Showing posts with label ziara siasa. Show all posts
Showing posts with label ziara siasa. Show all posts

NAPE MTAANI NA WANANCHI NDANI YA SOKO LA MWANJELWA JIJINI MBEYA

CONTACT WITH ELIMTAA BLOG BY: CALL :+255 788 056115 EMAIL: furahanews1@gmail.com Facebook: www.facebook.com/elimtaa Twitter: www.twitter.com/@elimtaa "ANY TIME CALL US FOR ADVERTISEMENT, OR ANY NEWS YOU WANT APPEAR TO Elimtaa Blog" Elimtaa 'more news update your mind'
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa  Nape Nnauye akicheza draft na vijana wafanyabiashara wa soko la Sido Mwanjelwa jijini Mbeya.
Nape yupo mjini Mbeya kwa ajili ya maandalizi ya sherehe za miaka 37 ya CCM ambazo kitaifa zitasheherekewa mkoani hapo.Katibu wa NEC alikutana na vijana mbali mbali ambao walifurahi sana kumuona kiongozi wao akiwa pamoja nao kiasi soko zima lilipuka kwa nyimbo za hamasa za CCM zilizoimbwa na Kapteni John Komba,Nape pia alipata fursa ya kusalimiana na baadhi ya madereva wa Taxi wa kituo maarufu cha Mafiati.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akila chakula cha mchana kwenye kibanda cha Mama Lishe anayefahamika kama Bi. Tandiwa Tewete kwenye soko la Sido Mwanjelwa mjini Mbeya.
 
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akikatiza katikati ya soko la Sido Mwanjelwa kwenda kwenye viwanja vya mpira vya soko hilo kushuhudia mechi ya mpira ya wafanyabiashara wa sokoni hapo.

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akiangalia mechi ya mpira kati ya timu ya soka ya sokoni Sido wauza Mitumba na wafungua Mabelo kwenye uwanja wa mpira wa sokoni Sido.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa timu za mpira sokoni Sido Mwanjelwa mjini Mbeya mara baada ya mpira kumalizika.
 Na Jamii Moja Blog

CCM YAJIVUNIA MAFANIKIO

CONTACT WITH ELIMTAA BLOG BY: CALL :+255 788 056115 EMAIL: furahanews1@gmail.com Facebook: www.facebook.com/elimtaa Twitter: www.twitter.com/@elimtaa "ANY TIME CALL US FOR ADVERTISEMENT, OR ANY NEWS YOU WANT APPEAR TO Elimtaa Blog" Elimtaa 'more news update your mind'
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mkutano wa CCM Mkoa wa Mbeya.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisisitiza jambo wakati akijibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano katika ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya.



   Wakati CCM inatimiza miaka 37 tangia kuanzishwa kwake februari 5 mwaka 1977,Chama hicho kinajivunia sana mafanikio makubwa kiliyopata hasa katika kudumisha Umoja na Mshikamano kwa  Watanzania ,kutunza na kuilinda Amani ya nchi hii na kujenga misingi imara ya uchumi wa nchi,akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano CCM Mkoa wa Mbeya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye  alisema  sherehe za miaka 37 zimeanza nchi nzima na zilizinduliwa rasmi tarehe 26 na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Dk.Ali Mohamed Shein Unguja Zanzibar.

  Kilele cha sherehe hizi  kitakua tarehe 2 februari ,Nape alisema “kwa nini tarehe mbili na sio tano ni kwa sababu tarehe tano ni siku ya kazi hivyo tumeona tufanye tarehe mbili ili tuwaruhusu watu wengi zaidi waweze kushiriki”

Sherehe hizi zitahitimishwa hapa jijini Mbeya kwenye uwanja wa Sokoine na zitahitimishwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete.

Viongozi mbali mbali wa Kitaifa wa CCM wameanza kuwasili na kesho anategemewa kuwasili Makamu Mwenyekiti  wa CCM (Bara) Ndugu Philip Japhet  Mangula ambaye pia ni mlezi wa mkoa wa Mbeya  akitanguliwa na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana.

  Nape alisema “Tarehe 2 asubuhi saa moja kutakuwa na matembezi ya mshikamano yatakayoongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama ,Rais Jakaya mrisho Kikwete matembezi hayo yatafanyika kwenye jiji la Mbeya yataanzia eneo la Soweto na yataishia kwenye ofisi za CCM mkoa wa Mbeya, baada ya matembezi hayo wananchi watakwenda kwenye viwanja vya Sokoine ambapo kutakuwa na burudani mbali mbali vikiongozwa na TOT, Vikundi vya muziki wa kizazi kipya, sherehe hizo zitaonyeshwa moja kwa moja na baadhi ya televisheni pamoja na kurushwa moja kwa moja na baadhi ya radio.

