Showing posts with label 2017 at 11:21AM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 11:21AM. Show all posts
Mchezaji Donald Ngoma si wa Mchezo..Akata Mzizi wa Fitina…Yanga au Simba? Jibu Hili Hapa

Mchezaji Donald Ngoma si wa Mchezo..Akata Mzizi wa Fitina…Yanga au Simba? Jibu Hili Hapa

Mshambuliaji wa Yanga, Mzimbabwe Donald Ngoma ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia timu hiyo katika Ligi Kuu Bara msimu ujao.
Kupitia kurasa rasmi za mitandao ya kijamii za timu hiyo wamethibitisha taarifa za usajili huo kwa kuandika “Donald Ngoma Raia wa Zimbabwe ni mali ya Yanga kwa mkataba wa miaka miwili.”
Ngoma ambaye alikuwa akihusishwa kujiunga wapinzani wa Yanga, Simba kabla ya kuzuka kwa taarifa za kujiunga na klabu ya Polokwane City inayoshiriki Ligi ya kuu ya Afrika Kusini ‘ ambapo alitua nchini usiku wa jana na mchana wa leo amesaini mkataba huo.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2spk6pw
via IFTTT


Utafiti wangu: ‘Massage Parlour’ ni Z’aidi ya Maduka ya Ngono

Utafiti wangu: ‘Massage Parlour’ ni Z’aidi ya Maduka ya Ngono

Wakuu niliamua kwa mara nyingine kujipa kazi ya kufanya “Utafiti” katika maeneo ya “Massage Parlour” katika jiji la Dsm na vitongoji vyake.Raha ya utafiti wa aina hii ni kujivika “uhusika” haswaa ili upate mambo ya ndani ya kujifunza hasa undani wa jambo lenyewe,ama hakika nimejifunza mengi na kwa kweli hii ndio Dsm,mambo ni motomoto ndani ya kuta nne za vyumba.
Nilianza kwa kutembelea “Massage Parlour” za mitaa ya Sinza(Sitataja majina kwa sababu maalumu).Humu nimejionea mambo mengi sana na mazito,ama hakika mji huu una mambo.Hizi si Massage Parlour tena bali ni maduka ya ngono yasiyo rasmi yenye leseni ya “Massage Centres”
Nilianza mitaa fulani ya Sinza ambapo pale nilikuta Massage yenye bei mbili tofauti,moja ya Tsh 25,000/= na nyingine ni 35,000/=,yaani hiyo ya elfu 25 haina choo na bafu la ndani kwa ndani wakati hiyo ya elfu35 maanake unapata chumba chenye choo ndani,huna haja ya kutoka kwenye korido kwenda kuoga au msalani.Ndani ya chumba unakutana na huduma kadha wa kadha,kwanza unaambiwa unataka huduma ya aina gani?Maana kuna
1)Soft Massage
2)Hard Massage
3)Medium Massage
4)Body to body Massage
5)Honey Massage nk
Huduma hizi zote zinapatikana humo ndani,yaani kama hiyo ya body to body maanake mtoa huduma anatoa kila kitu halafu anakupaka mafuta na kuanza kuusugua mwili wako akiwa mtupu,hiyo hard ni kwa wale wenye kutaka kunyoosha misuli,medium inakuwa kati ya soft na hard na wakati soft hiyo ni hatari sana maana inaamsha mambo yote ya dunia ya mwili.
Kifupi wakati wa kuingia unakuta wadada wamekaa kama sebuleni,na ukiingia pale wanaitana wooote na wanapanga foleni,hairuhusiwi kukubaliana na mmoja wakati wenzake hawapo pale sebuleni/mapokezi.Wakikusanyika wote unaambiwa uchaguwe wa kwenda kukuhudumia.Sasa ukiwa kauzu unapitia mmoja baada ya mwingine then unachaguwa.Yaani wakati wa kuchaguwa kila mtu analegeza macho na madoido ili achaguliwe yeye,inakuwa kama “ng’ombe mnadani”.
Baada ya hapo ni kwenda kupata huduma,huko ndani kwenye huduma ni balaa tupu,yaani ukitoka salama ni bahati,yaani ni kama bahati ya UKAWA kuanzisha maandamano mbele ya Central Polisi bila kibali cha maandamano halafu wakaachwa.Kiukweli hii ni aina ya biashara ambayo wale wadada wasioweza kujipanga foleni pale Sinza Ambiance basi wanakuwa huku,na pia kwa wale wasioweza kuopoa pale wanahamia huku.Nimejifunza kuwa biashara hii ni ngumu sana kupambana nayo moja kwa moja sbb binadamu wana mbinu nyingi sana.
Katika utafiti wangu nikagundua wateja wengi ni waume za watu ambao pengine wake zao hwafanyi au hawajui namna ya kufanya hizi massage.Wahudumu wengi wanakiri kuhudumia waume za watu hasa siku za weekend na mida ya jioni baada ya kazi,kwani watu wengi hawapendi kuingia mchana huku wakionekana.Na huduma hizi zinazotafutiana kutokana na mazingira na mazingira.Huko Mikocheni,Mbezi na Masaki bei zake ni kubwa sana.Wachina na Wafilipino wengi wanafanya baishara hii na ile “extra” kwa mgongo wa Massage Parlour.
Kuna centres nyingine wapo kikazi haswaa,hii ni kwa sababu kuna watu wenye matatizo ya neuros(?),migongo na wameshauriwa na madaktari wanatumia sehemu hizi kwa ajili ya matibabu ya migongo na viuno.Hiivyo si wote wapo kwa ajili ya ile “biashara”.
Mashoga wengi hushinda na hawa wadada,na hukaa humu na kufanya kazi hiyo,pia wavutaji wa shisha na madawa pia humu ndio centres zao.Mtu anaingia anajidunga anasinzia mpaka anaamka ndio anatoka.Kifupi kila unapozuia hili binadamu anavumbua hili,kila kitu kina majibu yake.Humu ndani ya Masage Parlour ni hatari wakuu…Kuingia bure kutoka lazima uwe umakauka.
Hii ni sehemu ya kwanza ya muendelezo wa utafiti wangu ndani ya hizi Massage Centres…Nipatapo wasaa nitakuja tena hapa kumalizia.
Muwe na siku Njema Wakuu

