Showing posts with label Ukatili. Show all posts
Showing posts with label Ukatili. Show all posts

'UKEKETAJI' Mfumo jike unaoendekeza mfumo dume



Na Gordon Kalulunga.

KWA mujibu waWIKIPEDIA, kamusi huru, inaeleza kuwa Ukeketaji ni neno linalotokana na mzizikeket, ambao unabeba maana ya kuharibu. 
 
Mara nyingi tendo laukeketaji unaitwa pia "tohara" kwa kulifananisha na upasuaji mdogo wa wanaume lakini mambo ni tofauti kabisa.

Hapa sehemu za nje za viungo vya uzazi zinakatwa kusudi wasifurahie sna tendo la ndoa, hivyo wawe waaminifu zaidi kwa waume wao.

Kinyume na tohara ya wavulana matabibu wanaona hasara nyingi katika desturi hiyo. Ukeketaji unasababisha wasichana wengi kufa na wengine wengi kupatwa na maumivu makali wakati wa hedgi, wa tendo la ndoa na wakati wa kujifungua.

Kwa sababu hizo serikali nyingi za dunia zimeupiga marufuku. Pia madhehebu kadhaa yanatoa mafundisho kuwa ni kinyume cha masharti ya dini yao.


Kila mwaka ifikapo Februari 9, hapa nchini tunaanzimisha siku ya kupinga ukeketaji. Leo hii tunajitahidi kama nchi kupinga vikali vitendo tulivyovipachika jina la ukatili wa kijinsia ama wengine wanaita majina kadha wa kadha likiwemo jina la mila na desturi zilizopitwa na wakati.
Mambo haya yanapingwa zaidi na watu waliopo mijini, lakini wale waliopo vijijini kwao hali zile ni za kawaida sana na  kizuri au kibaya hata watu waliopo serikalini wanaungana na baadhi ya watu wa vijijini kwao hususani katika suala la ukeketaji.
 
Mwaka 2012-12013, nikiwa chini ya mpango wa fellowship chini ya mfuko wa kusaidia vyombo vya habari nchini Tanzania Media Fund(TMF), nikibobea katika uandishi wa afya ya uzazi, nilifika mkoani Mara katika wilaya za Bunda, Butiama na Musoma na kubaini mamboi kadhaa.
Baada ya serikali kuonekana kuzuia na kukataza mila ya baadhi ya makabila hapa nchini kuwakeketa wasichana, mkoani Mara, baadhi ya makabila yanayokeketa yamebuni mbinu mpya.
 
Mbinu inayotumika kwa sasa kuwakekata wasichana hao ni kuandaa sherehe inayofanana na siku ya kuzaliwa yaani(Birthday).
 
Baadhi ya wananchi na viongozi wa afya wilayani Musoma na Bunda mkoani Mara walioomba hifadhi ya majina yao, wanasema bado ukeketaji unandelea kufanyika kwa wasichana hasa nyakati shule zikifungwa.
Wanasema mbinu inayotumika ili kukwepa mkono wa sheria kwa wakeketaji ni kuwakusanya mabinti wachache au mmoja mmoja na kuwakeketa huku wakiimba nyimbo za kumpongeza binti kwa kuazimisha siku yake ya kuzaliwa.
‘’Mbinu inayotumika kwasasa na vifaa vya mangariba ni vile vile, lakini ilikukwepa mkono wa sheria na kukamatwa wazazi wa wasichana na mangariba hao, hupanga mbinu nzito na baada ya kuwakeketa wasichana hao uimba wimbo wa Happy birthday’’ walisema kwa nyakati tofauti wananchi hao.
Baadhi ya wasichana wanaoishi wilayani Musoma waliohojiwa na mwandishi, walisema wao tayari wamekeketwa na hawaoni ubaya wa kitendo hicho kwasababu ndiyo mila na desturi za makabila yao.
 
‘’Ni kawaida tu, mbona hata wanaume wanaenda jando! Tatizo labda ni kwamba ninapotaka kukutana kimwili na mtua siye wa kabila la kwetu huwa naona aibu kidogo maana hata nikienda nae mimi nachelewa kufika kileleni wakati yeye anawahi na hisia zangu zinakuwa mbali’’ alisema ‘’Judith’’ jina siyo halisi.
 
