Showing posts with label 2017 at 01:31PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 01:31PM. Show all posts

Hatariii.. Kocha wa Botswana Amefunguka Haya ya moyoni Kuhusu Mbwana Samatta…!!!

Kocha wa Botswana, Peter Butler ameukubali uwezo wa mshambuliaji wa Taifa Stars, Mbwana Samatta aliyepachika mabao mawili kwenye mchezo wa kirafiki, ambao ulichezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Samatta aliwaadhibu Botswana kwa kufunga bao la kwanza dakika ya pili, baadaye kufunga la pili kwa shuti la adhabu kiufundi dakika ya 87, pia alionekana kuwa hatari kwenye lango la Botswana mara kadhaa.
Utofauti wa matokeo umetajwa kusababishwa na Mshambuliaji huyo wa KRC Genk ya Ubelgiji kutokana na uwezo wake mzuri wa kucheka na nyavu alionao, licha ya muda mwingi Botswana kuoneka kumiliki asilimia kubwa ya mchezo.
“Ni ngumu kucheza ugenini kwa huku Afrika, lakini timu yangu imejitahidi kucheza vizuri, muda mwingi tulikuwa tunamiliki mpira lakini haikutusaidia pamoja na kuwa tulibadili mfumo kwa lengo la kutaka tutengeneze nafasi.
“Nahodha wa Tanzania ‘Samatta’ alicheza vizuri na ndiye aliyekuwa mchezaji hatari zaidi kwetu kipindi chote cha mchezo, amefunga mabao mawili ambayo yameleta utofauti, kwa kipindi chote Tanzania walikuwa bora kwenye eneo lao la ushambuliaji ukilinganisha na timu yangu.
“Tumepata ushindani wa kutosha kitu ambacho nilikuwa nakihitaji kwenye timu yangu, ambayo imeundwa na vijana nadhani hata kwa Tanzania itakuwa hivyo kwakuwa tumewapa upinzani, bila shaka kocha naye atakuwa ameufurahia upinzani tulioutoa kwa timu yake,” alisema Butler.
Kocha huyo wa Botswana aliwai kuzitumikia klabu ya West Bromwich Albion mwaka 1992–1994 ambapo alicheza mechi 70 na kufunga mabao 3 akitumika kama kiungo na baadaye alitua Notts County ambako hakudumu kwa misimu mingi na mwishowe alisajiliwa West Ham United zote za nchini Uingereza.
Kipa wa Botwana, ambaye alitunguliwa mabao mawili na Samatta, Kabelo Dambe anayekipiga kwenye klabu ya Platinum Stars nchini Afrika Kusini alisema mshambuliaji huyo ni moja katiwashambuliaji bora Afrika, ambao amekumbana nao.
“Amenifunga mabao ambayo si mepesi, lile la kwanza ilikuwa nilisogea kidogo ili kulifanya goli kuwa dogo kwa mshambuliaji, lakini alinifunga kwenye hali ile na hata bao la pili alitumia akili kwasababu niliwapanga wachezaji wenzangu kwenye ukuta.
“Alichokifanya nahodha wa Tanzania ni kupiga mpira kwa haraka kabla ya hata sijakaa sawa golini, lakini tulijitahidi kucheza vizuri ila hatukuwa na bahati ya kufunga mabao kitu ambacho wenzetu waliweza,” alisema Dambe.
TAZAMA HARMORAPA ALIVYO TIMUA MBIO BAADA YA KUIONA BASTOLA

from Blogger http://ift.tt/2n9p3B1
via IFTTT


MPYA: Askofu Gwajima atema cheche,NAPE kufukuzwa uwaziri huko EFM

Leo Akofu Gwajima ametembelea kituo cha redio cha EFM kwa ajili ya kuwapa pole kama wanahabari walioathiriwa kwa kiasi fulani na uvamizi uliotokea Clouds MG kama alivyoahidi siku ya jana.Wakati kila mtu akitaka kujua ni nini hasa anachokiongea Askofu huyo wa kanisa la Ufufuo na Uzima.Sisi tunakuletea video kuhusu yote yanayojiri huko sasa hivi.
Askofu Gwajima amesalimiana na wanahabari na wahariri katika kituo hicho na kuwaambia wasikate tamaa lakini pia wazingatie taaluma yao inavyohitaji katika kazi zao.
TAZAMA JAMAA HUYU ALIVYOKOSWA KOSWA NA KIFO KWA AJARI MTONI

from Blogger http://ift.tt/2nqHX9M
via IFTTT


Harmonize: Mapenzi yetu na Wolper sio ya kiki

Harmonize: Mapenzi yetu na Wolper sio ya kiki

Harmonize amefunguka kuwa ni kweli waligombana na mpenzi wake Jacqueline Wolper na haikuwa kiki kama watu wanavyofikiria.
Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM Jumatano hii, kuna baadhi ya vitu vilisababisha wagombane lakini kwa sasa kila kitu kinaenda sawa.
“Kuna vitu vilitokea tukajikuta hatuko sawa, lakini Mungu ndio mwenye kheri tukawa tupo pamoja tukajua kabisa kuwa hiki kitu Jack hakipendi au mimi. Sasa hivi kila kitu kinaenda sawa na mapenzi yetu sio ya kiki, nafasi yetu kwenye jamii imefanya ionekane kuwa ni kiki,” amesema Harmo.
Hitmaker huyo wa Matatizo ameongeza kuwa alianza kuwa na mahusiano na Wolper muda mrefu tangu kipindi hana gari anatembea kwenye bajaji.

from Blogger http://ift.tt/2nyVgCC
via IFTTT


Kategori

Kategori