelea na uchunguzi wa kina kuhusu mauaji yanayoendelea mkoani Pwani.
“Ni kweli kuna tatizo la mauaji Pwani lakini askari wetu wapo kazini mchana na usiku kutafuta suluhisho la tatizo,” alisema Sirro.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2rZVAN9
via IFTTT


TFF Wakanusha Kutowalipa Posho Serengeti Boys

TFF Wakanusha Kutowalipa Posho Serengeti Boys

Kufuatia taarifa zilizokuwa zikienea na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii, zikidai kuwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewatelekeza wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17(Serengeti Boys), TFF imejitokeza na kukanusha taarifa hizo.
Taarifa hizo za uongo zilidai kuwa Serengeti Boys hawakulipwa posho na kushutumu viongozi wa juu wa shirikisho kuhusu jambo hilo.
“Tunapenda kuwajulisha wazazi na umma kwa ujumla kwamba vijana wetu walilipwa posho zao zote wakiwa kambini Morocco na Cameroon na zile za mashindano ya AFCON nchini Gabon.” wamesema TFF
Kwa mujibu wa Taarifa kutoka TFF, zimeeleza kuwa Shirikisho linafanya taratibu za kupeleka maombi kwenye Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (Football Development Fund FDF) ili kuweza kuwalipa vijana na benchi la ufundi sehemu ya posho zilizokuwa bado hazijakamilishwa wakati wa michuano ya kufuzu kwa AFCON 2017.
“Tumeshtushwa na taarifa hizo ambazo tafsiri yake ni kuharibu uhusiano mwema kati ya shirikisho, wazazi na wachezaji ambao wanatarajiwa kuitumikia timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 maarufu kama Ngorongoro Heroes.”
TFF wamesema kuwa wanawatambua vijana wa Serengeti Boys kwani bado ni sehemu ya kikosi cha Ngorongoro Heroes na hivyo ukifika wakati wataitwa kambini kwa ajili ya michezo ya kimataifa ya U-20.
Aidha, Wametoa shukrani kwa kuushukuru umma ambao wameendelea kuchangia Mfuko wa FDF ambao kimsingi kazi yake ni kutafuta rasilimali kwa ajili ya maendeleo ya mpira.
“Tunaomba michango iendelee kwani bado tuna changamoto za mashindano mbalimbali kwa timu za wanawake na vijana ikiwemo fainali za wanawake Afrika zitakazofanyika Ghana hapo mwakani kwa timu ya Twiga Stars na AFCON 2019 kwa Serengeti Boys ambayo itakuwa mwenyeji.”
Mfuko wa Maendeleo ya Mpira – FDF ulianzishwa kwa lengo la kutafuta rasilimali za maendeleo ya mpira wa miguu hasa kwa wanawake na vijana pamoja na miundombinu ya mchezo huo.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2rfbtCe
via IFTTT


Mkuu wa wilaya awashukia Mgambo wanaojifanya Trafiki

Mkuu wa wilaya awashukia Mgambo wanaojifanya Trafiki

MKUU wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga, amewapiga marufuku askari mgambo wilayani hapa wanaokamata pikipiki zinazobeba abiria, maarufu kama bodaboda na kuonya kuwa hiyo si kazi yao. 
Mwanga alitoa onyo hilo juzi alipokuwa katika ziara ya kusikiliza kero mbalimbali zikiwamo za maji na umeme zinazowakabili wananchi wa Kata ya Lugoba, Halmashauri ya Chalinze.
Alhaji Mwanga alisema hayo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusiana na vitendo vya mgambo kukamata bodaboda.
Alisema mgambo ambao ni askari wa akiba. Hivyo hawaruhusiwi kukamata bodaboda kutokana na kwamba si askari waliopewa jukumu hilo.
“Askari mgambo ambao ni askari wetu wa akiba hamruhusiwi kukamata bodaboda kwani si askari mliopewa jukumu hilo. Kwa kufanya hivyo mnakwenda kinyume cha sheria, ” alisema Mwanga.
Naye Mkurugenzi wa Kituo cha Uzalishaji Maji katika Mto Wami, Mhandisi Christina Mchomba, akizungumzia kero ya maji, alisema utafiti walioufanya katika mto huo umebaini uwapo wa tope kubwa.
Kutokana na kero hiyo, alisema wanaendelea na mradi huo kwa kufanya upanuzi wa mitambo ambayo inaenda sambamba na ujenzi wa matangi 19 ambayo yatasaidia kuhifadhi maji.
Mchomba alisema moja ya matangi hayo linajengwa katika kijiji cha Mazizi lenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni mbili, litasaidia kero ya muda mrefu ya upatikanaji wa maji katika kijiji hicho.

from Blogger http://ift.tt/2rk1pDh
via IFTTT


Tukio Hili Linaweza Kuwa Ushahidi Kwamba Tukifa Tunarudi Duniani kwa Miili Mingineโ€ฆ!!!?

