Showing posts with label 2017 at 02:18PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 02:18PM. Show all posts
JAJI ALIYEMUOMBA RAIS MAGUFULI KUJIUZULU AIAGA DUNIA

JAJI ALIYEMUOMBA RAIS MAGUFULI KUJIUZULU AIAGA DUNIA

Aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Upendo Msuya amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Kairuki jijini Dar es Salaam alipokuwa anapatiwa matibabu.
Jaji Msuya amefariki dunia ikiwa ni miezi miwili tu tangu alipojiuzulu wadhifa huo ambapo kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa tarehe 16 Mei, 2017 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi inaeleza kuwa Mhe. Rais Magufuli ameridhia maombi ya kuacha kazi kwa kiongozi huyo kuanzia tarehe 15 Mei, 2017.
Taarifa iliyothibitishwa na mtoto wa marehemu, Kelvin Msuya imeeleza kuwa msiba wa mama yake utakuwa Tegeta, jijini Dar es Salaam.

from Blogger http://ift.tt/2tFJNTn
via IFTTT


MAMA AUAWA AKIWA KIWA ANAIBA MAHINDI SUMBAWANGA

MAMA AUAWA AKIWA KIWA ANAIBA MAHINDI SUMBAWANGA

Mkazi wa Kijiji cha Lyapona, Kata ya Kaengesa, Sumbawanga mkoani Rukwa, Victoria Kalungwizi (67), ameuawa kwa marungu kwa tuhuma za kuiba mahindi shambani.
Tukio hilo lilitokea juzi katika kijiji hicho saa 11 jioni kwa Kalungwizi kupigwa na watu katika sehemu mbalimbali za mwili kwa fimbo na rungu hadi kufariki dunia. Kutokana na tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando, alisema Jeshi la Polisi mkoani hapa linawasaka watu watatu wanaodaiwa kumuua mtu huyo.
Alisema chanzo cha mauaji hayo ni tuhuma dhidi ya Kalungwizi kuwa mwizi wa mahindi. Alisema alishukiwa kuwa ameiba mahindi katika shamba la Michael Mkombozi. Kamanda Kyando alisema mbinu waliyotumia watu hao ni kumvizia akiwa anavuna mahindi katika shamba ambalo si lake.
Alisema baada ya kumkuta walianza kumshambulia kwa kumpiga sehemu mbalimbali za mwili kwa fimbo na marungu hadi kumsababishia kifo papo hapo. Kamanda Kyando alisema baada ya watuhumiwa kutekeleza mauaji hayo, walitoroka na kukimbilia kusikojulikana na kwamba juhudi za polisi kuwatafuta zinaendelea.
Kyando aliwataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mikononi kwa kuwaua watuhumiwa bali wawe wanawafikisha kwenye vyombo vya sheria ili sheria ichukue mkondo wake.
HT @ Nipashe
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2t3dd2z
via IFTTT