Wakazi wa Mbeya waombwa kujitokeza kwa wingi wakati wa mapokezi ya Mwenyekiti wa  Chama Cha Mapinduzi  tarehe moja na pia washiriki kwenye matembezi na sherehe zitakazofanyika tarehe2.

Maadhimisho ya sherehe hizi yataambatana na shughuli mbali mbali nchi kote ,ikiwa pamoja na shughuli  za utunzaji wa mazingira kama kupanda miti,kushiriki shughuli za maendeleo kujenga shule na zahanati,usafi  pamoja na kutembelea wagonjwa hospitalini.

DR.SLAA AKERWA NA UJINGA WA CHADEMA MBEYA MJINI








(Picha na Furaha Eliab, Mbeya)
Dr.Wilbroad Slaa, leo katika viwanja vya CCM ILOMBA Jijini Mbeya, amesema licha ya mapokezi mazuri aliyooneshwa na wafuasi wake, lakini hajafurahishwa na jeneza lililokuwa limetengenezwa huku msalaba wake ukiwa na jina la mtu aliyehai Zitto Kabwe.


Amesema hali hiyo haipendezi kwasababu ishara ya jeneza inatisha hasa ikionesha taswira ya kumzika mtu aliye hai.

Alisema kumfukuza Zitto ni ishara ya chama chake kuthubutu kufanya yale watakayoyasimamia watakapoingia Ikulu ambapo yeyote atakayekiuka,  atashughulikiwa na kumtaka Rais Jakaya Kikwete kuchukua hatua kwa wanaokiuka sheria za nchi.

Kwa upande wake Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu), alisema amepata taarifa za Chama Cha Mapinduzi(CCM), kuandaa kambi la vijana wa kuvuruga mikutano ya Chadema ambalo lipo katika shule ya Sekondari ya Chimala wilayani Mbarali, inayomilikiwa na Umoja wa Wazazi wa CCM Mkoani Mbeya.

Taarifa hiyo imepuuzwa na baadhi ya viongozi wa CCM na UVCCM, ambao wamesema kambi la vijana hao ni kwa ajili ya halaiki ya sikukuu ya miaka 37 ya CCM Taifa, sherehe zinazotarajiwa kufanyika Jijini Mbeya na mgeni rasmi atakuwa ni Rais Jakaya Kikwete.
Na Habari na Kalulunga

MECHI MBILI ZA AWALI LIGI KUU KUTOCHEWA SOKOINE

Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi Mbeya, Bashiru Madodi



UWANJA wa Sokoine kutochezewa mechi mbili za mwanzo ukisubiliwa kuwa imara kwa kuchezewa mpira kufuatia matengenezo yaliyofanyika.
Akizizungumzia sababu za kutochezea mpira kwa msimu huo ambapo umeomwa kutochezewa kwa muda wa wiki mbili, Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya, Bashiru Madodi alisema Chama cha Mpira Mkoa wa Mbeya  (Mrefa) kimeomba kutochezwa mechi Mbili.
Madodi alisema kuwa uwanja huo uliofanyiwa marekebisho katika sehemu kuu mbili sehemu ya kuchezea na Magoli umekamilika na kuwa unaweza kuchezewa mpira.
Kutokana na kuto kuwa vizuri uwanja huo Mrefa wameomba kwa Chama cha mpira Taifa TFF kuhahilisha kuchewa mechi Mbeli zilizo takiwa kuchezwa uwanjani hapo.
Alisema  Mrefa wameomba kuahilisha mechi hizo mblili kufuatia kuto komaa vizuri kwa nyasi zilizo pandwa na kuwa wananchi wasiwe na wasiwasi kufuatia kuto cheza kwa mechi hizo mbli za awali.
Kufuatia ukarabati huo ukiwa ni wa awamu ya kwanza kufanyika Madodi alisema kuwa kutakuwa na awamu ya pili ambayo itahusisha ukarabati wa vyoo kiwanjani hapo.
Madodi alisema kuwa ukarabati uliofanywa uwanjani hapo umekuwa ni mkubwa kuwahi kutokea na TFFwamesema kuwa sasa uwanja wa Sokoine unaonekana kuwa ni miongoni mwa viwanja bora vya mpira hapa nchini.

HAYA NDIO MATOKEO YA UCHAGUZI WA MWENYEKITI WA CHAMA MAARUFU CHA UPINZANI NCHINI JANA LIVE!!



Habari zilizotufikia muda si mrefu zinathibitisha kwamba Mkutano Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi umemchagua tena James Mbatia(Pichani) kuwa Mwenyekiti wa chama hicho kwa kipindi kingine cha kuanzia Januari 2014-2019.



Katika uchaguzi huo, Mbatia alikuwa akichuana kwa mbali na aliyekuwa Kamishna wa chama hicho mkoa wa Katavi Charles Makofila na mpaka mwisho Mbatia ameshinda kwa kura 201 huku Makofila akiambulia kura 26 na kura moja ikiharibika.