Tukio Hili Linaweza Kuwa Ushahidi Kwamba Tukifa Tunarudi Duniani kwa Miili Mingine…!!!?

Mtoto mmoja wa kiume huko India aliwahi kuwaacha hoi wazazi wake baada ya kuanza kudai aliwahi kuishi kabla ya kizaliwa
Mtoto huyo wa kiume, Taranjijt Singh anasema aliwahi kuishi miaka michache nyuma, ambapo alifariki kwa ajali ya pikipiki akiwa bado mdogo.
Mtoto huyo akiwa na umri wa miaka miwili alianza kusema kuhusu maisha yake ya nyuma na alikuwa akitoroka sana nyumbani . Alikuwa akiwaambia wazazi wake kwamba anakumbuka kijiji alichokuwa akiishi na hata jina la shule aliyokuwa akisoma.
Alikumbuka pia jina la baba yake wa zamani {kabla hajafa}. Awali ilionekana kama aina fulani ya kisirani cha mtoto, lakini ilibidi wazazi wake waanze kuwa na wasiwasi kwa kadiri alivyokuwa akiongezeka kiumri.
Mtoto huyo alikumbuka pia siku aliyokufa . Aliwaambia wazazi wake kwamba, alikufa September 10,1992. Alikufa baada ya kugongwa na pikipiki wakati akiwa kwenye baiskeli akiwa anakwenda shuleni asubuhi. Baada ya ajali hiyo alipata majeraha kichwani na alifariki siku ya pili baada ya ajali.
Baba yake wa sasa hivi, Ranjit Singh, anasema, mtoto wake alipozidi kusisitiza kuhusu maisha yake ya zamani, waliamua na mkewe kumpeleka huko kijijini anakodai kwamba, ndiko alikoishi kabla hajafa. Awali hawakuweza kumpata mtu ambaye alikuwa anafanana na maelezo ya mtoto huyu. Mkazi mmoja wa kijiji hicho aliwaomba waende kijiji cha jirani kinachofuata.
Kwenye kijiji hicho walikwenda kwenye shule ya kijiji ambapo mwalimu mkuu wa shule hiyo alithibitisha kamba, September 10, 1992 alikufa mwanafunzi wa shule hiyo kwa ajali ya pikipiki. Kupitia shuleni hapo, walibaini mahali wazazi wa mtoto yule aliyekufa kwa ajali ya pikipiki, walipokuwa wakiishi.
Ni kweli waliwakuta wazazi ambao walithibitisha kufiwa na mtoto katika tarehe na njia iliyoelezwa. Baba wa sasa wa mtoto huyu, Tanjit Singh alieleza kwamba, mtoto wao aliwaambia kwamba madaftari aliyokuwa nayo wakati wa ajali yalilowa damu baada ya ajali ile na alitaja kiwango cha fedha ambazo zilikuwa kwenye mkoba wake wa shule.
Mama wa zamani wa mtoto huyu ambaye kwa maana hiyo ni mama wa mtoto aliyefariki mwaka 1992 aliposikia hivyo aliangua kilio kikubwa , kwani maelezo hayo yalikuwa sahihi bila doa la kosa. Alisema vitabu na fedha hizo bado vipo, kwani aliviweka kwa kumbukumbu ya kifo cha mwanaye .
Baadae mtoto huyu alirudi na wazazi wake wa sasa nyumbani kukiwa na maswali yasiyo na majibu. Wazazi wake wa zamani pamoja na ndugu zake, walikwenda kumtembelea kwao baadae. Mtoto huyu aliibaini picha ya siku ya ndoa ya wazazi wake, ambayo walikuja nayo wakati walipokwenda kumtembelea kwa wazazi wake wapya.