Dhana hiyo ya kukeketa baadhi ya makabila yanaamini kuwa kukeketa kutalinda ubikira wa wasichana na kuwafanya wanawake wasiwe wahuni (Malaya).
Pia wapo watu wengine wanaamini kwamba kumkeketa msichana ni heshima kwa mwanamke.
 
Baadhi wanasema hali hiyo inaongeza raha ya kujamiiana kwa waume zao, na kitendo hiki kinaaminika kuongeza uwezekano wa wanawake kuolewa na kuimarisha uwezo wa kuzaa.
 
Madhara yake ni nini?
Wataalam wanasema kuwa kukata sehemu za via vya uzazi kunaweza kusababisha kutoka damu nyingi. Hii inaweza kusababisha kifo au upungufu mkubwa wa damu kwa mkeketwaji hatimaye kufariki dunia.
 

Maambukizi ya magonjwa.
Mambukizi ya magonjwa ya naweza kutokea kwasababu ya kutumia vifaa vichafu na pia yanaweza kutokea kwa kutumia dawa za kienyeji za kuponyesha vidonda.
Maambukizi yanaweza yakaenea hadi kwenye tumbo la uzazi, mirija ya kupitishia mayai, na kwenye mayai ya uzazi na kusababisha maumivu ya mara kwa mara hata ugumba. Mambukizi ya magonjwa yanaweza kusababisha kifo.
 
Kubana mkojo:
Baada ya kukeketwa wanawake wanaweza kubana mkojo kwasaa nyingi au siku nzima kwasababu ya maumivu au kwa kuogopa kupitisha mkojo kwenye vidonda. 
 
Hata baada ya vidonda kupona mwanamke aliyeshonwa uke, tundu linaweza likawa dogo mno kuweza kutoa mkojo.
 
Matatizo wakati wa siku za hedhi:
Kama mlango wa uke ni mdogo sana kiasi cha kutoruhusu damu ya hedhi kutoka vizuri, damu inaweza kukusanyika ndani ya uke na tumbo la uzazi.
Hii inaweza kusababisha maambukizi ya magonjwa, na tumbo la uzazi kuvimba kwasababu ya damu ya  hedhi.
 
Ushauri;
Jamii inapaswa kuendelea kuelimishwa kuhusu ubaya wa kitendo hicho cha ukeketaji kabla ya kutumia nguvu, maana katika jamii ya wanaokeketwa inaamini kuwa hakuna mwanamke anayeweza kuolewa bila kukeketwa.

Lakini tujiulize kuwa je nani anaendeleza mfumo dume katika jambo hili? Jibu linaweza kuwa ni kwamba, wanawake wanaendeleza mfumo jike kwa kuutukuza mfumo dume.
Maswali yafuatayo ni vema yakajulikana vizuri kuwa, Je wanawake hawawezi kuolewa bila kukeketwa? Je wanawake wakikataa kukeketwa wanaume hawatawaoa?
Basi cha kufanya ili kufanikiwa katika suala la ukeketaji wa wanawake, ukemewe kwa nguvu zote za jamii, kuwaeleza wanawake wanaoendekeza mila hiyo ambayo tafsiri yake ni mfumo jike kuendekeza mfumo dume.
Mwandishi 0754 440740
kalulunga2006@gmail.com

UZINDUZI WA HARAKATI KATIKA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA


Bendi ya Jeshi la Polisi wakiongoza maandamano ya wanaharakati. 
Wanaharakati kutoka Taasisi mbalimbali wakiwa na mabango yaokwenye maandamano yaliyoanzia Uzuri Sinza na kuishia katika ukumbi wa ubungo plaza jijini Dar es salaam leo.

wanaharakati wakiwa kwenye ukumbi katika kupinga ukatili wa kijinsia ulioadhimishwa leo jijini Dar es salaam. 

SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA


Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili kanda ya Kaskazini na Meneja Miradi wa Shirika lisilo la kiserikali la NAFGEM,Honorata Nasuwa akizungumza na wanahabari(hawako pichani ) juu ya uzinduzi huo,kushoto kwake ni Afisa Ushawishi na utetezi (KWIECO) na mratibu wa maadhimisho hayo kanda,Hilary Tesha.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya maandalizi ya uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili kanda ya Kaskazini.
Baadhi ya waandishi wa habari mkoa wa Kilimanjaro wakifuatilia taarifa juu ya uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.
Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya siku 16 zakupinga ukatili na aliyekuwa Mwenyekiti wa dawati la Jinsia,Grace Lyimo akizungumza jambo katika kikao cha kamati hiyo na wanahabari.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia taarifa hiyo.


Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
Mahakama ya Nkasi yamwamuru mume ajenge nyumba ya mtalaka wake aliyoibomoa

Mahakama ya Nkasi yamwamuru mume ajenge nyumba ya mtalaka wake aliyoibomoa

 Picture


Picture Maria Tarafa (wa kwanza kushoto) akiwa na watoto wake wanne aliozaa na Ndebile Kazuri akiwa amekaa kwenye kifusi cha sehemu ya nyumba anayokaa, mumewe ameibomoa nyumba hiyo ili kumfukuza eneo hilo. 

MAHAKAMA ya mwanzo Mjini Namanyere, Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa imetoa amri ya kumtaka Ndebile Kazuri kujenga nyumba ya aliyekuwa mke wake Maria Tarafa iliyopo kijijini Isale ambayo aliibomoa akishinikiza mtalaka wake aondoke eneo ambalo alikuwa akikaa kabla ya kutengana.  Mwishoni mwa mwaka jana (2013) Mahakama hiyo ilivunja ndoa ya wanandoa hao wenye watoto wanne baada ya Kazuri kuwasilisha kesi mahakamani akitaka ndoa yake na mkewe ivunjwe. Hata hivyo baada ya kuvunjwa kwa ndoa hiyo mke amewasilisha kesi mahakamani hapo akitaka mali za ndoa hiyo zigawanywe na mume awajibike kuwatunza watoto wake, jambo ambalo halikuzungumziwa kwenye kesi ya awali.  Akizungumza na mwandishi wa habari hizi juzi, Bi. Tarafa alisema Mahakama ya mwazo imetoa amri ya kumtaka mtalaka wake kujenga nyumba aliyomvunjia yeye na watoto wake wanne akishinikiza aondoke nyumbani hapo, bila kupewa haki ya mgao wa mali zilizochumwa wakati wa ndoa.  “…Juzi tumetoka Mahakamani nilikwenda kufungua kesi nikiiomba mahakama igawe mali ambazo tulichuma na mume wangu muda wote wa ndoa yetu lakini mume wangu hataki zigawanywe, ila mahakama imemuamuru kwanza ajenge nyumba ambayo amenivunjia pale nyumbani nikiwa na watoto akitaka niondoke nyumbani, ameambiwa awe ameimaliza kabla ya Februari 14,” alisema Bi. Tarafa akizungumza kwa njia ya simu.  Alisema Kazuri alivunja nyumba ambayo mkewe alikuwa akiishi na watoto wake wanne siku chache baada ya mahakama ya mwanzo wilayani Nkasi kuvunja ndoa yao, jambo ambalo Bi. Tarafa hakukubaliana nalo kwani alitegemea watagawana mali ya ndoa yao na yeye kupata nyumba ya kuishi.  “…Katika muda wote wa ndoa yetu tumefanikiwa kupata mali kama nyumba tatu ambazo zote zipo eneo moja la kijiji cha Isale, ng’ombe zaidi ya 127, mbuzi 30 pamoja na mashamba zaidi ya hekari 70 mali ambazo hazikuzungumziwa kabisa na mahakama, lakini baada ya ndoa kuvunjwa nashangaa mwenzangu ananibomolea hata nyumba ambayo nilikuwa naishi mimi na wanangu…sasa naomba kila mmoja agawiwe haki yake,” alisema Bi. Tarafa.  Kazuri alifungua kesi katika Mahakama ya Mwanzo, Namanyere Wilaya ya Nkasi Oktoba 28, 2013, kesi namba 26/2013 iliyosikilizwa na Hakimu aliyetajwa kwa jina la B. Stanley; na Novemba 18, 2013 hakimu huyo baada ya kuisikiliza kesi aliamuru ndoa ivunjwe.  Mahakama ilivunja ndoa hiyo na kuamuru Bi. Tarafa aondoke na watoto wawili kati ya wanne waliozaa na mumewe kipindi wakiishi kama mke na mume bila kueleza namna watoto hao watakavyo pata huduma toka kwa baba yao. Mahakama pia iliamuru watoto wa miaka 7 na 9 watabaki kwa baba yao na wenye miaka chini ya saba kubaki na mama yao. Mahakama hiyo ya mwanzo pia iliamuru mke apewe magunia 9 ya mahindi kati ya 10 ambayo walizalisha wote na bati 7 zilizokuwa nyumbani.  Kwa upande wake Kazuri akizungumzia juu ya mali ambazo mkewe anazilalamikia, alisema mali hizo alipewa na babayake wakati anaanza maisha hivyo bado ni mali ya babayake mzazi ambaye alidai yupo hai hadi sasa. Hata hivyo tarifa zaidi zinasema baba yake na Kazuri (Kazuri Moshi) alifariki mwezi Machi 2004 na mali zake kurithishwa kwa watoto wake akiwemo Kazuri.  Katika mgao huo mtalaka wa Kazuri alisema walipewa jumla ya ng’ombe 65 lakini wamezizalisha hadi kufikia idadi kubwa hivi sasa, ambapo ni zaidi ya ng’ombe 127 pamoja na mashamba.  
*Imeandaliwa na www.thehabari.com kwa kushirikiana na TAMWA
MUME AMKATA MKONO MKEWE

