Showing posts with label 2017 at 10:40AM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 10:40AM. Show all posts
Inawezekana Kupata Mume au mke Mzuri Kupitia Facebook?

Inawezekana Kupata Mume au mke Mzuri Kupitia Facebook?

Katika safari ya mapenzi wanandoa huwa wanakutana katika maeneo mbalimbali, wapo wanaokutana vyuoni,shuleni, kwenye nyumba za ibada, sokoni, kwenye daladala, kuunganishwa na mtu mwingine, au baada ya kusikia sauti kwenye simu, redioni, hotelini na sasa wengine kupitia mitandao ya kijamii kama facebook
Ukweli ni kwamba katika mitandao unapoanzisha uhusiano na mtu usiyemfahamu inawezekana ameona picha yako tu nakukuambia kuwa anakupenda na wewe ukiona picha yake ukaridhika naye mkaamua kuanzisha uhusino ni vyema kuonana kabisa ili kuwa na uhakika na uhusiano mnaotaka kuanzisha kwani unahitaji kumfahamu zaidi na ndipo utakapoweza kufanya maamuzi ya kukubali au kukataa.
Anaweza kuwa rafiki yako wa kawaida lakini uhusiano ukaja baada ya kuonana mkafahamiana zaidi, kwani ukikurupuka na kutaka kuoana haraka haraka na yule ambaye mna chat tu kwenye mitandao unaweza kujikuta unajuta baadaye kwa maamuzi yako ni vyema kufahamiana zaidi ya kuchat ili kuwa na uhakika na maamuzi yako.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2t1A7ps
via IFTTT


MAVAZI Yanayoshawishi NGONO Vyuoni

MAVAZI Yanayoshawishi NGONO Vyuoni

VIONGOZI wametakiwa kulisaidia taifa kwa kukemea aina ya mavazi yanayovaliwa na wanafunzi wa vyuo vikuu nchini ambayo licha ya kuleta vishawishi vya ngono yamekuwa yakidhalilisha utu wa mwanamke.
Kauli hiyo ilitolewa juzi na kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa, Amour Hamad Amour wakati akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Bustani kilichopo katika Halmashauri ya Mji wa Kondoa. Alisema kuna haja ya viongozi kukemea suala la mavazi yasiyofaa kwa wanafunzi hasa ya vyuo vikuu ambayo mengi yamekuwa yakitia aibu.
“Hapa naona ni tofauti kila mmoja kavaa kiheshima, lakini kwenye vyuo vikuu hali ni tofauti mavazi mengi yanayovaliwa yanaleta vishawishi vya ngono na kufanya maisha ya wasichana kuwa hatarini,” alisema.
Pia katika hotuba yake aliwataka wanafunzi kuacha siasa za majitaka na kutafuta njia za kujiletea maendeleo. “Pia mfikirie zaidi kujiajiri hata kwenye kilimo kwani kunalipa, vijana ndio nguvu kazi ya taifa lazima walete mabadiliko lakini ukikaa unaleta siasa chafu, kujihusisha na vikundi viovu, uasherati na matumizi ya dawa za kulevya tutakosa viongozi wazuri wa kuliendeleza taifa,” alisema.
Aliwataka kupiga hatua za kimaendeleo kwani maendeleo ya Watanzania yanatakiwa kuletwa na watu wote. Sambamba na kuzungumza na wanafunzi hao kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge aliweka jiwe la msingi katika ukumbi wa mikutano wa RC Mission. Ukumbi huo utakapomalizika utatumika kwa shughuli mbalimbali za kijamii kama mikutano na makongamano.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2sZD6gq
via IFTTT


Kimenukaa,,Thea Afunguka Haya Mazito Kuhusu Yeye Kutegemea Mapedeshee Ili Maisha Yake Yaende..!!!

STAA wa filamu nchini, Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ amefunguka kuwa hana mpango na hategemei mapedeshee kuendesha maisha yake kwani madhara yake ni makubwa.
Akibonga na Risasi Jumamosi, Thea alisema katika maisha yake hajawahi kutegemea wanaume mapedeshee wamwendeshee maisha yake kwani kuna hasara kubwa kwa sababu mastaa wengi wa kike wanaoishi kwa kuwategemea hujikuta wakiachwa na kurudi chini kabisa hivyo ni funzo kubwa.
“Siwezi na sijawahi kutegemea mapedeshee kuendesha maisha, mastaa wa kike wengi tumewaona wakiendesha magari ya thamani, wakiishi kwenye nyumba nzuri lakini wanapoachwa wananyang’anywa kila kitu, wanafilisika wanarudi chini, mimi tangu nimetengana na Mike Sangu sijawahi kumwanika mwanaume yeyote kwamba ni mpenzi wangu,” alisema Thea.

from Blogger http://ift.tt/2nRI1fx
via IFTTT


Kategori

Kategori