Awali mwanasayansi, Vikram Chauhan, alikataa kukubaliana na maelezo kuhusu mtoto huyu , lakini baadae alijipa moyo wa kuanza uchunguzi. Alitembelea vijiji vyote viwili , cha zamani alikozaliwa na kufa na hiki cha sasa alipozaliwa.
Alizungumza na wazazi wote na kupata maelezo ambayo yalimfanya kuona kuna jambo la maana kuhusiana na kifo na ‘kufufuka’ kwa mtoto huyu. Kwenye kijiji alichozaliwa na kufa mtoto huyu, muuza duka mmoja alikiri kwamba ni kweli , mtoto kama huyo alikuwepo na yeye alimkopesha madaftari jana yake na alipogongwa alikuwa akielekea dukani kwake kumlipa madaftari hayo.
Chauhan alichukua sampuli ya mwandiko wa mtoto huyu na ule wa kwenye madaftari ya marehemu. Ilipokwenda kupimwa na wataalamu wa mwandiko, ilibainika kwamba, ilikuwa ni ya mtu mmoja.
Kumbuka kwamba mwandiko wangu hauwezi kuwa sawa na wa mtu yeyote, kama ilivyo alama za vidole. Kila mwandiko una sifa zake maalum ambazo haziwezi kupatikana kwenye mwandiko wa mtu mwingine.
Wataalamu wana uwezo wa kubaini mwandiko wa kughushi hata kama umefanywa na mtaalamu wa kiasi gani wa kughushi miandiko.
Kubwa zaidi ni kwamba mtoto huyu ambaye alishaanza kusoma kwenye maisha yake ya kabla ya kifo, hivi sasa hajapelekwa shule, kwa sababu familia yake ya sasa ni maskini. Hata hivyo katika jambo la kushangaza zaidi alipotakiwa kuandika alifabeti za kiingereza na ki-punjabi aliweza kufanya hivyo bila tatizo. Kama hajasoma ingewezekana vipi kufanya hivyo? Anatumia akili ya zamani ya kabla hajafa.
Familia yake ya zamani imeomba kukabidhiwa mtoto wao, lakini familia yake ya sasa imesema hapana, huyo ni mtoto wao. Kisheria, bila shaka, familia yake ya sasa ambayo ni maskini sana, wakati ile ya zamani ilikuwa na uwezo, ndiyo yenye uhalali wa kuishi na mtoto huyu.
Huenda baada ya sayansi kuthibitisha kwamba watu hufa na baadae kurudi wakiwa wanamiliki miilia tofauti, familia kama hii ya zamani ya mtoto huyu, ndipo itakapoweza kupata haki.
Hata hivyo, bila shaka kila familia kati ya hizo mbili, itakayoishi naye, itakuwa na mashaka ya aina fulani.
Ni vigumu kupingana na maelezo ya mtoto huyu, ambaye tangu akiwa na umri wa miaka miwili, alikuwa akizungumzia kuhusu kumbukumbu alizonazo juu ya maisha yake ya nyuma. Ugumu wa kupinga unatokana na ukweli kwamba, hatimaye maelezo yake yalithibika
Jambo hili linathibitisha maisha baada ya kifo
Lakini sio maisha baada ya kifo peke yake bali pia kukubali kwamba huenda binadamu ataendelea kuwepo, kwa sababu uwepo {being} haujapotea na hauwezi kupotea. Mwili wako utaharibika, lakini uwepo wa binadamu hauwezi kupotea.
Karibuni kwa maoni ndugu zangu woote!
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2rOFLuw
via IFTTT