Wajumbe waliohudhuria mkutano huo walikuwa  228 kati ya 289.

HUU NDIO UKWELI WA MAMBO . CHADEMA KUINGIA UCHAGUZI MKUU 2015 IKIWA DHAIFU

MWENYEKITI WA CHADEMA

SAFARI ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuelekea katika uchaguzi mkuu wa 2015 imeelezwa kuwa ni yenye kutia shaka na kimetabiriwa kufika mwaka huo kikiwa dhaifu.
Mwenendo wa matukio ambayo umma umeendelea kuyashuhudia ndani chama hicho wiki hii, msingi wake ukiwa ni kuvuliwa uongozi Zitto Kabwe na kuvuliwa uanachama kwa Dk. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba, ndiyo yaliyoibua hisia za namna hiyo miongoni mwa umma na jamii ya wasomi walioko ndani na nje ya chama hicho.
Tayari baadhi ya wasomi na wanasiasa wenye ushawishi hapa nchini, wakiwemo viongozi wa kada mbalimbali, wamekwisha kukaririwa kwa nyakati tofauti wakieleza kuona hatari ya kifo inayokikabili Chadema, kutokana na uamuzi wake huo wa kuwavua uanachama makada wake wawili na kutishia kuchukua uamuzi kama huo kwa Zitto.
Ndani ya Chadema na katika Kamati Kuu ya chama hicho, baadhi ya wajumbe wake nao wamekaririwa kutoa kauli zinazoonyesha kuona hatari ya kifo inayokikabili chama chao.

Mbunge wa Iringa Mjini, Mchugaji Peter Msigwa, amekaririwa ndani ya Kamati Kuu ya chama hicho hivi karibuni, akisema kuwa ni heri chama hicho kipoteze Uchaguzi Mkuu wa 2015, lakini Zitto aondolewe.
Mbali na Msingwa, miongoni mwa wasomi wanaoheshimika hapa nchini, na makada wa chama hicho, Mabere Marando na Profesa Mwesiga Baregu, nao wametoa kauli za kukionya chama hicho juu ya uamuzi wake huo na kueleza hatari wanayoiona mbele.
Marando amesikika ndani ya Kamati Kuu ya chama hicho akisema kuwa, anaona mwelekeo ule ule wa NCCR-Mageuzi kuipata Chadema.
Ni kutokana na hilo, matukio ya hivi karibuni kabisa ya kutekwa na kujeruhiwa kwa Mwenyekiti wa chama hicho Wilaya ya Temeke, Joseph Yona, lakini pia kuzuka vurugu ndani ya Kamati Kuu na lile la wafuasi wa chama hicho walio katika pande mbili zinazopingana, kupigana nje ya Mahakama Kuu ya Dar es Salaam, ambako Zitto alikuwa akitafuta haki yake ya uanachama, yanafananishwa na yale yaliyopata kutokea ndani ya chama cha NCCR-Mageuzi kati ya miaka ya 1990 na 2000.

Inaelezwa kuwa miongoni mwa mambo ambayo yalichangia chama cha NCCR-Mageuzi, ambacho kilikuwa chama kikuu cha upinzani nchini kupoteza nguvu zake wakati huo, ni migogoro ya kiuongozi ambayo ilisababisha watu kutwangana hadharani, kama ilivyo sasa kwa Chadema.

Tayari Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, amekitaka Chadema kujiepusha na vurugu na uvunjifu wa amani wakati kinapotatua mgogoro wake na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wake, Zitto Kabwe.

Wakati hayo yakitokea, huko Kigoma baadhi ya wananchi nao wamekaririwa wakieleza kufedheheshwa na kauli iliyotolewa na baadhi ya viongozi wa Chadema ya kumuita Mbunge wao kuwa ni Mbunge wa Mahakama na wametamka bayana kwamba iwapo Zitto atatimuliwa, chama hicho kisahau kuungwa mkono mkoani humo.

Askofu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana anayetoka Mkoa wa Kigoma, Dk. Gerald Mpango, ambaye amekuwa mpenzi mkubwa wa siasa za mageuzi na ameshiriki mikakati mingi ya kuijenga Chadema, amesikika akisema kuwa hatua ya kumtoa Zitto haitakiacha salama chama hicho, licha ya kuwahi kufanya hivyo kwa Dk. Amani Kabourou na David Kafulila.

Wasomi ambao wameelezea matukio yanayotokea ndani ya Chadema, wameonyesha shaka kama chama hicho kitaweza kufanya vizuri katika uchaguzi mkuu ujao na kuonya kuwa kisipotafuta suluhu mapema, kuna dalili za kuanguka.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Prosper Ngowi, aliliambia Gazeti hili kwamba nyakati hizi si sahihi kwa chama hicho kuweka kipaumbele migogoro.

