Showing posts with label Airtel. Show all posts
Showing posts with label Airtel. Show all posts

MAWAKALA ZAIDI YA 300 MWANZA WAWEZESHWA KUPATA MIKOPO




 Afisa Masoko wa Airtel kanda ya ziwa akiongea na mawakali mara baada ya kuendesha seminar inayowapatia fulsa Mawakala wa Airtel Money nchini nzima kupata mikopo kupitia simu zao za mkononi




Wakala wa Airtel Money katika maeneo ya Metro Mwanza, Bwn John Hainga akichangia mada wakati wa semina ya mawakala inayowapatia  fulsa ya kupata mikopo isiyo na dhamana ijulikanayo kama Timiza Mikopo kwa Mawakala



 KAMPUNI ya simu za mkononi nchini Tanzania Airtel imeendelea kuboresha huduma zake  kwa wateja hususani wajasiliamali wanaojihusisha na shughuli mbalimbali za kibiashara, ikiwa ni pamoja na utoaji wa huduma za Airtel Money , kwa kuwawawezesha mawakala kupata mikopo inayoitwa " Timiza mikopo kwa Mawakal " Kupitia simu zao za mikononi.


Airtel imewakutanisha  mawakala wa Airtel Money kutoka sehemu mbalimbali za jiji la Mwanza ili kuwapatia mafunzo ya uboreshaji na ukuzaji vipato katika biashara zao.




"Ukosefu wa  elimu ya uendeshaji biashara kwa wajasiliamali walio wengi hapa nchini umeendelea kuwa ni tatizo linaloshusha kiwango cha mapato kwa wajasiliamali kupitia shughuli zao hivyo kuzorotesha uchumi wa taifa .

 Kwa kutambua tatizo hili Airtel imeona ipo haja kuwapatia mafunzo ya uendeshaji biashara yatakayomwezesha mjasiliamali kutambua njia bora ya uendeshaji biashara, Ikiwa ni pamoja na utoaji mikopo isiyo na dhamana  kwa zaidi ya mawakala 20,000  kote nchini Ili kusaidia kukuza biashara za mawakala , kuongeza faida zaidi katika shughuli zao na pia upatilkanaji wa huduma ya za fedha katika jami". alisema meneja kanda ya ziwa wa Airtel, Bwana Raphael Daudi.

Kwa upande wake mmoja ya wakala aliyehudhuria semina hiyo  bwana John Paschal alisema" tunayofuraha kuwezesha kupata mikopo kupitia huduma hii ya Timiza mikopo kwa mawakala. Na hii itaturahisishia kuboresha biashara zetu kwani sasa tuna uhakika wa mitaji.  Lakini pia mafunzo haya yatatusaidia sana katika kutunza mahesabu na kuendesha biashara zetu kwa ufanisi zaidi."




Airtel katika kukabiliana na changamoto za kijamii na kiuchumi kwa wateja wake imefanikiwa kuzindua huduma hii ya timiza mikopo kwa mawakala, huduma itakayowawezesha mawakala  wa airtel money kote nchini kupata mikopo isiyo na dhamana ya kuanzia sh. 50,000/- hadi 500,000/-





By MichuziBlog

Wafanyakazi wa Airteli washiriki kupaka rangi chechea

 Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso akishiriki kupaka rangi katika darasa la Chekechea linalokarabatiwa kwa hisani ya Wafanyakazi wa Airtel kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika Shule ya Msingi Kumbu Kumbu iliyopo Block 41, jijini Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia ni Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule hiyo, Joyce Mtanga (wa pili kulia) na Mwalimu, Flossy Mbwilo.
 