China Wazindua Basi la Ajabu Linaloruhusu Magari Kupita Chini Yake..Linaweza Kupakia Abiria Zaidi ya 300 kwa Mkupuo..!!

China Wazindua Basi la Ajabu Linaloruhusu Magari Kupita Chini Yake..Linaweza Kupakia Abiria Zaidi ya 300 kwa Mkupuo..!!

CHINA inaendelea kufanya makubwa kwenye ulimwengu wa teknalojia na sasa inazindua basi kubwa la aina yake ambalo kwa chini litaruhusu magari mengine kupita kama ilivyo kwenye daraja.
Mfumo huu mpya wa usafiri ni sawa na mwendo kasi zinazohudumia wakazi wa Jiji la Dar es Salaam lakini huu ni wa kisasa zaidi.
Basi hilo lenye mita mbili kwenda juu linaitwa TEB na litaanza kuhudumia umma wa Wachina kuanzia Agosti mwaka huu.
Likitumia nguvu ya umeme, basi hilo linauwezo wa kubeba hadi abiria 300 kwa mara moja huku likiwa na urefu wa futi 72 na upana wa futi 25. Basi hili litaweza kupita hata sehemu yenye foleni kwa sababu ya upana wake na nafasi ya wazi iliyo kwa chini ikiyaacha magari mengine kwenye foleni
Video ya basi hilo la kwanza kutengenezwa, ilizua mjadala huku likiwashangaza wengi baada ya kuwekwa hadhari mwishoni mwa Mei.
Majaribio ya basi hilo tayari yameshafanyika katika mji wa Qinhuangdao ulioko kaskazini mashariki mwa China.
Basi hilo ambalo lina uwazi mkubwa chini yake kiasi cha kuruhusu magari mengine kupita, linaweza kukimbia hadi kufikia kilomita 60 kwa saa huku likivuka reli pamoja na kupita katika njia za barabara za kawaida.
“Faida moja kubwa ni kuwa basi hili litatumia nafasi ndogo wakati linapokuwa ya barabarani,” Injinia wa mradi huo Song Youzhou aliliambia shirika la habari la China Xinhua.
Basi la TEB linafanya kazi kama ambavyo Subway linafanya lakini gharama za utengenezaji ni nafuu zaidi ukulinganisha na Subway,” anaeleza injinia mwingine Bai Zhimini.
Basi hilo la TEB litaweza kufanya kazi inayofanywa na mabasi ya kawaida 40 kulingana na maelezo ya watengenezaji wake. Hata hivyo, bado haijafahamika ni lini litatumika kwa wingi katika miji mbalimbali nchini China.
Kwa mara ya kwanza, wazo la kuwa na basi la aina hii lilionekana kama mzaha hasa baada ya kampuni inayolitengeneza kuonyesha mchongo mdogo kwenye maonyesho ya kimataifa ya teknolojia za hali ya juu ya Beijing.
Baada ya maonyesho hayo, kampuni mzalishaji ilitengeneza basi la kwanza ambalo lilifanyiwa majaribio na kuonyesha ufanisi mkubwa barabarani. Mamilioni ya watu walivutiwa na kushangazwa na basi hilo baada ya video yake kuwekwa mtandaoni.
Niliona picha za basi hili muda si mrefu uliopita lakini sasa naona zimegeuka kuwa basi kweli. Basi hili limejengwa kwa mwendo wa Kichina,” anasema mmoja wa watu waliolishuhudia basi hilo.
Likitazamwa kama mwarubaini wa foleni, TEB limeweza kuwa la aina yake kwa kuwa litaweza kutumia njia moja na magari mengine, pia halitalazimika kusimama wakati magari mengine yakisimama wakati wa foleni kali.
Barabara zetu bado zinakabiliwa na changamoto ya foleni,” anasema Wang Yimin mkazi wa mji ambao basi hilo lilifanyiwa majaribio ya kwanza.
Wazo la kutengeneza basi la aina hii lilikuwapo tangu mwaka 2010 wakati Jarida la Times lilipoandika makala ya kushawishi kampuni zenye uwezo kuwekeza kwenye usafiri ambao utasaidia kupunguza foleni barabarani.
Kampuni ya TEB Technology Development ilionekana kuvutiwa na wazo hilo na kuamua kulifanyia kazi. Mradi huo ambao kama utaweza kwenda kama unavyotarajia utasaidia tatizo la foleni na unaelezewa kuwa ni wa gharama nafuu ukilinganisha na aina nyingime za usafiri wa umma.
Vyombo vya habari vya Serikali ya China vilielezea kuwa uzinduzi wa huduma hiyo ulikuiwa wenye mafanikio makubwa huku tukio lake likivutia vyombo vya habari vya kimataifa kama shirika la habari la kimataifa la Reuters ambalo pia lilipewa nafasi ya kutembelea mradi huo pamoja na kufanya mahojiano ya kina.
Bila haka kama aina hii ya mabasi ingeletwa Tanzania na hususani Jiji la Dar es Salaam, pengine ingekuwa ni suluhisho la tatizo la kujazana kwenye mwendo kasi zetu ambazo zinaonekana kushindwa kuhudumia umma.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2t8NIZb
via IFTTT


Hawa hadi leo wanatisha, lakini walikuwa ghali tangu wakiwa makinda.

