Showing posts with label 2017 at 06:09PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 06:09PM. Show all posts
MKURUGENZI WA WILAYA YA SONGWE APEWA MIEZI MIWILI KUJIREKEBISHA

MKURUGENZI WA WILAYA YA SONGWE APEWA MIEZI MIWILI KUJIREKEBISHA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amempa miezi miwili kuanzia leo Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Songwe, Bw. Elias Nawera abadili mwenendo wake kiutendaji na ashirikiane vizuri na Mkuu wa wilaya hiyo Bw. Samwel Jeremiah.
Amesema Serikali ya awamu ya Tano inawataka watumishi wote kufanya kazi kwa ushirikiano na kuheshimiana na atakayeshindwa kufanya hivyo hatavumiliwa.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana (Alhamisi, Julai 20, 2017) wakati akizungumza na watumishi wa wilaya ya Songwe akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Songwe.
Amesema watumishi wote wanatakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano ili malengo ya Serikali ya kuwahudumia wananchi yaweze kufikiwa. Pia waheshimiane sehemu za kazi na kila mtu azingatie mipaka ya madaraka yake.
“Mkurugenzi hapa hamsikilizi Mkuu wa wilaya anaondoka kituo cha kazi bila ya kuaga na amewagawa wakuu wa Idara. Namtaka afanye mabadiliko ya utendaji wake ndani ya miezi miwili na Mkuu wa Mkoa fuatilia jambo hili.”
Pia amewaagiza Wakuu wa Wilaya wote wasimamie utendaji wa wakurugenzi wa Halmashauri kwenye maeneo yao ili kuhakikisha wananchi wanahudumiwa ipasavyo.”Serikali hii si ya mchezo. Serikali hii inahitaji watumishi waadilifu wa kuwatumikia Watanzania.”
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Bibi Chiku Galawa amesema wamejipanga kuhakikisha changamoto zote zinazoukabili mkoa zinaboreshwa pamoja na kufikia malengo ifikapo 2020.
Ametaja malengo hayo kuwa ni kuhakikisha mkoa huo unakuwa kinara katika ukusanyaji wa mapato, kila mwananchi awe na bima ya afya pamoja na kuwa na hospitali katika kila wilaya.
Kuhusu mpango wa Serikali wa kuwa na uchumi wa viwanda amesema tayari wameshaanzisha viwanda vya maziwa, kukamua alizeti ikiwa ni kuunga mkono mpango huo.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, JULAI 20, 2017

from Blogger http://ift.tt/2uQcPF8
via IFTTT


Andre Silva atimkia Ac Milan.

Andre Silva atimkia Ac Milan.

Kati ya vilabu vinavyofanya balaa kubwa sana klatika msimu huu wa usajili ni Ac Milan na wanaonekana wamepania sana kurudisha heshima yao iliyopotea kwa miaka kadhaa sasa kwa kununua wachezaji wakubwa.
Leo klabu hiyo imetawala vichwa vya habari baada ya kumnunua moja kati ya washambuliaji waliokuwa wakisakwa na vilabu vingi msimu huu Andre Silva, mshambuliaji huyo amesaini Ac Millan kwa dau la euro 38m akitokea klabu ya Fc Porto.
Msimu ulioisha Silva alifunga jumla ya ,mabao 20 katika michezo ya ligi kuu nchini Ureno pamoja na ile ya UCL huku timu ya taifa akifunga mara 17 na kuassist mara 7 katika michezo 33 na tayari wachambuzi mbali mbali akiwemo pia mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo wamemmtaja Andre kama mwokozi mpya wa Ureno.
Cristiano Ronaldo amemtabiria mazuri Andre Silva katika siku zijazo na akisisitiz kwamba hata yeye akiondoka anaamini Ureno itakuwa salama “Kama nikistaafu soka naamini bado Ureno itakuwa salama kwani tuna mshambuliaji bora Andre Silva’ alisema Cristiano Ronaldo.

from Blogger http://ift.tt/2rSnxYW
via IFTTT


Mnyika Aaapa Kula Sahani Moja na Askari wa Bunge Aliyemsukuma Juzi Bungeni..!!!

Mnyika Aaapa Kula Sahani Moja na Askari wa Bunge Aliyemsukuma Juzi Bungeni..!!!

Mbunge wa Kibamba (Chadema), John Mnyika amesema atachukua hatua kwa kitendo cha kusukumwa kilichofanywa na askari wa Bunge mwishoni mwa wiki.
Alisema atafanya hivyo mara baada ya kumaliza msiba wa mmoja wa waasisi wa chama hicho, Philemon Ndesamburo.
“Nitatoa tamko na kuchukua hatua nikimaliza msiba, leo (jana) na kesho (leo) nipo msibani huku Moshi, lakini nitafafanua na kuzungumzia hilo nikimaliza,” alisema.
Mnyika alitolewa bungeni kwa nguvu na askari wa Bunge baada ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kuwaamuru kumtoa ndani akidaiwa kukiuka kanuni za Bunge wakati akichangia mjadala wa Wizara ya Nishati na Madini.
Pia, mbunge huyo alipewa adhabu ya kutohudhuria vikao saba vya Bunge, huku askari hao wakimtoa ndani kwa nguvu na kumsukuma.

from Blogger http://ift.tt/2rWIu6p
via IFTTT


Kategori

Kategori