“Katika hili naweza kusema kuwa hiki si kipindi kizuri kwa Chadema kulumbana, kwasababu kama tunavyofahamu kuwa tunaelekea katika kipindi cha uchaguzi mkuu mwaka 2015, nilitarajia Chadema kama chama kikubwa cha upinzani kingetumia muda huu kujiimarisha zaidi kiweze kufanya vizuri katika uchaguzi wa 2015.

“Priority (kipaumbele) yao kwa sasa kilitakiwa kiwe kuangalia namna nzuri ya kuweka mikakati imara ya kuongeza madiwani, kuchukua viti vingi zaidi katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu, lakini pia kushinda majimbo mengi zaidi na ikiwezekana hata katika nafasi ya urais,” alisema Profesa Ngowi.

Alisema anashangazwa na kitendo cha sasa cha kuweka malumbano kama kipaumbele chao, hali ambayo inawadhoofisha katika kupanga mikakati imara ya ushindi.

“Wataalamu wa masuala vya vyama vingi wanasema kuwa kila lengo kubwa la chama cha upinzani, ni lazima katika kutafuta hiyo dola kuwe na mipango ya muda mrefu, sasa naona kama Chadema, moja ya chama kikubwa cha upinzani wameacha kufanya hilo kwa sasa na wameweka nguvu kubwa katika kutafuta migogoro, jambo ambalo linaweza kuwaangusha,” alisema Profesa Ngowi.

Alisema mgogoro uliopo kwa sasa hawezi kusema mshindi ni nani, bali busara inapaswa kutumika kumaliza tatizo lililopo kuweza kupata mwelekeo mzuri kuelekea mwaka 2015.

“Naweza kusema kuwa bado wana nafasi ya kusuluhisha hadi kufikia uchaguzi wa serikali za mitaa na kuelekea uchaguzi mkuu ujao,” alisema Profesa Ngowi.

Kwa upande wake, Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Profesa Peter Maina, alisema mambo yaliyojitokeza yataifikisha Chadema 2015 ikiwa dhaifu.

Alisema mgogoro uliojitokeza mpaka Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto kukimbilia Mahakamani, umetokana na uongozi wa chama hicho kushindwa kutumia busara kutatua mgogoro huo mapema.

“Niseme tu kwamba kuna watu ndio wameufikisha huu mgogoro hapo ulipo, ilikuwa rahisi kutumia busara kuumaliza pale wenzake na Zitto (Dk. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba) walipokiri kuandaa waraka na kusema ulikuwa siyo kwa nia mbaya.

“Lakini kuna watu wazito ndani ya Chadema kama kina Profesa Safari, Mabere Marando na wengine walipoona jambo hili inasemekana waliomba suluhu ya haraka, lakini inaonekana kuna watu upande wa chama hicho hicho hawataki suluhu na matokeo yake ndiyo haya ya kupelekana Mahakamani,” alisema Profesa Maina.

Alisema kitendo cha kulumbana nyakati hizi ni kusababisha chama hicho kuingia katika uchaguzi mkuu kikiwa dhaifu.

“Huu ni wakati wao wa kutafuta suluhu, naamini chama hakitakufa, lakini kitafika katika uchaguzi mkuu kikiwa dhaifu, hakitakuwa na nguvu kama ya awali, lazima viongozi wa Chadema wafahamu kuwa wakati mwingine haraka haina faida, uharaka uliotumika kushughulikia mgogoro haukuwa na faida.

“Kwa mfano, angalia Katibu Mkuu wa chama, Dk. Willibrod Slaa alivyofanya kipindi kile, badala ya kusuluhisha mgogoro, yeye anakwenda jimboni kwa Zitto kufanya mkutano, hapa inaonekana dhahiri hakuwa na nia ya kuleta suluhu, bali kuendeleza mgogoro, nafikiri busara hazikutumika toka awali na ndiyo maana leo hii mgogoro umekuwa mkubwa,” alisema Profesa Maina.

Katika hatua nyingine, Profesa Maina alisema kauli ya mwasisi wa chama hicho, Edwin Mtei, ya kusema Zitto hatakiwi ndani ya Chadema, inakiumiza zaidi chama, kwani haionyeshi demokrasi katika chama.

“Kauli ya Mtei inazidi kuonyesha nia ovu waliyonao baadhi ya watu ndani ya Chadema, kusema Zitto akatafute chama siyo maneno ya kuonyesha ukomavu kidemokrasia, niseme kwamba Mtei yeye anakiumiza zaidi chama, huu siyo wakati wa kulumbana ni wakati wa kutafuta suluhu kurudisha heshima ya chama.

Akizungumzia kitendo cha Zitto Kabwe kukimbilia Mahakamani alisema mbunge huyo amefanya hivyo kujikinga kutokana na hatua zilizopangwa kuchukuliwa dhidi yake.