Hawa hadi leo wanatisha, lakini walikuwa ghali tangu wakiwa makinda.

Kylian Mbappe anatajwa kuwa na thamani ya zaidi ya euro 100m kiasi ambacho kinaweza kuweka rekodi mpya ya usajili, Mbape ana miaka 19 tu lakini kuna hawa wachezaji watano ambao nao ni hatari hadi sasa na walinunuliwa kwa pesa ndefu wakiwa hawajafikisha miaka 20.
5.Sergio Aguero. Mwaka 2006 alikuwa na umri mdogo tu wa miaka 17 ambapo klabu ya Atletico Madrid walimuona akiichezea klabu ya Independiente na kutokana na uwezo wake mkubwa waliona kiasi cha euro 15m kinatosha kumchukua mshambuliaji huyo.
4.Sergio Ramos. Beki wa kutumainiwa wa klabu ya Real Madrid lakini mwanzo alikuwa akikipiga Sevilla na ilipofika mwaka 2005 Real Madrid walimnunua Ramos kutoka Sevilla kwa dau la euro 18.5m akiwa na umri wa miaka 19 tu na sasa amekuwa mlinzi bora haswa.
3.Wayne Rooney. Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United alinunuliwa akiwa na miaka 18 kutoka katika klabu ya Everton mwaka 2004 na katika michezo 460 ambayo ameichezea klabu ya Manchester United mshambuliaji huyo amefunga jumla ya mabao 198.
4.Gabriel Jesus(19). Ukiongelea kinda ambaye amefanya makubwa ndani ya muda mfupi ni Jesus, huwezi amini kwamba huyu Jesus ndio ambaye mwaka 2014 alikuwa akipaka rangi mitaani nchini Brazil, alinunuliwa kwa euro 27m kutoka Palmeiras na hadi sasa anaonekana bora sana kuendana na thamani yake.
5.Lucas Moura. Kama ilivyo kwa Jesus huyu naye ni Mbrazil ambaye alikuwa akikipiga katika klabu ya Sao Paulo na tangu akiwa hajafikisha miaka 15 vilabu vikubwa duniani vilishaanza kumgombani lakini PSG walifanikiwa kumsaini kwa euro 28m, alikuwa na miaka 19 tu wakati akisajiliwa.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2rOqMRf
via IFTTT


Cristiano Ronaldo apata watoto mapacha.

Cristiano Ronaldo apata watoto mapacha.

Miezi iliyopita tuliandika juu ya tetesi za kuwepo kwa mwanamke mmoja ambaye hajulikani ni nani lakini alikuwa na mimba ya mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo, jambo hilo limekuwa siri kubwa katika familia ya Ronaldo lakini hadi mama yake mzazi analijua hilo.
Sasa taarifa mpya zinasema siku ya Alhamisi mwanamke huyo amejifungua watoto mapacha wa kike na wa kiume ambao wanafahamika kwa majina ya Mateo na Eva, kituo kimoja cha habari nchini Ureno kimedai siku sio nyingi Cristiano Ronaldo ataiambia dunia kuhusu ujio wa watoto hao.
Kituo cha televisheni cha SIC kimedai hadi sasa hakuna picha hata moja ambayo watoto hao wamepigwa na kikishindwa kufahamu watoto hao wamefichwa wapi kwa wakati huu lakini kikisema wana uhakika na taarifa hiyo ya kuhusu mapacha wa Cristiano Ronaldo.
Hakuna taarifa yoyote kutoka kwa upande wa Ronaldo wala wakala wake kuhusu hilo lakini blogspot kubwa,website na magazeti makubwa ikiwemo gazeti kubwa kabisa nchini Ureno cha Daily Correio Da Manha limeandika kuhusiana na watoto hao.
Ronaldo ambaye kwa sasa ana mpenzi mpya Georgina Rodriguez inasemekana mwanamke ambaye amezaaa naye ni mwenyeji wa bara la America na hii haitakuwa mara ya kwanza kwa mwanasoka huyu kuzaa na mwanamke asiyejulikana kwani hata mtoto aliyenaye mama yake hajulikani.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2t8nINp
via IFTTT


Je Wajua ..Simba Hujitibu Maradhi Mbalimbali Yanayomsumbua kwa Kula Majaniโ€ฆ!!!!?

Je Wajua ..Simba Hujitibu Maradhi Mbalimbali Yanayomsumbua kwa Kula Majani…!!!!?

