Showing posts with label 2017 at 11:34AM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 11:34AM. Show all posts
TAARIFA MUHIMU KWA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI ZOTE NCHINI

TAARIFA MUHIMU KWA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI ZOTE NCHINI

Tarehe 22 June 2017, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alilipia VIUADUDU vya kutokomeza Mbu wa Malaria lita 100,000 na kuagiza vigawanywe kwenye Halmashauri zote nchini.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu anapenda kuwatanganzia Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuwa VIUADUDU hivi vitaanza kugawiwa leo (jana) kwa Halmashauri za Mikoa 14 yenye kiwango kikubwa cha Maambukizi ya Ugonjwa wa Malaria. Mikoa hii (na kiwango cha maambukizi ya malaria kimeonyeshwa kwenye mabano) ni;- Kagera (41%), Geita (38%), Kigoma (38%), Ruvuma (23%), Tabora (20%), Mtwara (20%), Mara (19%), Morogoro (14%), Shinyanga (17%), Lindi (17%), Pwani (15%), Mwanza (15%), Katavi (14%) na Simiyu (13%),
Mikoa mingine ambayo haijatajwa itagawia Viuadudu katika Awamu ijayo.
Idadi ya Lita zitakazogawanywa kwa kila Halmashauri zilizo katika Mikoa hii tayari imeshaainishwa.
Wizara inawakumbusha Waganga Wakuu wa Mikoa/Wilaya kufanya Upuliziaji wa Viuadudu kwa kuzingatia Miongozo ya Wizara ya Afya. Hii itawezesha kupata matokeo tarajiwa ya kutokomeza mbu ili kudhibiti ugonjwa wa Malaria nchini.
Aidha, Wizara ya Afya inapenda kumshukuru kwa dhati na kumpongeza Mhe.Rais Dkt. Magufuli kwa kuongeza chachu katika Mapambano dhidi ya Malaria Nchini.
Imetolewa na;
Catherine Sungura
Kaimu Msemaji- Idara Kuu Afya
26 June 2017
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2sMbHji
via IFTTT


Rais Mugabe Katika Muonekano Mpya…!!!

Rais Mugabe Katika Muonekano Mpya…!!!

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe kwa mara ya kwanza amepigwa picha akiwa amenyoa nywele zake wakati alipohudhuria mazishi ya mwanajeshi wa zamani.
Wengi wanaamini ni mara ya kwanza Mugabe kunyoa nywele zake na hata ndevu.
Picha hizo zimeonekana baada ya kuchapishwa katika mitandao ya kijamii na kuvutia watu wengi hasa raia wa Zimbabwe waliotoa maoni yao.
Baadhi wamesema kuwa mtindo alionyoa umechangia aonekane kijana huku wengine wakisema kuwa wameshangaa kitendo hicho na kujiuliza lengo lake ni lipi.

from Blogger http://ift.tt/2pdLhGh
via IFTTT


Kweli Wapo Wabunge Waliommiss Jakaya Kikwete…Leo Kaibuka Bungeni na Kushangiliwa Dakika Kumi

Kweli Wapo Wabunge Waliommiss Jakaya Kikwete…Leo Kaibuka Bungeni na Kushangiliwa Dakika Kumi


Dodoma. Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete ameshangiliwa kwa muda wa zaidi ya dakika 10 mara baada ya kuingia bungeni leo asubuhi.
Spika wa Bunge Job Ndugai amesema haijawai kutokea mgeni kushangiliwa katika kipindi chake chote alichokuwepo bungeni.
Bunge limeanza leo mjini Dodoma.

from Blogger http://ift.tt/2oUb6r0
via IFTTT


Kategori

Kategori