Showing posts with label 2017 at 02:37PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 02:37PM. Show all posts
RAIS MAGUFULI AANZA ZIARA YA SIKU 5 MKOANI TANGA

RAIS MAGUFULI AANZA ZIARA YA SIKU 5 MKOANI TANGA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mkata wakati alipokuwa njiani kuelekea mkoani Tanga kwa ajili ya ziara ya kikazi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wa Mkata waliosimama pembeni ya barabara kuu ya Chalinze- Segera (hawaonekani pichani) mara baada ya kumaliza kuhutubia katika kijiji cha Mkata mkoani Tanga.
Viongozi mbalimbali wa mkoa wa Tanga akiwemo Wabunge na wakuu wa Wilaya wakipiga makofi wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akihutubia Mkata mkoani Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa waliosimama pembeni ya barabara kuu ya Chalinze Segera katika eneo la Kwa mkonga wakati akiwa njiani kuelekea Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wa Kabuku mara baada ya kumaliza kuwahutubia wakati akielekea mkoani Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Kabuku Handeni mkoani Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela kabla ya kuwahutubia wananchi wa Hale mkoani Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Hale mkoani Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mmoja ya wakazi wa Hale mkoani Tanga mara baada ya kuhutubia katika eneo hilo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM Hadija Juma mara baada ya kusoma ujumbe ulioandikwa kwenye sare aliyovaa mama huyo.
Wananchi wa Muheza wakimpokea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kufika katika eneo hilo la mjini akiwa njiani kuelekea Tanga. PICHA NA IKULU.

from Blogger http://ift.tt/2v4Ysdj
via IFTTT


RAY Kigosi Amtolea Povu Wema Sepetu Sakata la Roma Kupotea

RAY Kigosi Amtolea Povu Wema Sepetu Sakata la Roma Kupotea

Mwigizaji Ray Kigosi Aamua Kumjibu Wema Sepetu Kama ifuatavyo Baada ya Wema Kuwashutumu wanakalia kupiga picha na Makonda huku hawajui wala kumuuliza Roma Alipo:
“NAFIKIRI NI VEMA MTU KUELEZA HISIA ZAKE JAPO SIO BUSARA KWA MWENYE HISIA HIZO KUZIELEZA BILA WEREDI NAWASIHI WASANII WENZANGU KUPOTEA KWA ROMA ISIWE SABUNI YA KUTAKATISHA UCHAFU WA MTU SOTE TUMESIKITISHWA NA JAMBO HILO NA TUMEONYESHA KWA VITENDO aร 
MIMI NIMEPOST INSHU YA ROMA TANGU JANA USIKU WEMA SEPETU WEWE ULIKUWA HUJAPOST CHOCHOTE TUSEME ULIKUWA HUNA UCHUNGU? ALAFU LEO UNAANDIKA KUWA BONGO MOVIE HAWAPO PAMOJA NA TUKIO LA ROMA HUKU NI KUTUGOMBANISHA NA WANANCHI WANAOTUAMINI. SISI BONGO MOVIE MARA NYINGI SANA TUNAKUWA PAMOJA KWENYE MATUKIO YA BONGE FLEVA TOFAUTI NA WAO. KAMA UNA UGONVI NA MTU HAYO NI MAMBO YAKO BINAFSI ILA USITUFANYE SISI TUONEKANA WABAYA MBELE YA JAMII UTAKUWA KICHAA KAMA USIPOPATA MAUMIVU KWA TUKIO LA ROMA NIMESIKITISHWA SANA POST YAKO @wemasepetu KAMA UNADHANI HUU NI MUDA MUAFAKA WA KUTAFUTIA POINT KATIKA TUKIO LA ROMA MKATOLIKI UMEFELI HILI NI JANGA LETU SOTE. @wemasepetu #(KINA ROMA WAKO WAPI?)” Ray

from Blogger http://ift.tt/2o9A3zS
via IFTTT


Kimenukaa..Chadema Waonyesha Dhahiri Kumchukia Zitto,Watoa Waraka Huu Mzito Kuhusu ACT Wazalendo na Ubunge wa Afrika Mashariki..!!!

Kimenukaa..Chadema Waonyesha Dhahiri Kumchukia Zitto,Watoa Waraka Huu Mzito Kuhusu ACT Wazalendo na Ubunge wa Afrika Mashariki..!!!