“Kitendo cha Zitto kukimbilia mahakamani si kitendo cha ajabu bali amekwenda sehemu aliyoona haki itatendeka dhidi yake, unapoona mambo yanafanywa na mpinzani wako na unaona unaweza usitendewe haki una haki ya kwenda Makahamani kwahiyo wanaosema kwamba Zitto amekosea si kweli kwasababu yeye si mtu wa kwanza kwenda Mahakamani,” alisema Profesa Maina 

Na Nijimambo
 Meya wa Bukoba ajizuulu baada ya ripoti ya CAG

Meya wa Bukoba ajizuulu baada ya ripoti ya CAG

CAG Waziri mkuu alituomba tufanye ukaguzi maalum,   Mwaka 2013 tulifika bukoba na kufanya kikao cha kwanza na wadau.   Katika kikao hicho nilitoa maombi ambayo mliyafuata nawashukuru,madiwani na wananchi walitusaidia sana. Natoa taadhari kwamabtulikuwa na adidi za rejea amabazo ndizo  tulizofuata,tulipokea mombi ya wananchi wengi lakinio hayakuwepo katika  adidu za rejea,hatukuyafanyia kazi Kilichobainika Tunapohitaji maendeleo,tunafanya vitu kwa nia njema bila kufuata taratibu.
Kuhusu uwekezaji wenye mashaka kwenye kituo cha kuosha magari,zabuni haikuwa shindanishi ni kiyume na taratibu cha taribu anataja kifungu kilichokiukwa.
Waliosaini ni Khamis kaputa na anatory amani huku wakijua ilikuwa ni  makosa kufanya hivyo bila idhjini ya kikao cha madiwani,pia kamupuni  husika ya ASEC ilikuwa haijasajiliwa na BRELA.   hailipi kodi TRA
2.Issue ya Viwanja   kati ya wananchi 800 waliotakiwa kugawiwa viwanja ni 300 waliogawawia kutokana na migogo ya viwanja kimila.
Manispaa ilingia makubaliano na UTT kupima viwanja elfu 5 kwa  kuggawana faida ya asilimia 50 kwa 50 baina ya UTT manispaa ilisainiwa  na kaimu meya ngalinda bila kupata idhini ya baraza la madiwani
Pia walikopa fedha kutoka UTT bila kupata ridhaa ya waziri mwenye thamana.  3.Issue ya matengenzo ya barabara mpya
Manispaa ya bukoba iliingia mkataba na mkandarsai aitwaye KAJUNA  INVESTMENT mkataba ulikuwa wa sh  138 milioni alilipwa fedha za dharula  amabzo hazikuwa na nyaraka hivyo malipo ya mkandarasi huyu yaliongezwea  hadi kufikia sh  sh 227 kwa kutumia barua  iliyosainwa na tofauti na  hali ya awali.haikuwapa idhini ya mkandarsi wa serikali na  kinyume na  kanuni za manunuzi ya umma.anasoma kifungu kilichokiukwa.
4.issue ya Ujenzi wa soku kuu   Utaratibu wa kutaka kujenga soko kuu la bukoba haikupata idhini ya  madiwani ya kumlipa mkandarasi mshauri OGM  milioni 789 huku pia  akawaita madiwani na kuwaeleza kuwa mkandarasi anahitaji jumla la  miliini 590 mlioni. Mmojawapo wa madiwani mhg lunagisa alikataa pale  pale kwenye kikao.
5.Issue ya kuhamisha wafanyabisha wa bukoba   Mh Meya anatory aman aliomba mkopo kwa kazi hiyo bila kibali cha madiwani na mawaziri.mkpo huo hata hivyo haukupoatika 6.Mkandaasi wa OGM hakuwa kwenye orodha ya walioomba zabuni  ya kufanya kazi ya ukandarasi ushauri wa kufanya kazi katika ujenzi wa  soko kuu lakini alionekana kwenye rodha baadye ya waliolipwa  .Wakandarasi wote waliolipwa fedha hizo walikuwa hawalipi kodi TRA-hivyo TRA ina haki ya kuwadaiu hizo kodi.
7.Ujenzi wa stendi kuu ya bukoba   Mradi huu hakutengezwa kwenye gazeti la sertikali lakini walipata  mkandarasi na kumlipa fedha za kazi hiyo kinyume na taratibu za  serikali.gazeti lilotangaza tenda hiyo halikupatikana.  Pia timu ya  ukaguzi ilitembelea eneo al kazi na kubaini kuwa mkandarasi alilipwa  fedha nyhingi tofauti na kazi aliyoifanya.