MUME AMKATA MKONO MKEWE

Na  Imelda Mtema
NI mkasa wa kusikitisha kama siyo kutisha, unaowafanya wanaume  wengi wa siku hizi  waonekane ni makatili na majanga matupu mbele ya jamii.


Akizungumza na Joyce Kiria(kulia), Leah (kushoto) alisema kwamba siku zote aliishi na mumewe kwa uvumilivu mkubwa.
Kitendo hicho cha kinyama, kimemkuta mwanamke Leah  Benard mkazi wa Kijiji cha Kifufu, mkoani wa Geita baada ya kukatwa kiganja chake cha mkono kwa panga na mumewe (jina kapuni).
Kisa cha kufanyiwa unyama huo kinadaiwa kuwa ni mwanamke huyo kukataa kwenda kuchukua chakula kwa mama yake mzazi ili familia hiyo ile.



Mkono wa Leah baada ya kukatwa na mumewe.
Akizungumza na mwandishi wetu, Leah alisema kwamba siku zote aliishi na mumewe kwa uvumilivu mkubwa kutokana na vipigo vya mara kwa mara alivyokuwa akivipata.
 

“Nilikuwa nikipokea vipigo vikali wakati mwingine bila sababu za msingi lakini nilikuwa nikivumilia.
“ Kisa cha kukatwa mkono ni kukataa kwenda nyumbani kwa mama yangu kuchukua chakula cha kula pale nyumbani, kitu ambacho ni kinyume na utaratibu wetu wa maisha,” alisema Leah.
Mwanamke huyo alisema kwamba mumewe alimlazimisha kwenda kuchukua chakula hicho lakini alipokataa alipigwa na  kulazimika kuondoka mpaka nyumbani kwa wazazi wake kukwepa  kipigo zaidi.

Leah aliendelea kudai kwamba siku nyingine saa saa mbili usiku akiwa anapika chakula cha familia, alishtukia mkono wake ukiwa umebaki mfupi na kusikia maumivu makali, alipogeuka akamuona mumewe akikimbia.
“Sikuwa na wazo lolote nilikuwa nikipiga kelele ya kuomba msaada na baadhi ya majirani wakajitokeza kwa kuwa damu zilinitoka kwa wingi nikapoteza fahamu,” alisema Leah.
Leah aliongeza kuwa alizinduka akiwa akiwa  hospitali kitu ambacho kilimfanya ajisikie vibaya  kwa kuwa hakuwa na kosa la kusababishiwa ulemavu wa ukubwani.

Mwenyekiti wa kitongoji hicho cha Kifufu, Ali Malima, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa kijiji kinamsaka mume wa Leah.
Kutokana na kitendo hicho alichofanyiwa,  mwanamke huyo amelazimka kuwa na maisha magumu hivyo anawaomba Watanzania walioguswa na habari hii  wamsaidie kumchangia ili aweze kupata mkono wa bandia.
Kama umeguswa  na matatizo yake, unaweza kumchangia kwa namba  0753 787126.
 Shukurani zaidi ziende kwa Wanaharakati wa Kutetea Haki za Wanawake (HAWA), Joyce Kiria kupitia kipindi chake cha Wanawake Live kwa kuweza kufutilia habari hii kwa kina.      


Na GPL

Binti wa miaka 15 atekwa kwa siku tatu na kubakwa Makete Njombe


Jeshi la polisi wilayani Makete  mkoani Njombe linamshikilia  Fransis Pilla (36) mkazi wa kijiji cha Iwawa na kata ya Iwawa  wilayani hapa kwa makosa  mawili ya  utekaji nyara na  ubakaji  kwa binti mwenye umri wa miaka 15 ambaye jina lake limehifadhiwa.