Wafanyakazi wa Airtel Tanzania, Kitengo cha Mawasiliano na Raslimali Watu wakishiriki kupaka rangi katika darasa la Chekechea linalokarabatiwa kwa hisani ya Wafanyakazi wa Airtel kama sehemu ya  huduma kwa jamii, katika Shule ya Msingi Kumbu Kumbu iliyopo Block 41, jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso akiupamba ukuta kwa kiganja cha mkono kilichopakwa  rangi nyekundu wakati waliposhiriki kupaka rangi darasa la Chekechea linalokarabatiwa kwa hisani ya Wafanyakazi wa Airtel kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika Shule ya Msingi Kumbu Kumbu iliyopo Block 41, jijini Dar es Salaam jana. Wanashuhudia (kutoka kulia) ni Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule hiyo, Joyce Mtanga, Mwalimu, Flossy Mbwilo na Afisa Uhisiano na Matukio wa Airtel, Dangio 

Wafanyakazi wa Airtel kupitia Mradi wake wa Airtel “Tunakujali” waendelea kuchangia Maendeleo katika Jamii.  Kwa hakika, safari ya maili elfu huanza na hatua. Mradi ulioanza mwaka mmoja uliopita katika Shule ya Msingi ya Kumbukumbu sasa tunaona matunda yake kwa kuona maendeleo yaliyopo katika shule ya msingi Kumbukumbu iliyopo Kinondoni jijini Dar Es Salaam. Hii yote ni kwa hisani ya wafanyakazi wa kitengo cha Rasilimali watu na kitengo cha mawasaliano kwa kufanya matembezi ya Hisani mwaka jana kwa ajili ya kusaidia shule hiyo.

Wafanyakazi wa Airtel mwishoni mwa wiki iliyopita waliungana pamoja katika harakati za mwisho za kukarabati darasa la awali katika shule ya msingi ya Kumbukumbu. Shule hiyo ni miongoni mwa shule ambazo zipo katika mradi wa Airtel “Tunakujali”, ambapo Airtel wamekuwa wakizisaidia shule mbali mbali hapa nchini. Mwaka jana wafanyakazi wa Airtel walikabidhi kisima cha maji safi na salama katika shule hiyo.

Awali shule hiyo haikuwa na maji, ambapo wanafunzi na walimu walipata tabu na kuwawia ugumu wa kupoteza muda wa masoma kwa kutafuta maji. Wakiwa katika makabidhiano ya kisima hicho  alishuhudia ubovu wa darasa la chekechea na watoto hao kukaa, hivyo walitoa ahadi ya kukarabati darasa hilo na kuwapatia madawa. Unapotoa ahadi japo sio shurti ni wajibu kuitekeleza, na kutokana na umuhimu huo Wafanyakazi wa Kampuni ya simu ya Airtel waliamua kutimiza dhamira yao na kuanza mchakato wa kukarabati darasa hilo kupitia mradi wao wa Airtel “Tunakujali”. Airtel  "Tunakujali" ni miongoni mwa miradi ya kijamii inayoondeshwa na wafanyakazi wa Airtel ili kuweza kusaidia jamii inayowazunguka.
UZINDUZI WA REDIO JAMII UVINZA: MKUU WA MKOA AHIMIZA WELEDI, UADILIFU NA AMANI

UZINDUZI WA REDIO JAMII UVINZA: MKUU WA MKOA AHIMIZA WELEDI, UADILIFU NA AMANI

DSC_0177
Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mwalimu Hadijah Nyembo (kulia) akitoa nasaha zake kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya (wa pili kulia) kuzungumza na wakazi wa wilaya ya Uvinza kwenye sherehe za uzinduzi wa kituo cha redio jamii Uvinza FM mkoani Kigoma. Kutoka kushoto ni Meneja wa huduma za kijamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi, Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ambao ndio wadhamini wakuu wa redio Uvinza FM, Bi. Rose Haji Mwalimu na Mkurugenzi Mtendaji wa Uvinza FM Radio Bi. Nuru Kalufya.(Picha na Zainul Mzige wa MOblog).
Na Mwandishi wetu, Uvinza - Kigoma
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya amesisitiza uadilifu katika vyombo vya habari jamii kwa kutangaza habari zisizoumiza hisia kwa wananchi wengine na kuepuka migogoro.
Akizindua kituo cha redio jamii cha Uvinza FM, Luteni Kanali Mstaafu Machibya alisema kuwa vyombo vina wakati mgumu hasa katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2015.