FAHAMU TARATIBU ZINAZOTUMIWA NA WATUMISHI WA UMMA KUPATA UHAMISHO

FAHAMU TARATIBU ZINAZOTUMIWA NA WATUMISHI WA UMMA KUPATA UHAMISHO

1. Mamlaka za Uhamisho
Kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na 8. ya mwaka 2002 ikisomwa na Kanuni zake pamoja na Taratibu za Uendeshaji za mwaka 2003 Mamlaka ya Uhamisho kwa watumishi wote wa Umma ni Katibu Mkuu Ofisi Ya Rais-Menejimenti ya Utumishi Wa Umma na;
Kwa maelekezo ya Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi Wa Umma kwa barua Kumb Na. C/CB.271/431/01/62 ya tarehe 8/06/2006 na Kumb Na. C/CB.271/431/01/J/144 ya tarehe 27/08/2007 Mamlaka ya Uhamisho katika Uhamisho wa watumishi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa yamekasimiwa kwa;
Katibu Mkuu Ofisi Ya Waziri Mkuu TAMISEMI kwa watumishi wanaohama kutoka Halmashauri moja kwenda nyingine nje ya Mkoa;
Katibu Tawala Mkoa kwa uhamisho wa watumshi wanaotoka Halmashauri moja kwenda nyingine ndani ya Mkoa na;
Mkurugenzi wa Halmashauri kwa watumishi wanatoka kituo kimoja kwenda kingine ndani ya Halmashauri.
2. Aina za Uhamisho
Kuna aina mbili za Uhamisho, nazo ni;
Uhamisho wa Kuomba
Taratibu za Kuomba Nafasi:-
Mtumishi atapaswa kuomba nafasi ya uhamisho kwa kuwasilisha maombi yake ya uhamisho kwa Mkurugenzi wa Halmashauri au Mamlaka anayotaka kuhamia kupitia kwa Wasimamizi wake wa kazi katika kituo chake cha kazi alichopo na Mkurugenzi wake.
Wasimamizi wa mtumishi anayeomba uhamisho watapaswa kuhakikisha maombi ya mtumishi yanafika katika mamlaka husika yakiwa na maoni yao kuhusu maombi hayo na sio kuzuia maombi. Iwapo kutakuwa na sababu ya msingi ya kuzuia maombi mwajiri amjulishe mtumishi kwa kumrejesha katika miongozo iliyopo
Iwapo Mwombaji hataridhika na maoni /sababu za mwajiri /Msimamizi wa kazi kukataa maombi yake mwombaji atawasilisha maombi yake kwa Katibu Tawala wa Mkoa kwa ushauri na kama hataridhia maombi yatawasilishwa kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI yakiwa na vielelezo muhimu kuthibitisha maombi hayo kukataliwa na Mkurugenzi na kueleza sababu za yeye kuomba uhamisho huo.
Mkurugenzi/Msimamizi wa kazi atayeombwa nafasi ya kuhamia atapaswa kumjibu mtumishi kupitia kwa Mkurugenzi wake kwa barua akimweleza kupatikana kwa nafasi hiyo kumetokana na nini ikiwa ni pamoja na kutaja Check Namba za watumshi waliofariki au kuacha kazi.
Iwapo mtumishi wa umma ataomba uhamisho kwa sababu za kumfuata mume au mke, kujiandaa kustaafu baada ya kukaa miaka kumi nje ya mkoa anaotarajia kustaafia na kukaa katika kituo kimoja kwa zaidi ya miaka mitano anaweza kufikiriwa kugharamiwa gharama za uhamisho hata kama ataomba uhamisho mwenyewe.
Mtumishi anayeomba uhamisho atapaswa kuwasilisha maombi yake kwa Katibu Mkuu au Katibu Tawala Mkoa au Mkurugenzi akiambatanisha barua iliyomkubalia kuhamia katika kituo anachotaka kuhamia. Aidha ni muhimu amjulishe mwombaji iwapo atagharimiwa uhamisho au la kufuatia kupata nafasi hiyo
Angalizo:
Hairuhusiwi Mtumishi yeyote kutumia mtu mwingine isipokuwa yeye mwenyewe au Mwajiri wake kwa njia ya posta au Mkono kuwasilisha maombi yake ya uhamisho. Inashauriwa kutumia njia ya EMS au regista kwa urahisi wa ufuatiliaji.
Upatikanaji wa Majibu:-
Watumshi wote walioomba uhamisho watapata majibu yao kwa barua kupitia kwa waajiri wao na sio vinginevyo.
Aidha kwakuwa uhamisho huu ni wa wazi watumishi waliokubaliwa au kaukataliwa uhamisho watapata taarifa za awali kupitia Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI yaani http://www.pmoral.go.tz mapema mwezi Julai kwa maombi yatakayopokelewa kuanzia Januari hadi Juni na mapema mwezi Januari kwa maombi yatayopokelewa kuanzia mwezi Julai hadi Desemba kwa kuwa Ofisi yetu imejipanga kushughulikia masuala ya uhamisho mara mbili kwa mwaka ili kuepusha mwingiliano wa majukumu katika vituo vya kazi kwa mwaka.
Mtumishi atakayekuwa na malalamiko kuhusu maombi yake ya uhamisho anashauriwa kuelekeza maombi yake kwa Mamlaka iliyomwamisha kupitia kwa mwajiri wake na msimamizi wa kazi akiambatisha maombi yake ya awali na vilelezo vingine muhimu kama sababu za kuomba uhamisho na ushahidi wa kufikisha barua yake kwa Mamlaka ya uhamisho.
Malalamiko ya mtumishi aliyeomba uhamisho na hakupata majibu au hakuridhika na majibu aliyopatiwa malalamiko yake yatashughulikiwa ndani ya siku saba bila kujali muda wa uhamisho yaani June au Desemba.
Baada ya mtumshi kupata majibu /barua ya uhamisho atapaswa kuripoti ndani ya siku kumi na nne tangu amekabidhiwa barua yake ya uhamisho vinginevyo atachulikuliwa ni mtoro kazini.
b. Uhamisho wa Kawaida
Uhamisho huu ni wa kawaida ambapo Mwajiri au Msimaimizi wa kazi anafanya uhamisho kwa sababu za kuboresha utendaji.
Hata hivyo ili uhamisho huo ufanyike pia Mamlaka za uhamisho zinatakiwa kujiridhisha uwepo wa nafasi wazi katika Halmashauri anayohamishiwa mtumishi wa hakusababishi upungufu katika Sehemu mtumishi anakotoka au anakohamia.
Uhamisho huu kwa kawaida unagharamiwa na Halmashauri inayompokea mtumishi na ile inayomruhusu kwa kumlipa gharama za kufunga mizigo kama ilivyoelezwa kwenye Kanuni L (8 na 13) ya Utumishi wa Umma ya Kudumu toleo la 2009 na marekebisho yake ya mwaka 2010 kwa wakati. hivyo ni muhimu Mamlaka za Uhamisho kijiridhisha na uwezo wa Halmashauri kugharamia uhamisho huo ili kuepuka kuzalisha madeni kwa Serikali
Pamoja na utaratibu wa uhamisho kuwa ni uhamisho kufanyika mara mbili kwa mwaka, uhamisho huu wa kawaida unaweza kufanyika wakati wowote katika jitihada za kunusuru utendaji katika kituo alichopo mtumishi au anachohamishiwa mtumishi kwa manufaa ya umma.
Angalizo:
Mtumishi atakayebainika kughushi saini za viongozi, kuomba au kupokea rushwa katika ngazi yoyote atachukuliwa hatua kali za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kumfikishwa mbele ya vyombo vya dola kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria.
Ni muhimu kwa Waajiri kujiridhisha na majibu ya barua za uhamisho kutoka katika Mamlaka za uhamisho ili kuona kama maombi yake yalifuata taratibu sahihi na watumishi waliopata majibu wanatayarishiwa mapema data sheet na kumbukumbu za utumishi na mshahara ili kuepusha usumbufu kwa watumishi na waajiri wanaowapokea watumshi.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2t4IKw2
via IFTTT


