Showing posts with label 2017 at 01:19PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 01:19PM. Show all posts
Picha 20: Kutoka uwanja wa Kinesi Dar uzinduzi wa Ndondo Cup 2017

Picha 20: Kutoka uwanja wa Kinesi Dar uzinduzi wa Ndondo Cup 2017

Msimu wa nne wa mashindano ya Ndondo Cup umezinduliwa rasmi Jumamosi Juni 17, 2017 kwenye uwanja wa Kinesi jijini Dar es Salaam huku mchezo wa ufunguzi ukizikutanisha Stim Tosha dhidi ya Makuburi na dakika 90 zikamalizika bila timu hizo kufungana.
Mgeni rasmi aliyezindua mashindano hayo alikuwa ni DAS wa Wilaya ya Ubungo James Mkumbo ambae alimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Ubungo.
Msimu mpya wa Ndondo Cup 2017 ndio umeanza, endelea kufuatilia mashindano haya kwa kuhudhuria viwanjani kushuhudia games mbalimbali, unaweza pia kuangalia live kupitia Azam TV na Clouds TV lakini pia kupitia mitandao kama http://ift.tt/1vJep6E, Dauda TV, http://ift.tt/2so7qRx, pia unaweza kupata habari kupitia mitandao ya kijamii facebook (NdondoCup), Twitter (@NdondoCup) na Instagram (ndondo_cup).
Hapa unaweza kuangalia picha za matukio mbalimbali ya uzinduzi wa Nodndo
 ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2sof5iy
via IFTTT


EWURA Wasitisha Mchakato wa Kuiongezea Leseni Kampuni ya IPTLโ€ฆ.Ni Baada ya Waziri Mkuu kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu

EWURA Wasitisha Mchakato wa Kuiongezea Leseni Kampuni ya IPTL….Ni Baada ya Waziri Mkuu kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesitisha mchakato wa kushughulikia maombi ya IPTL ya kuongezewa muda wa leseni yake ya biashara kwa miezi 55 ili iendelee kuzalisha umeme na kuiuzia TANESCO.
Mbali na kusitisha mchakato huo, EWURA imesitisha pia upokeaji wa maoni kutoka kwa umma na wadau mbalimbali kuhusu kusudio lake la kuiongezea muda wa kufanyakazi nchini Kampuni ya IPT
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2sjDJUk
via IFTTT


Wabunge โ€˜Wasasambuanaโ€™ Bungeni..Ni Kuhusu Ripoti Hii ya Twaweza..!!!

Wabunge ‘Wasasambuana’ Bungeni..Ni Kuhusu Ripoti Hii ya Twaweza..!!!

Hatimaye mvutano wa wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chadema umehamia katika ripoti ya utafiti kuhusu masuala ya kielimu uliokuwa ukitolewa na shirika lisilo la kiserikali la Twaweza.
Wabunge wa Chadema walichangia kwa kueleza namna Serikali ilivyoshindwa kutambua mchango mkubwa unaotolewa na walimu hasa wa sayansi.
Mbunge wa Serengeti (Chadema), Marwa Chacha amesema Serikali imeitelekeza elimu na kuwafanya vijana wa Kitanzania waishi kwa kupata elimu ya kubahatisha.
Hata hivyo, wabunge wa CCM, Hawa Ghasia na Fatuma Tawfiq ambao walijibu kuwa kauli za wabunge wa Chadema ni za uchochezi kwa kuwa Serikali imekuwa ikifanya mambo yake kwa utaratibu na ubora wa hali ya juu.
Awali, Mkurugenzi wa Twaweza, Aidan Eyakuze aliwaambia wabunge kuwa hali bado ni mbaya kwa wanafunzi wa Kitanzania hasa shule za msingi.

from Blogger http://ift.tt/2nYEhZs
via IFTTT


Mwanamume aiambia mahakama kwamba hawezi kuacha kuvuta bangi

MWANAMUME aliyeambia mahakama kwamba hawezi kuacha kuvuta bangi kwa sababu ya kazi anayofanya, Jumatano alifungwa jela miaka mitatu kwa kupatikana na kisu akiwa na nia ya kutenda uhalifu.
Alfred Geventi Timona alikiri kwamba alipatikana na kisu na misokoto 12 ya bangi alipokamatwa na maafisa wa usalama katika barabara ya Mbagathi mnamo Novemba 21, 2016.
Mahakama ilisema mshtakiwa hakuweza kueleza alinuia kufanya nini na kisu alichopatikana nacho siku hiyo.
“Mshtakiwa hakueleza kwa nini alikuwa na kisu usiku. Kwa sababu hii mahakama imeridhika kwamba alinuia kutenda uhalifu alivyoshtakiwa,” alisema Hakimu Mkuu Mwandamizi wa Kibera Elizabeth Juma.
Maafisa wa urekebishaji wa tabia walisema kwenye ripoti kwamba mshtakiwa hakufaa kupewa kifungo cha nje kwa sababu alikataa kufichua habari muhimu kuhusu familia na maisha yake.
Kuzoa takataka
Ripoti ilisema kwamba Geventi alikiri kwamba alikuwa mraibu wa bangi kwa sababu anafanya kazi ya kuzoa taka mtaani Kibera.
“Ninapendekeza kwamba mshtakiwa hafai kifungo cha nje kwa sababu hakueleza anakoishi na hakufichua waliko jamaa zake,” ilisema ripoti iliyoandikwa na afisa wa urekebishaji wa tabia wilaya ya Kibra, Ann Mungai.
Bi Juma alimtoza faini ya Sh20,000 kwa shtaka hilo na akamfunga jela miaka mitatu kwa kupatikana na kisu akijiandaa kutenda uhalifu.
TAZAMA JAMAA HUYU ALIVYOKOSWA KOSWA NA KIFO KWA AJARI MTONI

from Blogger http://ift.tt/2mTJcdo
via IFTTT


Kategori

Kategori