Akiongea na vyombo vya habari wilayani hapa afisa upelelezi wa jeshi la polisi wilaya ya Makete Bw Gozbert Komba  amesema kuwa siku ya tarehe 15 mwezi huu walipokea taarifa  kutoka kwa msamaria mwema ambaye pia ni mwajiri wake bw. Erick Mbilinyi (34) ya      mtendewa kutekwa na kufungiwa ndani ya nyumba ambayo haijakamilika ujenzi wake maarufu kwa jina la pagale ambapo walifika katika jumba hilo  na kumkuta akiwa amefungwa kamba mikononi na miguuni.


Amesema kuwa  mara baada ya kumkuta mtendewa huyo akiwa ametekwa walimhoji na yeye kukiri  kuwa amebakwa na  hajaoga tangu afanyiwe ukatili huo na hivyo kurahisishia  kupatikana kwa vipimo kutoka kwa madaktari kuwa ni kweli binti huyo amebakwa na kuongeza kuwa walikuwa wana mahusiano ya kimapenzi.


Katika hatua nyingine mrakibu huyo amebainisha kuwa  mtendewa huyo alisema kuwa alitekwa nyara kwa siku tatu,   na hajala chakula kwa siku zote hizo ambapo alitekwa nyara tangu tarehe 3  mwezi Januari mwaka huu  majira ya saa saba mchana  mpaka tarehe 5 mwezi huu majira ya saa saba na nusu mchana
Amesema polisi wanatarajia kumfikisha mahakamani siku chache zijazo
Na Jiachie
Wanaharakati wazungumzia kukamatwa kwa wakeketaji haramu

Wanaharakati wazungumzia kukamatwa kwa wakeketaji haramu


Kufuatia kuwakamata wanawake 38 nchini Tanzania,kwa kuwafanyia ukeketaji haramu kundi la wasichana wa mji wa Same, wanaharakati wamelipokea suala hilo kwa mtazamo tofauti, wakitaka sheria ifanye kazi.
Wanawake hao walikamatwa wakati wakicheza ngoma za asili katika nyumba moja, ambako polisi iliwakuta wasichana 21 wenye umri kuanzia miaka mitatu hadi 15, waliokwisha keketwa. Flora Nzema amezungumza na Jovita Mlay mwanaharakati wa masuala ya ukeketaji, ambaye kwanza anaelezea namna alivyoipokea hatua ya kuwafikisha wahusika mahakamani. Je kufikishwa mahakamani kwa wanaoounga mkono vitendo vya ukeketaji kutasaidia kukomesha vitendo hivyo nchini Tanzania?
Na Dw.de

DAWATI LA KUPINGA UKATILI NA UNYANYASAJI WA KIJINSIA LA POLISI MBEYA

Wajumbe wa dawati hilo wapo katika ziara ya kutembelea vituo mbalimbali ikiwa ni katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kiijinsia 





Mmoja wa wajumbe wa dawati la Ukatili na Unyanyasaji wa kijinsia la polisi mkoa wa Mbeya Mary Gumbo akikabidhi zawadi ya sabuni kwa watoto yatima waishio katika kituo cha Malezi na Matunzo ya watoto Yatima cha Msamaria Mwema kilichopo Songwe wilayani Mbeya











JAMII ya watoto yatima imeshauriwa kutokatishwa tama na maisha magumu yanayoikabili badala yake iendelee kushirikiana na wadau wanaoijali katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazoikabili. 
Mkuu wa Dawati la Ukatili na Unyanyasaji wa kijinsia la polisi mkoa wa Mbeya mkaguzi msaidizi wa jeshi hilo Samora Saranga aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Malezi na Matunzo ya watoto Yatima cha Msamaria Mwema kilichopo Songwe wilayani Mbeya. 
Saranga aliyeambatana na wajumbe wengine wa dawati hilo kutembelea kituo hicho alisema watoto yatima wanapaswa kutambua kuwa maisha wanayoishia yapo katika mipango ya mwenyezi Mungu na si wao wala wazazi wao waliopenda jamii hiyo iishi hivyo. 
Ziara ya wajumbe wa dawati hilo kituoni hapo ni mwendelezo wa ziara katika vituo mbalimbali ikiwa ni katika kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia. 
Na Lyamba Lya Mfipa

