Showing posts with label 2017 at 02:47PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 02:47PM. Show all posts
MAAGIZO Aliyoyatoa Waziri Nchemba Kwa Polisi Kuhusu Kutekwa kwa Msanii Roma

MAAGIZO Aliyoyatoa Waziri Nchemba Kwa Polisi Kuhusu Kutekwa kwa Msanii Roma

Msanii wa hip hop Roma Mkatolikia alikamatwa April 5 usiku ambapo taarifa zilianza kuenea katika mitandao ya kijamii kuwa alikamatwa studio za Tongwe Records na watu wasiojulikana akiwa na wenzake na wakapelekwa kusikojulikana.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba ambaye ndio anahusika na usalama wa raia, ametumia ukurasa wake wa instagram kuonesha kuguswa na tukio la kutekwa kwa Roma Mkatoliki na Moni.
Waziri Nchemba ameeleza kuwa amewaagiza polisi kufuatilia na kutoa taarifa kwa umma.
“Nimeshtushwa kwa kutokuonekana kwa Msanii Roma na Wenzake mpaka sasa. Nimeshtuka zaidi nilipofuatilia na kuambiwa hakuna kituo chochote cha polisi kinachowashikilia. Nimeelekeza Polisi wafuatilie kwa karibu kujua undani wa tukio hili na hatima yao na kutoa taarifa kwa umma”

from Blogger http://ift.tt/2npFduh
via IFTTT


Kimenukaaa..Ofisi ya Mwakyembe Yakana Tetesi za Roma Kushikiliwa Polisi

Kimenukaaa..Ofisi ya Mwakyembe Yakana Tetesi za Roma Kushikiliwa Polisi

Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, sanaa na Michezo imesema imepokea kwa mshtuko taarifa za kutoweka kwa Mwanamuziki Ibrahim Mussa kwa jina la kisanii “Roma Mkatoliki” tangu tarehe 5 Aprili 2017.
Katika taarifa yake iliyotolewa jioni ya jana na kusainiwa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa wizara Zawadi Msalla, amesema kuwa wizara hiyo kwa dhamana yake katika tasnia ya sanaa, imefuatilia kwa karibu suala hilo kwa kuwa lina muelekeo wa jinai na kwamba hashikiliwi katika kituo chochote cha polisi.
“Hata hivyo taarifa kutoka vyombo vya dola zinathibitisha kuwa Roma Mkatoliki hashikiliwi katika kituo chochote cha polisi”.Amesema Zawadi.
Amesema kutokana na hali hiyo, wizara imewaomba wadau mbalimbali na wananchi kwa ujumla kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa zozote zitakazo saidia kujua alipo msanii huyo.
Hata hivyo, mapema jana baadhi ya wasanii wa muziki na filamu nchini wamezungumza na wanahabari kuhusiana na hilo, na kutoa taarifa kuwa wamezunguka katika vituo karibu vyote vya polisi jijini dar es Salaam lakini hawajaweza kupata taarifa zozote kumuhusu Roma, huku wakidai kuwa Kamanda wa Polisi Simon Sirro ameahidi kulitolea ufafanuzi siku ya kesho Jumamosi.

from Blogger http://ift.tt/2nO4RUW
via IFTTT


Kategori

Kategori