9.Mradi wa maji   Kila kata iliyopangwa kuwekwa mradi wa maji ilitakiwa kuchangia  asilimia 2 hivyo kata anakotoka meya ilitiumiza kigezo na kupata huduma  hiyo.fedha za kata zilitolewa na meya kwa kata yake.hivyo kitendo cha  kata ya meya kupata huduma hakuwa na tatizo.Tuhuma hizi  kuwa meya  alitoa huduma kwa kata yakle ni uongo.  10.Issue ya uuzwaji viwanja vya wazi.   Mkataba wa kununua kiwanja kinacholalamikiwa hakufuata taratibu za ununuzi   Ni katika bweni la sekondari ya PEACE inayomilikiwa na  Meya.Tunapendekeza kuundwa kwa trimu maalum kuchunguza tuhuma hizi kwani katika eneo hili hatukufikia mwisho
11.Ujenzi wa barabara kwa lami kwenye kata ya meya toafuti na fedha zilizoombwa   Manispaa iliomba milioni 30 kukaqrabati barabarab hiyo akini TAMISEMI  ilitao milioni 300 na walihoji TAMISEMI walisema hilo ni la kawaida  hivyo tuhuma hizo ni UONGO.
12.Mradi wa Ujenzi wa Bwawa   Hakuwahi kujadiliwa na baraza la madiwani,ulikuwa ni mradi wa wajanja tu.
13.Issue ya wafganyabishara soko kuu kutolipa kodi   Manispaa Imekosa mapato sh milioni 256 zimpotea kutokana na chanzo  hizo cha wafanyabishara wa soko kuu kutolipa kodi kutokana na mgogoro  unaondelea.
14.Issue ya matumizi ya gari Sm 4663   Gari hili limekuwa likiegeshwa kwa ofisi ya redio kasibante ya  kagasheki. Kumbukumbu za TRA zinaonesha kuwa ni mali ya halmashauri  lakini alipohojiwa kagasheki alidai kuwa alinunua kwa fedha zake. Lakini halmshauri haina kumbukubu zozote juu ya gari hilo.
Tunapendekeza alilrejeshwe kwenye halmshauri kama ataona ni manufaa  kwa wananchi lakini kama haitawezekana basi gari hilo libadilishiwe  usajhili ili lionekbnane ni la kiraia.
15.Uteuzi wa wakala wenye upendeleo kwenye ushuru wa basi   Zabubi ya aliyepata rufaa ilitenguliwa kwani haikuwa imesajiliwa na mamlaka husika   Alibadilisha jina na kuomba tena kasha kupata,muombaji aliyeomba kwa tozo ya juu alinyimwa.
Manispaa ilifanya upendeleo na kukosa sh million 46 kwa mwaka16:Issue ya posho kwa madiwani katika safari ya mafunzo nje ya wilaya. Madiwani wawili walitakiwa kulipwa sh laki 4 kila mmoja kwa safari  hawakusafiri lakini fedha hizo hazikurudishwa kwa manispaa na kukatiwa  risiti,.hazionekjani zilipo
17.Issue ya vibanda vya maduka   Ukaguzi hakudhibitisha kuwepo tatizo la katika dai hili kwani nyaraka  zinaonesha kutokuwepo tatizo.bali inashauri kuwepo kwa mkanganyiko na  wapangaji wake.
18.Issue ya deni katika uwanja wa mpira kaitaba.   Uwanja ulikarabatiwa na kiwanda cha sukari kagera kwa madai ya  kurejeshewa fedha zake.sehemu ya fedha hazijarudishwa.Tume inapendekeza  kufanya muafaka na kiwana au itafute fedha za kulipa deni.
19.Kutowajibika ipasavyo kwa ukaguzi wa ndani.   Kipo kwa ajili ya kushauri na kuziba mianya ya matumizi mabaya ya fedha.   Aliyekuwepo amehojiwa juu ya miradi hiyo na kwamba halikuwa hajui lolote na hakuweza kumshauri mkurugenzi ipasavyo.
20.Mteuzi katika bodi ya maji.upendeleo kwa mmoja wa madiwani   Waziri mwenye thamana aliteuwa
Hitimisho.   Hatukuweka chumvi,tuliyosema ndiyo ukweli tupu   Namshukuru waziri mkuu kwa kunipa kazi hii ya kukaguzi katika manispaa.
Utaratibu wa uwasilisahji wa ripoti maalum tutaipeleka kwa aliyeomba ukaguzi huu.   ASANTENI AMEMALIZA
Mwanry anaongea sasa Kwa niaba ya waziri mkuu naomba nitoa taarifa hii kama ifuatavyo
Maelekezo ya waziri mkuu.  Makosa ya meya anatory kufanya makubaliano bila idhini ya madiwani na  taratibu za serikali basi ajipimemwenyewe na kujiuzuru kwa maslahi ya   manispaa ya bukoba.
Akikataa basi madiwani wamuondoe.
Watumishi wa manispaa wachukuliwe hatua   Bw Khamis kaputa avuliwe madaraka   Mhandisi,mweka hazina nk wapoteze vyeoi vyao
Wakandarasi wote waliopata fedha bila taratibu wazirejeshwe.