MTOTO AVUNJWA KIDOLE NA MWALIMU WAKE BAADA YA KUJA NA NYWELE NDEFU SHULENI


Jacline Staniely[9] akiwa nyumbani baada ya kutoka hospitali kutibiwa
Picha ya Xray ikionyesha cha kati kilichovunjika
Pf3 ya polisi



Wiki ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na watoto ikiwa imeanza kuadhimishwa duniani Novemba 25 mwaka huu bado vitendo hivyo vimezidi kushamiri Mkoani Mbeya ambapo mwanafunzi wa darasa la nne shule ya msingi Aiport Kata ya Iyela jijini Jacline Staniely[9] kuumizwa mkono wake wa kushoto.

Jacline akiongea kwa ridhaa ya mama yake amesema alipigwa kwa kutumia ubao na mwalimu wa shule hiyo Novemba 19 mwaka huu na mwalimu Kanyika kwa kosa la kuwa na nywele ndefu.
Mwanafunzi huyo amedai kuwa siku ya tukio alipigwa vibaya na kumsababishia maumivu makali ambapo siku hiyo mama yake alikuwa safarini Nairobi Kenya hivyo hakupata matibabu ambapo alilazimika kumwambia mwalimu jirani[Bibi]ambaye alimpeleka hospitali kutibiwa.
Hata hivyo Jackline amesema kuwa kutokana na maumivu makali alilazimika kufanya mtihani wa Taifa wa darasa la nne bila kupata matibabu ya kutosha.

Baada ya kurejea kutoka safari mama yake mzazi aitwae Rehema Adamson Ndeje[28] mkazi wa Block T jijini Mbeya amesema baada ya maumivu ya mwanae usiku ilimlazimu kwenda shuleni ili kujua kulikoni,ndipo alipoonana na mwalimu Kanyika baada ya kukutanishwa na Mwalimu mkuu.

Mama Jackine amesema hicho ni kipigo cha tatu kukubwa kwa mwanae kupigwa na mwalimu huyo ambapo alionesha makovu yaliyodaiwa yalitokana na vipigo vya mwalimu huyo miguuni akidai majeraha hayo yalidumu kwa miezi mitatu.

Hata hivyo Rehema aliamua kwenda Polisi Mwanjelwa kutoa taarifa za tukio na kila alipoitwa mwalimu huyo hakutokea ndipo jalada likapelekwa kituo kikuu cha kati ambapo mwalimu alikamatwa na mhanga kupewa PF 3 kwa ajili ya matibabu ambapo alipigwa picha na kuonekana moja ya kidole cha kati cha kushoto kuoneka kuathirika kutokana na kupigwa kwa kutumia ubao.

Mzazi huyo amesema hana ni mbaya na mwalimu Kanyika lakini kitendo cha kumwadhibu mwanae mara kwa mara ndicho kimemtia shaka hata kuamua kutoa taarifa Polisi ili sheria ichukue mkondo wake.
Mwandishi wa habari hii alipofika shuleni ili kujua mustakabali wa suala hili mwalimu alitoa nje mwandishi akidai yeye ana majukumu mengine lakini baada ya kufuatilia mkuu huyo alichukua gari lake aina ya RAV 4 na kwenda nyumbani kwa Mzazi wa mtoto na kwenda naye hospitali akiwa ameambatana na mmoja wa walimu wa shule hiyo ambaye ni jirani ambapo Jackline humwita Bibi.

Mwandishi alimtafuta mmoja wa wanaharakati wa kijinsia ambaye alikiri kupokea lalamiko hilo ingawa alijibu kwa mkato kuwa mtoto huyo kaumia kidogo tu na ni usanii mtoto huyo kufungwa POP na kwamba bado PF3 haijajazwa kitu hivyo hawezi kuzungumzia lolote.

Kumekuwa na malamiko mengi katika Dawati hilo kutokana na matukio kutochunguzwa kwa wakati hali inayotoa mwanya kwa vitendo hivyo kuibuka mara kwa mara na wahalifu kutoroka mkono wa sheria lakini baadhi kuwa na utendaji duni licha ya taarifa kutolewa kwa wakati.
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya ameahidi kulifuatilia suala hilo na ikibainika mtuhumiwea atafikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma zinazomkabili.

Habari na Ezekiel Kamanga 
Mbeya yetu

Kategori

Kategori