Kwa taarifa za uhakika kutoka Dodoma, kupitia kikao cha Kamati ya Kanuni ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki utafanyika kama ilivyotangazwa na Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai kwa kuzingatia Ibara ya 50 ya Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kanuni za Kudumu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika kikao chake kilichoketi jana hadi majira ya saa nne usiku, taarifa hizo zinathibitisha kuwa ombi la KIONGOZI MKUU wa ACT, kutaka chama hicho kipewe haki na nafasi ya kuweka mgombea uchaguzi wa EALA, limetupiliwa mbali kwa sababu halikuwa na mashiko ya kimantiki wala msingi wa kikanuni.
Kiuhalisia kamati hiyo imeungana na Spika Ndugai na kumpongeza kwa kusimamia kanuni za uchaguzi huo hasa kwa kuzingatia msingi wa Kanuni ya 12 inayosema kuwa Uchaguzi wa EALA utafanyika kwa kuzingatia uwiano wa vyama vyenye uwakilishi bungeni.
Chama kama ACT chenye mbunge mmoja katika Bunge la lenye idadi ya wabunge 393 ni sawa na 0.00% ambayo ni sawasawa na kiti au viti 0. Kwa hiyo taratibu zinakiengua kuwa katika mchakato wa kugombea hata nafasi moja.
Vile vile kanuni ya 5(5) ya Nyongeza ya Tatu ya Kanuni za Bunge inasema “chama chochote cha siasa chenye HAKI ya kusimamisha mgombea wa EALA kinaweza kuweka wagombea watatu katika makundi ya wagombea ubunge.”
Mantiki ya hoja kutokana na msingi huo wa kikanuni, inaonesha kuwa vyama vingine tofauti na CHADEMA, CUF na CCM, haviwezi kusimamisha wagombea kwa sababu havikidhi kigezo cha Kanuni ya 12 ya Kanuni za Kudumu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kimsingi Spika amesimamia haki iliyokuwa inaporwa au kupokwa katika chaguzi za EALA zilizopita. Kwa uamuzi huo bila shaka sasa uchaguzi utahusisha vyama vitatu ambavyo ni CCM (6), CHADEMA (2) na CUF (1) ambavyo ndivyo vinakidhi vigezo vya kuweka wagombea.
Ibara ya 50 ya Mkataba wa wa EAC, inaelekeza na kutoa mamlaka kwa kila bunge la nchi mshirika kuchagua wawakilishi kwa mujibu wa kanuni za bunge la nchi husika na huo ndio utaratibu uliopo sasa ambao wapeleka maombi wanaujua vyema.
Ni wazi pia uamuzi huo utakuwa umezingatia masuala mengine ambayo yanafanana na suala hilo na tayari yanaweka precedences. Mathalani hata sasa vipo vyama ambavyo pamoja na kuwa na uwakilishi bungeni (mbunge mmoja), ambayo ni sawa na asilimia 0.000 katika bunge la sasa, hata katika baadhi ya maamuzi yanayozingatia kanuni za namna hiyo au zinazofanana na hizo, taratibu za kisheria zilizopo zinawaweka kando katika masuala kadha wa kadha kama ruzuku au kupata wabunge wa viti maalum. Hiyo inadhihirisha kuwa vyama vikafanye kazi ya siasa kuongeza viti bungeni ili vipate au kuongeza nafasi za wagombea wa EALA watakaowakilisha nchi yetu kwenye bunge hilo.
Ni muhimu wakajua kuwa nafasi hizi za EALA kwa utaratibu uliopo sasa hazigawiwi tu kama sandakarawe au jugu ama pipi. Ni matokeo pia ya kazi kubwa iliyofanyika wakati wa kampeni uchaguzi uliopita.
Tusubiri uteuzi kuelekea uchaguzi EALA.
Tumaini Makene

from Blogger http://ift.tt/2nzZGbO
via IFTTT


Ushauli wa Zitto Kabwe baada ya Rais Magufuli KUTENGUA uteuzi wa leo!!

Image result for Zitto Kabwe
Baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli march 23, 2017 kufanya mabadiliko madogo kwenye baraza la Mawaziri ambapo sehemu ya mabadiliko hayo ni kamteua Waziri mpya wa Habari, Sanaa, Utamaduni na michezo. Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe ametoa maoni kuhusu mabadiliko hayo.
TAZAMA JAMAA HUYU ALIVYOKOSWA KOSWA NA KIFO KWA AJARI MTONI

from Blogger http://ift.tt/2o87AJk
via IFTTT


Kategori

Kategori