Showing posts with label 2017 at 02:00PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 02:00PM. Show all posts
Baraka The Prince – Ben Pol Kaimba Upumbavu ..!!!

Baraka The Prince – Ben Pol Kaimba Upumbavu ..!!!

Baraka The Prince amemchana msanii mwenzake, Ben Pol kwa kumwambia hakuna chochote alichokifanya katika kazi yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Tatu’ licha ya kutengeneza kiki kubwa mitandaoni.
Baraka amesema hayo kupitia ukurasa wake wa kijamii Istagram huku akilalamika kwa kusema hakutegemea kuona kazi hiyo kwa jinsi alivyojitoa msanii huyo kwa kuweka picha zenye utata katika mitandao na kuwafanya watu kuwa na shauku kubwa kujua ni jambo lilipelekea vile.
“Nimekuwa ‘disappointed’ sana huu wimbo…Kwa jamaa alivyojitoa nilidhani ni kitu kikubwa kumbe upumbavu..’Save our music”.Ameandika Baraka

from Blogger http://ift.tt/2rD1PbY
via IFTTT


Wakenya Nao Wacharuka Kumuulizia Roma..Wadai Mbona Viongozi Wapo Kimya

Wakenya Nao Wacharuka Kumuulizia Roma..Wadai Mbona Viongozi Wapo Kimya

Mtangazaji wa Kenya Willy Tuva Amefunguka Haya:
@Regrann from @mzaziwillytuva – WHERE IS ROMA? VIONGOZI MBONA KIMYA?
East Africans love Tanzania’s Hip Hop star @roma2030. How can he and his friends disappear without a trace?
What crime did he commit? Alikamatwa na majambazi au polisi? Kama ni polisi, kosa lake ni gani? Kama ni majambazi hatua gani imechukuliwa kuwatafuta? Nauliza #WhereIsRoma
VIONGOZI NA VYOMBO HUSIKA TUSAIDIENI KUJUA!! Msinyamaze, kama ilivyokuwa kwa @naytrueboy na hii pia SAIDIENI

from Blogger http://ift.tt/2o9UBJX
via IFTTT


Magari Yaliyokutwa Kwenye Kontena Yawapandisha Kizimbani

WATU wanne wamefikishwa mahakamani katika kesi mbili tofauti za uhujumu uchumi, kwa kuingiza nchini magari sita kwa kuficha na nguo za mitumba, maarufu kama makontena ya Magufuli, na kuisababishia serikali hasara ya kukosa mapato ya Sh. milioni 478.7.
Katika kesi ya kwanza, watu wawili akiwamo raia wa Zambia, Agustino Kalumba (36) wamefikishwa mahakamani wakikabiliwa na mashtaka matatu ya kula njama, uhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya kukosa ushuru wa Sh. milioni 287.8.
Mbali na Kalumba mshtakiwa mwingine ni, Sultan Hassan (29) maarufu kama Mwarabu.
Washtakiwa walisomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.
Upande wa Jamhuri uliongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga akisaidiana na Wakili wa Serikali Batilda Mushi.
Katuga alidai kati ya Desemba mosi, mwaka jana na Machi mosi washtakiwa wakiwa na wengine ambao hawapo mahakamani walikula njama ya kutenda kosa la kusafirisha mali iliyofichwa.
Katika shtaka la pili, washtakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa kuwa kati ya Desemba mosi na 31, mwaka jana katika Bandari ya Dar es Salaam, iliyopo Temeke jijini Dar es Salaam, waliingiza gari tatu aina ya Range Rover Sports za rangi nyeusi, nyeupe na ‘daki bluu’.
Upande huo wa Jamhuri ulidai kuwa gari hizo ziliambatana na nguo, mabegi na viatu vya mitumba wakiwa na lengo la kuwadanganya maofisa watoza ushuru.
Katika shtaka la tatu, ilidaiwa kuwa kati ya Desemba mosi, mwaka jana na Machi mosi katika bandari hiyo, washtakiwa waliingiza mali wakiwa wameficha na kuisababishia serikali kukosa mapato ya Sh. 287,801,825.19 iliyokuwa kwenye kontena namba MSKU 9914168.
Hakimu Simba aliwaeleza washtakiwa hao kwamba kesi inayowakabili ni uhujumu uchumi, hivyo hawatakiwi kujibu chochote kwa sababu mahakama yake haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.
Katuga alidai kuwa upelelezi upo katika hatua za mwisho kwa ajili ya kuchanganua kama kesi hiyo itasikiliza na mahakama hiyo au Mahakama Maalumu ya Ufisadi.
Hakimu alisema kesi hiyo itatajwa Aprili 12 na washtakiwa wapelekwe mahabusu.
KESI NYINGINE
Katika kesi nyingine, Hassan na Ramadhani Hamis wamesomewa mashtaka matatu ikiwamo kula njama, uhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya Sh. milioni 190.9.
Washtakiwa hao walisomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage.
Katuga alidai kuwa Kati ya Desemba mosi, mwaka jana na Machi mosi washtakiwa walikula njama ya kutenda kosa la kuingiza mzigo ukiwa umefichwa.
Katika shtaka la pili, ilidaiwa kuwa Januari 24 katika Bandari ya Dar es Salaam, iliyoko Wilaya ya
Temeke, jijini Dar es Salaam, washtakiwa waliingiza magari matatu aina ya Range Rover Sports baada ya kuyaficha pamoja na nguo, viatu na magodoro ya mitumba.
Upande wa Jamhuri ulidai katika shtaka la tatu kuwa kati ya Desemba mosi, mwaka jana na Machi 4, washtakiwa waliingiza nchini magari matatu kwa kuficha na kuisababishia serikali kupata hasara ya sh. 190,923,267.76.
Katuga alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
Hakimu Mwijage alisema washtakiwa hawatakiwi kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.
Alisema washtakiwa wataendelea kukaa mahabusu hadi Aprili 12 kesi yao itakapotajwa.
Tazama video Mtoto amvua kofia Papa Francis

