Showing posts with label 2017 at 06:12PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 06:12PM. Show all posts
Fundi Mbao Atiwa Mbaroni kwa Kubaka Watoto Wake Wawili wa Kuzaa..

Fundi Mbao Atiwa Mbaroni kwa Kubaka Watoto Wake Wawili wa Kuzaa..

FUNDI mbao, Japhet Lendiman (38) mkazi wa Daraja Mbili, anashikiliwa na Jeshi la Polisi, baada ya kubaka watoto wake wa kike wa darasa la sita na kidato cha kwanza.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi ili kubaini kiini cha tatizo hilo ni nini na kufuatiwa na hatua ya kufikishwa mahakamani. Mtuhumiwa huyo anashikiliwa na Jeshi la polisi tangu Juni 6, mwaka huu na upelelezi unaendelea kubaini undani wa tukio hilo.
Akimzungumzia mtuhumiwa huyo, mmoja wa majirani wa eneo hilo la Daraja Mbili (jina limehifadhiwa) alidai kuwa mzazi huyo amezoeleka kwa tabia hiyo mbaya mtaani kwao. Alidai kuwa mtuhumiwa huyo amezoea kubaka watoto wake mara kwa mara wakati mama yao akiwa kazini na kwamba Mei 28 majira ya saa 9:00 alasiri alimbaka tena mtoto wake (Jina tumelihifadhi) wa darasa la sita shule ya Msingi Daraja Mbili ndipo taarifa zilipoanza kuzagaa mtaani.
“Siku hiyo ya tukio lililosababisha mzazi huyo kukamatwa mtoto aliona sasa uvumilivu umefika mwisho, alikwenda kwa mama mkubwa na kutoa taarifa jinsi baba yake anavyomwingilia na kueleza kuwa anataka kunywa sumu ili afe,” alieleza jirani huyo. Alisema baada ya maelezo hayo mama mkubwa aliamua kuhoji watoto wote wa shemeji yake akiwemo mwingine wa umri wa miaka 14 (jina limeifadhiwa) ambaye yupo kidato cha Kwanza Sekondari ya Felix Mrema, alikiri kuingiliwa na baba yake tangu mwaka 2016. Aliendelea kueleza kwamba mama yao mkubwa ambaye ni muuguzi (jina limehifadhiwa ) katika moja ya hosptali mkoani Arusha, aliamua kutoa taarifa kwa mwenyekiti wa mtaa na Polisi.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2sUllOT
via IFTTT


KENYA: MGOMBEA AAHIDI KUBORESHA BIASHARA YA UKAHABA AKISHINDA

KENYA: Mgombea Ugavana wa Jimbo la Kisumu amewaahidi wapiga kuwa kuwa ataweka mazingira rafiki kwa wanaofanya biashara ya kuuza miili yao (makahaba) na kuhakikisha wanapata faida endapo watamchagua katika uchaguzi mkuu ujao.
Dkt. Hezron Mc’Obewa, ambaye anarusha karata yake ya ugavana katika jimbo hilo kumng’oa kiongozi aliyepo sasa, Jack Ranguma aliyasema hayo siku ya Jumanne alipokuatana na makahaba zaidi 300 katika Taasisi ya Goan.
Mgombea Ugavana Jimbo la Kisumu Dkt. Hezron Mc’Obewa (mwenye shati jeupe)
Dkt. Mc’Obewa alisema kuwa atashinikiza mikutano ya kimataifa iwe inafanyikia pia Kisumu ili makahaba hao waweze kupata soko.
“Watu hawa hulipa vizuri wanapokwenda nchi za ugenini, na wafanyabiashara hao hupata hadi Ksh 200,000 kwa usiku mmoja” alisema mgombea huyo. “Mikutano hii mikubwa ndiyo huleta wateja watakaowalipa ninyi kwa viwango vywa kimataifa” aliongeza.
Mbali na ahadi hiyo iliyozua gumzo maeneo mengi, mgombea huyo amewaahidi kuwa atahakikisha kunakuwapo ajira za kutosha ili watu wawe na fedha kwenye mifuko yako.
“Biashara yenu ninyi itakuwa na faida kama wanaume watakuwa na fedha mfukoni, na hii ndio sababu lazima tuhakikishe tunamaliza ukosefu wa ajira” alisema Dkt. Mc’Obewa.
Mgombea huyo alisema kiongozi wa sasa wa jimbo hilo hawajali kabisa makahaba hao ambao chini ya mwamvuli wa Kisumu Sex Workers Sacco. Hivyo amewasihi kumchagua yeye ili waweze kufurahia biashara yao na atahakikisha anaimarisha ulinzi dhidi yao.
“Wakati mwingine unapata mteja ambaye anakupakiza kwenye gari lake, lakini usalama wako unakuwa ni mdogo, au unafayia kazi katika mazingira machafu ambayo yanahatarisha afya yako. Haya yote ndiyo tunataka yabadilike”, alisema.
Aidha, mgombea huyo aliwataka makahaba hao kujisajili katika Shirika la Taifa la Bima ya Afya (NHIF) ili kuweza kupata huduma za kitabibu.
Tazama video Mtoto amvua kofia
 Papa Francis

from Blogger http://ift.tt/2nn27O0
via IFTTT


Kategori

Kategori