SIMBA ni miongoni mwa wanyama ambao ni jamii ya paka, ukiondolea mbali kwamba ndiye mnyama mkubwa anayewinda katika jamii yao hiyo, lakini pia ni wanyama ambao hupenda kuishi kwa makundi makundi. Kwa lugha nyingine naweza kusema wanaishi kifamilia kama ilivyo kwa binadamu na familia zao huweza kuwa na simba takribani kumi na watano.
Njia rahisi ya kuwatambua kwa jinsia zao ni muonekano pamoja na majukumu, wakati simba dume shingoni likiwa limejaa manyoya mengi, simba jike huwa na manyoya sawa mwili mzima, hapo ni kwa mtazamo wa namna wanavyoonekana.
Katika majukumu, simba hugawana kazi ya kuhakikisha chakula cha kutosha kinapatikana katika familia, hilo ni jukumu la simba jike na simba jike aendapo mawindoni jukumu la simba dume ni kulinda mipaka tu. Uzito wa mnyama huyu huwa kati ya kilo 120 mpaka 240 inategemea na umri pamoja na afya.
Uhai wa simba kuishi ni kati ya miaka 10 mpaka 14 lakini kwa simba wa Afrika hufika hadi miaka 17 na zaidi. Simba huanza kufundisha mbinu za uwindaji watoto wake tangu wakiwa wadogo kabisa, ambapo huwatanguliza mbele na kuanza kuwabughuzi kwa kuwapiga piga ngwala, jambo ambalo hufanya watoto wake kuwa wenye hasira na wakali sana na mbinu hizo ndio hutumia akiwa anawinda ukubwani.
Simba mara zote hupendelea kukaa sehemu ambazo kuna miamba mizuri, pamoja na nyasi kavu kavu ambazo hufanana kwa mbali na rangi yake, kwakuwa huishi kifamilia dume ndio huanzisha makazi mapya, ambapo likiunguruma kwa sauti yake, sauti hiyo husafiri umbali mrefu na sehemu inayoishia ndio huwa mpaka wa makazi yao na kama katikati ya sauti hiyo itakumbana na makazi ya simba wengine, basi dume jingine litaitikia, hapo kinachofuata ni simba hao kuhama lakini kama hawatakubaliana kutoka basi madume ya pande hizo mbili yatakutana kuoneshana ubabe na litakalokubali kushindwa litaondoka na familia yake.
Simba dume huchukia sana jike akizaa dume, hasira yake huja pindi anapoyafikiria madaraka, kwani hutambua jamaa hao ndio watakao kuja kumpindua ili wao ndio wawe watawala, hivyo chuki yake hukuwa kila watoto hao wanapozidi kuongezeka kimo. Jukumu kubwa la kuyalinda madume hayo huwa chini ya mama yao, siku akizembea tu simba dume huvinyonga kikatili, mtifuano huo huwa hauishii kwa watoto tu. Hata simba dume linapozeeka na kushindwa kutimiza majukumu yake kwa ustadi hufukuzwa kabisa na wanafamilia wenza na nafasi yake itachukuliwa na simba dume ambaye anachipukia kwa wakati huo.
Kwa jina la kisayansi simba huitwa Pantela Leo, kuna msemo usemao akikosa nyama basi hula majani, msemo huu si sahihi inapotokea simba anakula majani si sababu ya njaa, bali hutumia baadhi ya mimea hasa majani, kama tiba pindi anaposumbuliwa na ugonjwa hususani tumbo.
Pamoja na kutumia tiba hiyo, lakini pia wana tabia ya kunyanyapaa simba mwenzao hasa anapopata ugonjwa ambao huonekana ni hatarishi katika jamii yao, badala ya msaada wenzie huamua kumtenga na kumfukuza ili kuepuka ugonjwa huo kusambaa zaidi.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2sPKSsD
via IFTTT