Alipopewa nafasi, Meya ametangaza kujiuzulu rasmi nafasi yake!
Na Dullonet

WANAMBEYA WAMPOKEA KWA UTOFAUTI KINANA



KATIBU mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Abrahaman Kinana ameitaka serikali kurudisha viwanda vyote vilivyo kufa iuli kuongeza ajira kwa vijana.

Akizungumza na wakazi wa jiji la Mbeya katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanya vya Ruanda Nzovwe jijini humu, Kinana alisema kuwa serikali ivirudishe viwanda vyote ili kuleta ajira kwa vijana ambao wapo mtaani na kukosa ajila.

Kinana alisema, kuwa Mkoa wa Mbeya zamani ulikuwa na viwanda vingi lakini vilibinafsishwa na viongozi wa serikali nia na kuzitafuna pesa na waliovichukua kushindwa kuviendeleza kisha kufungwa.
Alisema kuwa mtu alipo kuwa anataka kuchukua kiwanda alisema atakiendeleza lakini imekuwa kintume nma viwanda vingi vimekufa na kusababisha nchi kuw ana vijana wengi wasio kuwa na ajila.
“Viwanda vingi vilipo kuwa vikibinafsishwa ilidaiwa kuwa vitaendeleza chaajabu waliokuwa wakivichukua walishindwa kuviendeleza na hatimaye kuvifanya kuwa maghala ya kuhifadhia vitu mbalimbali,” Alisema Kinana.
Aidha kinana alisema kuwa atakutana na watu wanao husika na viwanda serikalini na kufanya utaratibu wa kuvirudisha viwanda hivyo ili kuleta ajira kwa vijana wa kitanzania ambao wengi wapo mtaani pasipo kuwa na ajira yeyote.
Alisema kuwa walioshidwa kuviendesha viwanda hivyo wavirudishe serikjalini ili viendelezwe na kuzalisha ajira kwa wananchi na kuwa anajua kuwa viwanda hivyo avitarudishwa hivihivi na vitauzwa.
“Viwanda hivyo havitarudishwa bure najua vitauzwa na katika uuzaji huo kunawatu watapata ulaji na hakunakukwepa wajanja wengi hapa nchini,” aliongeza Kinana.
   Kinana alisema kuwa serikali ichukue mashamba ambayo muwekezaji ameshindwa kuyaendeleza ambayo kwa sasa yamekuwa yakikodishwa kwa wananchi.
“Serikali iyachukue mashamba ya Mpunga ambayo yalibinafsishw ana serikali kwa lengo la kuongeza ajira kwa wananchi ambapo muwekezaji alisema kuwa atayasimamia na kuleta ajila sasa anakodisha kwa wananchi kinyume na alivyo takiwa kufanya alivyo sema wakati anachukua,” Alisema Kinana.
Katika mkutano huo ambao ulihudhuliw ana wananchi kutoka katika kona mbalimbali za wananchi walio fika katika mkutano huo walisema kuwa Kinana ni kama Hatati Baba wa Taifa Julius Nyerere kwani vitu alivyo visema vipo tofauti na viongozi wengine wa CCM.
Walisema kuwa kuhusiana na ufufuaji wa viwanda atatusaidia kuboresha maisha yetu na kupata ajira kitu ambacho hakijawahizungumzwa na viongozi wengene wote.
Mmoja wananchi  walio kuwapo katika mkutano huo wa adhara, John Mkombe, akizungunza na Elimtaa kuhusiana na kile kilicho zungumza na Kinana alisema, kuwa maneno analiyo yasema Kiongozi huyo ni kama Mwalimu (Baba wa Taifa) kwani amezungumza vitu vinavyo wagusa moja kwamoja.
Alisema viongozi wengine wakekuwa wakija na kutaka wapigiwe makofi na kuzungumza vitu ambavyo havina tija kwao na kuonge kwa kuilinda serikali lakini Kinana ametoa maneno makali kwa serikali.
Kinana alisema kuwa atazungumza na Rais Jakaya Kikwete kuhusina na ufufuaji wa viwanda ili viwanda vifuifuliwe na wananchi wapate manufaa ya viuwanda hivyo

KINANA NA MASHINE ZA EFD



  • CHELEWENI KUNUNUA HUENDA BEI IKASHUKA
  • HATAZIKIWEPO MASHINE MAKANJANJA WA TRA WATAKUWEPO TU
  • KINANA NI KAMA MWALIMU JK





