Showing posts with label 2017 at 06:47PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 06:47PM. Show all posts
UKIFANYA MAKOSA HAYA UTAHESABIKA KUWA UMEBAKA

UKIFANYA MAKOSA HAYA UTAHESABIKA KUWA UMEBAKA

Kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na mjadala mkubwa hasa kwenye mitandao ya kijamii na vituo vya habari kuhusu suala la watoto waliojifungua kurudi shule. Wengi walisikika wakisema sio kila anayepata mimba huwa alitaka au alijamiiana kwa kupenda, kwamba baadhi walibakwa.
Katika hilo, tukaona kwa ufupi tuelezee maana ya kubaka katika sheria ilivyo. Watu wengi hudhani kuwa, ili upatikane na kosa la kubaka, ni lazima utumie nguvu au kujamiiana na mtu pasipo idhini yake. Lakini katika uwanja wa sheria, kubaka ina maana pana zaidi ya hiyo.

Kuna aina mabalimbali ya matendo ukiyafanya hata kama ulijamiiana na mtu kwa idhini yake, lakini mbele ya sheria itafahamika kuwa ulibaka.

Kwa mujibu wa kanuni za adhabu, mtoto wa chini ya umri wa miaka 10, anachukuliwa kama hawezi kufanya kosa lolote, hivyo hawezi kuwajibishwa kwa alichofanya au kuto kufanya. Aidha, mtoto wa miaka chini ya 12 hatochukuliwa kama alitenda kosa, hadi pale itakapothibitishwa wakati wa kutenda au kutokutenda jambo alikuwa akifahamu.
Kwa mujibu wa sheria, mtoto wa chini ya umri wa miaka 12, anachukuliwa kuwa hawezi kujamiiana.
Kisheria, ni kosa kwa mwanaume kumbaka mwanamke. Na itachukuliwa kuwa mwanaume amembaka mwanamke endapo kitendo alichokifanya kitaangukia katika moja ya mambo haya;
Si mke wake, au ni mke wake lakini wameachana na hivyo akajamiiana naye bila idhini yake.
Kujamiiana na mwanamke kwa idhini yake, lakini idhini hiyo imepatikana kwa kutumia nguvu au vitisho kwa kumuweka mwanamke katika vitisho vya kumuua au kumjeruhi wakati umemshikilia kinyume na sheria.
Kujamiiana na mwanamke kwa idhini yake, lakini idhini hiyo imepatikana wakati akiwa hajitambui ama kwa kupewa madawa na mwanaume au mtu mwingine ili tu kuthibitisha kuwa kulikuwa na makubaliano ya awali.
Kwa idhini ya mwanamke, lakini mwanaume akijua kuwa yeye si mumewe, na idhini hiyo imepatikana kwa mwanamke huyo kuaminishwa kuwa yeye ni mke wa mwanaune huyo kihalali.
Kwa idhini au bila idhini ya mwanamke wakati akiwa na umri wa chini ya miaka 18, labda wawe wameoana na mwanamke ana umri wa zaidi ya miaka 15 na wakati wa kufanya tendo hilo hawakuwa wameachana.
Aidha, kama ni kiongozi katika taasisi yoyote ama ya serikali au la, ukituma manufaa ya uongozi wako kumbaka mwanamke, utaadhibiwa kwa mujibu wa sheria.
Ili kuthibitisha kuwa mtu amebakwa, kumuingilia mtoto wa kike au mwanamke, hata kama ni kidogo, inatosha kuthibitisha kuwa amebakwa. Lakini ushahidi wa majeraha katika mwili, hautoshi kuthibitisha kuwa mwanamke alibakwa.
Unaweza kuisoma hapa chini The Sexual Offences Special Provision Act, 1998 kwa uelewa zaidi kuhusu masuala hayo.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2tbopZH
via IFTTT


Barnaba Alizwa na Wezi, Aomba Walau Wamrudishie Passport yake

Usiku wa kuamkia leo Barnaba ameibiwa begi lake lililokuwa ndani ya gari lake likiwa na vitu vya thamani ambavyo ni pamoja na baadhi ya kazi zake ambazo hazijatoka zilizokuwa kwenye hard disc, kamera na laptop mbili.
Barnaba amepost ujumbe Instagram kuwaomba wasamaria wema kumrudishia na kutoa maelezo jinsi ya kuwasiliana naye na kati ya vitu vilivyopotea ipo pia hati yake kusafiria(passport).
Ameandika:

“Za asubui Ndugu Zangu wapendwa Usiku wa kuamkia Leo Nimeibiwa Begi langu Dogo Tu si Kubwa Sana ambalo lilikuwa ndani ya Gari langu | lakini ndani Yake Kulikua Na Laptop ๐Ÿ’ป za mac mbili moja Pro x moja Letina ya ukubwa Kidogo Theni Kuna external mbili moja Rangi Ya orange ๐ŸŠ moja Ya kijani Na Kuna File Zangu zilikua Na Mikataba Mbali Mbali lakini Kikubwa zaidi Ndani Yake Kuna PASPORT Yangu ambayo Ukifungua ndani Inasoma Jina La ELIASI BARNABASI INYASI and Kuna Vitu Vingi Sana Vidogo vidogo Vyenye Thamani Kubwa Kama Camera ๐ŸŽฅNa vingine Lakini Naomba sana Sana Waungwana Kama Kuna mtu Yotote atabaini au kujua Vilipo au hata kupelekewa Basi Naomba wasamalia Wema mnirudishie Au kuniletea Na Napatikana kwa No 0743505010 Mungu Awabariki Na naamini Aliyenavyo ajaiba Bali amepitiwa katika njia ya kutafuta Ridhiki Nami kwa jina la mungu nitamsamehe Na nimesamehe ila Kama Ana Rohoo nzuri Na ameguswa Basi Naomba waungwana mnipigie hata Kama Umeokota ๐Ÿ˜ฐ๐Ÿ˜ญ” Alipost Barnaba

TAZAMA HARMORAPA ALIVYO TIMUA MBIO BAADA YA KUIONA BASTOLA

from Blogger http://ift.tt/2nnBr1e
via IFTTT


Maswali yaanza kuibuka kuhusu ajali iliyohusisha gari la Jaguar

Inaonekana kuna ishu kibao kuhusiana na ajali iliyosababishwa na gari la msanii Jaguar.
Jumanne ya tarehe 21 gari aina ya Range Rover Sport lenye nambari ya usajili KCB 808J ilisababisha ajali liyopoteza maisha ya vijana wawili wa bodaboda. Ajali hii ilitokea katika katika barabara la Makutano kuelekea Sagana mida ya saa tisa za jioni siku hiyo.
Taarifa za awali kutoka kwa mashuhuda zilisema kwamba aliyekuwa kwenye usukani wakati wa ajali alikuwa ni mwanadada fulani anayesemekana kuwa rafiki wa karibu wa msanii huyo wala sio Jaguar aliyekuwa akiendesha gari hilo.
Hata hivyo, cha kushangaza ni kwamba Jaguar aliandikisha taarifa tofauti kabisa katika kituo cha polisi cha Sagana. Kulingana na yeye, aliyekuwa akiendesha wakati ajali hiyo ilipotokea alikuwa ni yeye.
Maneno ambayo yamerudiwa na mkuu wa polisi wa eneo hilo kulingana na ‘statement’ aliyoitoa Jaguar. Hilo linadhihirisha kwamba kuna gemu ya karata inayoendelea kuchezwa. Je, msanii Jaguar anajaribu kufanya ‘cover-up’? Na kama ni kweli, wengi tutajiuliza ni kwanini.
Hii ni ajali ambayo ilipoteza maisha ya vijana ambao familia zao zilikuwa zikiwategemea sana. Hili ni suala lenye uzito sana na halifai kuchukuliwa kuwa nyepesi Kama ni kweli Jaguar anahusika katika kinachoendelea basi atakuwa amefeli kama kiongozi mtarajiwa.
Siku zote sheria lazima ifuatwe na haki itendeke. Kama ilikuwa ni ajali ya kawaida ni kwanini ajaribu kudanganya kuhusu kilichotokea? Naamini vyombo husika vitafuatilia suala hili kiundani zaidi.
TAZAMA JAMAA HUYU ALIVYOKOSWA KOSWA NA KIFO KWA AJARI MTONI

from Blogger http://ift.tt/2n1Lp7B
via IFTTT


Kategori

Kategori