“Changamoto hii inaweza kuepukika kwa kuhakikisha habari zinazotolewa zinalenga kuendeleza utamaduni wa amani, upendo, utulivu na uvumilivu na kuepuka viashiria vinavyoweza kusambaza chuki kwa lengo la kufanikisha chaguzi salama.

Mkuu wa Mkoa huyo amesisitiza umuhimu wa kuutumia uhuru wa kutoa na kupata habari vizuri kwa kusema kwamba uhuru huo usitumike kutoa habari zinazopendelea upande mmoja na kukandamiza mwingine kwa kuwa hali kama hiyo husababisha machafuko.

“Kwa mujibu wa Ibara ya 18 (b) ya Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, kila mtu anayo haki ya kutafuta, kupokea na kutoa habari bila ya kujali mipaka ya nchi, lakini haki hiyo iende sambamba kwa kuzingatia Sheria za nchi na kuhakikisha habari hizo haziumizi hisia za wananchi wengine,”
DSC_0206
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya akisoma risala wakati wa uzinduzi wa kituo cha redio jamii Uvinza FM ambapo alilipongeza shirika la UNESCO kwa juhudi kuwaweka karibu wananchi na serikali kupitia mawasiliano ya redio.

Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya ameitaka redio jamii Uvinza kuonyesha uwezo wao ili waweze kujitangaza na kujijengea imani kwa wanajamii wao kuwa wanaweza. “Ni kwa hali hiyo tu mtaweza kujulikana, kutambulika na kupata udhamini na matangazo ya kutosha.”
Amewataka wanajamii kukitumia vyema kituo chao cha redio ili kiwe chachu ya kuleta na kukuza maendeleo katika vijiji, wilaya, mkoa na taifa kwa ujumla.

Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa ameitaka redio jamii ya Uvinza kutangaza habari zenye kuonyesha madhara ya mila potofu na kujenga uelewa wa jamii kuhusu mila hizo hususan mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), kufichua wagonjwa wanaohofia kuwa na dalili za ugonjwa wa ebola na uharibifu wa mazingira.

Amelipongeza shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kutoa msaada wa vifaa vya kituo hicho na kuendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo wanahabari jamii, Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kuruhusu matangazo ya Uvinza FM Redio yarushwe kupitia mnara wake na waanzilishi wa kituo hicho.
DSC_0120
Mwalikishi wa Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ambaye pia ni mshauri na mkufunzi wa redio jamii, Bi. Rose Haji Mwalimu akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues kwenye sherehe za uzinduzi wa kituo hicho cha redio jamii Uvinza FM uliofanyika wilayani Uvinza mkoani Kigoma.
“Ninayapongeza mashirika hayo ya Umoja wa Mataifa na Airtel kwa ufadhili wao, Ruchugi Salt Works na Asasi za kiraia (EHENA) kwa ushirikiano wao kwa jambo hili”.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mwalimu Hadijah Nyembo amewakumbusha waandishi wa habari kuepuka kutangaza habari zinazoleta hofu katika jamii kwa kutangaza habari zinazotoa maelezo ya ufafanuzi kutoka chombo husika.

Amekemea matumizi ya lugha isiyo sahihi na kutoeleweka kwa wasikilizaji kwa kusema kwamba redio inalenga makundi yote ya umri kwa hiyo Matangazo yalenge wananchi wote.

“Redio Uvinza isiwe chombo cha propaganda, zingatieni mojawapo ya madhumuni ya kuanzishwa kwa redio zenu ambayo yanalenga kuhamasisha mshikamano, Amani, upendo, utulivu, umoja na utaifa, alisema Mwalimu Nyembo.”