WANANCHI wametakiwa kuendelea kubisha kununua mashine za kielekroniki za kutolea risiti (EFD) ili zizidi kushuka bei.
Hayo yalibainishw ana Kinana wqakati akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Mbeya katika mkotano wa Hadhara ambapo alisema kuwa waendelee kusita kununua mashine hizo ili kusababisha ziendelee kushuka bei.
Alisema, kuwa mashine hizo awali zilikuwa zinauzwa kwa bei ya shilingi milioni 2 na zikashishwa mpaka milioni 1.2 na sasa zinauzwa kwa shilingi laki 8 ambapo wakiendelea kusitakununua huenda zikashuka zaidi.
Alisema, yeye ana hoji ni kwanini zinashuka bei na je zinatofautigali na aliye nunua wakati ule zilikuwa zinanini na sasa hazina nini mpaka zikashuka bei kiasi hicho.
“Je wananchi wange nunua kwa wakati ule zinauzwa milioni 2 maana yake pesa za hapo juu kutoka milioni 2 hadi laki 8 zingeliw ana wajanja kunanini kunaupunguzwaji wa bei kama hazinautofauti au kuna wajanja wana kula cha juu,” alisema Kinana.
 Alisema, kuwa mashine hizi zimeletwa ikiwa ni mara ya tatu ambapo mashine za kwanza kuletwa ziliondolewa na kuwa hazifai zikaletwa zingine nazo zikaondolewa na sasa zimeletwa hizi wananchi wataziamini vipi kama zinafaa na haziko kama zile za awali zilizo ondolewa.
Kinana alisema, mashine hizo inadaiwa kuwa zitakuwa zikizibiti ulipaji wa kodi na kuwabana walio kuwa wakipitia njia za panya na kujinufaisha lakini yeye hana imani kwa asilimia zote kama mashine hizo zitaweza kudhibiti wala rushwa badara yake watabuni njia za kuchukua rushwa hata kama kuna mashine hizo.
“Mashine hizi hazita zuia moja kwa moja walarushwa wanao kula rushwa badala yake watabuni njia nyingine ya kuchukua rushwa kwa wafanyabiashara hata zikiwepo mashine hizo,” alisema Kinana.
Alisema maelezo yaliyo tolewa kuhusiana na mashine hizo ni mazuri sana sasa kama serikali inataka mwananchi huyo alipekodi vizuri ingetoa mashine hizo ili kuhakikisha analipa kodi vile inavyo takiwa.
“Kama serikali inataka kukusanya kodi inezitoa mashine hizo kwa wafanyabiashara bure kwa wafanyabiashara wanao anza biashara na kuangalia makusanyo ya kodi bara baada ya kuona biashara inaenda vizuri ataendelea kuitumia na kama haitaenda vizuri anyang’anye kuliko inavyo fanya hivi sasa na kudai itarudisha kidogokidogo kwa mwananchi pesa alizonunulia,” Aliongeza Kinana.
Kinana alisema kuwa serikama inampango wa kurudisha pesa hizo kwa mfanyabiashara anayetumia mashine hizo ingependeza kama mashine hizo zingetolewa bule kwa wafanyabiashara kama mkopo ili wawakape katika kodi wanayoikusanya.
Hivyo aliwataka wafanyabiashara hao kuchelewa kununua mashine hizo ili kusubili bei zishuke kama zilivyo shuka kutoka milioni 2 hadi laki 8 hivi sasa.
Mashine hizo zilisababisha wafanyabiashara kufunga maduka yao wakizikataa mashine hizo na kusababisha polisi kutupa mabomu na kumwaka maji ya kuwasha kwa wafanyabiashara wa Mbeya na wafanyabiashara wa Soko la Kaliakoo jijini Dar es salaam nao wakizipinga mashine hizo kugoma kufungua maduka yao.
Kufuatia kusitasita kuzitumia mashine hizo za EFD serikali iliongeza muda wa kufikia ukomo wa kutumia vitabu vua risiti madukani na kutumia mashine kutoa lisiti na kuwa mwisho wake kuwa ni disema 31 ili kusubili ambao hawajanunua wanunue.
Kinana alisema nda huo ulio ongezwa hautoshi hivyo iongeze mda wa ukomo wa utumiaji wa vitabu katia utoaji wa risiti.


BAADHI YA WAPIGAPICHA NAO WALIKUWEPO KATIKA ZIARA, WALIFANYA YAO HAWA NI BAADHI TU

John Bukuku Mpigapicha na Mmiriki wa Mtandao wa Fullshwangwe
Vinance Matinya Mpigapicha wa Gazeti ya Jamboleo

 Walikuwepo wapigapicha wengi lakini hawa ndio waliopita karibu na kamera ya Elimtaa

VIONGOZI WA LIOKUWEPO KATIKA ZIARA YA KINANA MBEYA

KINANA ALIVALISHWA VAZI LA KISAFWA NA VIONGOZI WA KISAFWA JIJINI MBEYA

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro (Shati ya Kaki) Meya wajiji la Mbeya Athanas kapunga (Upande wa kulia kwa mkuu wa Mkoa)
Mary Mwanjelwa anayezungunza na Shambwe Shitambara kulia na Katikati John Bukuku Mmiliki wa Mtandao wa Fullshangwe

Hao ndio baadhi ya viongozi mkoani Mbeya ambao kamera ya Elimtaa iliwatia katika lensi yake.
 

Kategori

Kategori