Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema amedhamiria kununu treni ya umeme baada ya Rais John Magufuli kuonyesha dhamira ya kujenga reli ya kisasa(standard gauge).
Gwajima ameyasema hayo leo katika ibada ya Jumapili huku akimsifu Rais Magufuli kwa kuchukua hatua hiyo.
Alisema licha yeye ni mchungaji wa Taifa na anaamini ipo siku Dar es Salaam yote itakwenda kanisani kwake kusali.
Rais wa Tanzania Mh Dkt. John Magufuli amevitaka vyombo vya habari nchini kuweka mbele uzalendo kwani wao wana mchango mkubwa katika kuliinua ama kuliangamiza taifa.
Mhe. rais ameyasema hayo alipokuwa akizungumza Ikulu bada ya kupokea hati za utambulisho za mabalozi na kuwaapisha viongozi mbalimbali akiwemo waziri mpya wa habari utamaduni sanaa na michezo Mhe. Dkt. Harrisoni Mwakyembe.
Rais akasema inashangaza kuwa mataifa ya nje yanathamini na kuheshimu jitihada zinazofanywa na serikali na ndio maana hata rais wa benki ya dunia alikuja nchini kwa mara ya kwanza lakini baadhi ya wananchi hawaoni jitihada hizo, wanabeza.
Kiongozi huyo akawataka viongozi kutovunjika moyo wafanye kazi na wananchi waache kulalamika bila ya kutoa ufumbuzi wa hayo malamiko yao.
Katika hafla hiyo alikuwepo makamu wa rais mama Samia Suluhu Hassani ambaye alisema kila mtu anapaswa kufanya kazi huku ,kaimu jaji mkuu Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwataka viongozi kuzingatia maadili.
TAZAMA HARMORAPA ALIVYO TIMUA MBIO BAADA YA KUIONA BASTOLA
Jeshi la Polisi mkoani Tanga linamshikilia mwalimu wa Shule ya Sekondari Mkwakwani kwa kumpiga na kumsababishia madhara ya kiafya mwanafunzi, Suleyman Mohamed (18).
Mwanafunzi huyo inadaiwa alichapwa viboko juzi asubuhi na mwalimu huyo wa zamu aliyekuwa akiwaadhibu wanafunzi waliochelewa na waliokuwa wakipiga kelele darasani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba amesema tayari mwalimu huyo yuko mikononi mwa jeshi hilo na upelelezi wa suala hilo unaendelea.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwilapwa amewataka walimu kuwa waangalifu wakati wakiwaadhibu wanafunzi ili kukwepa madhara kwa wanafunzi.
“Tunalifuatilia kwa karibu tukio hili. Niseme kwamba tutachukua hatua stahiki ikithibitika kuwa umefanyika uzembe,” amesema Mwilapwa.
Baada ya kuchwapwa, mwanafunzi huyo amelazwa katika Hospitali ya Rufani ya Bombo ikielezwa kwamba tayari amepatiwa rufaa kuhamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda leo March 14 2017 ametembele moja kati ya maeneo yaliyokubwa na Mafuriko yaliyotokana na mvua iliyotokea March 13 2017, Buruguni Mnyamani ndipo Paul Makonda ametembea na ameagiza Nyumba 36 zilizokuwa pembezoni mwa Bonde la Mto Msimbazi kuanza kuvunjwa kesho.
‘Kuna Nyumba 36 zitaanza kubomolewa kesho na Nyumba hizo zimegawanyika kwenye makundi matatu kundi la kwanza wameshalipwa na wameshapewa viwanja Mabwepande la pili kuna watu pia wamepewa Mwabwepanda wamejenga kule na huku wamepangisha na kundi la mwisho ni wale ambao hawajapata fidia zao’- Paul Makonda
‘Wale ambao wamejenga pembezoni mwa Mto au umejenga pembezoni kwenye mabonde ni waambie ukweli hakuna pesa yeyote ambayo watapata ngoja niseme tu ukweli mimi si mwanasiasa ninayetafuta sifa za kijinga acha niwaambie tu ukweli‘-Paul Makonda
WANANCHI WAOMBA SERIKALI KUODOA TAKA KIZIMBANI MAKAMBAKO MKOANI NJOMBE