Chombo cha habari jamii Uvinza FM Redio ni cha kwanza kuanzishwa mkoani Kigoma katika halmashauri mpya ya Uvinza.
DSC_0153
"Hongereni sana UNESCO serikali inatambua mchango wenu",...... Ni maneno ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya akimpongeza Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ambao ndio wadhamini wakuu wa redio jamii Uvinza FM, Bi. Rose Haji Mwalimu kwa niaba ya UNESCO. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Uvinza FM Radio Bi. Nuru Kalufya.
Chombo hicho kimetakiwa kutumika kuwaunganisha wanajamii, kuepuka kutangaza hisia au uvumi kwa kueleza ukweli na kuwatunzia heshima wasikilizaji wao kwa kuwa wana haki ya kuheshimiwa na kutoumbuliwa masuala yao binafsi.
Uzinduzi huo umeshuhudiwa pia na Mkuu wa wilaya ya Uvinza Mheshimiwa Mwalimu Hadijah Nyembo, viongozi wa chama na serikali, viongozi wa dini, Shirika la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Kampuni ya simu za mkononi AIRTEL, wanakijiji na wananchi wa halmashauri ya Uvinza.
Wengine ni wanahabari 30 wanaohudhuria mafunzo ya maadili, jinsia na habari za migogoro kijijini Uvinza, kutoka redio jamii za wilaya 8 ambazo ni Karagwe, Bunda, Mwanza, Kahama, Sengerema, Maswa, Simanjiro, Loliondo, Mpanda, Ngara. Kutoka Zanzibar ni Unguja North, na Southern Pemba (Pemba).
DSC_0082
Meneja wa huduma za kijamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi, akitoa salamu kwa wakazi wa wilaya ya Uvinza kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Airtel ambao wametoa udhamini wa mnara wao kurusha matangazo ya kituo cha redio jamii Uvinza FM ili kupanua wigo wa usikivu kwa redio hiyo.
DSC_0257
Mkurugenzi Mtendaji wa Uvinza FM Radio Bi. Nuru Kalufya akitoa neno la shukrani kwa mkuu wa mkoa na wadhamini wa kituo hicho cha redio jamii Uvinza FM.
DSC_0054
Meneja wa huduma za kijamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi akishiriki kutoa burudani na kikundi cha wakinamama wachimba chumvi Uvinza.
DSC_0164
Baadhi ya viongozi wa dini na jeshi la polisi waliohudhiria uzinduzi huo...Kutoka kulia ni Sheikh Mkuu wa wilaya ya Uvinza Hassan Hamisi, OCD wa Wilaya ya Uvinza S.P Nobert Mahala, Mchungaji wa SDA, Pius Mutani, Mchungaji wa EAG Uvinza, Daniel Magunge na Diwani wa kata ya Ngumka, Abdallah Masanga.
DSC_0333
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali za jamii waliokuwa wakihudhuria warsha ya siku nane iliyokuwa ikiendelea kwenye kituo cha redio jamii Uvinza FM na wakazi wa wilaya hiyo waliohdhuria sherehe za uzinduzi wa kituo hicho.
DSC_0231
DSC_0226
DSC_0264
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kituo cha redio jamii Uvinza FM chini ya ufadhili wa Shirika la UNESCO na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania. Wanaoshuhudia tukio hilo kutoka kulia ni Meneja wa huduma za kijamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi, Mwalikishi wa Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ambaye pia ni mshauri na mkufunzi wa redio jamii Bi Rose Haji Mwalimu pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Uvinza FM Radio Bi. Nuru Kalufya.
DSC_0267
Sasa kimezinduliwa rasmi.
DSC_0285
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya akifanyiwa mahojiano mafupi ndani ya studio za redio jamii Uvinza FM na Mtangazaji wa kituo hicho, Kadisilaus Simon mara baada ya kuzindua rasmi redio hiyo.
DSC_0304
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya akisaini kitabi cha wageni ndani ya studio za redio jamii Uvinza FM.
DSC_0308
Mtangazaji wa kituo cha redio jamii Uvinza FM, Kadisilaus Simon akitekeleza majukumu yake kwa furaha kabisa mara baada ya kupewa baraka na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya.

Kategori

Kategori