Claudio Bravo aipeleka Chile fainali, Ureno chali

Claudio Bravo aipeleka Chile fainali, Ureno chali

Hakika ulikuwa mchezo mgumu sana kama ulivyotarajiwa kati ya mabingwa wa Ulaya timu ya taifa ya Ureno dhidi ya Chile ambao ni mabingwa wa America.
Mchezo huo wa nusu fainali ya confedaration cup ulimalizika dakika 90 kukiwa hakuna timu iliyopata bao na hata zilipoongezwa 30 ili kumalizia 120 milango bado ilikuwa ni migumu.
Baada ya hapo muamuzi aliamuru kupigwe mikwaju ya penati ambapo ndio Ureno waliondolewa baada ya Chile kufunga mikwaju yote mitatu ya mwanzo ya penati huku Wareno wakikosa.
Shukrani kwa mlinda lango wa Chile Claudio Bravo ambaye aliokoa penati tatu za Ricardo Quaresma, Moutinho na Nanj huku za Chile zikiwekwa kambani na Vidal,Sanchez na Aranguiz.
Baada ya mchezo huo ambao Bravo anyeidaki Man City alikuwa mchezaji bora wa mechi sasa Chile wanakwenda fainali wakisubiri mshindi kati ya Ujerumani na Mexico kwa ajili ya fainali hiyo ya Confedaration Cup.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2skhluH
via IFTTT


Mbwana Samatta Ashindwa Kufurukuta Hispania..!!

Mbwana Samatta Ashindwa Kufurukuta Hispania..!!

Timu ya KRC Genk anayocheza Mtanzania Mbwana Ally Samatta imeshindwa kutamba ugenini dhidi ya wenyeji CeltA Vigo baada ya kukubali kichapo cha magoli 3-2 mchezo wa robo fainali wa Europa League.
Kwa matokeo hayo Genk wamejiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele kwani wanahitaji ushindi wa goli moja tu ili waweze kutinga hatua ya Nusu Fainali ya Michuano hiyo.
Magoli ya KRC Genk yalifungwa na Jean Boetius dakika ya 10 na Thomas Buffel aliyeingia akitokea benchi dakika ya 68, kwa upande wa wenyeji magoli yao yalifungwa na Pione Sisto dakika ya 15, Iago Aspas dakika ya 17 na John Guidetti dakika ya 38, kipigo hicho kinailazimu Genk katika mchezo wa marudiano Luminus Arena April 20 itabidi wapate ushindi wa kuanzia goli 1-0 ili wafuzu nusu fainali.

from Blogger http://ift.tt/2oBjgY9
via IFTTT


Wanasayansi Wagundua Uhai Katika Sayari ya Saturn..!!!

