Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mkutano wa CCM Mkoa wa Mbeya.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisisitiza jambo wakati akijibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano katika ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisisitiza jambo wakati akijibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano katika ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya.
Wakati CCM inatimiza miaka 37 tangia kuanzishwa kwake
februari 5 mwaka 1977,Chama hicho kinajivunia sana mafanikio makubwa kiliyopata
hasa katika kudumisha Umoja na Mshikamano kwa
Watanzania ,kutunza na kuilinda Amani ya nchi hii na kujenga misingi
imara ya uchumi wa nchi,akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa
mikutano CCM Mkoa wa Mbeya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye alisema
sherehe za miaka 37 zimeanza nchi nzima na zilizinduliwa rasmi tarehe 26
na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Dk.Ali Mohamed Shein Unguja Zanzibar.
Kilele cha sherehe hizi
kitakua tarehe 2 februari ,Nape alisema “kwa nini tarehe mbili na sio
tano ni kwa sababu tarehe tano ni siku ya kazi hivyo tumeona tufanye tarehe
mbili ili tuwaruhusu watu wengi zaidi waweze kushiriki”
Sherehe hizi zitahitimishwa hapa jijini Mbeya kwenye uwanja
wa Sokoine na zitahitimishwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Mapinduzi na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete.
Viongozi mbali mbali wa Kitaifa wa CCM wameanza kuwasili na
kesho anategemewa kuwasili Makamu Mwenyekiti
wa CCM (Bara) Ndugu Philip Japhet Mangula ambaye pia ni mlezi wa mkoa wa Mbeya akitanguliwa na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu
Abdulrahman Kinana.
Nape alisema “Tarehe 2 asubuhi saa moja kutakuwa na
matembezi ya mshikamano yatakayoongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama ,Rais
Jakaya mrisho Kikwete matembezi hayo yatafanyika kwenye jiji la Mbeya yataanzia
eneo la Soweto na yataishia kwenye ofisi za CCM mkoa wa Mbeya, baada ya
matembezi hayo wananchi watakwenda kwenye viwanja vya Sokoine ambapo kutakuwa
na burudani mbali mbali vikiongozwa na TOT, Vikundi vya muziki wa kizazi kipya,
sherehe hizo zitaonyeshwa moja kwa moja na baadhi ya televisheni pamoja na
kurushwa moja kwa moja na baadhi ya radio.
Wakazi wa Mbeya waombwa kujitokeza kwa wingi wakati wa
mapokezi ya Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi tarehe moja na pia washiriki
kwenye matembezi na sherehe zitakazofanyika tarehe2.
Maadhimisho ya sherehe hizi yataambatana na shughuli mbali
mbali nchi kote ,ikiwa pamoja na shughuli
za utunzaji wa mazingira kama kupanda miti,kushiriki shughuli za maendeleo
kujenga shule na zahanati,usafi pamoja
na kutembelea wagonjwa hospitalini.