from Blogger http://ift.tt/2rJ1STj
via IFTTT


RAY na Mama Kanumba Kimenuka….

RAY na Mama Kanumba Kimenuka….

Mama mzazi wa aliyekuwa nyota wa filamu bongo, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa siku ya kumbukumbu ya mwanaye makaburini Kinondoni, alimfyatukia msanii wa filamu nchini, Vincent Kigosi ‘ray’ aliyekuwa swahiba wa mwanaye kuwa, hajawahi kumuona hata siku moja makaburini hapo kuomboleza kifo cha mwanaye miaka yote ambayo hufanya kumbukumbu hiyo.
Akizungumza na Amani makaburini hapo, Aprili 7, mwaka huu, mama Kanumba alisema kuwa, tangu aanze kuazimisha kumbukumbu za mwanaye hajawahi kumuona Ray akiomboleza wala hata kuungana naye makaburini kama mastaa wengine wanavyofanya. “Yaani sijawahi kumuona huyo Ray akijumuika na sisi makaburini, utadhani yeye ataishi milele duniani.
Kumbuka somo la leo kutoka kwenye Biblia linatufundisha kuwa, kila binadamu atakufa,” alisema mama Kanumba. Aidha, mama huyo alisema kuwa kama Ray na mwanaye waliwahi kuwa na ugomvi basi amsamehe kwani binadamu tumefunzwa kusamehe na sasa hayupo tena duniani.
“Unajua huenda walikoseana marehemu akiwa hai lakini mpaka leo naona kama ana kinyongo, asamehe tu. Naongea hayo kwa sababu sijawahi kuona akimuenzi hata kwa kufika makaburini kuungana na sisi, utadhani hakuwahi kuwa na uhusiano naye.
Nawashukuru sana wasanii wa kike wao ndiyo huungana na mimi katika maombolezo ingawa kwa mwaka huu hawakujitokeza lakini siwezi kuwasema vibaya kiukweli,” alisema mama huyo.
Baada ya habari hizi kutoka kwa mama Kanumba, Amani juzi lilizungumza na Ray aliyeamua kufunguka kuwa, yeye humuenzi Kanumba kwa njia nyingi tu si lazima kujionesha makaburini na si lazima kuutangazia umma.
“Mimi najua marehemu alikuwa rafiki yangu na nimekuwa nikimkumbuka na kumuenzi kwa mambo mengi tu si lazima kuungana na mama Kanumba makaburini ndiyo nionekane,” alisema Ray kwa sauti yenye kumshangaa mama Kanumba kwa madai yake hayo.