Majambazi wajeruhi na kupora fedha na dhahabu katika mgodi

Majambazi wajeruhi na kupora fedha na dhahabu katika mgodi

Kundi la watu wanaosadikiwa kuwa majambazi wamevamia mgodi wa dhahabu wa wachimbaji wadogo katika kijiji cha Nyakavangala kilichopo katika tarafa ya Isimani wilayani Iringa na kupora fedha tasilimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 80 na gramu 400 za dhahabu huku wakiwajeruhi watu tisa.
Majeruhi wa tukio hilo la uporaji ambao baadhi yao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa wamesimulia tukio hilo lililotokea siku ya tarehe 9 mwezi huu majira ya saa moja jioni ambapo kundi hilo la watu walivamia mgodini hapo na kuanza kuwasaka watu waliowataja kwa majina na kuwalazimisha baadhi ya wachimbaji kuwaonesha walipo watu hao.
Baadhi ya majeruhi hao wameiomba serikali kujenga kituo cha polisi katika eneo hilo la mgodi ili kuimarisha usalama wakisema kuwa uporaji huo ulifanyika kwa muda mrefu huku kukiwa hakuna msaada wowote kutokana na eneo hilo kutokuwa na kituo cha polisi wala huduma ya mtandao wa simu hali iliyowafanya majambazi hao kufanya tukio hilo kwa muda wa zaidi ya saa kwakuwa walijua hawatabughudhiwa wala kufurushwa na vyombo vya usalama.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amesema Jeshi la Polisi linaendelea kuwasaka waporaji hao tangu walipopata taarifa hizo hapo jana na kuongeza kuwa serikali inashirikiana na wachimbaji katika eneo hilo la Nyakavangala kuratibu ujenzi wa kituo cha polisi ili kudhibiti usalama wa eneo hilo huku muhudumu wa afya wa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa Bi Gloria Mnyonge akielezea hali za majeruhi hao.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2reiXFI
via IFTTT


Washauri wakuu wa waziri mkuu wa Uingereza wajiuzulu

Washauri wakuu wa waziri mkuu wa Uingereza wajiuzulu

Washauri wawili muhimu wa waziri mkuu wa Uingereza, Theresa May wamejiuzulu.
Pia kuna ripoti kwamba wanachama wakuu wa chama tawala cha Uingereza, cha Conservative, wametishia kuanza kutafuta kiongozi mpya, endapo washauri hao hawatotolewa kazini.
Mpambe wake, Nick Timothy, alisema anabeba dhamana kwa mchango wake katika kampeni ya chama, lakini alisema bado anaamini manifesto ilikuwa sawa, manifesto ambayo mwanachama mmoja maarufu alisema ni mbaya kabisa katika historia.
Msemaji wa chama amesema, mwenzake Bwana Timothy, Fiona Hill, piya amejiuzulu.
Bibi May anajaribu kuunda serikali ambayo haina wingi wa viti bungeni, kwa kutegemea chama kimoja cha Ireland Kaskazini.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2r6U9vm
via IFTTT


Wanahabari toka Ubelgiji wapo nchini kumfuatilia Samatta

Wanahabari toka Ubelgiji wapo nchini kumfuatilia Samatta

Waandishi wawili wa habari wamesafiri kutoka Ubelgiji kuja nchini kwa ajaili ya kumfuatilia mshambuliaji wa kimataifa Mbwana Samatta anaecheza kwenye klabu ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji.
Gauyentie Bogouet pamoja na Marc Cornelissen ambao wanaandikia gazeti la Het Belang van Limburg na website ya http://www.HBVL.BE wana siku tatu tangu wafike Tanzania na leo watatembelea familia ya Mbwana Samatta.
Lengo kuu la safari yao ni kutaka kujua kwa undani alipotoka Samatta njia alizopita kabla ya kutua Genk maisha na tamaduni za taifa anakotokea.
“Tupo hapa kwa siku mbili sasa (jana) tumekuja kwa ajili ya kutaka kujua zaidi kuhusu Samatta alipotoka alikopita na namna alivyofanikiwa kufika Genk. Kesho (leo) tutatembelea nyumbani kwao kwa ajili ya kukutana na familia yake,” alisema Cornelissen mara baada ya kumalizika kwa mechi ya Tanzania vs Lesotho.
Waandishi hao walikuwepo kwenye mechi kati ya Stars dhidi ya Lesotho na walishuhudia Mbwana Samatta akifunga goli katika mchezo huo uliomalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1.
Huenda ziara yao ikawa na faida kwa wachezaji wa Tanzania kwa sababu wamepata fursa ya kushuhudia mechi na kuwaona baadhi ya wachezaji wakiwa katika kiwango bora katika mchezo huo hivyo huenda katika ripoti yao wakashauri vilabu vya Ubelgiji kuja Tanzania kusaka vipaji.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2t8wivC
via IFTTT


Kategori

Kategori