Showing posts with label 2017 at 04:14PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 04:14PM. Show all posts
KIJUE KISIWA KITAKATIFU AMBACHO NI WANAUME PEKEE WANAORUHUSIWA KWENDA

KIJUE KISIWA KITAKATIFU AMBACHO NI WANAUME PEKEE WANAORUHUSIWA KWENDA

Kisiwa cha Okinoshima nchini Japan, ambapo wanawake hawaruhusiwi kufika, kimetambuliwa kama Turathi ya Ulimwengu na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa, Unesco.
Kisiwa hicho cha Okinoshima huchukuliwa kuwa kitakatifu kiasi kwamba ni wanaume pekee wanaoruhusiwa kuzuru, gazeti la Asahi Shimbun linasema.
Na hata wanapofika huko, hawaruhusiwi kuondoka na chochote, hata kipande cha nyasi.
Watu wakiwa wanavuka eneo la bahari kuelekea kisiwani hapo
Jopo maalum liliwasilisha pendekezo kwa Unesco watambue rasmi kisiwa hicho kama turathi ya ulimwengu mwezi Mei.
Katika kisiwa hicho, kuna madhabahu ya Munakata Taisha Okitsumiya, ambayo ni ya kumtukuza miungu wa baharini.
Madhabahu hayo yalijengwa karne ya 17.
Katika kisiwa cha Okinoshima, kuliandaliwa matambiko kwa ajili ya usalama wa meli na pia wakazi wa Japan walitumia kisiwa hicho kuwasiliana na wakazi wa rasi ya Korea na China kati ya karne ya nne na tisa, gazeti la Japan Times linasema.
Kisiwa cha Okinoshima kama kinavyoonekana kwenye picha toka angani
Bado kuna miiko kuhusu kisiwa hicho, mfano wanawake kupigwa marufuku.
Wageni wa kiume pia hutakiwa kwanza kuvua nguo zao zote na kufanya tambiko la kujitakasa.
Aidha, hawatakiwi kufichua chochote kuhusu waliyoshuhudiwa wakiwa kwenye kiswa hicho.
“Haya ni baadhi ya mambo ambayo itabidi yazingatiwe iwapo kitaorodheshwa kuwa turathi,” anasema Asahi Shimbun, na kueleza kuwa huenda kisiwa hicho kikawa maarufu sana kwa utalii.
Zamani, hata kabla ya madhabahu kujengwa, kisiwa cha Okinoshima kilikuwa kikitumika kwa matambiko na mabaharia na pia kilihusika katika mashauriano ya kibiashara kati ya watu wa Korea na watu wa China.
Maelfu ya vitu vya kale, vilivyowekwa katika kisiwa hicho kama zawadi kutoka maeneo ya mbali, vimepatikana katika kisiwa hicho ikiwa ni pamoja na pete za dhahabu kutoka rasmi ya Korea, gazeti la Japan Times linasema.
HT @ BBCSwahili
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2tJtkQ1
via IFTTT


Tanzania na Rwanda miongoni mwa nchi ambazo raia hawana furaha duniani

Tanzania na Rwanda miongoni mwa nchi ambazo raia hawana furaha duniani

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionNorway ndiyo imechukua nafasi ya kwanza kama nchi yenye watu walio na furaha zaidi duniani
Tanzania Rwanda na Burundi zimeorodheshwa kuwa kati ya nchi zenye watu wasio na furaha duniani.
Rwanda iko nafasi ya 151 , Tanzania nafasi ya 153 huku Burundi ikiwa nafasi ya 154 kati ya nchi 155.
Norway ndiyo imechukua nafasi ya kwanza kama nchi yenye watu walio na furaha zaidi duniani, kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa na kumshinda jirani wake Denmark, ambayo ichukua nafasi ya kwanza mwaka uliopita.
Ripoti hiyo inaangazia furaha watu waliyo nayona ni kwa nini.
Denmark, Iceland, Uswisi na Finland zinachukua nafasi tatu za kwanza huku nchi ya Jamhuri ya Afrika ya katika ikichukua nafasi ya mwisho kati nchi zenye watu wasio na faraha duniani.Haki miliki ya pichaAFP
Mataifa ya magharibi mwa Ulaya na Marekani pia nayo yako na watu wenye furaha duniani wakati Marekani ikichukua nafasi ya 14 na Uingereza nafasi ya 19.
Nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara na zile zinazokumbwa na mizozo, zina alama za chini. Syria ilichukua nafasi ya 152 kati ya nchi 155 huku Yemen na Sudan Kusini, nchi zinazokumbwa na njaa zikichukua nafasi za 146 na 147 mtawalia
Nchi zenye watu walio na furaha na wasio na furaha Duniani
Nchi zenye watu walio na furaha DunianiNchi zenye watu wasio na furaha Duniani
1. Norway 146. Yemen
2. Denmark 147. Sudan Kusini
3. Iceland 148. Liberia
4. Uswizi 149. Guinea
5. Finland 150. Togo
6. Uholanzi 151. Rwanda
7. Canada 152. Syria
8. New Zealand 153. Tanzania
9. Australia 154. Burundi
10. Sweden 155. Jamhuri ya Afrika ya Kati
Mada zinazohusiana

from Blogger http://ift.tt/2nVPEl3
via IFTTT


Kategori

Kategori