from Blogger http://ift.tt/2p2FtQs
via IFTTT


RPC Kinondoni Akana Kuhusika na Zuio la Mkutano wa Nape Nnauye,Afunguka Juu ya Askari Kuonyesha Bastola..!!!

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni Susan Kaganda, amesema kuwa yeye hakutoa maelekezo ya kuzuia mkutano wa aliyekuwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Nape Nnauye pamoja na Waandishi wa Habari Jana Protea Hotel.
Akifafanua kupitia kipindi cha Maisha Mseto cha Times Fm mapema Leo asubuhi, Susan amedai yeye kama Kamanda hana mamlaka ya kuingilia biashara binafsi (Protea Hotel), na alikwenda pale kuhakikisha Usalama unaimarika zaidi na si vinginevyo.
“Protea ni private Hotel sio Mali ya Serikali, ile ni Biashara huru kamanda hawezi kuzuia, lakini nilikuta Waandishi wengi pale na alipata fursa ya kuongea nao.
” Mimi kazi yangu ni kusimamia Usalama wa Raia na Mali zao, mkutano unanihusu ukiwa wa Hadhara” alisema RPC Susan.
Alipoulizwa kuhusiana na kipande cha ‘Picha Jongefu’ (video) inayomuonyesha mtu anayedhaniwa kuwa Askari akimtolea silaha Nape Nnauye, amesema hawezi kuliongelea swala hilo kwa sasa mpaka uchunguzi utakapokamilika kwa maana kipande hicho hakionyeshi Sura ya mtu Huyo.
“Jeshi la Polisi tunawafundisha Askari wetu kutumia nguvu kwa namna wanavyokutana na mazingira, sikuwepo sikuona nilielezwa na ndio maana nilikwenda nikamuuliza Mh uko sawa akanijibu yuko salama,”
“Lakini kama kuna Silaha imetumika kama ambavyo nimeona kwenye vyombo vya Habari tunalifanyia Uchunguzi, sikuwepo eneo la tukio picha ile inaonyesha KISOGO, kuwa mtulivu tunachunguza” alifafanua.
TAZAMA HARMORAPA ALIVYO TIMUA MBIO BAADA YA KUIONA BASTOLA

from Blogger http://ift.tt/2n1Fdf7
via IFTTT


Mayweather Akubali Kuzichapa na Conor McGregor Juni 10, 2017 kwa Dau Kufuru la Bilioni 200…!!!

Mabondia Floyd Mayweather na Conor McGregor watapanda ulingoni Juni 10, mwaka huu wameuteua ukumbi wa T-Mobile Arena mjini Las Vegas kuwa shehemu. ya pambano lao.
Kila mmoja ametaja bei yake ya kupandia ulingoni kuwa dola za Kimarekani Milioni 100, ila kiuhalisia bondia McGregor atatakiwa kushusha bei ili kuhamishia ujuzi wake wa UFC katika ndondi.
Mayweather amesema rasmi amerejea ulingoni kwa ajili ya McGregor baada ya kustaafu akiwa amepigana mapambano 49 na kushinda yote rekodi sawa na ya gwiji, legendary Rocky Marciano na hilo litaitwa “Pambano la Karne”.


DOWNLOAD APPS YA TZTOWN HAPA

http://ift.tt/2ms2574
WANANCHI WAOMBA SERIKALI KUODOA TAKA KIZIMBANI MAKAMBAKO MKOANI NJOMBE


from Blogger http://ift.tt/2nd3xys
via IFTTT


Kategori

Kategori