Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akicheza draft na vijana
wafanyabiashara wa soko la Sido Mwanjelwa jijini Mbeya.
Nape yupo
mjini Mbeya kwa ajili ya maandalizi ya sherehe za miaka 37 ya CCM ambazo
kitaifa zitasheherekewa mkoani hapo.Katibu wa NEC alikutana na vijana
mbali mbali ambao walifurahi sana kumuona kiongozi wao akiwa pamoja nao
kiasi soko zima lilipuka kwa nyimbo za hamasa za CCM zilizoimbwa na
Kapteni John Komba,Nape pia alipata fursa ya kusalimiana na baadhi ya
madereva wa Taxi wa kituo maarufu cha Mafiati.
Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akila chakula cha mchana kwenye kibanda
cha Mama Lishe anayefahamika kama Bi. Tandiwa Tewete kwenye soko la Sido
Mwanjelwa mjini Mbeya.
Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akikatiza katikati ya soko la Sido
Mwanjelwa kwenda kwenye viwanja vya mpira vya soko hilo kushuhudia mechi
ya mpira ya wafanyabiashara wa sokoni hapo.
Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akiangalia mechi ya mpira kati
ya timu ya soka ya sokoni Sido wauza Mitumba na wafungua Mabelo kwenye
uwanja wa mpira wa sokoni Sido.
Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya
viongozi wa timu za mpira sokoni Sido Mwanjelwa mjini Mbeya mara baada
ya mpira kumalizika.
Na Jamii Moja Blog