KIJUE KISIWA KITAKATIFU AMBACHO NI WANAUME PEKEE WANAORUHUSIWA KWENDA

Kisiwa cha Okinoshima nchini Japan, ambapo wanawake hawaruhusiwi kufika, kimetambuliwa kama Turathi ya Ulimwengu na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa, Unesco.
Kisiwa hicho cha Okinoshima huchukuliwa kuwa kitakatifu kiasi kwamba ni wanaume pekee wanaoruhusiwa kuzuru, gazeti la Asahi Shimbun linasema.
Na hata wanapofika huko, hawaruhusiwi kuondoka na chochote, hata kipande cha nyasi.
Watu wakiwa wanavuka eneo la bahari kuelekea kisiwani hapo
Jopo maalum liliwasilisha pendekezo kwa Unesco watambue rasmi kisiwa hicho kama turathi ya ulimwengu mwezi Mei.
Katika kisiwa hicho, kuna madhabahu ya Munakata Taisha Okitsumiya, ambayo ni ya kumtukuza miungu wa baharini.
Madhabahu hayo yalijengwa karne ya 17.
Katika kisiwa cha Okinoshima, kuliandaliwa matambiko kwa ajili ya usalama wa meli na pia wakazi wa Japan walitumia kisiwa hicho kuwasiliana na wakazi wa rasi ya Korea na China kati ya karne ya nne na tisa, gazeti la Japan Times linasema.
Kisiwa cha Okinoshima kama kinavyoonekana kwenye picha toka angani
Bado kuna miiko kuhusu kisiwa hicho, mfano wanawake kupigwa marufuku.
Wageni wa kiume pia hutakiwa kwanza kuvua nguo zao zote na kufanya tambiko la kujitakasa.
Aidha, hawatakiwi kufichua chochote kuhusu waliyoshuhudiwa wakiwa kwenye kiswa hicho.
“Haya ni baadhi ya mambo ambayo itabidi yazingatiwe iwapo kitaorodheshwa kuwa turathi,” anasema Asahi Shimbun, na kueleza kuwa huenda kisiwa hicho kikawa maarufu sana kwa utalii.
Zamani, hata kabla ya madhabahu kujengwa, kisiwa cha Okinoshima kilikuwa kikitumika kwa matambiko na mabaharia na pia kilihusika katika mashauriano ya kibiashara kati ya watu wa Korea na watu wa China.
Maelfu ya vitu vya kale, vilivyowekwa katika kisiwa hicho kama zawadi kutoka maeneo ya mbali, vimepatikana katika kisiwa hicho ikiwa ni pamoja na pete za dhahabu kutoka rasmi ya Korea, gazeti la Japan Times linasema.
HT @ BBCSwahili
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2tJtkQ1
via IFTTT