from Blogger http://ift.tt/2obJjG6
via IFTTT


Rasmi..Okwi Kutua Simba ..Kaburu Afunguka Haya Mazito Juu ya Ujio Wake..!!!

MAKAMU wa Rais wa Simba, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’, ameonekana kuwaweka gizani mashabiki wa Yanga kutokana na kitendo chake cha kila wakati kumtaja Mganda Emmanuel Okwi.
Okwi ni miongoni mwa wachezaji wanaotajwa kuwatia tumbo joto Yanga, zaidi ikiwa ni kutokana na kile alichowafanyia wakali hao wa Jangwani Septemba 2012 alipoiongoza Simba kuwapiga watani wao hao wa jadi mabao 5-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa kufahamu hilo, kwa muda wote ambao Okwi amekuwa nje ya kikosi cha Simba, mabosi wa klabu hiyo wamekuwa wakilitaja jina lake kwamba wapo mbioni kumrejesha kama sehemu ya kuwatisha Yanga.
Hali hiyo ilijirudia kwa mara nyingine juzi kupitia kwenye mitandao ya kijamii, ambapo Kaburu aliposti video ya mechi waliyoichapa Yanga mabao 5-0 na kuweka ujumbe uliosomeka: ‘Usiyemtaka anakuja’.
Ujumbe huo ulionekana kama kutuma salamu Yanga kwa wakati huu ambao timu hizo zinafukuzana kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Bara, Simba ikiwa kileleni kwa pointi zake 55, huku wapinzani wao hao wakifuatia na pointi 53.
Kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi kuwa Okwi anatarajiwa kurejea Msimbazi baada ya klabu yake hiyo ya zamani kumalizana na SC Villa ya Uganda anayochezea kwa sasa.
BINGWA lilizungumza na Kaburu kuhusu mchezaji huyo ambapo alisema, Kamati ya Utendaji ya Simba haina pingamizi kuhusu usajili wa Okwi kama benchi la ufundi litahitaji huduma yake.
Alisema kwa muda ambao Okwi ameishi na kutumikia kikosi cha Simba, hawana wasiwasi naye na kwamba Msimbazi ni sawa na nyumbani kwa Mganda huyo.
“Okwi, Simba ni nyumbani kwake, kama kocha atahitaji huduma yake, basi hatuna pingamizi,” alisema Kaburu.
Credit – Bingwa
TAZAMA HARMORAPA ALIVYO TIMUA MBIO BAADA YA KUIONA BASTOLA

from Blogger http://ift.tt/2nWx1Sl
via IFTTT


Kategori

Kategori