Wanasayansi Wagundua Uhai Katika Sayari ya Saturn..!!!

Mwezi wa Enceladus ambao uko kwenye sayari ya Saturn huenda ukawa mahali bora zaidi pa kwenda kutafuta maisha nje ya dunia.
Tathmini hii inatokea kufuatia uchunguzi katika sayari hiyo yenye kilomita 500 uliofanywa na Cassini.
Uchambuzi wa kemia wa Cassini unaonyesha matundu ya maji moto kwenye sakafu ya bahari ya Enceladus, maeneo ambayo yanahusishwa na kuwepo kwa maisha, hapa duniani.
Kuwepo kwa maji haya sio thibitisho kamili kwamba vitu vilivyo na uhai vinaishi katika mwezi huo mdogo lakini teknolojia zinaweza kutumika kupima maji hayo na kutoa ushahidi zaidi.
“Tuna uhakika kuwa kitu chenye uhai kinaweza kuishi kwenye bahari ya Enceladus lakini lazima tufanye utafiti zaidi,” alisema mwanasayansi wa Cassini kutoka Taasisi ya Utafiti ya Southwest, San Antonio, Dkt. Hunter Waite.
“Iwapo hakuna maisha huko, ni sawa, lakini ikiwa maisha yapo itakuwa bora zaidi,” alieleza BBC.
Bahari iliyopo kwenye Enceladus inakisiwa kuwa na kina kirefusana sana na yapo majimaji kwa sababu ya joto linalotokana na mvuto wa mara kwa mara kutoka kwenye sayari ya Saturn.
Cassini tayari amedhibitisha kwamba maji hayo yanashikana na sakafu ya bahari kutokana na aina ya chumvi na silika ambayo pia imeonekana katika mashimo.
Lakini wanachotaka kujua sana wanasayansi ni ikiwa maswala fulani yanayotendeka duniani pia yanaweza kufanyika katika Enceladus – kitu kinachoitwa serpentinisation, ambayo hutengeneza gesi ya hidrojeni.
“Kwa viumbe hai, hidrojeni huwa ni kama kama pipi – ni chakula wanachokienzi,” alieleza Dkt Chris McKay, mwanabiolojia wa maswala ya anga wa shirika la Nasa.
“Ni nzuri sana kwa kuvipa nguvu, na inaweza kusaidia viumbe vidogo sana. Kupata hidrojeni itakuwa vizuri sana na itakuwa moja ya ushahidi utakaoonyesha uwezekano wa kuwepo na uhai.”
Viumbe hai anavyozungumzia Dkt McKay vinaitwa methanojeni kwa sababu vinatengeneza gesi ya metheni vinapogusana na hidrojeni na gesi ya kaboni .
Nasa, ambayo inaongoza ujumbe wa Cassini , ilitakikana kufanya tangazo la hidrojeni miezi michache baada ya uchunguzi wa mwisho waroketi ya mwezini, Oktoba mwaka wa 2015.
Ziara ya Cassini sasa inakamilika . Baada ya kuizunguka Saturn kwa muda wa miaka 12, inaendelea kuishiwa na mafuta na sasa itawachiliwa kuingia kwenye anga ya dunia hiyo ya Saturn mwezi Septemba, kuhakikisha kuwa haiwezi kugongana na Enceladus na kusababisha kuchafuka kwake.

from Blogger http://ift.tt/2oxnePT
via IFTTT


Rais Joseph Kabila Aibuka Akiwa na Sura Mpyaโ€ฆ

Rais Joseph Kabila Aibuka Akiwa na Sura Mpya…

Rais wa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Joseph Kabila amesema kuwa atamteua waziri mkuu ndani ya saa 48 zinazokuja wakati akihutubia wabunge mjini Kinshasa.
Hata hivyo Rais Kabila leo ameoneka akiwa na sura tofauti kinyume na kawaida yake. Kabila ambaye kawaida hunyoa nyele kabisa, leo ameoneka akiwa na nywele nyingi kichwani pamoja na masharubu.
Wadhifa huo wa waziri mkuu utashikiliwa na mwanachama upinzani kama sehemu ya makubaliano yaliyoongazwa na kanisa katoliki.
Kabila pia aliahidi kuandaa uchaguzi baadaye mwaka huu lakini hakutangaza tarehe kamili.

from Blogger http://ift.tt/2oHk1js
via IFTTT


Kategori

Kategori